Khaaa! wauzza madawa waanikwa?

LOOOK

JF-Expert Member
May 17, 2011
3,389
672
Mchungaji wa Kanisa la Full Salvation, Christopher Mtikilla ‘ameifungukia’ kauli ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa, baadhi ya viongozi wa dini nchini wanajihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya, Ijumaa Wikienda linashuka naye.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Ijumaa iliyopita, Mtikilla alisema tamko la JK ni la kweli kwa vile wapo baadhi ya viongozi wa dini wasiofuata maadili ya kazi yao na kufanya biashara hiyo. Akaongeza kuwa, yeye anamjua mmoja (jina tunalo)
MamaLwacrop.jpg
“Rais alisema kweli, wala wasipinge. Kama kuna kiongozi yeye hafanyi biashara hii, ajue kuna wenzake wanafanya,” alisema kwa kujiamini Mtikilla.

Aidha, Mtikilla ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha DP, alimtaja mchungaji mmoja wa kanisa la kiroho la jijini Dar es Salaam ambaye ana waumini wengi kuwa, na yeye anafanya biashara hiyo na watu wengi wanajua.

“Mfano…(akamtaja jina) yule ni mfanyabiashara wa haya madawa, nani asiyejua bwana. Huyu na wenzake wengi ndiyo siri nzito ya kuwa matajiri wakubwa kwa sababu ya fedha haramu
. imgres.jpg
Pia, alisema kuwa, mchungaji huyo alidakwa na madawa miaka ya karibuni, baadhi ya viongozi hao wa dini walisikia, lakini akahoji, “ni kwa nini hawakutoa tamko?”
Mchungaji Mtikilla aliongeza kuwa, haoni sababu ya viongozi wa Baraza la Maaskofu Tanzania kumkomalia JK kuweka hadharani majina ya viongozi wa dini wanaojihusisha na madawa ya kulevya.

Akahoji: “Mbona kuna maovu mengi yanayofanywa na viongozi wa dini ikiwemo ubakaji, ulawiti, utapeli na ushirikina lakini baraza halitoi tamko lolote?

“Kila mmoja ana mapungufu yake, serikali kuna mahali inakosea kwa sababu suala hili siyo la kulizungumzia kwenye majukwaa bali kama wapo wanaotuhumiwa, wakamatwe na uchunguzi wa kina ufanyike ili sheria ichukue mkondo wake
Archbishop-Dr-Valentino-Mokiwa.jpg
“Pia viongozi wa dini wanakosea sana kutoa tamko dhidi ya rais. Hakuna sehemu ambapo maandiko matakatifu yanawataka kutumia jazba kukabili changamoto wanazokutana nazo.
“Kama kiongozi hafanyi haya, ajue kuna wenzake wanajihusisha na michezo isiyofaa, ikiwemo hili la biashara ya madawa ya kulevya. Tuache kuteteana na kujificha nyuma ya mwavuli wa dini. Siku hizi wengi hawaaminiki, wanajali fedha kuliko huduma ya kuchunga kondoo wa Bwana,” alisema Mtikila.

Wiki mbili zilizopita, katika hafla ya kumsimika Askofu John Ndimbo wa Kanisa Katoliki, Mbinga, Ruvuma, Rais Jakaya Kikwete alisema kuna baadhi ya wachungaji wanaojishughulisha na biashara ya madawa ya kulevya.
Alisema watumishi hao wa Mungu wamekuwa wakitumia nafasi zao kwenye paspoti kuingiza au kutoa madawa ya kulevya.

Ndipo maaskofu wanaounda Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) walipokutana Juni Mosi, mwaka huu mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti, Mchungaji Peter Kitula na kumpa saa 48 Rais Jakaya Kikwete kuwataja kwa majina viongozi aliodai wanafanya biashara hiyo haramu.

Viongozi wengine wa dini wanaounda jumuiya hiyo ni Askofu Valentino Mokiwa (Anglikana, pia ni Kaimu Mwenyekiti), Alex Malasusa (KKKT) na Moses Kulola (EAGT).
Wengine ni maaskofu kutoka makanisa ya Moravian, African Inland, Baptist Tanzania, African Brotherhood, Church of God na Kanisa la BibliaMakanisa mengine yaliyopo kwenye Jumuiya hiyo ni Mbalizi Evangelist, Mennonite, Presbyterian, Salvation Army na Tanzania Yearly Meeting.
Miaka ya karibuni, kumekuwa na baadhi ya wachungaji wa kiroho wanaolalamikiwa na baadhi ya waumini wao kwa kuwa na utajiri mkubwa.

Waumini hao wamekuwa wakiwatuhumu wachunga kondoo wao kuwa, wanamiliki mamilioni ya fedha, magari ya kifahari, nyumba za kisasa huku wao, wakiwa kama kondoo, wanaishi maisha ya ufukara wa kutupwa.

Hata hivyo, uchunguzi wa kina wa gazeti hili umebaini kuwa, baadhi ya wachungaji nchini, wanashindana kumiliki magari ya bei mbaya huku baadhi ya kondoo wao wakishindwa kulipia kodi ya chumba cha shilingi elfu thelathini (30,000/=) kwa mwezi

H A HA HA ETI JINA TUNALO ALAFU PCHA CHINI HUYOMWANDISHI BONGE LA MJANJA HAWEKI JINA HALAFU ANAWEKA PICHA DUUU!! HATA MIE NAWASIWASI BORA NIHAMIE DINI YA WAPAGAN.
 
Unamaanisha nini kutoa picha hizo.
Look angalia! unaushaidi?
 
H A HA HA ETI JINA TUNALO ALAFU PCHA CHINI HUYOMWANDISHI BONGE LA MJANJA HAWEKI JINA HALAFU ANAWEKA PICHA DUUU!! HATA MIE NAWASIWASI BORA NIHAMIE DINI YA WAPAGAN.
Kwani wewe unafata maandiko au unafata viongozi wa dini...
 
Kwani wewe unafata maandiko au unafata viongozi wa dini...

Mkuu imani haiendi bila matendo,
Yesu alisimama na kuwaambia kwa mtu yoyote amshuhudie kuwa ana dhambi na kulikuwa hakuna mtu wa kushuhudia hilo, alikuwa anafundisha imani na anaonyesha matendo,

Kama hao wachungaji wapo basi wanafundisha injili mfu, injili ambayo haipo, Pepo hawezi kumfitini pepo mwenzie, Kama Askofu anauza madawa ya kulevya kamwe hawezi kukemea ulevi, uzinzi, na vitu kama hivyo kwa sababu atakuwa anawakana pepo wenzie (mwenye masikio na asikie, naongea kwenye hali ya juu kabisa ya kiroho)
 
"Pia viongozi wa dini wanakosea sana kutoa tamko dhidi ya rais. Hakuna sehemu ambapo maandiko matakatifu yanawataka kutumia jazba kukabili changamoto wanazokutana nazo"

siamini kuwa kauli hii imetoka kwa Mtikila, kweli kuna mageuko
 
Wakuu huko simo kabisa.... kama president mwenyewe kaishia kumumunya maneno kwa kushindwa kuwataja wahusika, mimi nitatoa wapi jeuri ya kuchangia hapa?
 
"Pia viongozi wa dini wanakosea sana kutoa tamko dhidi ya rais. Hakuna sehemu ambapo maandiko matakatifu yanawataka kutumia jazba kukabili changamoto wanazokutana nazo"siamini kuwa kauli hii imetoka kwa Mtikila, kweli kuna mageuko
.Luke:13:32 'Akawaambia, nendeni mkwamwambie yule MBWEHA, nipo leo na kesho nikitoa pepo na kuwaponya wagonjwa, na siku ya tatu, nitakamilishwa'.
 
Mara nyingi huyu Mtikila anatumika kama microphone ya watu. Ni mvurugaji mzuri wa hoja. Hata hivyo nitamkumbuka kwa suala la mgombea binafsi.
 
Mtikila anatumika kama buffering agent, anajua kudance na beat vizuri.
 
Mara nyingi huyu Mtikila anatumika kama microphone ya watu. Ni mvurugaji mzuri wa hoja. Hata hivyo nitamkumbuka kwa suala la mgombea binafsi.
mimi nitamkumbuka kwa kumwita rostam fisadi mchana halafu usiku anaenda kumwomba hela,..that's all
 
Mchungaji wa Kanisa la Full Salvation, Christopher Mtikilla ‘ameifungukia' kauli ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa, baadhi ya viongozi wa dini nchini wanajihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya, Ijumaa Wikienda linashuka naye.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Ijumaa iliyopita, Mtikilla alisema tamko la JK ni la kweli kwa vile wapo baadhi ya viongozi wa dini wasiofuata maadili ya kazi yao na kufanya biashara hiyo. Akaongeza kuwa, yeye anamjua mmoja (jina tunalo)
View attachment 32393
"Rais alisema kweli, wala wasipinge. Kama kuna kiongozi yeye hafanyi biashara hii, ajue kuna wenzake wanafanya," alisema kwa kujiamini Mtikilla.

Aidha, Mtikilla ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha DP, alimtaja mchungaji mmoja wa kanisa la kiroho la jijini Dar es Salaam ambaye ana waumini wengi kuwa, na yeye anafanya biashara hiyo na watu wengi wanajua.

"Mfano…(akamtaja jina) yule ni mfanyabiashara wa haya madawa, nani asiyejua bwana. Huyu na wenzake wengi ndiyo siri nzito ya kuwa matajiri wakubwa kwa sababu ya fedha haramu
.View attachment 32394
Pia, alisema kuwa, mchungaji huyo alidakwa na madawa miaka ya karibuni, baadhi ya viongozi hao wa dini walisikia, lakini akahoji, "ni kwa nini hawakutoa tamko?"
Mchungaji Mtikilla aliongeza kuwa, haoni sababu ya viongozi wa Baraza la Maaskofu Tanzania kumkomalia JK kuweka hadharani majina ya viongozi wa dini wanaojihusisha na madawa ya kulevya.

Akahoji: "Mbona kuna maovu mengi yanayofanywa na viongozi wa dini ikiwemo ubakaji, ulawiti, utapeli na ushirikina lakini baraza halitoi tamko lolote?

"Kila mmoja ana mapungufu yake, serikali kuna mahali inakosea kwa sababu suala hili siyo la kulizungumzia kwenye majukwaa bali kama wapo wanaotuhumiwa, wakamatwe na uchunguzi wa kina ufanyike ili sheria ichukue mkondo wake
View attachment 32396
"Pia viongozi wa dini wanakosea sana kutoa tamko dhidi ya rais. Hakuna sehemu ambapo maandiko matakatifu yanawataka kutumia jazba kukabili changamoto wanazokutana nazo.
"Kama kiongozi hafanyi haya, ajue kuna wenzake wanajihusisha na michezo isiyofaa, ikiwemo hili la biashara ya madawa ya kulevya. Tuache kuteteana na kujificha nyuma ya mwavuli wa dini. Siku hizi wengi hawaaminiki, wanajali fedha kuliko huduma ya kuchunga kondoo wa Bwana," alisema Mtikila.

Wiki mbili zilizopita, katika hafla ya kumsimika Askofu John Ndimbo wa Kanisa Katoliki, Mbinga, Ruvuma, Rais Jakaya Kikwete alisema kuna baadhi ya wachungaji wanaojishughulisha na biashara ya madawa ya kulevya.
Alisema watumishi hao wa Mungu wamekuwa wakitumia nafasi zao kwenye paspoti kuingiza au kutoa madawa ya kulevya.

Ndipo maaskofu wanaounda Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) walipokutana Juni Mosi, mwaka huu mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti, Mchungaji Peter Kitula na kumpa saa 48 Rais Jakaya Kikwete kuwataja kwa majina viongozi aliodai wanafanya biashara hiyo haramu.

Viongozi wengine wa dini wanaounda jumuiya hiyo ni Askofu Valentino Mokiwa (Anglikana, pia ni Kaimu Mwenyekiti), Alex Malasusa (KKKT) na Moses Kulola (EAGT).
Wengine ni maaskofu kutoka makanisa ya Moravian, African Inland, Baptist Tanzania, African Brotherhood, Church of God na Kanisa la BibliaMakanisa mengine yaliyopo kwenye Jumuiya hiyo ni Mbalizi Evangelist, Mennonite, Presbyterian, Salvation Army na Tanzania Yearly Meeting.
Miaka ya karibuni, kumekuwa na baadhi ya wachungaji wa kiroho wanaolalamikiwa na baadhi ya waumini wao kwa kuwa na utajiri mkubwa.

Waumini hao wamekuwa wakiwatuhumu wachunga kondoo wao kuwa, wanamiliki mamilioni ya fedha, magari ya kifahari, nyumba za kisasa huku wao, wakiwa kama kondoo, wanaishi maisha ya ufukara wa kutupwa.

Hata hivyo, uchunguzi wa kina wa gazeti hili umebaini kuwa, baadhi ya wachungaji nchini, wanashindana kumiliki magari ya bei mbaya huku baadhi ya kondoo wao wakishindwa kulipia kodi ya chumba cha shilingi elfu thelathini (30,000/=) kwa mwezi

H A HA HA ETI JINA TUNALO ALAFU PCHA CHINI HUYOMWANDISHI BONGE LA MJANJA HAWEKI JINA HALAFU ANAWEKA PICHA DUUU!! HATA MIE NAWASIWASI BORA NIHAMIE DINI YA WAPAGAN.

Mkuu
Ipo tofauti kati ya PCT na CCT, Askofu Moses Kulola na EAGT hawako CCT nachofahamu askofu Kulola na EAGT wako PCT ambayo ni Pentecostal Council of Tanzania na CCT ni Christian Council of Tanzania. Kwa hiyo inawezekana kuna maelezo mengi tu ambayo unaweza kuwa umeyapotosha.
 
source: gazeti la ijumaa weekenda! mods thread kama hizi naomba mzitrash, JF hatuwezi kuaccept source of information kutoka kwenye magazeti ya Shigongo huku ni kuivunjia heshima forum hii. au napendekeza thread hii hiamishiwe kwenye jukwaa la udaku.
 
Back
Top Bottom