Kesi

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
Last week niliitwa kwenye kikao cha kesi ya kifamilia.
Mimi nikiwa mmoja wa viongozi wa serikali ya mtaa nilikuwepo kikaoni kwa nafasi yangu.
Shtaka lilikua baina ya Mke na Mume, ambapo mke ndiyo alikua mlalamikaji, majadiliano yalikua hivi :
> Mke :- Wazee hapa mimi namlalamikia Mume wangu tatizo ni kwamba hataki kujishughulisha mfano hapa tunapoishi hii nyumba tumepewa na Baba yangu mimi hivyo anaishi ukweni, Shamba tunalolima ametupa Mama yangu, Ng'ombe tulizonazo tumepewa na Mjomba wangu, yaani huyu mume wangu yeye hana anachokifanya humu ndani, yeye ni kula kulala.
Hata pesa za chakula hapa hom nimimi ndiyo nahudumia kutokana na biashara zangu ndogondogo.
IKAFIKA mw/kiti wa kikao kumpa muda Mume nae aseme yake.
> MUME :- Wazee nadhani mmemsikia Mke wangu, lakini pamoja na yote na mimi nina malalamiko yangu kwamba ni kweli vitu vyote alivyovisema tumepewa na wakwe zangu ni kweli, hata hivyo bado mimi namlalamikia Kaka yake ambae ni Shemeji yangu yeye ana magari matatu ameshindwa hata kutuletea gari moja! . Yaani ana roho mbaya sana, mnafikiri sisi tutakaa mpaka lini bila gari ? .
 
Hahahahahaaaa jamaaa ye anachoangalia maisha mazuri, hajali kitu kingine wala nini
safi sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom