Kesi za uchaguzi siyo za mchezo mchezo

kalistibukhay

Member
Dec 15, 2011
10
3
Makosa makubwa kutengua matokeo ya Ubunge kwa ushahidi wa kusikia-Jaji Moses

Jaji Moses Mzuna aliyetupilia mbali kesi dhidi ya mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amesema ni makosa makubwa kwa mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi kwa ushahidi wa kusikia.Jaji huyo amesema ili kutengua matokeo ni lazima kuwe na ushahidi ulio wazi tena wa vielelezo visivyotia shaka.Jaji huyo ameendelea kusema ni kosa kubwa kumuondoa kiongozi wa wananchi kwa ushahidi wa hovyo hovyo.
Jaji huyo pia amesema wanaofungua kesi za uchaguzi wanapaswa kujua kesi za kupinga matokeo si za mchezo mchezo.Amesema kwa njia hii ndipo mahakama zetu zitakapoheshimika.
 
Mods unganisha hii thread na ile nyingine

mods msiunganishe, kuna points zimesimama, ni nzuri kuzijadili.
huwezi chezea maamuzi ya watu kwa ku consider ushahidi wa hovyo hovyo. hongera jaji Mzuna.
 
Back
Top Bottom