Kesi za ufisadi ziwekewe muda wa kukamilishwa kama za Wabunge?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
a. Kutalazimisha uchunguzi kukamilika mapema
b. Kutaondoa wingu la tuhuma dhidi ya watu
c. Kutapunguza gharama za kuendesha kesi kwa miaka mingi
d. Watu wafikishwe mahakamani wakati uchunguzi/upepelezi umeshakamilika - kama haujakamilika wanafikishwa mahakamani kwanini?
e. Kuhakikisha kesi zinaisha haraka na kwa ufanisi kunatoa mwanya wa kuwashughulikia watu wengi zaidi katika muda mfupi
f. Kama kesi za Wabunge zinaweza kupangiwa majaji na kusikilizwa mfululizo hadi kutolewa hukumu kesi za ufisadi zingefayiwa kazi kama inavyotaka sheria ya Uhujumu Uchumi ambapo mahakama maalum inakaa.

Kwa ufupi haiwezekani na haipaswi kesi hizi kuendelea kuwa zinasikilizwa miaka mitano au sita na hapo ni kabla ya rufaa! Ucheleweshaji wa kesi hizi ni mbinu ya kuchelewesha haki na kuwajibishana.
 
naongezea zaidi, kwenye katiba mpya kuwepo na kipengele cha ku'review rufaa zote wakati wa utawala mpya.
 
Good idea lkn watunga sheria wakupiga madeski si ndio hao mafisadi wenyewe so wanaweza kweli wakagonga madesk kupitisha hyo kitu?
 
Kwa kuwa kesi zenyewe pia ni kiini macho ndio maana hukumu pia inachelewesha. Watuhumiwa walifunguliwa kesi ili kuwaridhisha wananchi ili muone serikali yenu ni makini. Kesi hazikufunguliwa ili haki itendeke.

Nadhan wanataka zisikilizwe tu hadi watuhumiwa wafe ndio hukumu itatolewa
 
Mwanakijiji,

Kwahiyo wewe unatetea mafisadi wapate special prievilege kwa ku fast track kesi zao wakati mpwa wangu Saidi Ubaya na kesi yake ya kuiba Gagulo la mama Pili pale Buguruni kwa Mnyamani anasota Lupango mwaka wa pili sasa ushahidi haujakamilika. Mimi nadhani kama tunazungumzia haya maswala tusisitizie tu kesi siende haraka zote tu kwa sababu wanasema wenyewe " Justice delayed is justice denied".
 
  • Thanks
Reactions: tz1
Mkuu inahitajika kwa mashauri yote yaliyopo mahakamani na si EPA tu, Mkapa alishawahi kusema..."MAHAKAMA ZETU NI WEZI WA MUDA.."
 
Utawala mpya upi zumbemkuu ? Naona tukipata katiba mpya basi kutakuwa hakuna sheria zingine. Hiyo Katiba inaweza kuwa kubwa kweli kweli!
mkuu Kimbunga katiba tutakayoipata chini ya utawala wa CCM hakika haitakidhi matakwa ya wananchi, lazima tupate katiba mpya ya kweli chini ya utawala mpya, sio kutoka kwa JK, ndo maana nashauri kiwepo kiraka cha ku'review rufaa zote za kesi ili kubaini zile hukumu za kifisadi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom