Kibaki amerudi Ikulu

Where are the African presidents? AU hili sio swala la Kenya peke yake hivi sasa. Mbona wako kimya badala ya kutoa hukumu yao hivi sasa wakati raia wasio na hatia wanateketea.

JK, M7, Mbeki etc. Where are you? Stand up to be counted.

You forget that this is simply a club of eminent dictators in Africa who love everything from the west except their way of democracy!
 
kenya.jpg

our_kenya.jpg

kenyaonfire.jpg

1_236683_1_3.jpg

071231-kenya-hmed-135a.h2.jpg

CHINI VIKOSI VYA GSU/FFU VYAIVIRINGA UHURU PARK RAILA ASIJE HAPA

0,1020,1056976,00.jpg

_________________________________________________________________

VIDEO YA KUONYESHA UNYAMA DHIDI YA WAFUASI WA UPINZANI
MUHIMU: BONYEZA KWENYE HIO PICHA YA ASKARI NA BUNDUKI YAKE

http://www.spiegel.de/politik/ausland/0,1518,525958,00.html

The kenya we know will never be the same whatever comes out of this. The kenyan media tried to show police and army brutality against tanzanian from pemba in the 2000 election.

I hope that tanzaniam media will return the favor at this time when the military rule in kenya has sealed off the local media.
 
Marekani wameshamtambua Kibaki and that settles it.. unfortunately.

Nimesikia pale CNN kuwa State Department ime-withdraw statement yake ya kumtambua Kibaki hadi hapo Kenya ikapotatua mgogoro wa kisiasa uliotokana na uchaguzi huu, na kurudisha amani kwa wananchi.
 
Nimesikia pale CNN kuwa State Department ime-withdraw statement yake ya kumtambua Kibaki hadi hapo Kenya ikapotatua mgogoro wa kisiasa uliotokana na uchaguzi huu, na kurudisha amani kwa wananchi.

Ni kweli Mkuu,Serikali ya Marekani haijatambua Matokeo ya Uchaguzi wa Urais kenya,pia Serikali za Uingereza na Canada hazijaitambua serikali ya Kibaki.Cha ajabu na kustaajabisha ni kwamba,Serikali zetu za kiafrika zipo kimya na mpaka sasa,mauaji yanaendelea kwani ni Raia 125 wamekwishakufa,wapo wapi African Union? Au ndio ile Tabia ya kulinda marafiki?.
 
Quote:-

"Nimesikia pale CNN kuwa State Department ime-withdraw statement yake ya kumtambua Kibaki hadi hapo Kenya ikapotatua mgogoro wa kisiasa uliotokana na uchaguzi huu, na kurudisha amani kwa wananchi."

Hawa vinyonga hatuwezi kuwaamini, off course wame-support the whole nonesense behind the scene, na kwenye hizi siasa chafu that is all what counts, kuliko haya wanayosema kwenye public, it too late!

Cha muhimu ni je hawa viongozi wetu wa Afrika wako wapi?
 
Narudia. Tumeona Uganda ( mnakumbuka OAU ilifanya mkutano wake Kampala wakati wa Idi Amin?). Tumeona Burkina Faso (mnamkumbuka Thomas Sankara?). Tumeona Zimbabwe. Tumeona Sudan. Na hapa pia hakuna jipya litakalofanyika. Roho ya mwafrika haina thamani mahali popote hata pale tunapopaita kwetu. halafu tunashangaa kwa nini hakuna mtu anayetuchukua serious!Mungu alinusuru bara letu. Mungu awanusuru jirani zetu.
 
Quote:-

"Nimesikia pale CNN kuwa State Department ime-withdraw statement yake ya kumtambua Kibaki hadi hapo Kenya ikapotatua mgogoro wa kisiasa uliotokana na uchaguzi huu, na kurudisha amani kwa wananchi."

Hawa vinyonga hatuwezi kuwaamini, off course wame-support the whole nonesense behind the scene, na kwenye hizi siasa chafu that is all what counts, kuliko haya wanayosema kwenye public, it too late!

Cha muhimu ni je hawa viongozi wetu wa Afrika wako wapi?

Bendera fuata upepo, wanasubiria mmoja aanze uone wote watakavyofuata..
 
Ambacho huwa sielewi hao waangalizi wao huwa wanakazi gani? hapa si ndo wangetimiza jukumu lililo waleta kwa kusema kweli na kushinikiza haki itendeke?
 
  • Thanks
Reactions: amu
Ambacho huwa sielewi hao waangalizi wao huwa wanakazi gani? hapa si ndo wangetimiza jukumu lililo waleta kwa kusema kweli na kushinikiza haki itendeke?

Mkuu Rwabugiri,

Ingawa mimi huwa sina tabia ya kuwatetea hawa waangalizi wa kimataifa lakini katika hili nitawatetea kidogo. Kwa wale ambao tulikuwa tunafuatilia media ya kenya on Saturday watamkumbuka yule mama mzungu aliyemsimamisha Kivuitu kuendelea na speech yake akisisitiza kuwa matokeo ya Kajiado North kama sikosei ni tofauti na yale ambayo yalisomwa kituoni wakati yeye au mwakilishi wake akiwepo. Baadaye pia aliendelea kusema kuwa matokeo ya Kamukunji pia ni tofauti na yale yaliyosomwa mwanzoni baadaye ulimsikia kivuiti akijikosha kuwa kajiado imefutwa na kamukunji imefutwa!

Mwakilishi wa EU alihojiwa na KTN akasema kuwa matokeo ya sehemu za meru ni tofauti na yale ambayo walipata wao. Hata tamko la EU limequestion matokeo ya Molo.

Serikali ya mabavu ya kenya ilivyoona hawa jamaa wameanza kutoa madai yao public on sunday ndipo ikakataza live broadcasting na baadaye kibaki akaapishwa kimya kimya tu.

Katika hili walisema hata feed za KTN zinatumwa kimya kimya kwenye mitandao kama kalenjin.net nk zilikuwa zinaonyesha haya ingawa sasa hivi hata mtandao wa kalenjin nao hauna live info.

Yaani kenya sasa hivi imekuwa North Korea! ni aibu kabisa ingawa baadhi ya watanzania walikuwa wakifurahia ushindi wa Kibaki jana.
 
Yaani kenya sasa hivi imekuwa North Korea! ni aibu kabisa ingawa baadhi ya watanzania walikuwa wakifurahia ushindi wa Kibaki jana.

Kwa bahati mbaya, ndiyo demokrasi. Hatuwezi wote tukakubaliana. Poleni sana kwa hayo yaliyowasibu. Sidhani kama kuna mtanzania anayefurahia kuona mambo yanayotokea Kenya. Kama yupo, ana matatizo yake binafsi. Au ni ule ugonjwa tulio nao, kila kitu kwetu ni mzaha! Poleni sana
 
Quote:-

"Sidhani kama kuna mtanzania anayefurahia kuona mambo yanayotokea Kenya."

Hizi ni label za kawaida hapa inapotokea mijadala mikali ya ishus, mkuu nina documentary ya Mobutu-The King Of Afrika, a very shameful thing to watch, kilicho nishangaza humo ndani ni just two years baada ya Mobutu kumuuua Lumumba, Mwalimu alikwenda kutembelea huko tena yeye na Mobutu wako kwenye gari la wazi wakiwapungia mikono wananchi, tena kwa furaha sana, sasa ina maana Mwalimu alikuwa ana-support yale mauaji ya Lumumba?

Jawabu ni hapana, lakini life has to go on, wa-Tanzania tuliwa-support Biafra, baadaye tukajirudi na kuwa friends na Federal government of Nigeria, ndio maana ya siasa na kuganga yajayo badala ya kulalia yaliyopita, Kibaki, ameshaapishwa kuwa the next president wa Kenya for the next Five years, leo nilikuwa ninaaangalia TVT jinsi viongozi wetu wa upinzani walivyojitokeza kukosoa uchaguzi huo, lakini mwishoni wote wamekubali kuwa baada ya kuapishwa kwa Kibaki, haitakuwa rahisi kubatili matokeo, na wamewaomba wananchi wa Kenya kuweka taifa lao mbele zaidi ya special interest zao, je ina maana hawa nao wanam-support Kibaki? Jawabu ni hapana isipokuwa kama politicians wanaelewa kuwa rais aliyekwisha apishwa labda kuna uwezekano wa 25% kuwa anaweza kubadilishwa,

Hatupendi yaliyotokea huko kwenye mchakato mzima wa uchaguzi wao, lakini pia tunaelewa kuwa imekuwa ni kawaida yao kuwa vurugu wakati wa uchaguzi, tunakumbuka Moi kila wakati alikuwa akishinda kwa ujanja huu huu na damu kumwagika, na bado tukaendelea kuwa marafiki naye kama taifa,

Kuna some of us ambao to put a side mambo ya vurugu za demokrasia kupindishwa, tungependa pia kujua elimu yake ya siasa yaani uchaguzi mzima, na pole pole tumeshaanza kujifunza yaliyojiri na yale ambayo hayakujiri kutoka pande zote mbili kufuatia political strategies zao, inaonekana kuwa so far Botswana ndio peke yao wenye uchaguzi wa halali katika Afrika, sasa what that says about the rest of us Afrikans, kwamba tunafurahia yanyoendelea kwenye nchi zetu?

Kama hatufurahii tumefanya nini so far? Je does that gives us a platform kuwa-label wengine kuwa wanafurahia yalliyotokea Kenya jana?
 
I cant wait for a time ambayo Tanzania itakuwa na kizazi kipya ambacho hakihalalishi ubaya wowote unaoendelea kwa kutoa mfano wa ubaya uliofanywa na Nyerere. Inaonekana kwa baadhi ya watu kila kibaya alichofanya nyerere ni sababu tosha ya kusupport ubaya wowote utakaondelea sasa hivi.

Jawabu ni hapana, lakini life has to go on, wa-Tanzania tuliwa-support Biafra, baadaye tukajirudi na kuwa friends na Federal government of Nigeria, ndio maana ya siasa na kuganga yajayo badala ya kulalia yaliyopita, Kibaki, ameshaapishwa kuwa the next president wa Kenya for the next Five years, leo nilikuwa ninaaangalia TVT jinsi viongozi wetu wa upinzani walivyojitokeza kukosoa uchaguzi huo, lakini mwishoni wote wamekubali kuwa baada ya kuapishwa kwa Kibaki, haitakuwa rahisi kubatili matokeo, na wamewaomba wananchi wa Kenya kuweka taifa lao mbele zaidi ya special interest zao, je ina maana hawa nao wanam-support Kibaki? Jawabu ni hapana isipokuwa kama politicians wanaelewa kuwa rais aliyekwisha apishwa labda kuna uwezekano wa 25% kuwa anaweza kubadilishwa,

Mambo ya kutetea uovu kwa sababu tu miaka 30 iliyopita kuna uovu mwingine Tanzania iliuunga mkono ni very dissapointing. Maisha ya watu yanateketea katika wakati ambao kila mtu atahalalisha hili kwa mifano mingine mibaya iliyopita.

kutokemea uovu na kuacha life iendelee kwa sababu rais ameshinda uchaguzi ndiyo yamekuwa yanawanyima CUF uchaguzi kila mwaka zanzibar na huku mamia wakiuwawa na polisi na jeshi. Martin Luther King aliwaomba viongozi wa kidini marekani miaka ile ya sitini wasijiunge na vurugu ila pia wasikae kimya bila kukemea uovu uliokuwa unafanyika.

Hatupendi yaliyotokea huko kwenye mchakato mzima wa uchaguzi wao, lakini pia tunaelewa kuwa imekuwa ni kawaida yao kuwa vurugu wakati wa uchaguzi, tunakumbuka Moi kila wakati alikuwa akishinda kwa ujanja huu huu na damu kumwagika, na bado tukaendelea kuwa marafiki naye kama taifa,

Kuna some of us ambao to put a side mambo ya vurugu za demokrasia kupindishwa, tungependa pia kujua elimu yake ya siasa yaani uchaguzi mzima, na pole pole tumeshaanza kujifunza yaliyojiri na yale ambayo hayakujiri kutoka pande zote mbili kufuatia political strategies zao, inaonekana kuwa so far Botswana ndio peke yao wenye uchaguzi wa halali katika Afrika, sasa what that says about the rest of us Afrikans, kwamba tunafurahia yanyoendelea kwenye nchi zetu?

Nina matumaini kabisa kuwa wewe si msemaji wa waliokuwa wanaunga mkono yanayofanywa na serikali ya Kibaki.

Kama hatufurahii tumefanya nini so far? Je does that gives us a platform kuwa-label wengine kuwa wanafurahia yalliyotokea Kenya jana?

Ku-label watu ndio mchezo wa kawaida kabisa hapa JF na ndio kumkoma nyani giladi huko bila kumwangalia usoni.
 
Mungu wangu wa mbinguni, yaani watu wanachomwa moto kanisani. Na sasa wakalenjin kwa maelfu wamechukua silaha na wanataka kusafisha wakikuyu wote walio Rift Valley.

