Kesi ya wapinzani kuhusu uchaguzi yapigwa mweleka mahakamani

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,276
125
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi ya vyama vinne vya upinzani kupinga uchaguzi mdogo wa madiwani unaotarajiwa kufanyika kesho.


Badala yake, mahakama imesema uchaguzi uendelee kama kama ulivyokuwa umepangwa.


Uamuzi huo ulitolewa jana baada ya mahakama hiyo kumaliza kusikiliza hoja za wakili wa upinzani, Mpare Mpoki na mawakili watatu wa serikali, Joseph Ndunguru, Paul Ngwembe na Abraham Senguji.


Jaji Njengafibili Mwaikugile alisema mahakama imefikia uamuzi huo kwa sababu walalamikaji hawakupeleka ushahidi zaidi ya kuwasilisha idadi ya watu.


“Hakuna ushahidi unaoonyesha kwamba kundi hilo la watu 50,000 lipo, kundi hilo ni la kufikirika tu, wapo lakini hawapo,” alisema Jaji Mwaikugile.


Alisema kuna idadi nyingine ya wapigakura kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, wanaohitaji haki ya kupiga kura na mahakama ikisimamisha uchaguzi, itakuwa imewanyima haki yao ya msingi.


Baada ya kutolewa uamuzi huo, Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, alisema hawajaridhika na wataendelea kupigania haki zao za msingi.


Naye Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Haki za Binadamu, Salum Bimani alisema wataendelea na madai yao ya kutaka Katiba ibadilishwe kwa sababu madai yao ni ya msingi hayajafanyiwa kazi.


Awali, akiwasilisha hoja zake wakili Mpoki alisema, ombi la kutaka uchaguzi usimamishwe linatokana na kesi waliyofungua mahakamani hapo wakitaka watu 50,000 waandikishwe kabla ya kufanyika uchaguzi.


Wakiwasilisha hoja zao kwa zamu, mawakili wa serikali walisema tume ndio iliyopewa uwezo wa kuandaa uchaguzi na kuandikisha wapiga kura, zoezi la kuandikisha ni refu linachukua siku 120 na linahitaji kupitia hatua mbalimbali.


Katika ombi lao la msingi, vyama vya Chadema, TLP, NCCR-Mageuzi na CUF, vilikuwa vinataka mahakama kuzuia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuendelea na uchaguzi wa madiwani, utakaofanyika kesho.


Kuhusu ombi la msingi, Jaji Mwaikugile alisema kesi ya msingi ya iliyowasilishwa na walalamikaji ni kwamba, watu waongezwe katika dafutari la kudumu la wapiga kura ambalo alisema litasikilizwa Februari 15, mwakani. Kesi hiyo ilifunguliwa Oktoba 5, mwaka huu.

My take

Hakuna kuweka mpira kwapani mambo hadharani tuone sera za kuzomea zinavyo fanyakazi
 
chadema huwa hawana rekodi ya kushinda mahakamani
Funga domo. Ile kasi ya maandamano ualiyosababisha Aquilina kupigwa risasi na polisi na kufa iliishaje wewe? Walishindwa ktk mahakama ya Hakimu mkazi lakini serikali iliangukia pua mahakama kuu.
Unaongea usichojua.
 
Back
Top Bottom