Kesi ya Tundu Lissu live toka Singida

Nilifikiri Bwana Njau ana akili lakini kwa jinsi hii kesi inayofumuka nalazimika kwa mara nyingine tena kuwashukuru wananchi wa Singida kwa kumchagua Lissu. Ni watu aina ya Lissu ndio wanastahili kuitwa WAHESHIMIWA. Na kama Mheshimiwa Lissu anasoma hapa basi nakuomba uwaogeshe na maji maridi hao vilaza wa ccm na ukiweza zima machine ya oxygen tumalize haya mashauri once and for all.
 
Nilifikiri Bwana Njau ana akili lakini kwa jinsi hii kesi inayofumuka nalazimika kwa mara nyingine tena kuwashukuru wananchi wa Singida kwa kumchagua Lissu. Ni watu aina ya Lissu ndio wanastahili kuitwa WAHESHIMIWA. Na kama Mheshimiwa Lissu anasoma hapa basi nakuomba uwaogeshe na maji maridi hao vilaza wa ccm na ukiweza zima machine ya oxygen tumalize haya mashauri once and for all.

Nimeipenda hii FMJ "Ukiweza zima machine ya Oxygen".
Nilizani nimechoka mimi tu kumbe nina afadhali
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mwenendo wa kesi unaendelea, shahidi anayelalamika kuwa CHADEMA waliweka mawakala wengi, wakiwemo wa vyama vingine, kumejitokeza barua za mawasiliano kati ya John Chiligati kumtaka Augustino Mrema, awaunge mkono kupinga Tundu Lissu. Na kwa barua zinazosomwa hapa Mahakamani zinaonyesha kuna ushirikiano rasmi kati ya CCM na TLP.


Lissu amesimama kuweka pingamizi , kuwa Hamadi Tau ndo alipaswa kuileta hii barua, anatoa sababu kwa kumsomea jaji Kifungu cha 34(3)iii, sheria ya ushahidi

Kweli CCM ni janga la Taifa! eti Chiligati anaandika barua kuunga mkono TLP dhidi ya tundu lissu?

Naomba hii kesi iendelee muda kidoogo ili tufaidi jinsi Tundu Lissu anavyowasambaratisha hao Mbwiga!
 
Nimezipenda sana hizi scripts. I wish tungekuwa tunapata za kesi zote ili angalau na sisi tujenge kauzoefu kidogo ka mambo ya mahakamani. Thanks sana mkuu kwa kazi hii nzuri. Tunamtakia ushindi mnono TL katika hii kesi.

