Kibaka auawa mwanza.

Shomari

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,112
241
Kijana mmoja ambaye hakuweza kutambulika jina lake mwenye umri kati ya miaka 20 jana amepata kipigo kikali kutoka kwa Wananchi wenye hasira kutokana na kosa la kukwapua na kutaka kubaka.

Tukio hilo limetokea katika maeneo ya Pasiansi chini karibu kabisa na kiwanda cha kutengeneza bia wilayani Ilemela.

Ikiwa ni saa 12 na nusu Asubuhi , inasemekana kijana huyo pamoja na mwenzake ambaye alifanikiwa kutoroka waliwavamia akina mama wawili waliokuwa wamejidamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kwenda kujipatia riziki katika shughuli zao za dagaa, inasemekana mmoja wa vijana hao ambaye hajaonekana mpaka sasa alimvamia mmoja kati ya wale akina mama huku akitaka alipwe deni lake. Wale kina mama walishangaa na kujiuliza ni deni gani hilo, ndipo mmoja kati ya vijana hao wawili ( aliyekimbia ) akafanikiwa kuwany'angany'a wale kina mama fedha kiasi cha shilingi 15000 pamoja na simu aina ya Nokia .

Baada ya kuwa wamewanyang'anya mali zao, wale vijana bila haya wala uoga wa aina yeyote ile wakaanza kuwavua nguo wale kinamama na kulazimisha tendo la ndoa bila kujali kwamba wale akina mama wana umri sawa na bibi zao. ''Mmoja kati yao alianza kumlazimisha mwenzangu kumla denda'' alisikika mmoja kati ya hao mama akitamka.
Katika purukushani hizo ndipo wale akina mama wakawa wamefanikiwa kupiga uyowe wa kuomba msaada, mmoja kati ya wale vibaka akawa amekimbia pamoja na zile mali alizoiba na kumwacha mwenzake akiwa amejificha ndani ya majani,baada ya Raia kuwa wamefika pale walianza kutoa kipigo kwa yule kibaka mwingine aliyebaki pale.

Baada ya hapo alichukuliwa na kuanza kupelekwa kituo cha polisi lakini juhudi hazikuzaa matunda baada kibaka yule aliyeonekana kuwa na uzoefu wa kutosha kukimbilia katika mashamba ya mpunga yaliyoko katika maeneo hayo, Raia hawakukata tamaa bali walikula naye sahani moja na walipompata walizidi kumwongezea kipigo, walianza kumkokota tena lakini walipofika maeneo ya soko dogo la samaki pale Pasiansi yule kibaka alionekana kuishiwa nguvu za kukimbia na hata kutembea.

Hadi kufikia muda wa saa 2 asubuhi yule kibaka aliendea kupata kipigo toka kwa Raia wenye hasira huku baadhi yao wakiwa ni watu waliokuwa wakipita katika tukio wakielekea kazini, lakini kitu kimoja kilichowashangaza baadhi ya watu ni kwamba pamoja na kipigo chote kile cha takribani masaa mawili bado yule jamaa alionekana yuko fiti, baadhi ya watu walikuwa wakihisi huenda yule jamaa alikuwa na hirizi. Ndipo harakati za kutaka kumchoma moto zilipoanza haraka iwezekanavyo. Mpaka tunakwenda hewani yule jamaa alionekana kuwa nyan'ganyan'ga huku ikiwa haijulikani kama atapata ahueni, lakini habari zilizokuja kujitokeza hapo baadaye inasemekana yule kijana aliaga dunia.

Kama wanajamii tungependa kuwashauri vijana wenye nguvu zao kama huyu waacha tabia za kutaka kupata mali kirahisi badala yake wafanye kazi kwa bidii ili kuondokana na fikra chafu pamoja na kujiongezea kipato kwa njia iliyo halali.
 
Hii hukumu tungisogeza hadi kwa mafisadi tungeweza kujikomboa hata hawa wakwapua simu wasingekuwepo, kwani maisha yangekuwa bora kwa kila mtanzania na si bora maisha!
 
Back
Top Bottom