Haya yote kwa sababu ya nini? eti watu wachache waendelee kuwa madarakani na nchi i-move on? Inaonekana chaguzi za zanzibar kuanzia 95 hadi 2005 kungekuwa na JF basi tungejua mengi yanayofanywa na wabinafsi waliopa kuwa kabila fulani haiwezi kuongoza nchi yao. Kwa kenya wajaluo hawatakiwi na wakikuyu na kwa zanzibar wapemba wameambiwa kuwa hawawezi kuongoza zanzibar! mungu turehemu viongozi wetu wajifunze kutokana na hili.

Soma hii habari ya BBC:

http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/7166932.stm
 
Sasa tunahitaji analysis of why ODM did not 'win'. My quick reaction, pamoja na claims of Kibaki rigging: One of key strategy miscaculation by ODM is Kalonzo factor- they would have convinced him to support Raila- as Kalonzo got 800,000 votes- which would have boosted Raila votes!

ODM took Kalonzo lightly and concentrated on Kibaki!

Calculations zilikuwa sahihi kabisa. Kutokana na masuala ya ukabila,Raila alikuwa anafahamu kuwa asingeweza kuzipata kura za watu wa kabila analotoka Kalonzo na kwa maana hiyo zingeenda kwa Kibaki.Sasa kwa kuwa alikuwa na uhakika kuwa kura hizo hatozipati,alihakikisha kuwa Kibaki hatozipata pia,na namna pekee ya kufanya hivyo ni kumwambia Kalonzo ajitenge na agombee pia naye urais.Hivyo kura za watu toka Kabila analotoka Kalonzo zilibaki kwa Kalonzo.
 
Na kwanini always the "losers" ndo waweke utaifa wao mbele na si wale wanaochukua madaraka kwa nguvu.Mimi nawaunga mkono hawa wakenya wanaotumia nguvu kudai haki yao, kwani hata huyo Kibaki katumia nguvu kuingia madarakani.Huu ni mwanzo wa Kibaki kutoweza kuitawala kenya.
 
Quote:-

"Calculations zilikuwa sahihi kabisa. Kutokana na masuala ya ukabila,Raila alikuwa anafahamu kuwa asingeweza kuzipata kura za watu wa kabila analotoka Kalonzo na kwa maana hiyo zingeenda kwa Kibaki.Sasa kwa kuwa alikuwa na uhakika kuwa kura hizo hatozipati,alihakikisha kuwa Kibaki hatozipata pia,na namna pekee ya kufanya hivyo ni kumwambia Kalonzo ajitenge na agombee pia naye urais.Hivyo kura za watu toka Kabila analotoka Kalonzo zilibaki kwa Kalonzo."

Mkuu Nyangumi,

Heshima mbele, hili lako ni darasa zito kuhusiana na yaliyojiri, ndio hasa elimu ya siasa tunayoitafuta kuhusiana na uchaguzi huo.
 
haya yote ni kwa hisani ya kenyan-tanzania mwanaJF mwenzetu aliyeko msitari wa mbele huko kenya kutuletea kile ambacho Kibaki na ccm yake ya kenya ya mafisadi wamefanya.

Kauli zingine unaweza kuziita ni za kishenzi
 
Kauli zingine unaweza kuziita ni za kishenzi

Hata wakikukuyu wa forum ya mashada walikuwa wanawaita makabila mengine kwa lugha yako kabla yanayotekea leo hayajatoke.

Ita lolote lakini mimi nalinganisha yaliyotokea zanzibar dhidi ya wapemba mwaka 95 - 2005 na yale yanayotokea leo dhidi ya waluo na kabila zingine huko kenya.

Kama kawaida ya JF - dare to talk openly - Nimesema hili so wewe unaweza kuja na counter-argument au kuendelea kujionyesha ulivyo kwa kuendeleza matusi.
 
Na kwanini always the "losers" ndo waweke utaifa wao mbele na si wale wanaochukua madaraka kwa nguvu.Mimi nawaunga mkono hawa wakenya wanaotumia nguvu kudai haki yao, kwani hata huyo Kibaki katumia nguvu kuingia madarakani.Huu ni mwanzo wa Kibaki kutoweza kuitawala kenya.

Hilo ndilo swali hata mimi najiuliza hapa. Mtu anaiba uchaguzi, kisha anatumia polisi na jeshi kuuwa waandamanaji, baadaye akichoka kumwaga damu anaanza kusema kuwa walioshindwa ndio waweke utaifa mbele (huku akitoa mifano ya marekani na mambo ya miaka mingi iliyopita) ili nchi i-move on! ajabu!

Polepole tu tutafika. Naomba mungu JF iwe bado hewani wakati wa uchaguzi ujao wa zanzibar!
 
Back
Top Bottom