Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Anonymous

Senior Member
Feb 3, 2006
125
320
Februari 26, 1982 Tanzania ilitikisika baada ya kutokea taarifa kuwa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATC) imetekwa. Lilikuwa ni tukio la kwanza la aina yake kuwahi kutokea katika nchi hii na kuzua mijadala kote duniani.

=====
KWA UELEWA, SOMA:

1) Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

2) Nini kilipelekea vijana wa Tanzania kuteka ndege ya ATC 1982 Mwanza?

Aidha, soma hii:

Februari 26, 1982 nchi ilitikisika baada ya kutokea taarifa kuwa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATC) imetekwa. Lilikuwa ni tukio la kwanza la aina yake kuwahi kutokea katika nchi hii na kuzua mijadala kote duniani.

Kutokana na hali ya kisiasa iliyokuwa ikiendelea nchini tangu Tanganyika ilipojipatia Uhuru Jumamosi ya Desemba 9, 1961, wako Watanzania ingawa wachache ambao hawakuridhishwa na uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kiasi kwamba wako waliodiriki hata kuteka ndege ya abiria ya Tanzania kwa lengo la kuishinikiza Serikali kukubaliana na madai yao.

Miongoni mwao ni vijana watano walioteka ndege aina ya Boeing 737 ya Shirika la Tanzania (ATC) aina, Boeing 737 ikiwa mjini Mwanza.

Huo ulikuwa ni utekaji wa kwanza wa aina yake tangu ATC lilipoanzishwa Ijumaa ya Machi 11, 1977 baada ya kuvunjika kwa Shirika la Ndege la Afrika Mashariki (EAA) Januari 1977 na kisha kufa rasmi Jumanne ya Februari 1, 1977.

Utakaji wa ndege hiyo ulikuja siku moja baada ya kutekwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kuwait, Alhamisi ya Februari 25, 1982. Ndege hiyo ilitekwa katika ardhi ya Beirut, Lebanon ikirejea kutoka Libya. Ilikuwa na abiria 150.

Pamoja na kwamba utekaji wa kwanza wa ndege katika anga la Tanzania ulifanyika mwaka 1972 na mwingine ukafanyika mwaka 1979, huu wa Februari 1982 ulikuwa wa kipekee kabisa na—ingawa ulikuwa ni utekaji uliohusiana na siasa—Serikali ya Tanzania haikutaka ijulikane hivyo.

Saa 11:00 jioni ya Ijumaa ya Februari 26, 1982, baada ya kuagana na ndugu, jamaa na marafiki, abiria kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza waliingia katika ndege ya ATC iliyokuwa na jina la Kilimajaro ubavuni mwake.

Kwa wasafiri wengi, Uwanja wa Ndege wa Mwanza haukuwa na sifa nzuri kutokana na kukosa usalama kiasi cha baadhi ya marubani kuutaja kama “kituo cha basi”.

Kulikuwa na makundi ya kawaida ya watu uwanjani hapo kama ilivyokuwa siku zote kwa wasafiri wa Mwanza—Dar es Salaam. Wengi wao walikuwa ni wale wenye asili ya India, Waarabu na wazawa wachache.

Pamoja na kwamba mambo yote yaliyonekana kuwa ya kawaida, kulitokea jambo dogo ambalo liliifanya safari ya ndege hiyo isiwe ya kawaida.

Boeing 737 ilipaa angani saa 11:20 ikielekea Dar es Salaam na ilitarajiwa kuwa ingetumia dakika 90, kutembea umbali wa takriban maili 500 kufika, lakini ikageuka kuwa safari ya juma zima na umbali wa kiasi cha maili 9,500—tena wakati wote abiria na wafanyakazi wa ndege hiyo wakiwa chini ya ‘mtutu wa bunduki’.

Dakika tano tu baada ya ndege hiyo kupaa angani, vijana wanne walisimama ghafla kwa wakati mmoja. Mmoja wao alijipenyeza kwa kasi hadi chumba cha rubani, kisha akaelekeza ‘bastola’ yake kwenye kichwa cha mmoja wa marubani, Kapteni Deo Mazula, na kumuamuru awapeleke Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta, Nairobi.

Baadaye ilikuja kujulikana kuwa majina ya watekaji wale ni Mussa Memba (25), Mohamed Ali Abdallah (26) na nduguye Abdallah Ali Abdallah (22), Mohamed Tahir Ahmed (21) na Yassin Memba (21). Ilikuja kujulikana pia kuwa kiongozi wao alikuwa ni Mussa Memba.

Wakati huohuo, watekaji nyara wengine, huku wakipunga ‘bastola’ bandia zilizotengenezwa kwa vigogo vya miti na ‘mabomu’ ya kutupwa kwa mkono, waliwatangazia abiria kuwa wao ni viongozi wa ‘Vijana wa Harakati za Mapinduzi Tanzania’ na kwamba shabaha yao ni “kuhakikisha kuwa Rais Julius Nyerere anajiuzulu”.

Wakati hayo yakitokea, Mwalimu Nyerere alikuwa Ikulu jijini Dar es Salaam akijiandaa kurejea nyumbani kwake baada ya kupokea risala kutoka kwa chipukizi waliomuahidi kuwa wataendelea “kuwa watiifu, wakakamavu na wenye bidii kwa kuwa tunafahamu mchango wetu unahitajika sana katika ujenzi wa nchi”.

Hadi wakati anaondoka ofisini kurejea nyumbani kwake akiwa amefurahishwa na risala iliyosomwa na mwenyekiti wa Taifa wa chipukizi, Frank Uhahula (15) wa darasa la saba katika Shule ya Msingi ya Tumbi, Kibaha mkoani Pwani, Mwalimu Nyerere hakuwa amejua kile kilichotokea upande mwingine wa nchi.

Mara baada ya watekaji hao kuanza purukushani katika ndege hiyo, waliwaamuru abiria wote wakae kimya kwenye viti vyao na wafumbe macho na kwa sababu ambazo hazikujulikana mara moja lakini za kustaajabisha, waliwalazimisha wafanyakazi wa ndege hiyo kuzima viyoyozi.

Wakati huo ndege ilikuwa ikiambaa angani kuelekea Kenya. Hali ya hewa katika ndege hiyo ilipoanza kuwa nzito na kukaribia kutovumilika tena, ndege ilitua Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi.

Hata hivyo, katika kipindi cha dakika kadhaa baada ya kutua, Mwalimu Nyerere alipewa taarifa kuhusu utekaji huo na kuambiwa kuwa tayari imeshatua Nairobi.

Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, John Samuel Malecela, wakati huo akiwa na miaka 48, aliteuliwa rasmi kushughulikia sakata la utekaji huo na mara moja aliondoka kwenda Kenya.

Mwalimu Nyerere alitaka kuwa na uhakika kwamba Serikali ya Kenya hairuhusu ndege hiyo iondoke katika ardhi yake.

Wakati hayo yakiendelea, polisi wa Kenya waliufunga Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta, pia wanajeshi kusambazwa kuuzingira uwanja.
2
Baada ya maofisa wa Serikali ya Kenya kupata habari kuwa ndege hiyo aina ya Being 737 ya Air Tanzania itatua kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, polisi waliufunga na wanajeshi kuuzingira uwanja huo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Robert Robert Ouko (51), ndio kwanza alikuwa ametua uwanjani hapo akitokea jijini Addis Ababa, Ethiopia na hiyo ilikuwa muda mfupi baada ya ndege hiyo ya Tanzania kutua.

Alipopewa habari za yaliyotokea, Dk Ouko hakusita. Alikwenda moja kwa moja kwenye chumba cha kuongozea ndege ambako alijaribu kulishughulikia jambo hilo kwa kuwasiliana na watekaji. Ndege hiyo ilikaa katika uwanja huo kwa saa sita tangu ilipotua hadi ilipoondoka.

Akizungumza kupitia redio ya mawasiliano ya ndege hiyo. Kwa mujibu wa jarida la The Weekly Review, mmoja wa watekaji alijitambulisha kwa jina la Luteni Wami na kusema yeye ni ofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

‘Luteni Wami’ alisema ni lazima Rais Nyerere ajiuzulu “la sivyo tutailipua ndege hii”. Dk Ouko alijaribu kujadiliana na mtekaji huyo, lakini baadaye alijibiwa kuwa “tayari nimeshaua abiria watatu, na nitaendelea kuwaua wengine zaidi”.

Dk Ouko alishtushwa na kauli hiyo. Alilazimika kumsihi mtekaji huyo kwa kumwambia: “Usiendelee kuua zaidi.”

Lakini ukweli wa mambo, hapakuwa na mauaji yoyote hadi kufikia wakati huo.
Kupitia mawasiliano ya redio yao ya upepo, mtekaji huyo alimwambia Waziri Ouko: “Sasa namuua huyu rubani.” Rubani mwingine aliyekuwa akisaidiana na Kepteni Mazula ni Oscar Mwamaja.

Dk Ouko alimjibu mtekaji huyo kwa kumwambia kuwa ikiwa atafanya kitendo cha kumuua rubani wa ndege hiyo atakuwa amefanya ujinga kwa sababu “atahitajika kuirusha ndege hiyo kwenda kwingine”.

“Ninaweza kuiendesha ndege hii mimi mwenyewe,” akafoka mtekaji huyo, “Mimi ni luteni wa anga.”

Kadiri muda ulivyosogea, kiwango cha uvumilivu cha mjadala kati ya Dk Ouko na watekaji kilianza kuzorota. Walianza kuonekana kama wanarukwa na wazimu. Mtekani mmoja aliyedhani kuwa muda unazidi kuwatupa mkono, kwa hasira kali alifoka: “Tutailipua hii ndege sasa hivi. Tutakufa sasa hivi. Leteni majeneza 100 sasa hivi.”

Kuona hana jingine la kufanya, Dk. Ouko alikubaliana na matakwa ya watekaji hao. Baada ya kuizuia ndege hiyo kwa muda wa saa kadhaa, ilipofika usiku wa manane Serikali ya Kenya iliona haina la kufanya. Ikaona ni heri wairuhusu hiyo iondoke ikatue nchi nyingine.

Mabishano yaliyodumu kwa saa kadhaa yakafikia mahali ambako watekaji hao walidai ndege hiyo ijazwe mafuta kwa ajili ya safari ya kwenda Saudi Arabia. Ndege ilijazwa mafuta tayari kwa safari ya Saudi Arabia.

Wakati huohuo, jijini Dar es Salaam kumbukumbu za kijeshi zilianza kuchunguzwa kutafuta jina la Luteni Wami. Jina hilo, kwa mujibu wa jarida la Africa Now, halikupatikana popote, na wala hakukuwa na cheo chochote cha luteni wa anga nchini.

Kwa upande mwingine, hata baada ya majina ya watekaji hao kujulikana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi Tanzania, Joseph ole Muturu Lemomo, wakati huo akiwa na miaka 45, alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa “majina ya vijana hao ni ya kawaida na si rahisi kugundua mara moja katika kumbukumbu za polisi iwapo waliwahi kuhusika na uhalifu wowote”.

Joseph Lemomo, mzaliwa wa Wilayani Monduli mkoani Arusha, alikuwa ameteuliwa mwaka mmoja uliopita (1981) kuchukua nafasi ya Menolf Mwingira.

Kabla ndege haijaondoka jijini Nairobi, watekaji hao waliiachia familia moja ya watu wenye asili ya Kiarabu. Familia hiyo ilikuwa ni ya watu sita. Waliteremka kutoka katika ndege hiyo. Mmoja wa mateka hao, Khadija Mohamed Hassan, aliwaambia wana usalama wa Kenya kwamba yeye na familia yake waliruhusiwa watoke kwa sababu mwanawe wa miezi 18, Mselem, alikuwa akilia sana bila kunyamaza kiasi cha kuwakera watekaji hao na kwa sababu hiyo, watekaji hao walimuona kama udhia.

Lakini maofisa wa Serikali ya Tanzania waliitilia shaka familia hiyo. Wasiwasi kwa maofisa wa usalama wa Tanzania uliongezeka zaidi pale familia hiyo iliposema kuwa walikuwa wakisafiri kwenda Dubai na kwamba kwa sababu tayari walikuwa mjini Nairobi, ingekuwa rahisi zaidi kwao kufika huko kwa kupitia Mombasa.

Bila wao kutaka, familia nzima ililazimishwa kupanda kwenye ndege ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania na kupelekwa Dar es Salaam.

Kesho yake, Jumamosi ya Februari 26, Mwalimu Nyerere akiwa nyumbani kwake akitafakari ziara yake ya siku nne katika kisiwa cha Pemba ambako angeweka jiwe la msingi la kiwanda cha mafuta ya karafuu, alitaka kujua zaidi yaliyotokea.
Ingawa Waziri Malecela (wa Mawasiliano na Uchukuzi), kwa mujibu wa Africa Now, aliwaambia waandishi wa habari jijini Nairobi kuwa watekaji walimtaka Mwalimu Nyerere ajiuzulu lakini aliporejea Dar es Salaam alisema watekaji hao hawakutoa madai yoyote.
3
Ikiwa kwenye uwanja huo wa ndege jijini Nairobi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Dk Robert Ouko alijadiliana na watekaji hao. Tanzania ilimteua waziri wake wa Mawasiliano na Uchukuzi, John Samuel Malecela, kushughulikia utekaji huo.

Akiwa jijini Nairobi, Waziri Malecela aliwaambia waandishi wa habari kuwa watekaji hao walimtaka Mwalimu Nyerere ajiuzulu, lakini aliporejea Dar es Salaam alisema watekaji hao hawakutoa madai yoyote.

Akiwa kama kiongozi wa kushughulikia utekaji huo, Waziri Malecela alitoa taarifa hizo hizo kwa Mwalimu Nyerere: “Watekaji hawakutoa madai yoyote.”

Kwa kuwaamini maofisa wake, Mwalimu Nyerere aliamini pia hata kile walichomwambia kuhusiana na utekaji huo.

Maofisa wa Serikali ya Tanzania waliopiga kambi nyumbani kwa Mwalimu Nyerere, kulingana na taarifa walizokuwa wakipokea, walianza kuchukulia kuwa utekaji huo haukuwa na shabaha zozote za kisiasa. Kwa kuwa baadhi yao hawakujua kisa halisi cha kutekwa kwa ndege hiyo, walibuni vya kwao.

Walianza kuambizana wenyewe kwa wenyewe, na wakamwambia na Mwalimu Nyerere pia, kwamba ‘inawezekana’ watekaji hao walikuwa wameiba kiasi kikubwa cha dhahabu na almasi ambazo walitaka kuzitoa nchini.

Waliamini pia kwamba walitumia utekajij huo kuvusha mali hizo na kwamba familia ya Kiarabu iliyotaka kwenda Dubai kwa kupitia Mombasa ilikuwa ni sehemu ya utekaji huo.

Namna jambo hilo lilivyoshughulikiwa lilizua maswali mengi sana nchini Kenya. Kama ilivyoelezwa awali, Dk Robert Ouko alijiingiza katika mjadala wa utekaji huo kwa sababu ndiyo kwanza tu alikuwa ametua uwanjani hapo akitokea kwenye mkutano mjini Addis Ababa na si kwamba alifika uwanjani hapo rasmi kwa sababu ya tukio hilo.

Ilikuwa ni sadfa tu kwamba Dk Ouko alitua uwanjani hapo wakati uleule ambao ndege ya Tanzania iliyotekwa nayo ilikuwa imetua.

Hata hivyo, utekaji huo haukutokea wakati mzuri kwa sababu mgogoro kati ya Kenya na Tanzania kuhusu kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulikuwa haujapoa.
Mgogoro kati ya Kenya na Tanzania ambao ulioanza taratibu kuanzia mwaka 1974, ulifikia kilele chake mwaka 1977 wakati nchi zote mbili—Tanzania na Kenya—zilipogoma kutoa michango yake ya uanachama wa jumuiya hiyo. Kwa kukosa bajeti yake ya mwaka wa fedha wa 1977-1978, jumuiya hiyo ikafa rasmi Ijumaa ya Julai Mosi, 1977.

Machungu aliyokuwa nayo Mwalimu Nyerere yaliyotokana na kuanguka kwa jumuiya hiyo bado alikuwa nayo. Kitendo cha Kenya kuiruhusu ndege hiyo kuondoka mjini Nairobi kiliongeza idadi ya maswali yaliyoulizwa na hata kutonesha kidonda cha machungu aliyokuwa nayo Mwalimu Nyerere kuhusu jumuiya hiyo. Hata hivyo, Serikali ya Kenya haikujiingiza kwa undani katika kulizungumzia suala hilo.

Wakati sasa watu wakitafakari kilichotokea, ndege ya ‘Kilimanjaro’ ilikuwa ikiambaaambaa angani kuelekea Jeddah, Saudi Arabia. Ilipopata habari, Serikali ya Saudi Arabia iliinyima ndege hiyo ruhusa ya kutua na kwa kuonyesha haikuwa inatania iliufunga uwanja wake.

Lakini, Kepteni Deo Mazula alipowasiliana na wasimamizi wa uwanja huo na kuwaambia kuwa ndege yake imeshasafiri umbali wa kiasi cha maili 1,600 tangu alipoondoka Nairobi na kwamba haikuwa na mafuta zaidi ambayo yangeiwezesha kuendelea na safari nyingine, Serikali ya Saudi Arabia wakaufyata. Wakairuhusu ndege hiyo itue.

Ndege ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mfalme Abdulaziz mjini Jeddah. Ruhusa ya kutua kwa ndege hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kujaza mafuta tu. Walinyimwa hata ruhusa ya kufungua mlango wa ndege hiyo.

Wakati huu hali ya hewa katika ndege hiyo ilikuwa imeanza kurejea katika hali yake ya kawaida. Viyoyozi vilikuwa vimeshaanza kufanya tena kazi na watekaji walijaribu kusemezana na watekwaji huku wakiwaambia shabaha yao ya kuiteka ndege hiyo.

Hata hivyo, ujumbe waliokuwa wakijaribu kuutoa haukueleweka sawasawa kwa abiria wa ndege hiyo. Watekaji walijitambulisha kuwa wao ni wanachama wa ‘Harakati za Kidemokrasia za Vijana wa Tanzania.’

Waliwaeleza abiria hao kuwa walitaka Rais Julius Nyerere ajiuzulu kwa sababu “...Watanzania wanaishi katika hali ya shida na hawana chakula.”

Mwisho wa mazungumzo yao waliwaambia abiria kuwa wamekusudia kuipeleka ndege hiyo nchini Marekani. Wakati wakisema hayo, watekaji hao walikumbuka kuwa kuna abiria mmoja alitoa bastola yake walipokuwa Uwanja wa Ndege wa Mwanza na kuikabidhi chumba cha marubani.
Ni utaratibu katika viwanja vya ndege vya Tanzania kwa abiria yeyote kuitoa silaha yake na kuikabidhi kwa wafanyakazi wa ndege hadi mwisho wa safari.

Walipokumbuka hilo, mmoja wa watekaji hao alimfuata Kepteni Mazula na kumtaka awapatie bastola hiyo. Mmoja wao, Mussa Memba alipoipokea alionekana kubabaika kidogo kana kwamba hakuwa na ujuzi wowote wa namna ya kuitumia silaha hiyo.
Alipokuwa amejikunja upande mmoja wa chumba cha rubani akiishika shika bastola hiyo, pengine akiishangaa au kuichunguza, ghafla risasi ilifyatuka. Risasi iliyofyatuka iliuparaza mgongo wa Oscar Mwamaja, rubani msaidizi wa Kepteni Mazula na kumjeruhi.

Baada ya kujaza mafuta kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mfalme Abdulaziz mjini Jeddah, kituo cha tatu kilikuwa ni Athens, Ugiriki. Pamoja na maombi mengi ya Serikali ya Tanzania ya kutaka ndege hiyo ishikiliwe ili isiondoke, maofisa wa Serikali ya Ugiriki walitangaza mapema kabisa, hata kabla Boeing 737 haijatua, kwamba ingeruhusiwa tu kujaza mafuta na kuondoka mara moja bila kuikawiza.
4
Baada ya Serikali ya Uingereza kupata habari kuwa ndege iliyotekwa ya Shirika la Tanzania (ATC) ingewasili Uwanja wa Stansted, waliuzingira kukabiliana na watekaji. Mara baada ya ndege kutua, magari matano yakiwa yamesheheni polisi yalifika na kuizingira ndege hiyo. Muda mfupi baadaye taa zote za uwanjani zilizimwa na magari ya kuzima moto yakaizingira ndege hiyo.

Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Anthony Balthazar Nyaki alifika uwanjani hapo, ingawa alichelewa.

Vijana walioteka ndege hiyo ni Mussa Memba (25), Mohamed Ali Abdallah (26) na nduguye Abdallah Ali Abdallah (22), Mohamed Tahir Ahmed (21) na Yassin Memba (21).

Balozi Nyaki alikuwa ameteuliwa mwaka uliopita (1981) kuwa balozi wa Tanzania nchini Uingereza kuchukua nafasi ya Amon James Nsekela aliyeishikilia nafasi hiyo kuanzia mwaka 1974.

Baadaye kidogo Balozi Nyaki alijitokeza kukabiliana na watekaji. Huu ukawa ni mchezo wa ama kuelewana au kutoelewana kati ya mwanadiplomasia na watekaji nyara waliotaka Rais wa nchi yao ajiuzulu.

Balozi Nyaki aliwasili Stansted saa 1:33 usiku (saa za Afrika Mashariki) ikiwa ni muda wa saa tano baada ya ndege hiyo kutua. Hata hivyo hakuonekana kuwa na wasiwasi.

Katika hali ya haraka kidogo na kumkasirikia balozi, watekaji walitaka kujua sababu za Balozi Nyaki kuchelewa kufika uwanjani hapo wakati ujumbe wao wa kumtaka afike uwanjani ulitumwa saa kadhaa zilizokuwa zimepita. Kwa kuwa walichukulia kuwa wamedharauliwa, hasira zao zilipanda hata zaidi.

Kwa utulivu, Balozi Nyaki aliwaelewesha kuwa yeye kama mtu aliyepata heshima ya kuwa mwakilishi wa Serikali ya Tanzania nchini Uingereza, angeweza tu kufanya kazi kwa kutegemea mawasiliano anayopewa na mwenyeji wake—yaani Serikali ya Uingereza. Aliwaambia kuwa angekwenda uwanjani hapo ikiwa tu angehitajika kufanya hivyo, na wala si kujiendea tu kwa matakwa yake yeye mwenyewe.

“Kambona yuko wapi?” walimuuliza.
“Sijui aliko,” aliwajibu.
“Inawezekanaje hujui?” waliuliza.
“Waingereza waliompa hifadhi ndio wanajua aliko,” alijibu kwa utulivu.

Waliposisitiza kwamba Kambona aletwe ili waweze kuonana naye, halafu wapatiwe maji, chakula na mafuta kwa ajili ya ndege. Kwa utaratibu kabisa Balozi Nyaki aliwajibu kwamba “mambo yote hayo mnayoyataka yako nje ya uwezo wangu”.

Lakini hayo yote—maji, chakula na mafuta ya ndege—yalikuwa ni matakwa madogo. Kuonana na Kambona na kupewa maji, chakula na mafuta kwa ajili ya ndege yao yalikuwa ni madai madogo. Hadi wakati huo, watekaji hawakuwa wametoa dai lao kubwa zaidi; Nyerere ajiuzulu.

Hatimaye likaja lile dai kubwa kuliko yote waliyokuwa nayo. Hilo ndilo lilikuwa shabaha yao. Ni lile dai ambalo wanasiasa wa Tanzania hawakutaka lijulikane. Dai hilo lilikuwa jambo zito kwa balozi yeyote—hasa kwa balozi wa Tanzania.

“Ni lazima Rais Julius Nyerere ajiuzulu,” walisema watekaji hao.

Balozi Nyaki hakuwa na haraka ya kuuliza wala kujibu maswali yao. Huenda tayari alikuwa amekwishapata fununu ya madai yao. Kwa hiyo hakuonekana kushtuka sana dai hilo lilipotajwa. Walipoona anakawia kuwajibu, walirudia dai lao: “Tunataka Nyerere ajiuzulu.”

“Mko wangapi ambao mnadai jambo hili?” aliwauliza.

“Elfu tatu (3,000),” walijibu.

“Watu elfu tatu?” alihoji Balozi Nyaki.

“Yaani watu 3,000 mnataka ajiuzulu mtu aliyechaguliwa na mamilioni ya watu?”

Mjadala huo ulielemea upande wa Balozi Nyaki. Balozi alijua kwa hakika kuwa hatimaye angekuwa mshindi wa mjadala huo. Kwa hiyo hakufanya haraka. Aliwasubiri waulize maswali zaidi ili naye apate wasaa wa kujibu yote ambayo wangeuliza. Alijua kuwa kama hangewasikiliza na kujibu maswali yao, wao pia hawangemsikiliza na kujibu maswali yake.

Kwa kutumia uzoefu wake wa kidiplomasia, alitambua kuwa alihitaji nafasi ya kutosha ya kuwauliza maswali, lakini ili watekaji hao wampe nafasi hiyo, ilikuwa ni lazima kwanza yeye aanze kwa kuwapa nafasi hiyo.

Baada ya mjadala kuendelea kwa kitambo fulani, watekaji walilainika na kuonekana kuwa wamekosa hoja za kumjibu Balozi Nyaki. Mmoja wao akasikika akinung’unika: “Ah! Nyie ndio wakubwa bwana!”

Pamoja na kuzidiwa na hoja za Balozi Nyaki, watekaji hao hawakutaka kujisalimisha. Badala yake walimwomba Balozi Nyaki awasaidie waweze kukutana na Oscar Kambona, ambaye aliwahi kuwa waziri wa tawala za mikoa wa Tanzania na pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Peter Alexander Rupert Carington.

Balozi Nyaki, kwa kutumia uwezo ule ule wa kidiplomasia, aliwajibu kuwa ili kutekeleza hilo atalazimika kwanza kuomba ushauri kabla hajafikiria kulitekeleza. Walipotaka kujua itamchukua muda gani kuomba ushauri hadi kulitekeleza, Balozi Nyaki aliwajibu: “Sijui.”
Hata hivyo, hawakujisalimisha.

Mwanadamu pekee ambaye sasa walitaka kumwona kuliko mwingine yeyote duniani alikuwa Kambona. Pamoja na kwamba walikuwa na njaa na kiu, ilionekana kana kwamba Kambona alikuwa muhimu kwao kwa wakati huo kuliko mahitaji hayo.

Ilihisiwa kwamba mtu aliyekuwa nyuma ya mambo yote hayo ni Kambona. Hata hivyo, Kambona alijitokeza mwishoni mwa mambo yote yaliyotendeka kwenye Uwanja wa Ndege wa Stansted.
5
Baada ya kuelemewa na hoja za Balozi Nyaki, mtu pekee ambaye walitaka kuonana naye alikuwa Oscar Kambona ambaye wengi walihisi kuwa alikuwa nyuma ya mambo yote hayo. Kambona alijitokeza mwishoni mwa mambo yote yaliyotendeka kwenye Uwanja wa Ndege wa Stansted.

Alipoulizwa sababu za kukawia kufika uwanjani hapo kuzungumza na waliotamani sana kumuona, Kambona alisema alilazimika kufanya hivyo kwa makusudi kabisa ili atoe nafasi kwa Balozi Nyaki afanye kazi yake.

Madai yaliyokuja kutolewa baadaye kwamba Kambona hakuwa Uingereza, bali alikuwa Nairobi, Kenya, wakati tukio hilo linafanyika hayajawahi kuthibitika. Ilidaiwa kuwa alikuwa Nairobi ili ilingane na madai kwamba alihusika na utekaji huo na ndiyo sababu ya ndege kulazimishwa na watekaji kwenda Nairobi.

Waandishi wa habari za uchunguzi waliofuatilia sana jambo hilo walisema orodha za abiria walioingia na kuondoka kwa ndege kutoka viwanja vya Kenya kabla na baada ya utekaji huo kufanyika, haikuonyesha kama Kambona alikuwa mmoja wa abiria hao.

Habari zilizochapishwa na jarida The Statesman la Uingereza zilidai kuwa wakati hayo yakitokea, Kambona alikuwa katika hospitali inayojulikana kwa jina la Royal Surrey ya jijini London.

Alipohojiwa baadaye, Kambona aliliambia jarida la Africa Now la Aprili, 1982 hakupenda kuhusishwa na tukio hilo.

“Ninaumia sana moyoni ninapohusishwa na watu hawa (wateka nyara),” alisema.

Alisema kama ambavyo hakuwahi kuwajua wala kukutana na watekaji hao, hakujua hata kilichokuwa kimetokea na kwamba alipata habari za kutekwa kwa ndege ya Tanzania sawasawa na namna ambayo mtu mwingine yeyote alivyozipata.

“Kwa kuyatafakari yote haya, hili linaonekana kuwa ni matendo ya mwanadamu na kudra za Mwenyezi Mungu ambaye kwake mimi nasali sana. Hakuna damu itakayomwagika,” alisema.

Hakufafanua kauli hiyo na wala hakuna aliyejaribu kuitolea ufafanuzi. Pengine Kambona alijua kitu ambacho wengine hawakukijua na hakutaka wakijue. Kwake yeye, matukio hayo ni “matendo ya mwanadamu na kudra za Mwenyezi Mungu”.

Inaelekea watekaji walikuwa tayari kufanya lolote ikiwa Kambona hangefika uwanjani hapo kusema nao. Haijulikani wangefanya jambo gani katika ardhi ya kigeni kama Uingereza ambayo tayari macho na masikio yote ya nchi hiyo na usalama wake yalikuwa yameelekezwa kwao na mahali walipokuwa kwa wakati huo.

Baada ya kusikia hivyo, Kambona alikwenda uwanjani hapo kuongea nao. Alizungumza nao. Kupitia vifaa vya mawasiliano vya uwanja huo, sauti ya Kambona ilisikika kwao. Nao waliitambua. Alipowaona aliwapungia kwa mikono yake miwili, nao walipomwona wakampungia, kisha wakajisalimisha.

Katika taarifa aliyoitoa baadaye, Kambona alisema alielewa ni “kitu gani kiliwachochea vijana hawa”.

Alisema walichochewa na hali mbaya ya kisiasa na ya kiuchumi iliyoko Tanzania hata wakafanya “kile tunachofikiri ni matendo ya kichaa, lakini walichoona kwa macho yao ni njia pekee ya kuuvuta ulimwengu kuitazama kuitazama hali ya watu wetu”.

Kwa kiasi fulani, Kambona alionekana ni mshindi aliyemaliza mbio za watekaji.

Baada ya mateka kuachiwa huru kutoka mikononi mwa watekaji wale, maofisa wa Tanzania waliendelea kusisitiza kwamba utekaji huo haukuwa na shabaha yoyote ya kisiasa wala dalili ya watu kutoridhika na hali ya maisha nchini Tanzania.

Wakati maofisa wa Serikali wakitoa madai hayo, wengine waliojiita ‘vijana wa harakati za mapinduzi’ walishambulia tena. Hali ya mambo ilianza kuwatatanisha hata wasafiri wa anga.

Ndani ya ndege nyingine ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) ambayo nayo ni Boeing 737, lakini yenye jina la Serengeti ubavuni, tofauti na iliyotekwa Mwanza ikaishia Uingereza ambayo ni Boeing 737 yenye jina la Kilimanjaro ubavuni, nayo ilikumbwa na zahama.

Katika ndege hiyo, Serengeti, iliyokuwa inakaribia kupaa angani kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanyaro (KIA) kuelekea Dar es Salaam, msichana mwenye asili ya Kiitaliano mwenye umri wa miaka 10 alikuta barua moja iliyobandikwa kwenye sinia la kusambazia vyakula mbele ya kiti chake.

Barua hiyo ilitiwa saini na vijana hao wa harakati za mapinduzi, ilieleza kuwa watekaji nyara hawajakamilisha lengo lao, ikiwa kama marejeo ya kushinidwa kwao kumlazimisha Mwalimu Julius Nyerere ajiuzulu. Barua hiyo ilisema kulikuwa na bomu ndani ya ndege hiyo. Lakini baadaye iligundulika kuwa hakukuwapo na bomu.

Habari hiyo ilichapishwa pia kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti la Uhuru la Alhamisi ya Machi 4, 1982.
6
Katika viwanja vya ndege vya Nairobi na Jeddah, Saudi Arabia ndege hiyo iliruhusiwa kutua, kujaza mafuta na kuondoka.

Kabla ya ndege hiyo kupelekwa Uingereza na kuamriwa kutua Uwanja wa Ndege wa Stansted badala ya Heathrow, ilikuwa imeweka kituo chake cha tatu jijini Athens, Ugiriki.

Baada ya kujaza mafuta kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mfalme Abdulaziz mjini Jeddah, kituo cha tatu kilikuwa Athens. Pamoja na maombi mengi ya Serikali ya Tanzania ya kutaka ndege hiyo izuiwe kuondoka, maofisa wa Ugiriki walitangaza mapema kabisa, hata kabla Boeing 737 haijatua, kwamba ingeruhusiwa tu kujaza mafuta na kuondoka mara moja bila kuikawiza.

Ikiwa imetua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Athens, aliletwa daktari mmoja ambaye aliingia kwenye ndege hiyo kwa kusudi la kutibu jeraha la risasi alilopata Oscar Mwamaja, rubani msaidizi wa Kepteni Deo Mazula. Daktari huyo alipoingia ndani, mmoja wa watekaji alimuuliza: “Mapinduzi hayajaanza huko Dar es Salaam au bado?”

Hata hivyo, pamoja na kwamba hawakuelewana vizuri katika lugha, daktari huyo hakuweza kumjibu kwa sababu alishangaa kuulizwa maswali yanayohusu siasa za Tanzania. Mtekaji huyo alidhani kuwa Watanzania ni watu ambao walikuwa wameudhika sana kiasi kwamba tukio moja kama hilo la kuteka ndege lingeweza kusababisha maasi ya jumla.

Baada ya kutibu jeraha la Mwamaja, daktari huyo alishuka kisha akawaambia maofisa wa uwanja hapo kuwa ndani ya ndege hakuona kielelezo chochote kilichoashiria kwamba kuna mtu mwingine aliyejeruhiwa—iwe kwa risasi au kwa silaha nyingine yoyote—isipokuwa rubani Mwamaja.

Kabla ya kuondoka Athens, watekaji walimwachia mtu mmoja aliyedaiwa kuwa alikuwa ni dereva wa lori mwenye asili ya Kisomali na kasisi mmoja wa Ubelgiji. Waliwaachia wawili hao kwa kile walichodai kuwa wao “si raia wa Tanzania”. Kisha wakaomba wapatiwe ramani ya anga lote la Ulaya.

Wakati mmoja, watekaji hao aliwaambia abiria kuwa wangewapeleka “kwa Kanali Gaddafi (Libya)”. Lakini ndege ilipoondoka Athens, watekaji walianza kuzungumza habari za Oscar Kambona (54) ambaye kwa wakati huo alikuwa akiishi uhamishoni Uingereza.

Kambona aliwahi kuwa waziri katika Serikali ya Tanzania kabla ya kukimbia nchi mwaka 1967 baada ya kushindwa kuelewana na Rais Nyerere katika siasa za Ujamaa na Kujitegemea.

Wakisukumwa na hamu ya kukutana na Oscar Kambona na ‘kuratibu’ mpango wa kumuandaa arejee Tanzania kuchukua nafasi ya urais badala ya Mwalimu Nyerere, watekaji hao waliiamuru ndege ipelekwe London, Uingereza.

Tangu mapema kabisa Serikali ya Uingereza ilikuwa imepata taarifa za kutekwa kwa ndege hiyo, lakini haikujua kuwa ingepelekwa huko. Kwa hiyo baada ya maofisa kujua kuwa ndege hiyo sasa ilikuwa ikielekea Uingereza, serikali ilielekeza itue Uwanja wa Stansted, nje kidogo ya jiji la London.

Kamati ya watu 35 ya maofisa wa Uingereza ya kushughulikia tatizo kama hilo la utekaji iliingia kazini mara moja kufanya kazi yake. Kamati hiyo ilifanya kikao chake cha dharura na cha haraka kilichokuwa chini ya uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, William Stephen Ian Whitelaw, na kuwajumuisha maofisa kadhaa wa usalama, mkuu wa polisi wa Jimbo la Essex, Peter Simpson akiwa miongoni mwao. Uwanja huo uko jimbo la Essex.

Uwanjani zilikuwapo ndege kadhaa na magari ya kubeba wagonjwa yakiwa na maofisa wa afya waliokuwa tayari kwa lolote. Yaliegeshwa kando ya eneo ambalo ndege ya Tanzania ingetua, huku vinasa sauti vikiwa vimewekwa mahali maalumu.

Askari wa kikosi cha watu wapatao 80 waliokakamaa na waliovalia kofia maalumu na nguo zisizopenya risasi, walijificha uwanjani hapo wakiwa na kazi ya kutazama na kusubiri kitakachotokea.

Hawa walikuwa ni askari wa kikosi maalumu cha huduma za anga chenye makao yake makuu katika mji wa Hereford. Walikuwa na silaha mbalimbali, zikiwamo SMG (sub-machine guns) na mabomu ya kutupwa kwa mkono.

Mara baada ya ndege kutua, magari matano yakiwa yamesheheni polisi yalifika na kuizingira ndege hiyo. Muda mfupi baadaye taa zote za Uwanja wa Ndege wa Stansted zilizimwa. Magari ya kuzima moto nayo yaliletwa kuizingira ndege hiyo.
Dakika chache baadaye alitumwa ‘mwanasaikolojia’ mmoja kwenda kuzungumza na watekaji hao.

Mwanasaikolojia huyo ambaye alitambulika kwa jina moja tu la Mike, alikuwa akizungumza kama mtu wa kati baina ya watekaji na maofisa wa Serikali ya Uingereza. kazi yake kubwa ilikuwa ni kuwachunguza, kuwashawishi na kuwalainisha.

Magari yote yaliyokuwa yameegeshwa karibu na eneo la ndege hiyo, yaliondolewa kwa tahadhari dhidi ya lolote lisilotazamiwa. Ilionekana kana kwamba hata watekaji walikuwa wamejiandaa kwa hali hiyo.

Wakati hali ya Uwanja wa Stansted ikiwa ni ya wasiwasi baada ya kuonekana kuwa watekaji hawaambiliki, balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Anthony Balthazar Nyaki alionyesha kuwa anao uwezo wa kukabiliana na watekaji hao. Lakini alichelewa sana kufika uwanjani hapo.
7
Baada ya maandalizi yote ya usalama na ndege kutua Uwanja wa Stansted, watekaji walianza kuzungumza na balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Anthony Nyaki.

Kama ilivyoelezwa awali, kwa kutumia umahiri wake wa kidiplomasia, Balozi Nyaki aliwazidi hoja watekaji ambao waliamua kumuomba awawezeshe kuongea na aliyekuwa waziri aliyehusika na tawala za mikoa, Oscar Kambona na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Peter Alexander Rupert Carington.

Lakini uzito wa hoja za Balozi Nyaki uliwafanya waone kimbilio pekee lilikuwa ni Kambona, ambaye alipoongea nao hakutaka kuonekana alihusika na utekaji huo na ndipo vijana hao watano walipojisalimisha.

Vijana walioteka ndege hiyo walikuwa Mussa Memba, aliyekuwa na umri wa miaka 25, Mohamed Ali Abdallah (26) na nduguye Abdallah Ali Abdallah (22), Mohamed Tahir Ahmed (21) na Yassin Memba (21).

Baadaye kulitokea taarifa mbili za kutegwa mabomu kwenye ndege mbili za ATC, ambazo zilionekana hazikuwa za kweli, na wala hazikuwa na uhusiano wowote na utekaji wa ndege aina ya Boeing 737 uliofanyika Februari 26, 1982.

Hata hivyo, kilichoonekana dhahiri ni kuwa matukio hayo mawili yalitokea katika muda usiozidi kipindi cha mwezi mmoja na yaliyofanana, yalihusu siasa.

Ingawa maofisa wa Serikali waliendelea kusisitiza kuwa yalifanywa na wahuni, maofisa wa usalama pamoja na polisi waliwekwa katika hali ya tahadhari muda wote.

Madai ya kwamba vijana walioteka ndege hiyo walikuwa wahuni yaliendelezwa na baadhi ya vyombo vya habari vya ndani. Vyombo vya habari vya nje havikulichukulia jambo hilo kijuu-juu.

“Vijana hao walikuwa wakionekana wakizurura mjini Dar es Salaam bila kazi, na inawezekana walikuwa wavuta bangi,” liliandika gazeti la Uhuru toleo Na. 5835.

Gazeti hilo lilimkariri mtu mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe, akisema: “Vijana hawa walikuwa wakirandaranda hapa Kariakoo na jinsi walivyokuwa wakizungumza maneno ya ovyo, tuliwachukulia kuwa ni wavuta bangi.”

Mtu mwingine ambaye naye hakutaka jina lake litajwe gazetini, aliliambia gazeti hilo akisema: “Baadhi ya vijana hao walikuwa wakionekana mara kwa mara katika eneo la Magomeni ... lakini walitoweka wiki chache zilizopita.”

Ingawa mambo yalionekana kuwa kimya, upelelezi wa hali ya juu ulifanyika kutafuta ni kitu gani kilichokuwa nyuma ya mfululizo wa matukio yanayofanana katika kipindi kimoja.

Wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere alifikia uamuzi wa kutowarejesha nchini wale watekaji watano waliokuwa wanashikiliwa Uingereza ili washitakiwe na kuhukumiwa. Kama ilivyokuwa kawaida, mawazo yake aliyabeba mwenyewe kwa kuona kuwa ni busara wakasikika katika mahakama za nje ya Tanzania kuliko za Dar es Salaam.

Mwalimu Nyerere pia, kwa wakati huo, alianza kupatana na Waziri Mkuu wa Uingereza, Margaret Hilda Thatcher, kuliko wakati mwingine wowote uliotangulia na aliwahi kusema ni “kwa sababu ya utawala wake wa sheria”.

Kwa mujibu wa jarida la African Defence Journal, Rais Nyerere alimuomba balozi wa Uingereza mjini Dar es Salaam, Peter Moon kufikisha shukrani zake binafsi kwa Waingereza, hususan kwa Waziri Mkuu Thatcher, kwa kazi aliyoifanya ya kuwashughulikia ‘wahuni’ walioiteka ndege ya Tanzania.”

Kwa hakika huo utekaji wa aina yake ulikuwa ni wa tatu.

Kuhusika kwa Serikali ya Tanzania katika kuteka ndege kulianza mwaka 1972 wakati wakimbizi wa Uganda walioukimbia utawala wa Idi Amin, wakisaidiwa na Watanzania, walijaribu kumrejesha Dk Milton Obote madarakani.

Sehemu ya uvamizi huo, kwa mujibu wa jarida la Africa Contemporary Record ni kuchukua ndege iliyojaa ‘waasi’ ili itue Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe. Ili kufanya mpango huo uwezekane, maofisa wa Uwanja wa Dar es Salaam waliamriwa kufumba macho wakati rubani wa Uganda “akiiba” ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Mashariki kutoka uwanjani hapo.

Alhamisi ya Septemba 14, 1972, kwa mujibu wa ukurasa wa 47 wa kitabu cha Terrorism in Africa, ndege ya Shirika la Afrika Mashariki iliibwa usiku na rubani asiyejulikana kwenye Uwanja wa Dar es Salaam.

Baadaye ndege hiyo ilikutwa kwenye Uwanja wa Kilimanjaro ikiwa imepasuka matairi. Ndege hiyo ilitekwa kama ilivyokuwa imepangwa na watekaji hao, ikaondoka Dar es Salaam kuelekea Kilimanjaro ambako ingewabeba hao waliopangwa, lakini ikatua vibaya ikapasua matairi yake, na mpango wote ukaishia hapo.
Matukio ya utekaji ndege Tanzania:

Matukio ya kutekwa kwa ndege nchini yalianza mwaka 1972 wakati wakimbizi wa Uganda walioukimbia utawala wa Idi Amin, wakisaidiwa na Watanzania, walijaribu kumrejesha Dk Milton Obote madarakani.

Sehemu ya uvamizi huo, kwa mujibu wa jarida la Africa Contemporary Record, ni kuchukua ndege iliyojaa ‘waasi’ ili itue kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe. Ili mpango huo uwezekano, maofisa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam waliamriwa kufumba macho wakati rubani wa Uganda “akiiba” ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Mashariki kutoka uwanjani hapo.

Alhamisi ya Septemba 14, 1972, kwa mujibu wa ukurasa wa 47 wa kitabu cha Terrorism in Africa (Ugaidi barani Afrika), ndege ya Shirika la Afrika Mashariki iliibwa usiku na rubani asiyejulikana kutoka Dar es Salaam.

Baadaye ndege hiyo ilikutwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro ikiwa imepasuka matairi.

Mpango ulikuwa rubani huyo atue Uwanja wa Kilimanjaro kuwabeba waasi hao, lakini cha kushangaza alipokuwa akitua alisahau breki ya magurudumu ya ndege. Kwa sababu hiyo magurudumu hayo yakapasuka na mpango mzima nao ukaishia hapo. Wakati huo baadhi ya Waganda walioukimbia utawala wa Idi Amin walikuwa wakikutana mjini Moshi, Kilimanjaro kupanga mikakati ya kuuangusha utawala wa Amin. Kufikia mwaka 1979 zaidi ya vikundi 25 vya Waganda vilivyokuwa na lengo la kuikomboa nchi hiyo vilikuwa vimeshaundwa na vilikuwa vikikutana Moshi.

Hatimaye vikaibuka na kile kilichokuja kujulikana kama “Roho ya Moshi”. Utekaji wa ndege hiyo ulikuwa ni sehemu ya mikakati yao wakisaidiwa na Tanzania.

Utekaji wa pili ulifanywa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Na, jarida moja liliandika kuwa huenda huo ulikuwa ni utekaji wa kwanza wa kielektroniki kuwahi kutokea duniani.

Utekaji huo wa kielektroniki uliofanywa na JWTZ ulifanyika mwaka 1979 wakati vita ikiendelea kati ya Tanzania na Uganda. Wakati huo, ndege za mizigo za Libya zilikuwa zikifanya safari zake za usiku kumpelekea silaha Idi Amin. Mpango ulibuniwa jeshini kuziteka ndege hizo.

Usiku wa manane, wanajeshi wa JWTZ wakiwa Mwanza, walisubiri hadi walipoona kwenye rada ndege mojawapo ikielekea Entebbe, upande wa Uganda, karibu na Ziwa Victoria.

Waliwasiliana na rubani wa ndege hiyo na kujitambulisha kwake kwamba wao ni waongozaji wa ndege kwenye Uwanja wa Entebbe na kumuonya kuwa uwanja huo unashambuliwa vikali na wanajeshi na kwa hiyo isingefaa atue huko.

Wasiwasi mkubwa ulimpata rubani huyo kiasi kwamba alilazimika kuomba ushauri. Wanajeshi wa Tanzania wakamshauri kuwa uwanja wa ndege ulio karibu zaidi ni ule wa Mwanza na kwamba kwa sasa ni salama zaidi kutua.

Rubani alijaribu kuuliza maswali kadhaa alijibiwa kwa uangalifu. Majibu hayo, na jinsi yalivyotolewa, yalimridhisha rubani huyo. Kwa hiyo akaachana na uamuzi wake wa kwenda kutua Entebbe na akaamua kwenda Mwanza.

Mara baada ya ndege hiyo kutua Mwanza, ikazingirwa na wanajeshi wa Tanzania. Hata hivyo, walishangazwa kubaini kuwa ilikuwa ni ndege ya mizigo ya Shirika la Ubelgiji, Sabena, badala ya ndege ya Libya na iliyobeba silaha. Ndege hiyo ya Ubelgiji ilikuwa safarini kwenda Entebbe kubeba kahawa ili kuipeleka Djibout.

Kwa jinsi hali ilivyokuwa mbaya kutokana na kile kilichofanywa na Tanzania, Rais Julius Nyerere alilazimika kwenda ubalozi wa Ubelgiji kuomba radhi.

Tanzania na Uganda hawakuwa na uhusiano mzuri tangu Jumatatu ya Januari 25, 1971, siku ambayo Jenerali Idi Amin aliipindua Serikali ya Dk Milton Obote. Tangu wakati huo kulikuwa na harakati nyingi kwa upande wa Tanzania zilizokuwa na lengo la kumrejesha Dk Obote madarakani.

Wakati hayo yaliposhindikana, huku uhusiano kati ya Tanzania na Uganda ukizidi kuzorota, mwaka 1978, Rais Julius Nyerere alitangaza vita dhidi ya “Nduli Idi Amin” baada ya majeshi ya Uganda kuvamia Kagera.

Alhamisi ya Novemba 2, 1978, Mwalimu Julius Nyerere alilitangazia Taifa kuhusu “uvamizi wa Idi Amin na uamuzi wa Tanzania wa kumpiga.” Akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa Diamond Jubilee, Mwalimu Nyerere alielezea uamuzi huo wa Serikali.

“Nimewaombeni mkusanyike tena hapa (ili)niwaelezeni jambo ambalo kwa sasa wote mnalijua. Lakini naona si vibaya nikieleza. Nitajaribu kueleza kwa ufupi,” alisema Rais Nyerere.

“Huyu mtu ameivamia nchi yetu. Sasa hiyo ndiyo hali. Tufanye nini! Tunayo kazi moja tu. Watanzania sasa tunayo kazi moja tu—ni kumpiga.”
 
Kwenye siasa na historia ya nchi hii kumewahi kutokea mapinduzi ya kijeshi katika utawala wa awamu ya kwanza(JK NYERERE regime) yaliyojulikana kama TANGANYIKA RIFFLES ..Japo huwezi kukuta jambo hili likizingumzwa sana au kuwekwa katika historia ya nchi naomba kueleweshwa yafuatayo:

1)Nini kilikua chanzo cha mapinduzi haya na lengo lake lilikua ni nini??
2)Mapinduzi yalivyoshindikana wale wahaini walichukuliwa hatua gani??
3)Kwa nini historia ya hii nchi hailizungumzii suala hili kama inavyo vizungumzia vita vya kagera??
4)Nasikia NYERERE na KAWAWA walijificha kigamboni kwenye moja ya nyumba za raia wa kawaida mambo yalivyokua magumu je ni kweli??

Natanguliza shukrani.
 
ninachofahamu na kuchukia ni histori aya uongo ya hawa mashujaa wa jadi akina mkwawa,mirambo, kinjekitile, abushir and the sort.Hao mahaini ni shemu tuu t ahistoria ya nchi inayohitaji kuwekwa katk kumbukumbu na hata ikibidi wahojiwe rasmi hao watu waliobaki na famila zao ili iandikwe historia kabili kwa angle zote.
 
ninachofahamu na kuchukia ni histori aya uongo ya hawa mashujaa wa jadi akina mkwawa,mirambo, kinjekitile, abushir and the sort.Hao mahaini ni shemu tuu t ahistoria ya nchi inayohitaji kuwekwa katk kumbukumbu na hata ikibidi wahojiwe rasmi hao watu waliobaki na famila zao ili iandikwe historia kabili kwa angle zote.

Ni kweli mkuu maana siku moja nlikua IRINGA cha ajabu ni kuwa historia ya mtemi Mkwawa tunayoisoma kwenye vitabu inaonekana ni ya kupikwa sana si kile ambacho wenyeji wanakifahamu.

Mkwawa anaonekana kuwa alikuwa ni kiongozi aliyetumia diplomasia sana na uchawi sana kutaka kupata suluhu na wajerumani lakini tunaambiwa alikua shujaa aliyepambana na wajerumani mpaka dakika ya mwisho wakati ukweli ni kuwa aliwakimbia wajerumani kwa kutaka kujiokoa baada ya diplomasia na utabiri wa mganga wake wa kienyeji kuwa atawashinda wajerumani kushindwa.

Ninachojiuliza hapa je ni kweli kuwa historia ya nchi hii nyingi ni ya kupika??
kwa nini matukio mazito kama haya ya mapinduzi ya kijeshi hayatajwi katika historia ya hii nchi?
 
Japo historia haisemi wazi juu ya mambo mengi sana Tanganyika na Tanzania ya leo, lakini Mwalimu Nyerere tangu awe kiongozi wa nchi hii amenusurika mapinduzi MATATU,

Moja ni la mwaka 1964, lapili ni la mwaka 1970 na la mwisho ni la mwaka 1980 (Sina uhakika sawa na hiyo miaka)

Jaribio la kwanza ndilo lilipelekea kuundwa kwa JWTZ na lilizimwa kwamsaada wa Malkia wa Uingereza aliyetuma makomandoo maalumu na wakafanikiwa, Jaribio la pili ndilo lililopelekea kuundwa kwa Usalama wa Taifa na kikosi maalumu cha ulinzi wa Rais,

na jaribio la mwisho ndio lilipelekea kubadili sera ya usalama wa Taifa kwa kuwapandikiza kila kwenye sekta na kuwa kila mtu ni mlinzi wa nchi hii (usalama)

Sikumbuki vema lakwanza kama liliongozwa na nani lakini Kambona ndie alimficha Mwalimu, lapili sikumbuki vema, lakini la mwisho liliongozwa na baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha Anga cha Ukonga Banana,

Na mipango yao iliharibikia palepale Banana baa baada ya mmoja wao kulewa na kuanza kuongea hovyo hasa akisema yeye anataka cheo cha uwaziri mkuu!

Enzi hizo 1980+ mmoja wa makamanda wa usalama wa taifa aliyeongoza kuwadhibiti waasi hao ni Mabere Marandu,

Na alifanikiwa kuongoza oparesheni za kumsaka na kumuua mmoja wa makomandoo ambae alikuwa ameandaliwa rasmi kumuua Nyerere,

Mapambano yalikuwa ni makubwa kutoka airport hadi kinondoni ulipo ubalozi wa Marekani sasa ndipo walipofanikiwa kumuua!

Jambo la kuwashangaza waasi wale (wanajeshi) wote Mwalimu aliwaita ikulu,

akamwambia kiongozi wa mapinduzi yale (simkumbuki) kuwa

"Shika bunduki uniue wewe mwenyewe kwamkono wako ili uwe rais wa nchi hii"

jamaa aliomba radhi huku akitambaa kisha mwalimu akasema

"nimewasamehe wote"

na aliwapa vyeo na kazi, wengi walikwenda kuwa mabalozi wa Tz nchi za nje!

Sisi hapa tunasema kama porojo tu, lakini yapo mengi sana nyuma ya pazia!

Watawala wanahisi kuyataja ni kama kuharibu sifa ya Tanzania na wengine wanaona kama itaharibu sifa ya Mwalimu.

Mimi binafsi nafikiri kama yatasemwa hadharani yataongeza sifa ya Mwalimu Nyerere na utawala wa ccm ya kale!

Atakuwa ni kiongozi pekee barani afrika na duniani aliyenusurika majaribio matatu ya uasi,

Atakuwa ni kiongozi wa kwanza duniani kuwasamehe waasi kwa mda huohuo wa uasi (baada ya kuwakamata) na kuwapa kazi nyingine za kitaifa

Atakuwa ni kiongozi pekee duniani aliye ng'atuka kwa amani na kwenda kuishi kijiji tena bila hata ulinzi, akitembelea land rover ya shamba miaka mitano tu baada ya jaribio kali la mapinduzi ya Banana Ukonga!

Hizo zote zilikuwa ni sifa zake ambazo watawala wa leo kwa makusudi ama kwakujua au kutojua wamefifisha nyota ya mwana wa Afrika mbele ya uso wa mataifa!

Na kwakuwafahamisha tu ni kuwa mmoja ya wanajeshi hao walioasi ni Meja Gen Hans Popi yule mwenye Sams Super Store pale Mbezi Makonde!

Kwakifupi hayo ndiyo ninayafahamu,
 
wengi wao hao wana anga walikuwa ni makaka wa familia moja iliyokuwa exposed nje na kupat amafunzo haba kipindi hicho ya urubani,mmoja wapo walikuwa rubani wa Mzee mkubwa.

Tetesi aliponea bahati kwa vile naye alikuwa safairini na mzee huku akijidaia kuwa mtiifu sana,ila kaka zake walinyea lupango kwa siku kadhaa,Leaders Club pia ilikuwa ni sehemu mojawapo ya kukutana sijui ndio iliwafanya wagombee uongezi sana.

Siku walikuwa wakilewa walikuwa ndio siku ya mwisho ya kupanda kwa hivyo walikuwa wakifurahia kuwa kesho yake wataitwa majina mapya.

Tetesi pia ni kwamba wake zao nao walikuwa mashushu na laiyebahatika ni ya huyo mpenda sifa na uongozi alipopasua kila alipokuwa akilewa.
 
Yericko Nyerere,

asante sana mkuu kwa kinifungua macho... Huyu MABERE MARANDO aliyeendesha hii operation ndiye huyu huyu wa CHEDEMA?? au majina yamefanana?? Kuna tetesi pia kuwa mwalimu mambo yalipoenda kombo kutokana na kikosi cha anga kumgeuka aliamua kuomba msaada kwa majeshi ya UINGEREZA na within a minitu kuna midege ilikuja na kusafisha wasaliti wote msituni na hakuna hata mabaki yaliyopatikana...je ni keli au ni stori za vijiweni??
 
Imeandikwa sana na inasomwa sana tu. Na kulikuwa na thread hapahapa jamvini si siku nyingi iliyoeleza kwa kirefu sana. Search!
Ilikuwa ni mutiny na si mapinduzi.

Lugha yoyote itakayotumika bado usalama wataifa unahiataji kuwa na mpango wa de classify baadhi ya documents kadiri miaka inavyokwenda ili kueleimisha watu.Kwani baadhi yao wanakuja kuwa wanasiasa,wengine wanakwenda usalama ,jeshini etc sasa wanakwenda wakiwa mbumbuku sana hawana fact za karibu za kuwasaidia kufany aquick analysis ktk shughuli za kila siku au wanapokutana na watu wenye historia fulani na nchi yetu.

Pia hao raia watakuwa kuwa preamble ktk kustage espionage platform kupitia raia.Enzi ya mwalimu tuliweza,watanzania walikuwa wambea sana,hakuingia mgeni bila kipira kuingia mtaani na king`ora kubwa siku hiyo hiyo na huyo mtu kupotea.Nyamisi yale meldan rover+Peugeot 404....israeli wameweza sisi inatushinda nini?

Nilitegemea baad aya mwalimu kipindi ch amwinyi kingewapeleka watanzania mbalia zaidi kuacha kuwa wambea kwa kila mtu ila kupitia channels zilizoweka na mfumo wa nchi.

Sasa hivi pembe za tembe zinaondoka wageni wanapewa urais haraka kuliko hata mama anavyoingia labour na kutoak ana mtoto.
 
asante sana mkuu kwa kinifungua macho...
Huyu MABERE MARANDO aliyeendesha hii operation ndiye huyu huyu wa CHEDEMA?? au majina yamefanana??
Kuna tetesi pia kuwa mwalimu mambo yalipoenda kombo kutokana na kikosi cha anga kumgeuka aliamua kuomba msaada kwa majeshi ya UINGEREZA na within a minitu kuna midege ilikuja na kusafisha wasaliti wote msituni na hakuna hata mabaki yaliyopatikana...je ni keli au ni stori za vijiweni??

Ndio ni Mabere Marandu huyu wa Chadema,

Nigeria walisaidia sana kuja kuleta amani, tulitawaliwa karibu mwaka mmoja!

Wengi wa waasi walisamehewa, lakini makomando na baadhi waliuawa na wengine kupelekwa Gwantanamo ya Afrika, hicho ni kisiwa kidogo kinachomilikiwa na Tanzania kipo kata ya Zanzibar na Tanganyika,

Sina uhakika kama badoo kinatumika ama kinatumika kwa siri zaidi!
 
Kambona ndiye aliyemuokoa Nyerere kwa kumficha kwenye mapinduzi ya 1964.

Mtafiti wa masuala haya anaitwa Nestor Luanda, machapisho yake haya hapa:

nestor luanda mutiny - Google Search

Companero,
Si kweli kwamba Oscar ndiye aliyemwokoa na kumficha Mwalimu katika mapinduzi ya 1964. Huyu mtafiti amekosea. Nadhani Kawawa alikuwa na jukumu kubwa zaidi kumshawishi Mwalimu kujificha kuliko Kambona. Kambona hakujua alipofichwa Mwalimu.
 
Companero,
Si kweli kwamba Oscar ndiye aliyemwokoa na kumficha Mwalimu katika mapinduzi ya 1964. Huyu mtafiti amekosea. Nadhani Kawawa alikuwa na jukumu kubwa zaidi kumshawishi Mwalimu kujificha kuliko Kambona. Kambona hakujua alipofichwa Mwalimu.

Kuasi kule kwa Wanajeshi Januari/20/1964 (Tanganyika Rifles) wala sio jambo la zamani sana kiasi cha kusema kwamba Historia ile imetupwa na hakuna anayesema ukweli,nilikuwa nahisi Viongozi kama Mwalimu,kawawa na Kambona wangeyaweka katika maandishi mambo yale muhimu ktk Historia ya Nchi yetu kabla hawajatutoka.Hakuna mahali mambo haya yameandikwa na ndio maana Vijana wanaotaka kujua historia ya Nchi yao wanakuja na hizi hear/say

Askari wale wa Tanganyika Rifles waliasi...Miongoni mwa mambo waliyokuwa wanadai ni hali nzuri ya maisha ya askari mtanganyika,mshahara ulikuwa mdogo,hawakupandishwa vyeo na hakukuwa na Watanganyika katika vyeo vya juu ndani ya Jeshi lile.Askari waliasi na kuingia mjini,na wengine walikwenda kwenye Makazi ya Maafisa wa kiingereza (Raia) na kuwashikilia.Waziri wa Ulinzi wakati huo alikuwa Oscar Kambona....Mwalimu na Mzee Kawawa kwa usalama wao walitoroshwa na kwenda kujificha,inasemekana Maficho yao yalikuwa Kigamboni.Waziri wa Ulinzi (Kambona) alijaribu kupita ktk Barracks na kuwaomba askari watulie bila mafanikio.

Hali ile iliendelea kuwa mbaya,na Mwalimu kwa ushauri wa Kambona na Kawawa akaomba msaada kwa Uingereza ili waje waokoe hali ile ambayo ilikuwa inaelekea kuwa mbaya,kufuatia kuasi kwa Askari wetu,askari wa Kenya na Uganda nao waliasi kwa sababu sawa kabisa na za UASI wa Tanganyika Rifles.Malkia alituma kikosi maalumu cha Askari wa Uingereza ambao walikuwepo ktk ghuba ya Aden,Askari hao walikuja na Meli kubwa ya kivita HMS Centaur ambayo ilikuwa na Makomandoo (45 RM),askari na helikopta.Walifanikiwa kutuliza maasi yale,na Mwalimu na Kawawa wakatoka mafichoni na kuonekana hadharani wakiwa na Waziri wa Ulinzi,ambaye alifanya kazi kubwa bila mafanikio kuwaomba askari(Waliokuwa wananuheshimu sana) waache uasi na madai yao yatafanyiwa kazi.Ukitaka kupata mambo mengi kuhusu maasi yale pitia kitabu "Dar Mutiny Of 1964" by Christopher MacRae
 
Back
Top Bottom