Kiapo cha Wakubwa katika Katiba Mpya

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
Katika wakati ambapo watu wanasubiri kuchangia maoni yao ya kutunga Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sisi wengine tuanjua ya kwamba hatutapata muda wa kuchangia hasa kulingana na kazi tunazozifanya au kuwa nje. Mimi kama mmoja ambaye naona kupata fursa ya kuchangia, nilikuwa na wazo juu ya Viapo kwa Viongozi wanaokuwa wanasimamia tunu za Watanzania, mfano rais, RC, DC, Makatibu wakuu na wengine wengi.

Hawa wanabeba kundi kubwa la watu wenye kibeba na kusimamia resources za taifa.

Katika Viapo vyao, huwa wanatumia Misaafu ya dini zao. Lakini kwa wale wasio na imani kama vile Baregu anaweka mikono kifuani.

Sasa, mimi naona katika Katiba kuwe na kipengele cha Viapo kama:-
i) Kuwa na kitabu maalumu cha viapo ambacho zaidi ya kuwa na Msaafu hiki kitabu ndo kiwa kiongozi wa kiapo chako;
ii) Kitabu hiki kiwe na Maadili ya kiongozi;
iii) Kionyeshe mambo muhimu ambayo kiongozi anatakiwa awe nayo katika utendaji wake;
iv) Jinsi kiongozi anatakiwa kusimamia resources za taifa;
v) Jinsi kiongozi anavyoweza kuwajibika bila kuwajibishwa; pamoja na
vi) Kuangalia malalamiko ya wananchi yanavyoweza kukuwajibisha bila hata kuwajibishwa kisheria.

Naomba Watalumaa wachangie juu ya hili

NAWASILISHA

 
Back
Top Bottom