Kiama posho serikalini chaja: Serikali, Bunge Mahakama wakaribia kubwaga manyanga chini

katika ili ntamkumbuka dr slaa,ambaye aliliasisi katika bunge wakati akiwa mbunge,akataja mpaka mshahara wa mbunge,bunge lilipotaka kumwajibisha akawachenga kuwa kataja malipo yale mwenyewe,pia kamanda zitto amesaidia sana kuleta mabadiliko,apa namkumbuka pia mh mbowe kwa kukataa posho pale bungeni na kuziita WIZI WA KITAASISI. Naanza kukubaliana na wengi kuwa sasa cdm inatawala kutokea nje ya ikulu,si katiba,si posho,si mashangingi,bado cdm itawasumbua sana!
 
Picha lianendelea wale wabunge walioingia mjengo kwa hela za kukopa kupigia kampeni matumbo joto.
 
mpango wa kuzifuta posho zote katika bajeti kuu ni suala la kitoto na hii inaonyesha wazi namna viongoz wetu wasivyokuwa na kujitoa fahamu na uzalendo umepoteaa. Watanzania tuamke na kuchukuwa hatua stahili
 
Zifutwe zifutwe hata jumatatu hiii ijayo....ili mishahara iangaliwe upya na iwe ya kuwezesha wote kupata mkate wa kila siku na mahitaji mengine ya maisha.....fungu la posho laweza kuwa added kwa basics za watumishi hata kama itakuwa ni peanut.......sababu hii si biashara kupata wengi kidogo kilichopo ni bora
 
mpango wa kuzifuta posho zote katika bajeti kuu ni suala la kitoto na hii inaonyesha wazi namna viongoz wetu wasivyokuwa na kujitoa fahamu na uzalendo umepoteaa. Watanzania tuamke na kuchukuwa hatua stahili

Ukisikia yallaaaaaaaaaa.......ujue limempata....mtajifunza kuishi upya bila posho
 
Ukiangalia vizuri utagundua kweli posho za wabunge hazina uhalali, posho ya nini wakati ni majukumu yake ya msingi.
 
Taifa la wapiga soga kama tumeweza kuishi bila umeme bila madktari basi tunaweza kuishi bila poshooooooooooo ila muangalie jeshini waungwana maafande wasije wakatuludi
 
Kama huo ndiyo mpango wa wabunge then kwa mara ya kwanza nitawasifu wabunge kwa uamuzi wa busara watakao ufanya!Haliniingii akilini mtu kulipwa sitting allowance tena akiwa ndani ya majukumu yake ya kazi!Futa posho kote muongeze mishahara wafanyakazi waserikali!!
 
mbombo ngafu!ss wameamua kumalizia hasira zao hadi kwa wananchi?ss wenye mishahara midogo si ndo watakua ombaomba?hii movie ya posho tamu sana ngoja season 2 ikianza sijui itakuaje
 
Mwalimu anapata sitting allowance lini? Serikali inatakiwa iache wizi, ifute posho, iongeze mishahara na ipunguze kodi hiyo ndio njia pekee watu wanaweza ishi. Wengi hufurahia posho sababu hazikatwi kodi, wanaona hata mishahara isipoongezeka sawa tu kwani inakatwa kodi kubwa!

sitting? kwani wakienda kusaisha mitihani hawalipwi? wafute kila kitu...
 
mbombo ngafu!ss wameamua kumalizia hasira zao hadi kwa wananchi?ss wenye mishahara midogo si ndo watakua ombaomba?hii movie ya posho tamu sana ngoja season 2 ikianza sijui itakuaje

Rekebisha - siyo "wananchi" bali "watumishi wa serikali"! Ushamfikiria mkulima anayekopwa hadi mazao/jasho lake? Yeye anakula POSHO wapi? Wenye kulilia posho ni asilimia ndogo mno ya WANANCHI!
Sekta binafsi kuna posho? Mama ntilie, mwendesha mkokoteni/guta/bajaj nani anamlipa posho?

Nilimskia rais jana akisema AMEKATAA watu kutoka Sekta binafsi kupigania nafasi na fursa zilizoko serikalini na kwamba watumishi wa umma wanaovumilia kufanya serikalini ndio watapata teuzi! Sasa futeni posho na mvumilie msubiri teuzi za nafasi za juu bila kushindanishwa na mtu!
 
Wanabodi. Ni vema kujua kuwa mfumo wa kulipana posho una madhara makubwa mawili
1. Ujengaji wa matabaka kazini
2. Uhararishaji wa wizi pamoja na kukwepa kodi

1. Kwa wale walioko serikalini mtafahamu kuwa mshahara wa watu walio wengi hauzidi Tzs 900,000/- (gross) na nijuavyo mimi ni vigumu kuishi kwa kiasi hicho kama mshahara wako halali ukajenga nyumba, ukapeleka mtoto shule na kununua gari. Kwa sehemu kubwa posho zimejenga matabaka maofisini, kwa kuwa endapo mnalingana cheo lakini idara uliyopo haina fursa za posho wewe ndoutaishia hivyo hivyo. Lakini mbaya zaidi, endapo mfanyakazi wa ngazi ya chini akilalamikakuwa mshahara hautoshi, wenzie hawawezi kumwelewa kuwa hautoshi maana wao wanafursa zakupata hela za ziada zaposho. Matokeo yake wale walio nacho wanazidi kuwa nacho na wale wengine wanaendelea kuwa na maisha magumu. Hii huleta mgawanyiiko na kukosa umoja (solidarity) wakati wa kudai haki za msingi za wafanyakazi

2. Kuna njia nyingi za kuhararisha wizi,ikiwepo pamoja na hii. Kwa wale ambao tumekuwa tunafanya uchambuzi wa miradi ya serikali,ni jambo la kushangaza kuwa maeneo mengine miradi inatengewa kiasi kikubwa cha hela, lakini unaweza kukuta baadhi ya miradi inatumia 45% ya gharama kwenye posho na matumizi yasiyo ya moja kwa moja (indirect expenditures). Mbaya zaidi ikumbukwe kuwa kwa mfumo huu wa posho kodi huwa haikusanywi na hivyo tunaikosesa serikali mapato

kudadadeki visasi hadi kieleweke na futeni posho zenu futeni posho hadi za walimu na mkae mkijua 2015 hamrudi. si ni visasi?
 
Kama kweli ipo hivyo basi watumishi wa uma wa kada za ualimu,utabibu,upolisi na wengine wote wenye mishahara midogo wategemee maumivu zaidi bajeti ijayo.Kwa nini?
Wabunge wapenda posho(All CCM except Makamba) na Shibuda wa Chadema wanafanya hivi kulipa kisasi cha kushupaliwa.Hawafanyi hivi kwa manufaa ya uma bali kwa kuwakomoa wengine.Wabunge still wana mishahara mikubwa ambayo inawatosha.Kinachopiganiwa ni kufuta posho zote na kuboresha mishahara ya watumishi wa uma.Wabunge hawatoridhia ongezeko lolote la mishahara linalokidhi kwenye bajeti ijayo ili kuwakomoa wote wanaoshupalia posho zao.Hivyo hakuna nafuu yoyote itakayopatikana hata kama posho zikifutwa kwa misingi hii ya kukomoa.Posho inatakiwa ifutwe ili kuleta ulinganifu(kama sio kupunguza gap) wa mapato ya wafanyakazi wa uma na pia kuhamishia fedha za posho kwenye programs za maendeleo.Bado hatuna bunge lenye uzalendo(speaking of majority)!Wanaendeshwa kwa visasi na kukomoa.Shame on them!!
 
Aliziwacha? Tunajuwa Zitto ndio kagoma kuzichukuwa.

usiseme aliziacha bali je Ameziacha? maana ninachoamini mpaka sasa analipwa kwani si lazima ziwe za bungeni inawezekana kwa chama kama katibu. si azikatae hizo? swala la posho linatia doa kubwa sana kwani tunalazimaika kukopa nje ya nchi hata kwa miradi ambayo tyngekuwa na uwezo wetu wa kufanya kwa pato la ndani lakini budget inagoma posho ni nyingi mno wataalamu wanadai ni zaidi ya 50% ya mishahara ya watumishi hulipwa kama malipo ya posho hizo.
 
Back
Top Bottom