Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Huyu jamaa katolewa kafara kama funzo kwa wengine. Hakuna aliye juu ya sheria. Jana nilifanikiwa kutembelea kituo kimoja cha polisi, na nikashuhudia jinsi gani hii kesi ya Zombe imewapa polisi utu na adabu. Polisi hawapigi tena watuhumiwa. Wanaogopa kufanywa kama Zombe.
 
Huyu mpuuzi kabisa ulokole haupate wapi, imefika zamu yake kulipa anaangaika tulia unyolewe kamaulivyowanyoa wengine na kuwafunga kwa kesi za kumbikiwa wakati hawana hatia, utakutana nao jela ndo ujue kuwa ulimwengu una sura mbili kama shilingi.

M/mungu siku hizi mkali sana naona kaamua kuacha kusubiri siku ya kiama kaamua kuwadhibu wakosaji hapahapa ulimwenguni.
 
Nilikuwa Post Office Moshi siku hiyo sitakaa nisahau.
Kuna mtu nilikuwa nimempa ride na mimi nilikuwa nimebaki kwenye gari nikimsubiri jamaa yangu huku nikila mziki laini ndani ya gari lenye namba za kigeni za SA.



Muziki ulipotoka Moshi ulihamia Tanga, Mavuno yakawa madogo bosi naye hakuridhika na uchaguzi ulikuwa karibu na umri wa kustaafu pia ulikuwa karibu, hivyo Bosi akaamua amsogeze kipenzi ili watengeneze fastafasta na kweli mambo ikawa kila siku majambazi yameuwawa na polisi. Bosi akastaafu lakini jamaa akasahau kuwa aliyekuwa anamkingia kifua hayuko tena madarakani, hayo ndio mazoea ya mafisadi wengi hujisahau kuangalia na kusoma alama za nyakati (Pole sana bwana Mushi, lakini pale Dar es salaam streat hukunywa bia zake wakati akimlambia alhaji wa visiwani?)
 
Niliposoma maelezo ya yule shahidi wa kwanza kwenye kesi ya Zombe basi nikajua kweli hawa jamaa nao walikuwa ni victims wa uhuni roho mbaya aliyokuwa nayo Zombe.

Kila kitu alichoelezea kilichowapata marehemu hao ni kama ambao yalishawahi kunipata mimi kwa amri za aina hiyo hiyo za Zombe.

Nilikuwa Post Office Moshi siku hiyo sitakaa nisahau.
Kuna mtu nilikuwa nimempa ride na mimi nilikuwa nimebaki kwenye gari nikimsubiri jamaa yangu huku nikila mziki laini ndani ya gari lenye namba za kigeni za SA.

Wakati bado nikiwa ndani ya gari mawazo yangu yakiwa mbali ghafla nikaona gari (through side mirror) Ghafla lime block nyuma yangu.

Gari aina ya defender ikiwa na maaskari wengine kanzu na wenye mavazi yao ya kipolisi huku waiwa na misilaa kama vile ni raid flani hivi ya majambazi.

Maajabu ni kwamba nilikuwa nikiwafahamu zaidi ya wawili ama watatu wa hao maaskari kanzu.

Ghafla mmoja wao akaingiza mkono na kuchomoa funguo za gari...Na kufungua mlango huku wakiniamrisha kushuka kutoka kwenye gari.

Nikamwambia mmoja wa wale niliokuwa nikiwafahamu..Ni nini tena ndugu yangu kuvamiana kama majambazi?

Yeye mwenyewe alikuwa akinieleza kwa masikitiko kuwa ni amri kutoka kwa Zombe.

Baada ya jamaa yangu naye kurudi kutoka Posta...Tukajumuishwa wote ndani ya gari na mmoja wa wale waliovalia kiraia akawa ndiye mwendeshajiwa gari lile nilolokuwa nalo...Baada ya kufikishwa kituoni ndio nikakutana na Zombe mwenyewe kwa mara ya kwanza!
Na ndugu zangu story ya shahidi yule ni kama yale yaliyonipata hivyo hivyo..Amri ilitoka kwa Zombe aliyekuwa upastairs ofisini kwake na kufoka walete wa*** huku juu.

Vitisho kama alivyosema yule bwana ni the same..Tofauti ni kwamba hakuwa na bunduki kama yule shahidi mwingine alivyokuwa akisema..Bali alikuwa na kamera...Na bastola moja ikiwa mezani nahuku akivuta midroo yake kwa vurugu nyingi..Na kuikamata bastola yake mara kwa mara..Huku tukiwa tumekalishwa chini ofisini kwake kama vile tayari sisi ni majambazi ama vibaka!

Huku akiongea kwa vitisho na mara nyingine kejeli..Huku akitupiga mipicha ya kila namna na kudai kuwa sisi ni majambazi na huku akitisha kutukanyaga usoni!

Jamaa yangu alikuwa akifikiri ni kama masikhara vile akatabasam...Jamaa akamtukana matusi ya nguoni na huku akisema jambazi mkubwa we na maneno kede kede.
Baada ya vitisho na unyanyasaji mwingi ndio tukapelekwa chini lock up kusubiri wadhamini.
Huyu bwana kusema kweli alikuwa anajuwa kabisa kuwa wale watu walikuwa innocent!

Na mimi huwezi kujuwa labda ni Mungu alisaidia kukawa na maafisa wengine waliokuwa wakijuwa kabisa kuwa amri ya bosi wao ilikuwa na walakini kwani mimi si jambazi na wao walikuwa wakifahamu kuhusu gari hilo.
Huu unyanyasaji wake naona umefikia kikomo na ni malipo ya Mungu kwa unyama wote aliwahi kuufanya dhidi ya raia wema huku akiwalinda majambazi!

Yeye ndiye mmojawapo aliyekuwa akitoa amri za kuwanyanyasa raia huku ujambazi ukishamiri akiwa in charge wa upelelezi.
Mabilioni waliyojivunia wakiwa na kina Mahita ni mtandao wa kigaidi uliokuwa ukiwalenga raia wema specifically na kuwa wasindikizaji wa majambazi kwenye matukio yao ya uamabazi!
Wewe unaweza kuona polisi wametokea ukadhani kuwa ni msaada ukaja ukashangaa wanakumalizia wao wenyewe!
Na hayo ndiyo yaliyotokea kwenye kesi hii ya Zombe!
Na asijidahi kuongea maneno ya dini sasa hivi!
Labda atakuwa amegeuka na kuwa mlokole akiwa huko jela...Kitu ambacho mke wake ambaye ni mlokole alikuwa akimlimlilia sana afanye hivyo !

Ama kweli Mungu si Zombe!

Pole sana kwa yaliyokupata. Wengi tunaamini kwamba malipo ya dhambi huwa ni hapa hapa duniani, na wala sio mpaka ufe ufike huko jehanamu. Natamani kusikia wamemgeuza bibi huko jela.
 
Niliposoma maelezo ya yule shahidi wa kwanza kwenye kesi ya Zombe basi nikajua kweli hawa jamaa nao walikuwa ni victims wa uhuni roho mbaya aliyokuwa nayo Zombe.

Kila kitu alichoelezea kilichowapata marehemu hao ni kama ambao yalishawahi kunipata mimi kwa amri za aina hiyo hiyo za Zombe.

Nilikuwa Post Office Moshi siku hiyo sitakaa nisahau.
Kuna mtu nilikuwa nimempa ride na mimi nilikuwa nimebaki kwenye gari nikimsubiri jamaa yangu huku nikila mziki laini ndani ya gari lenye namba za kigeni za SA.

Wakati bado nikiwa ndani ya gari mawazo yangu yakiwa mbali ghafla nikaona gari (through side mirror) Ghafla lime block nyuma yangu.

Gari aina ya defender ikiwa na maaskari wengine kanzu na wenye mavazi yao ya kipolisi huku waiwa na misilaa kama vile ni raid flani hivi ya majambazi.

Maajabu ni kwamba nilikuwa nikiwafahamu zaidi ya wawili ama watatu wa hao maaskari kanzu.

Ghafla mmoja wao akaingiza mkono na kuchomoa funguo za gari...Na kufungua mlango huku wakiniamrisha kushuka kutoka kwenye gari.

Nikamwambia mmoja wa wale niliokuwa nikiwafahamu..Ni nini tena ndugu yangu kuvamiana kama majambazi?

Yeye mwenyewe alikuwa akinieleza kwa masikitiko kuwa ni amri kutoka kwa Zombe.

Baada ya jamaa yangu naye kurudi kutoka Posta...Tukajumuishwa wote ndani ya gari na mmoja wa wale waliovalia kiraia akawa ndiye mwendeshajiwa gari lile nilolokuwa nalo...Baada ya kufikishwa kituoni ndio nikakutana na Zombe mwenyewe kwa mara ya kwanza!
Na ndugu zangu story ya shahidi yule ni kama yale yaliyonipata hivyo hivyo..Amri ilitoka kwa Zombe aliyekuwa upastairs ofisini kwake na kufoka walete wa*** huku juu.

Vitisho kama alivyosema yule bwana ni the same..Tofauti ni kwamba hakuwa na bunduki kama yule shahidi mwingine alivyokuwa akisema..Bali alikuwa na kamera...Na bastola moja ikiwa mezani nahuku akivuta midroo yake kwa vurugu nyingi..Na kuikamata bastola yake mara kwa mara..Huku tukiwa tumekalishwa chini ofisini kwake kama vile tayari sisi ni majambazi ama vibaka!

Huku akiongea kwa vitisho na mara nyingine kejeli..Huku akitupiga mipicha ya kila namna na kudai kuwa sisi ni majambazi na huku akitisha kutukanyaga usoni!

Jamaa yangu alikuwa akifikiri ni kama masikhara vile akatabasam...Jamaa akamtukana matusi ya nguoni na huku akisema jambazi mkubwa we na maneno kede kede.
Baada ya vitisho na unyanyasaji mwingi ndio tukapelekwa chini lock up kusubiri wadhamini.
Huyu bwana kusema kweli alikuwa anajuwa kabisa kuwa wale watu walikuwa innocent!

Na mimi huwezi kujuwa labda ni Mungu alisaidia kukawa na maafisa wengine waliokuwa wakijuwa kabisa kuwa amri ya bosi wao ilikuwa na walakini kwani mimi si jambazi na wao walikuwa wakifahamu kuhusu gari hilo.
Huu unyanyasaji wake naona umefikia kikomo na ni malipo ya Mungu kwa unyama wote aliwahi kuufanya dhidi ya raia wema huku akiwalinda majambazi!

Yeye ndiye mmojawapo aliyekuwa akitoa amri za kuwanyanyasa raia huku ujambazi ukishamiri akiwa in charge wa upelelezi.
Mabilioni waliyojivunia wakiwa na kina Mahita ni mtandao wa kigaidi uliokuwa ukiwalenga raia wema specifically na kuwa wasindikizaji wa majambazi kwenye matukio yao ya uamabazi!
Wewe unaweza kuona polisi wametokea ukadhani kuwa ni msaada ukaja ukashangaa wanakumalizia wao wenyewe!
Na hayo ndiyo yaliyotokea kwenye kesi hii ya Zombe!
Na asijidahi kuongea maneno ya dini sasa hivi!
Labda atakuwa amegeuka na kuwa mlokole akiwa huko jela...Kitu ambacho mke wake ambaye ni mlokole alikuwa akimlimlilia sana afanye hivyo !

Ama kweli Mungu si Zombe!

Pole sana Mushi. This was the kind of law enforcers we used to have by that time na wengi sana wameumia katika mikono yao. nadhani idadi ya watu waliouawa na majambazi, inakaribia kulingana na waliouawa mikononi mwa polisi. lakini kama alivyosema mmoja hapo juu, Mungu si Zombe na siku zote mtu hupata malipo ya matendo yake, kama si hapahapa duniani, basi mbele ya Allah.
Aliyoyafanya Zombe yanafahamika lakini yeye mwenyewe anayafahamu vizuri sana kuliko mtu mwingine. Ingekuwa vema kwake iwapo angeamua kutubu sasa na kumgeukia Mungu, kuendelea kuonyesha kiburi ni kujiongezea mzigo ambao hatoweza kuubeba mbele ya haki.
Pole Mushi, lakini ninaamini kuwa maisha yanaendelea kwako kama kawaida, hata kama hautasahau ya Zombe, msamehe na wewe utapata baraka zako
 
Mungu ana hekima za ajabu ambazo hatuwezi kuzicgunguza....

Fisi kung'oka jino kwa kutafuna nyama si jambo la kawaida....

Haya zombe ngoma iko ngumu sasa na roho ulizoamrisha zitolewe zimekushtaki kwa Mungu zinakulilia.... Mi simo
 
Yaani ukinitajia jina la Zombe najisikia kichefua - chefua! tena ingekuwa kunauwezakano hukumu ya kesi yake ingesomwa hata leo hii, ale miaka yake

Na hilo lililokuwa likubwa lao (Mahita) hili jamaa lilikuwa na vijana wa kazi waliokuwa wakiendesha shughuli za uporaji wa madini na pesa, wahindi wawatu wafanya biashara ya tanzannite mkoani Arusha walikiona cha moto.

Kosa walililofanya ni kumpeleka Bwana Kombe kuwa RPC Arusha, Mzee Wakimarangu alikwenda akaufyeka mtandao mzima, Ujambazi ukaisha. Walivyogundua kumbe wamempa machapakazi anawaramba mpaka vijana wao akaondolewa na kupelekwa makao makuu - Dar kwenda kuwa kamanda wa Kikosi cha usalama Barabarani.

Kombe alipoingia Arusha akatangaza, jamani sasa kazi kila mtu atakuwa salama pamoja na mali zake, hatutamwangalia mtu,Hawa vijana wa kazi kwenye vikao vyao wakajibu mapigo kwa kusema, hatuongei na mbwa tunaongea na mwenye mbwa.(hawaongei na RPC wanaongea na IGP)

Kombe akasema, anaapa kama hatawamaliza basi yeye anarudi zake moshi kulima mgomba na kazi ya upolisi haimfai.

Mahita..Zombe.. yote mijambazi
 
loh pole sana jmushi kwa mkasa wako...sasa wajimini naomba kuuliza hivi huko bongo sasa siku hizi nani wa kuaminika??maana viongozi full of ufisadi,polisi nao ndo ka hivi,sheria ni pwesa yako tuu,hospitalini nasikia nako ni mijihelaa tuu yatakiwa mwee balaah!
 
Halafu anali lia pale ushahidi unapotolewa na details zote za ugaidi wake zinapowekwa hadharani.

Hii ni kwasabab ushahidi unamwumiza roho kwasababu ni ukweli!
Halafu anajisahahu kama Saddam na kuanza kubwatuka kama vile alivyokuwa akifanya wakati akitoa amri zake za kijambazi na kigaidi dhidi ya innocent citizens.

Naomba waendesha mashtaka wasikubali intimidation zake na wa take tieir time wakati wa kesi hii na kumkaanga vizuri mpaka aive na kuelewa nini maana ya kunyanyaswa kwani malipo huanzia kwenye kusutwa,ukweli kuwekwa wazi,ujambazi wake kuainishwa pamoja na yeye kuwa embarassed na uchungu wa maelezo ya kesi na mashahidi halafu then huendelea pale anapokuwa sentenced hadi pale anapomalizia adhabu yake.
 
kuna forums fulani wanasema kuwa ZOMBE kafa
je kuna yeyote kwenye ukweli wa hili?
 
kuna forums fulani wanasema kuwa ZOMBE kafa
je kuna yeyote kwenye ukweli wa hili?

Ukweli Zombe hajafa, labda kama ni Breaking News!
Zombe anaendelea na kesi yake....
"Katika kesi hiyo itakayosikilizwa na Jaji Kiongozi Salum Massati kwa siku 13 mfululizo, upande wa mashitaka unategemea kuita mashahidi zaidi ya 50 na kuwasilisha vielelezo kadhaa vya kuthibitisha makosa dhidi ya washitakiwa"

kwa hiyo hata leo Zombe yuko Mahakamani...sasa hili la kufa limetokea lini?
 
Kesi ya mauaji ya wafanyabiashara, polisi adai aliamriwa abadilishe taarifa
* Ni kuhusu silaha zilizotumika kwa wafanyabiashara wa Mahenge
* Adai alishinikizwa kutoa bunduki na risasi zikapigwe porini

James Magai na Nora Damian

SHAHIDI wa 15 katika kesi ya mauaji ya kukusudia inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi, Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi (ACP), Abdallah Zombe na wenzake 12, Koplo C 7521, Xavery Joseph Kajela amedai kuwa alishinikizwa kubadili taarifa ya silaha na risasi alizowakabidhi baadhi ya watuhumiwa ili kuwalinda askari wenzake waliokabidhiwa silaha.

Akitoa ushahidi jana katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Koplo Kajela ambaye ni mtunza ghala la silaha katika Kituo cha Polisi Oysterbay, aliieleza mahakama hiyo kuwa siku tatu baada ya mauaji hayo, alishinikizwa na Mkuu wa Upelelezi wa kituo hicho, (OC-CID) SP Christopher Bageni kubadili taarifa ili kuonyesha kuwa baadhi ya risasi zilikuwa zimetumika katika mapambano ya askari na majambazi hao.

Akiongozwa na Naibu Kiongozi wa Waendesha Mashtaka wa Serikali, Jasson Kaishozi, Koplo Kajela alidai kuwa mbali na kushinikizwa kubadilisha taarifa ya idadi ya risasi zilizokuwa zimerejeshwa, pia SP Bageni alimwamuru ampatie askari mmoja silaha na risasi ili aende kufyatua porini.

Alibainisha lengo la shinikizo hilo, lilikuwa ni kuonyesha katika taarifa hiyo kuwa risasi ambazo zilikuwa zimepungua, ndizo zilizokuwa zimetumika katika mapambano baina ya askari na wafanyabiashara hao wa madini waliokuwa wameuawa kwa tuhuma za ujambazi.

Akisimulia zaidi mbele ya Jaji Salum Masatti anayesikiliza kesi hiyo, Koplo Kajela alidai kuwa siku ya tukio la mauaji ya wafanyabiashara hao, aliwakabidhi silaha baadhi ya watuhumiwa na kwamba wote walizirejesha zikiwa na idadi ya risasi walizokabidhiwa isipokuwa askari mmoja tu ambaye alitumia risasi kadhaa.

Koplo Kajela alifafanua kuwa Koplo Saad alimkabidhi bunduki aina ya SMG namba 3A0199P na risasi 30, lakini alirejesha bunduki na risasi 21 tu.

Alidai pia kuwa alimkabidhi Konstebo Rashid bunduki aina ya SMG namba 13059192 na risasi 30, alirudisha bunduki hiyo na risasi zote 30 wakati Koplo Rajabu alimkabidhi bastola aina ya Chinese na risasi nane ambazo pia alizirejesha zote.

Alidai askari wengine aliowakabidhi silaha hizo kuwa ni D 9321 Konstebo Rashid Mohamed, D 4656 Koplo Rajabu Hamis Bakari, ambao wote ni watuhumiwa walioko mahakamani na kwamba D 56 62 Koplo Saadi hadi sasa hajulikani aliko.

Aliendelea kudai baada ya kupokea na kuzikagua silaha hizo na kuandika taarifa katika kitabu cha kumbukumbu, siku tatu baadaye alipokea amri kutoka kwa SP Bageni kwamba anapaswa kubadilisha taarifa hiyo na kumpatia silaha na risasi Koplo Rajabu ili aende mahali popote afyatue risasi tatu na kisha kuandika taarifa nyingine kuwa risasi tatu zilitumika tofauti na taarifa ya awali kuwa askari huyo alirejesha risasi zote, alizokabidhiwa.

"Nilishinikizwa na uongozi yaani Mkuu wa Upelelezi kituoni (OC-CID) Christopher Bageni kuwa nimpe silaha na risasi Koplo Rajabu, ili akafyatue risasi tatu porini ili kumsaidia, kwani bosi alidai kuwa jambo hilo lilikuwa gumu," alieleza Koplo Kajela.

Alidai kutokana na shinikizo hilo, alitii na kumkabidhi Koplo Rajabu silaha na risasi na kurekebisha kumbukumbu katika kitabu hicho ili zisomeke kuwa risasi tatu zilitumika wakati awali hazikutumika.

Mbali na maelezo hayo, katika mahojiano na mawakili wa upande wa utetezi Koplo Kajela alieleza zaidi kama ifuatavyo.

Wakili Gaudioz Ishengoma: Unapopokea silaha na kukagua taarifa huwa uzipeleka kwa nani?

Shahidi Koplo Kajela: Huwa ninampa mkuu wa kituo.

Ishengoma: Sasa unakubaliana na mimi kuwa mwenye amri ya mwisho ya kuruhusu silaha itoke ni (OCS) Mkuu wa Kituo?

Koplo Kajela: Afisa yeyote mwenye cheo cha kuanzia Gazzetted anaweza kuruhusu silaha itoke.

Ishengona: Unaifahamu PGO ni nini?

Koplo Kajela: Ndio ni mwongozo wa utendaji wa kazi wa Jeshi la Polisi.

Ishengoma:
Nikisema kwa mujibu wa PGO OCS ndiye hutoa amri kuruhusu silaha itoke, tena kwa maandishi utasemaje?

Koplo Kajela: Pamoja na hayo.

Ishengoma:
Hayo maagizo ya Bageni yalikuwa ya maandishi au ya mdomo?

Koplo Kajela: Verbally (ya mdomo).

Ishengoma: Kwa hiyo hayo maandishi mekundu katika marekebisho ya taarifa aliyaandika Bageni au wewe?

Koplo Kajela: Niliandika mimi.

Ishengoma:
Katika kumbukumbu zako za utoaji wa silaha Kituo cha Polisi Oysterbay au mahali popote kuna mahali ambako kuna hizi taarifa ulizozieleza hapa leo?

Koplo Kajela: Taarifa ziko katika quotebook na hii ndio halisi.

Ishengoma:
Kwa hiyo Tibaigana anaweza kuwa pale Central akakuagiza kutoa silaha ukatoa na hata bila maandishi?

Koplo Kajela: Ndio inakubalika kwani inaitwa 'Verbal Command'.

Ishengoma: Hiyo amri ya SP Bageni ilikuwa ni halali?

Koplo Kajela:
Ndio ilikuwa halali.

Ishengoma:
Umesema wakati Bageni anakuamuru hivyo alikuambia kwamba unafanya hivyo ili kuwaokoa askari hao katika janga hili, je, huoni kama na wewe uliwasaidia?

Koplo Kajela: Nisingeweza kukataa kwa sababu ilikuwa ni hali ngumu na niliogopa.

Ishengoma: Lakini ulijua kuwa ilikuwa kinyume cha utaratibu?

Koplo Kajela: Nilijua, lakini nilishinikizwa.

Ishengoma: Kwa hiyo 'uli-forge'?

Koplo Kajela: Ndivyo inavyoonekana.

Ishengoma: Wewe kama askari polisi mwenye uzoefu wa miaka zaidi ya 25 kazini, si unajua kuwa askari anaruhusiwa kutii amri halali tu?

Koplo Kajela:
Kuna amri kwamba, tekeleza kwanza ndio uulize.

Ishengoma: Nikikuambia kwamba huna uthibitisho kuwa Bageni alikuamuru utii amri yake utasemaje?

Koplo Kajela:
Nimesema ilikuwa ni Verbal Command, unatekeleza kwanza ndio unauliza.

Wakili Majura Magafu: Mbona kuna maneno mengi tu umeyazungumza hapa na katika 'statement' yako uliyoitoa polisi hayako?

Koplo Kajela: Ni kwa sababu niliapa kusema ukweli.

Majura: Umesema ulilazimika kubadilisha taarifa ya awali na kurekebisha kwa kalamu nyekundu mbona katika maelezo yako hayaendani na maelezo ya awali ulipohojiwa na askari polisi?

Koplo Kajela: Niliyoyasema leo ndio sahihi.

Magafu: Kwa hiyo utapenda kuiondoa 'statement' hii hapa mahakamani kama sehemu ya ushahidi?

Koplo Kajela: Mahakama ndio itachambua na kuona yapi ya kweli.

Koplo Kajela alipoulizwa na Wakili Magafu iwapo alishamwambia OCS wa Oysterbay kuwa Bageni alimshinikiza, alijibu wote ni askari polisi na kwamba asingeweza kumshtaki kiongozi kwa kiongozi mwenzake.

Naye shahidi wa 16, Ramadhani Mfaume Juma ambaye ni ndugu wa marehemu Juma ambaye ni dereva teksi aliiambia mahakama kuwa wakati wakiwa msikitini kwa ajili ya ibada ya kuaga mwili wa marehemu Juma, gari ya polisi ilifika ikiwa na askari waliokuwa na bunduki huku wameficha nyuso zao.

Alidai walipofika Zombe alisema watu waliowaua ni majambazi wala si kwamba wanawaonea.

Alidai ingawa alikuwa hajawahi kumwona Zombe, lakini kinachomfanya amkumbuke hadi sasa ni kwa kuwa alitangaza kupitia vyombo vya habari kuwa wamewaua majambazi na pia alipokwenda msikitini Muhimbili.

Mahojiano kati ya Wakili Moses Maira na shahidi Juma yalikuwa kama ifutavyo.

Wakili Maira: Kama nikisema ulikuwa umeona kivuli cha Zombe, kwani siku hiyo Zombe hakuwepo Muhimbili, bali alikuwa amekwenda Uwanja wa Ndege kwenye msafara wa Rais utasemaje?

Shahidi Juma: Kwani siku ina saa ngapi, je, mimi nikikuambia leo nilikuwa Manzese na sasa niko hapa hutakubali?

Wakili Majura Magafu: Nikisema siku hiyo Zombe alikuwa kwenye msafara wa Rais kuanzia asubuhi hadi jioni utasemaje?

Juma:
Kwa kuwa unamtetea utasema hivyo, lakini mimi nasema alikuja na nilimwona.

Katika hatua nyingine, Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam jana ilikataa kupokea vielelezo vya picha vilivyotolewa na upande wa mashitaka katika kesi ya mauaji inayomkabili Zombe na wenzake 12.

Hatua hiyo ilifuatia muda mfupi baada ya shahidi wa 18 katika kesi hiyo, Sajini Nasibu kuanza kutoa ushahidi.

Nasibu aliieleza mahakama kuwa anafanya kazi Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kama mtaalamu wa kupiga picha katika kitengo cha utambulisho.

Alieleza Februari 22, mwaka 2006 akiwa kazini aliitwa na mkuu wake wa kazi na kupewa maelekezo ya kwenda kukagua tukio lililotokea Sinza la watu wanne kuuawa na polisi.

''Tulipewa maelekezo ya kupiga picha sehemu mbalimbali za tukio na tulipiga picha zaidi ya 10 na kuzikabidhi kwa timu ya wapelelezi tuliokuwa tumekwenda nao,'' alieleza Nasibu.

Kabla shahidi huyo, hajaendelea kutoa ushahidi wake mmoja wa mawakili wa upande wa mashtaka, Angaza Mwaipopo aliiomba mahakama ipokee picha hizo na kuwa vielelezo katika kesi hiyo.

Hatua hiyo iliibua mjadala mkali baina ya pande mbili za mashtaka na utetezi na mmoja wa mawakili upande wa utetezi, Majura Magafu aliieleza mahakama kuwa wanapinga kupokelewa kwa vielelezo hivyo kwa kuwa hawakuelezwa kama vitatumika wakati wa kuendesha kesi.

''Katika vielelezo walivyosema kwamba vitatumika wakati wa kuendesha kesi hiki hawakukiorodhesha na katika sheria ya ushahidi sura ya 6 kifungu cha 3 kinaeleza kuwa picha ni kielelezo,''alieleza Magafu.

Jaji Kiongozi Salum Masati baada ya kusikiliza hoja zote alikataa kielelezo hicho kisipokelewe katika mahakama hiyo. Pia alikubaliana na ombi la upande wa mashtaka la kutaka kuwasilisha hoja kuwa kielelezo hicho kipokelewe mahakamani leo.

Naye shahidi wa 17 katika kesi hiyo, Luteni Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Emmanuel Mkonga aliieleza mahakama kuwa Januari 7, mwaka 2006 alisafiri kutoka Mahenge kwenda Arusha kupitia Dar es Salaam akiwa na ndugu zake watano, wakiwemo marehemu Ephraim Chigumbi na Sabinus Chigumbi na kwamba walikuwa wakitumia gari la marehemu Jongo.

Alidai walipofika Arusha marehemu Ephraim na Sabinus walienda kwenye soko la madini na baada ya kurudi kwenye hoteli waliyofikia, aliwaona wakiwa na mkoba mkubwa uliokuwa umejaa hela ambazo hakujua zilikuwa ni kiasi gani.

Alieleza Januari 12, mwaka 2006 waliondoka Arusha na kurejea Dar es Salaam na siku hiyo, ndugu zake walifikia Hoteli ya Bondeni na yeye alikwenda kulala Keko kwa ndugu yao mwingine.

Alidai Januari 13, mwaka 2006 alipeleka gari gereji kwa ajili ya kwenda kupaka rangi na ndugu zake wengine walibaki hotelini.

''Januari 15, mwaka 2006 asubuhi nilienda gereji kufuatilia gari lakini ndugu yangu Vasco niliyekuwa nimeongozana naye alinieleza kuwa alipokea taarifa kutoka katika hoteli waliyokuwa wamefikia marehemu kuwa walikuwa hawajaonekana,'' alieleza Mkonga.

Nasibu alidai kuwa baada ya kwenda kufuatilia katika hoteli hiyo na vituo mbalimbali vya polisi bila mafanikio, waliwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kuangalia na walipoingia katika chumba cha maiti walikuta miili ya ndugu zao ikiwa na majeraha sehemu za usoni.

Alidai wakiwa Muhimbili walivamiwa na watu wasiowaelewa ambao walikuwa wamevaa kininja na kuwakamata na kuwapeleka Kituo Kikuu cha polisi ambako walionana na Zombe.

''Tulipofika kwa Zombe alitamka kuwa sisi ni majambazi na akaniambia mimi kuwa ndiye kinara wao kule Mahenge na kwamba nilikuwa nawafundisha ujambazi, nilifadhaika sana,'' alidai Nasibu.

Shahidi huyo alieleza waliwekwa mahabusu siku mbili na askari kuchukua maelezo yao na baadaye walitolewa nje na Zombe aliamuru waachiwe kwa kuwa hawakuwa majambazi.

Kesi hiyo namba 26 ya mwaka 2006 kwa mara ya kwanza, Zombe na wenzake 12 walifikishwa mahakamani Septemba 28, mwaka juzi mbele ya aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa mahakama hiyo, Laurian Kalegeya ambaye sasa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa.

Zombe alipandishwa katika mahakama hiyo, kwa mara ya kwanza Juni 9, saa 4.00 asubuhi na Juni 15 mchana alifutiwa shtaka la mauaji lilokuwa likimkabili peke yake mbele ya Kaimu Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Addy Lyamuya na kuunganishwa na wenzake 12 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Sivangilwa Mwangesi.
 
hii nayo siasa ? muone kwanza !

Kada
Hii si siasa ila ni habari mkuu .Unaweza kusoma na kupita si lazima uonyeshe upumbavu wako .Hii inaweza kuwa siasa in a way yes .Kwa nini JK hawakamati mafisadi kakazana huyu pekee ? Kweli aliua lakini wako mafisadi wanao tuua taratibu na tutakufa .Inaweza kuwa siasa kwa kuwa imepewa uzito mkubwa hadi mawakili wa kujitegemea kuendesha kesi , je wangapi DPP kawapa kibali cha kuwatumia mawakili wa kujitegemea? All in all nilikuwa natoa tu habari kama vile juzi ilitolewa hapa akisema anaonewa huyu Zombe huja question why leo ukurupukie hapa ?
 
Kada
Hii si siasa ila ni habari mkuu .Unaweza kusoma na kupita si lazima uonyeshe upumbavu wako .Hii inaweza kuwa siasa in a way yes .Kwa nini JK hawakamati mafisadi kakazana huyu pekee ? Kweli aliua lakini wako mafisadi wanao tuua taratibu na tutakufa .Inaweza kuwa siasa kwa kuwa imepewa uzito mkubwa hadi mawakili wa kujitegemea kuendesha kesi , je wangapi DPP kawapa kibali cha kuwatumia mawakili wa kujitegemea? All in all nilikuwa natoa tu habari kama vile juzi ilitolewa hapa akisema anaonewa huyu Zombe huja question why leo ukurupukie hapa
?

inaelekea una stress kichizi lunyungu..............

umetoa mada inayohusu wafungwa, then ukasema

(a)kada mpumbavu
(b)jk hakamati mafisadi

issues a and b hazihusiani kabisa na mada yako, second...nakushauri ukasome ile mada ya mwanakijiji ya tumewaudhi maana naona na wewe pia inakuhusu. Yaani umeudhika kupita kiasi, sababu ? sijui.. pole mzee na stress !

zaidi ya yote, umekiri kwamba hiyo sio siasa, na unafahamu fika kwamba hii ni seksheni ya siasa, lakini still umekuwa ignorant kupita kiasi na kupenyeza "habari" yako kwenye siasa....huu sasa nao pia ni UFISADI !! inafaa ukamatwe !!
 
Back
Top Bottom