Kha Kumbe JK yuko Sahihi!

Ushangiliaji wa waTanzania kwa Ivory Coast jana ni uthibitisho kamili kuwa waTanzania hawajali ushindi wa nchi bali mtu/watu. Wanaona kushangilia Drogba ni bora zaidi (kwa kuwa ni mchezani wa Chelsea) kuliko kuishangilia timu ya Taifa.

Nadhani JK alikwenda kuangalia hilo. Nina imani atakuwa ameogopa sana kuona hali hiyo. Maana kama wananchi wakiendelea hivyo, basi ina maana watachagua mtu kwenye uchaguzi ujao badala ya chama, na kwa popularity yake, atakuwa matatani (kura zitapungua sana). Ila sijui nani atakaekuwa mpinzani wake. Maana anaitajika Drogba kumng'oa.
 
Inasikitisha,!? Nilikuwa uwanjani ILIBOA sana, ingekua Yanga na Zamaleki tungesema walioshangilia ni mashabiki wa simba "UZALENDO UKO WAPI?"
 
Uzalendo ni kama mapenzi (kwa walio kwenye ndoa) ukiona mapenzi kwa mwenzio yanayumba, unachotakiwa ni kujiuliza kama unamtendea mwenzio mema kama ulivyoahidi siku ya ndoa. Ukiwa kweli unamtendea sahihi na kwa jitihada zako zote, basi nae atakutendea wema wa kukupenda vilevile kama sio zaidi.

Uzalendo hujengwa kwa muda mrefu unaotokana na imani kubwa wanayokuwa nayo wananchi kwa jinsi nchi yao inavyowajali, walinda na kuwatetea maslahi yao na ya familia zao kwa usawa, haki na utaratibu unaoeleweka/unaotegemewa kutoka kwa wenye mamlaka.

Tusipoweza kufikia kutimiza hayo kwa watu wote (au asilimia kubwa), basi Uzalendo utakuwa mbali na jamii zetu, na mara zote watu wetu watajivunia mafanikio na ustaarabu wa wengine.
 
Ushangiliaji wa waTanzania kwa Ivory Coast jana ni uthibitisho kamili kuwa waTanzania hawajali ushindi wa nchi bali mtu/watu. Wanaona kushangilia Drogba ni bora zaidi (kwa kuwa ni mchezani wa Chelsea) kuliko kuishangilia timu ya Taifa.

Nadhani JK alikwenda kuangalia hilo. Nina imani atakuwa ameogopa sana kuona hali hiyo. Maana kama wananchi wakiendelea hivyo, basi ina maana watachagua mtu kwenye uchaguzi ujao badala ya chama, na kwa popularity yake, atakuwa matatani (kura zitapungua sana). Ila sijui nani atakaekuwa mpinzani wake. Maana anaitajika Drogba kumng'oa.

Watanzania amuwajui si ni majuzi tu hapa nakumbuka Edibile Lunyamila akienda kwao Shinyanga mzee Lunyamila alikua anamfungia ndani kumuona T.Sh 50 na watu wanapanga mstari mrefu.

Hata huku tulipo dada ukimwambia nakupeleka Nando's duu ujue hiyo ni moja ya zile safari chache ambazo utamkuta tayari keshajitayarisha ukipiga horne tu mbio nje.
 
Wakuu tulipofungwa uwanja wote ulikuwa kimya. Tulipocheza vizuri tulishangalia. Drogba alizomewa. Mara he Drogba na wenzake wakaanza kushangiliwa. Mwishoni kabisa ndio kidogo tukawashangilia vijana wetu. Yaani tulikuwa hatueleweki kabisa!

hahahah hii kali
 
Watanzania amuwajui si ni majuzi tu hapa nakumbuka Edibile Lunyamila akienda kwao Shinyanga mzee Lunyamila alikua anamfungia ndani kumuona T.Sh 50 na watu wanapanga mstari mrefu.

Hata huku tulipo dada ukimwambia nakupeleka Nando's duu ujue hiyo ni moja ya zile safari chache ambazo utamkuta tayari keshajitayarisha ukipiga horne tu mbio nje.

hahaha JC ya kweli haya
 
Hawa ndo wapiga kura.............wooooooote wamefanana na Kafulila?....hawa wooote ndo 70%.

U cant trust mpiga kura wa bongo. kama vile hatuna mtima!! aagggggrrrrrr.
 
kuna mibongo myengine hata mazikoni kwa kawawa haikuenda eti inasevu mipesa ikamuone drogba! aaarghhh! acha nilog auti kidogo kupunguza jazba!!!! inauzi
 
Ndio! Mechi ya jana kati ya Taifa Stars na Ivory Coast imedhihirisha hilo!Hakika 70% ya Watanzania ni 'Bendera Fuata Upepo! Habari ndio Hiyo!

haukujua bado, umeona hata JF baadhi ya watu wanavyochangia maada?? somepeople they just can't stand alone!
 
.
Compa, Watanzania ni malimbukeni, hili ndio unalijua leo?. Baada ya uchaguzi mdogo Busanda na Biharamulo, nililisema, na nilishutumiwa kutukana watu bure!. Jana uwanja ulifurika, na kila tukipigwa chenga, uwanja unashangilia, tulipopigwa bao ndio kabisaaa. Hawa ndio sisi Watanzania na nchi yetu!.

- He! he! he! adabu adabu wakuu vipi jamani hebu for once muwaonee huruma wa-Tanzania japo kidogo, I mean what is the problem hapo? Wapenzi wa mpira wameenda uwanjani na kujionea kabumbu ya kweli ikiporomoshwa na wanaoijua vizuri na kuweza kutenganisha pumba na mchele ulipo, sasa mlitaka wafanye nini?

- Washangilie pumba na huku wanauona mchele? ahhgaggrrr! you wonder who is a really limbukeni here!

Respect

FMEs!
 
hiyo hata ulaya ipo wala siyo issue sana hata hivyo watu wenyewe unaowasema ni maskini hata uwezo wa mlo mmoja ni matatizo.
 
Ndio! Mechi ya jana kati ya Taifa Stars na Ivory Coast imedhihirisha hilo!Hakika 70% ya Watanzania ni 'Bendera Fuata Upepo! Habari ndio Hiyo!

tena bora watanzania....je wakenya si hata uwanjani wasingeenda?? Big up watanzania kwa na kwa uzalendo na pia hata timu pinzani pale inapoonyesha mpira safi kama wewe ni mpenzi wa mpira utashangilia tu. mbona wewe mwenyewe unashangilia mitimu ya uingereza??
 
labda walikuwa washabiki wa Chelsea na Arsenal.. na walikuwa wanawashangilia wachezaji wao wanaocheza Ulaya... au ni wale wenye hasira na Maximo na sasa wameamua kuasi cham..just guessing
 
Kuyumbayumba kule ni kielelezo cha ukosefu wa msimamo/mwelekeo wa wananchi na nchi!
 
Kuyumbayumba kule ni kielelezo cha ukosefu wa msimamo/mwelekeo wa wananchi na nchi!

Mkuu huoni kuwa angalau hapo kwenye mpira wa-TZ wanaonyesha msimamo uliokomaa zaidi kwa kushangilia gemu safi tu (hata kama si la upande wao) tofauti na uzalendo wa kinafiki wanaouonyesha katika siasa kwa kuchagua na kupigia makofi uozo miaka nenda miaka rudi.
 
Watanzania wana maajabu . Watanzania hawana wanalo liamini ila wana amnishwa na kufuata mkumbo ndiyo zao . Watanzania hawana muda wa kujiuliza kabla hawajaamua .Mambo haya wanayo kuanzia mpirani hadi maisha yao ya kila siku .
 
Bora tulifungwa maana pesa za walipa kodi zimepona kwani tungeshinda wachezaji na kocha wangeandaliwa ziara ya nchi nzima kwenda kuonyesha timu iliyoifunga IVORY.

Na pia huenda hata Bunge lingesimama kuwashangilia , Rais angeandaa sherehe Ikulu ya pongezi N.k.

Hizo pesa zipelekwe kutafuta maji vijijini kwani watu wetu wanaisha kwa kipindupindu.
 
Ungekuwa uwanjani ungeelewa mkuu, kwa asilimia kubwa Watanzania hawana msimamo!
Kwani kabla ya mechi ni nani aliyekuambia anaenda kuishangilia timu moja tu? Maybe waliofanya hivyo huo ndio msimamo wao, na huwezi ukasema hawakuwa na msimamo wakati msimamo wao ulionekana dhahiri. Au unadefine vipi msimamo?
 
Kuwa na msimamo ni kuyumbayumba/kutositasita katika pande mbili!
 
Back
Top Bottom