Kibaka akiokoka sheria inasemaje?

Amoeba

JF-Expert Member
Aug 20, 2009
3,292
781
Mhasibu alitoweka na 23M miaka 9 iliyopita, sasa anapiga simu kuwa amerudi na ameokoka, anataka kurudisha hiyo pesa (23M ) Lakini kwa masharti kuwa kesi IFUTWE. Je sheria inasemaje kwa mtu kama huyo, ni adhabu gani inayomkabili kama nikisisitiza kumtia mbaloni?
Kunatakiwa ulinganifu wa 23M kwa mika 9 na adhabu atayoipata, na kuona kama ni heri kumwachia au kumkomalia!
Wanazuoni tafadhali
 
Hii kali. Kabla hawajaja kujbu naomba kukuuliza hivi:
Huyo jamaa ametenda mengi mabaya, je ataomba radhi kwa yote aliyoyafanya kabla ya hapo? Mfano kuomba radhi waume wote wa wanawake alio cheat nao, au kuwatukana au kuwasengenya. Kama hapana kwa nini anataka kufanya selective confessions? Kuna wakati mtu unajibebesha guilty zisizo na sababu wakati Mungu anasema dhambi zako amezisahau na ni kama Mashariki ilivyo mbali na Magharibi. Amuombe Mungu amsaidie katika kuamua hilo.
 
Suala kubwa mimi navoona si kuokoka, suala ni KURUDI MJINI. yeye alivochukua hiyo pesa alitokomea kusikojulikana, kwa miaka 9 ameshafanyia biashara na imemllipa, na inawezekana anataka kuwekeza kwa hyo anajiweka sana ili awe free na kutamba mtaani!
 
kwanza mmsifu kuwa alizifanyia biashara hizo pesa. je angekuja na ndala tu? ni vizuri alipe na ka-interest. na asamehewe
 
kwanza mmsifu kuwa alizifanyia biashara hizo pesa. je angekuja na ndala tu? ni vizuri alipe na ka-interest. na asamehewe

Ni kweli mkuu.
Kwanza anapiga simu za payphone mitaani (anaogopa pingu), negociation yake anaomba kulipa 25tu hana zaidi, na anaonekana ana kiburi, anasema kama hiyo haitoshi hana jinsi atakuwa tayari kupanda kizimba! nataka kujua hukumu inayomkabili ili ipatkane hata jinsi ya kumtisha kdogo apande dau kama ana pesa. Hiyo 23M ilishasahaulika machungu yake, kama kichwa ngumu alambe miaka tu kama inalipa.
 
Huyo hamna cha kurudisha pesa wala nini,mnanikumbusha mambo ya JKna mafisadi wa EPA,nani kakwambia mwizi arudishe alichoiba ili asamehewe?Basi sheria zitakuwa hazina maana kwani hata kibaka aliyeiba kuku ndugu zake wanaweza rudisha kuku mahakamani na akasamehewa.
Huyo ni wa jela tu hata kama kaokoka,wokovu aende nao gerezani
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom