kesi za ndoa. slaa, Geofrey Mungai na Piuse Msekwa-light tourch

Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
825
najua kuna mjadala unaondelea katika thread ingine lakini hapa naomba niweke angalau mwanga kidogo kuhusu kesi zinzosahibiana na hii ya Dr. slaa ili mnapojadili mpate mwanga. si vema kuitazama kesi ya DR. slaa kisiasa ila kibinadamu kwa kuwa wao ni binadamu na ndo maana kanisa hasa katoliki limeweka sheria mbalimbali ili kurahisisha majibu kwa maswali mazito

1.. kesi ya kwanza ni ya sipka mstaafu piuse msekwa, kwenye miaka 70, huyu aliomba kanisa limruhusu kutoa talaka kwa mke wake wa kwanza na aruhusiwe kumwaoa Mkewe wa Sasa Ana Abdallah, kanisa lilifanya uchunguzi kwa muda mrefu na kwa bahati mbaya kanisa katoliki la Tanzania, lilielekea kuridhia talaka hiyo, siki chache kabla ndoa haijafungwa makao makuu ya kanisa katoliki yalikataza ndoa hiyo kufungwa KWA KUWA PIUSI MSEKWA ALIKUWA NA NDOA HALALI ILIYOFUNGWA KANISANI, NA KUWA NDOA ILE ISINGEWEZA KUVUNJWA KIRAHISI , MPAKA LEO PIUSI MSEKWA NA MAMMA ANA ABDALLAH WANAISHI KAMA VIMADA

2. Geofrey Mungai yeye aliishi na mwananmke kwa muda wa miaka 11, walijaliwa kuwa na watoto wawili lakini hawakuwa wamefunga ndoa, mnamo 2009 geofrey aliomba kufunga ndo na mchumba mpya waliyekutana huko iringa, yule mama alipeleka zuio kanisani na kwa vyombo vingine, lakini kanisa lilitupilia mbali zuio lile na kumruhusu geofrey mungai kufunga ndoa kanisani. SABABU: kuishi kama mke na mme kwa miaka 11 hakuimanishi kuwa kulikuwa na ndoa bali walikuwa wazinzi, na hakuna dhambi isiyosameheka.

3. kesi ya slaa inasahibiana sana na ya Mungai, ni kweli yeye na kamili waliishi pamoja kwa miaka 25, lakini kwa miaka 25 hawakufunga ndoa, sababu za kutofunga ndoa anazo yeye na kamili, kwamba 2009 mmoja wao ameamua kufunga ndoa na mushumbushi ni wazi kuwa zile sababu za kutoweza kuweka nadhiri hizo za milele zilikuwa na nguvu, kwamba walikaa kwa pamoja miaka 25 kama mke na mimi haijalishi, kanisa haliweza kuhalalisha uzinzi.hivyo nina uhakika slaa 100% atakubaliwa na kanisa kufunga hiyo ndoa. ni status ya josephine mshumbushi pekee itakwamisha hiyo ndoa, kwamba josephine alikuwa na ndoa nyingine kupitia KKKt kwa kweli hilo ni tatizo, labda KKT wamsamfishe na kukubali kutalikiwa kwa mama mshumbushi na mumewe wa kwanza.

nionanyo mimi, si vema kuweka hili swala kwenye mambo ya siasa, kote ccm na chadema kuna matatizo kama haya, kuna watu hawana mke kabisa, kuna wengine wanaishi na vimada nk, ni vema basi wakaachwa kushughulikia matatizo haya, na vyombo vya habari msikuze mno jambo hili. kwa kuwa sasa tunaelekea kwen ye mchakacho wa katiba mpya, kama tunataka mabadiliko basi hili nalo linaweza kuingizwa.
 
With all fairness,Dr kama kweli Josrphine ni mke wa ndoa wa mtu mwinginme,haijalishia wanapendana kiasi gani,kimaadili na kimaandikosi sahihi,yeye alikuwa padri anaelewa sana maandiko yanakataza kumuacha mke wa ujanani na pia biblia inakataza kuchukua mke wa mtu na mtu hana ruhusa kumwacha mkewe ispokuwa kwa dhambi ya uzinzi.Katika hili
Wafuatao ni wazinzi kwa mujibu wa biblia
1.Dr Slaa mwenyewe
2.Josephine
Rose kamili nae kama ana bwana kwa sasa ni mzinzi pia na huyo mume wa Josephine.
Maoni yangu Dr.Atubu arudi kwa mke wa ujanani,Josephine nae arudi kwa mumewe,ni tamaa tu zinawasumbua na zimedhaa dhambi ambayo itazaa mauti.
Kama kioo cha jamii amalize sual hili kwa kuzingatia Imani yake (ya kikristo) La sivyo dhambi hii itatafuna hadi wajukuu.
Maoni tu haya wadau nisipelekwe mabwepande please!
 
Kwa mjibu wa kanisa katoliki la ROMA, Mhe. Slaa hawezi kufunga ndoa ataishi tu na mwanamke na anaweza kuzaa nae watoto , kwa hiyo hata huyo Rose Kamili aliishi nae tu hakufunga nae ndoa takatifu. Kanisa katoriki linasema hivi, sacramenti ziko saba:-

  1. Ubatizo
  2. Kipaimala
  3. Kitubio
  4. Upadri
  5. Mpako wa mwisho
  6. Ekarist takatifu
  7. NDOA

Sasa kwa kua Mhe Slaa aliisha pata sacrament ya upadri basi NDOA kwake siyo halali, Ndoa yoyote kwa Mhe Slaa SIYO HALALI…… Labda ndoa anayodai Mhe. Rose Kamili ni ya serikali.Ndoa ya serikali mimi siwezi kuisemea au ndoa ile ya kuishi zaidi ya miezi sita nayo mimi siwezi kuisemea.

Nasisitiza ndoa yoyote kwa padri SLAA na ambae aliwahi kuwa katibu wa TEC siyooo halaliiiiiii
 
Nijuavyo mimi Makanisa ni mawakala wa serekali wa kufungisha ndoa, ndiyo maana hati za ndoa hutolewa na serekali na huandikwa "jamuhuri ya muungano wa tanzania hati ya ndoa" hivyo ndoa zote hutolewa kibali na serekali nayo huwapa mamlaka kama makanisa uwakala tu wakufungisha ndoa.

Ikiwa Dr. Slaa ameamuakufunga ndoa kupitia serekali moja kwa moja na baada ya tangazo la ndoa kubandikwa kwenye ubao wa manispaa atakayofungia ndoa na zikiwa zimepita siku 21 za pingamizi hakuna pingamizi basi Dr.Slaa atakuwa huru lakini kama kunapingamizi basi litasikilizwa liangaliwe kama limekizi vigezo kama limekizi ndoa haitafugwa.
 
Tatizo huyo mchumba wake ana ndoa halali ambayo haijavunjwa. Tusiangalie upande wa dk. Slaa tu
 
Back
Top Bottom