Khitma ya Prof Haroub Othman kesho inshaalah

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Kwa manoswali mjini nadhani msikiti wa Ngazija mnaujua na nadhani ndio wepesi wenu huo kule Maamur ni upanga si mbali sana na Diamond Jubilee au tuseme si mbali sana na tume ya mawasiliano


Khitma mbili kumuombea marehemu profesa haroub othman aliyefariki majuzi na kuzikwa huko zanzibar zitafanyika katika misikiti miwili tofauti jijini dar kesho alhamisi. Ndugu, jamaa na marafiki mnaalikwa kuhudhuria.




kwa mujibu wa mwana wa marehemu, tahir othman, hitma ya kwanza itafanyika kesho alhamisi saa kumi na moja jioni katika msikiti wa ngazija uliopo mtaa wa makjunganya katikati ya jiji la dar.




tahir amesema hitma ingine itafanyika hiyo hiyo kesho alhamisi baada ya sala ya i'sha (baada ya saa mbili usiku) katika msikiti wa masjid ma'amour uliopo upanga jijini dar.




familia ya marehemu profesa haroub othman inatoa shukrani nyingi sana kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa msaada mkubwa mliotoa wakati huu wa majonzi.




ni vigumu kumshukuru mmoja mmoja na si rahisi kufanya ama kusema lolote zaidi ya kumuomba mola awaongezee, maana yeye ndiye mpangaji wa yote.
 
Hatuna njia, ila kushukuru kudura za Mungu na kumsindikiza kwa dua zetu njema. Hakika kama ilivyoagizwa, mtu mwema husindikizwa na mema yake aliyoyaacha duniani. Mwenyezi Mungu ndiye msiri wa yote, lakini kwa yale tuliyobahatika kuyaona, Prof Haroub ameacha hazina kubwa duniani ambayo thawabu zake zitaendelea kumwendea huko aliko milele na milele. Ameacha elimu, ameacha hekima, ameacha watoto wema na ameshiriki mambo mengi mema wakati wote kwa nafasi yake na kwa kujitolea mno.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom