Ki-Moon ampongeza JK

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amempongeza Rais Jakaya Kikwete, kwa kuchaguliwa kuongoza Umoja wa Afrika (AU) katika kipindi cha mwaka mmoja.

Pongezi hizo alizitoa juzi usiku alipokutana naye katika Hoteli ya Sheraton ambako wamefikia wakuu wa nchi na viongozi wa kimataifa wanaohudhuria mkutano wa AU.

Ki-Moon alisema kwamba amefarijika kwa Kikwete kuchaguliwa kuwa kiongozi wa Afrika na kumuahidi kwamba atashirikiana naye.

Ki-moon alisema amekuwa akifanya kazi na Kikwete tangu akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania na kwamba, kuchaguliwa kwake katika wadhifa huo kutafanya waweze kushirikiana kukabiliana na changamoto zinazolikumba Bara la Afrika.

Katibu huyo alimuomba Kikwete kufanya mazungumzo na Rais Kibaki ili kumaliza mgogoro unaoikumba nchi hiyo.

Vilevile, Ki-Moon alimsifu Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk Rose Migiro kwa utendaji wake mzuri na kwamba ni mtu muhimu katika uendeshaji wa UN.

Kwa upande wake, Rais Kikwete alimhakikishia Ki-Moon kwamba atafanya mazungumzo na Rais Kibaki ili kuondoa hali iliyoko sasa nchini Kenya.

Alisema kazi yake ya kwanza kama Mkuu wa AU, atatuma ujumbe katika nchi zote zenye migogoro ambazo ni Chad, Comoro, Sudan na Kenya ili kupata picha halisi.

Katika hatua nyingine, Rais Kibaki akihutubia wakuu wa Nchi za
Ushirikiano wa Kimaendeleo Kaskazini mwa Afrika, alisema katika nchi yake hakuna tatizo la usalama.

Wakati Rais Kibaki akisema hayo bado hali katika nchi hiyo ni mbaya na kwamba jambo ambalo linamsumbua ni jinsi ya kuhakikisha kuwa watu waliopoteza makazi yao wanapata mengine
 
Kuna mahali nimesoma kwamba JK kawatuma watu kwenda kuangalia aina ya magomvi ya Sudan, Chad nk including Kenya . Hivi JK yuko Africa na anaenda AU kukutana na hawa watu kila siku ina maana hajui matatizo haya leo ndiyo anataka kuanza kujifunza ? Hata hand over notes pia hazitakiwa zinasema lolote ? Mbona JK anaanza usanii mapema ?
 
Back
Top Bottom