Hukumu ya kesi kupinga ubunge Sumbawanga mjini
Kesi ya uchaguzi ya kupinga kutangazwa kwa ndg Aeshi Hiraly CCM kuwa mbunge wa Sumbawanga mjini leo mashahidi wa pande zote mbili wamehitimisha kutoa ushahidi wao mbele ya jaji wa mahakama kuu mh Jaji`Bethuel Mpakani Kasefu Mmilla “J.4”(Judge incharge mahakama kuu Mbeya). Kesi hiyo inasikilizwa katika mahakama kuu mjini Sumbawanga, ambapo hoja za msingi zilizokuwa zikisikilizwa ni, moja, mchakato mzima wa uchaguzi kugubikwa na rushwa iliokuwa ukitolewa na mgombea wa CCM na pili ni uchakachuzi wa matokeo uliopelekea kutangazwa kwa bw Aeshi. Katika kesi hiyo iliyofunguliwa na bw Noberth Yamsebo aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA (mlalamikaji) anayetetewa na wakili mmoja toka mbeya na upande wa washitakiwa unatetewa na mawakili wanne. Kesi hiyo ilianza kusikilizwa rasmi tangu tarehe 27/03/2012 na leo tarehe 14/03/2012 ndio mashahidi wote wamemaliza kutoa ushahidi wao, upande wa mlalamikaji ulikuwa na mashahidi 25 na upande washitakiwa ulikuwa na mashahidi wanne tu ambao wawili kati yao “ bw Vitusi Silago mchambuzi wa mifumo manispaa ya Sumbawanga na bi Silvia Siriwa aliyekuwa mkurugenzi wa manispaa na msimamizi mkuu wa uchaguzi wa jimbo la sumbawanga mjini” (kwa sasa yuko halmashauri ya wilaya ya Ileje kama mkurugenzi) ndo wamefunga pazia la mashahidi. Vielelezo mbalimbali vilitolewa upande wa mlalamikaji na mashahidi kama ushahidi kuihakikishia mahakama kutilia manani hoja za msingi za kesi hii, moja kati ya vielelezo hivyo ni fomu mbalimbali zilizotumika kujaza, kujumlishia na kutangazia matokeo ya ubunge ambazo zilitumiwa kuchakachulia matokeo, mashahidi upande wa mlalamikaji walitoa ushahidi wao dhidi ya mgombea wa CCM ukiwepo wa kununuliwa pombe, kununuliwa baiskeli, kupewa fedha cash, ununuzi wa shahada za kupigia kura, ununuzi wa vinanda “keyboard” kwa ajili ya kwaya za makanisa mbalimbali na kuwa vyote hivyo vilitolewa kwa mashariti ya kumpigia kura mgombea wa CCM bw Aeshi. Leo mara baada ya wakili mojawapo toka wa upande washitakiwa kuiambia mahakama kuwa mashahidi toka upande wake wameisha, alisimama wakili upande wa mlalamikaji na kuomba kuwa kwakuwa kesi inaelekea mwisho basi itolewe fursa kuandaliwa majumuisho ya kesi, hoja iliyoungwa mkono na upande wa mshitakiwa, hatimaye katika kuitekeleza hoja hii, upande wa walalamikaji waliihakikishia mahakama kuu kuwasilisha majumuisho yao tarehe 26/03/2012 na washitakiwa wakaahidi kupeleka tarehe 10/04/2012, na mwisho kabisa mh jaji Bethuel Mpakani Kasefu Mmilla akahitimisha mjadala kwa kusema kuwa hukumu ya kesi hii itakuwa tarehe 30/04/2012, na ndo ukawa mwisho wa shughuli za leo kuhusiana na kesi hiyo ya uchaguzi wa Sumbawanga mjini. Katika hatua nyingine, waandishi wa habari walioko Sumbawanga na mkoa wa Rukwa kwa ujumla wamekuwa wakilalamikiwa kwa kutekwa na bw Aesh kwa kutoripoti matukio mbalimbali yanayotokea katika mwendelezo wa kesi hii tangu ianze kwani kwa kiasi kikubwa kumekuwa kukitolewa ushahidi ambao kwa kiasi kikubwa ni udhalilishaji wa bw Aeshi, moja kati ya viongozi waandamizi wa klub ya waandishi wa habari mkoa wa Rukwa alipoulizwa kuhusu hili alijibu kwa madaha kuwa “waandishi tunaangalia matukio yenye maslahi” na kusema kuwa hawajaahidiwa chochote na yeyote na kuwa wao wansubiria hukumu. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI SUMBAWANGA ILI HAKI ITENDEKE. AMINA. Nikiripoti moja kwa moja toka mahakama kuu kanda ya Sumbawanga PTZ​
 
Huu ni mkakati mchafu wa CCM wa kuwaondoa wabunge mahiri wa CDM.Shame on you CCM.Hata pamoja na ushenzi huu,your days are numbered.
Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi katika jimbo la Singida Mashariki, inaendelea katika Mahakama Kuu- Mkoani Singida. Wafuasi wa Chadema pamoja na wafuasi wa CCM wamejaa mahakamani kusikiliza kesi, na shahidi wa kwanza anahojiwa sasa, Mama huyu anayeitwa Sophia, ambaye ni shahidi anasema hakumbuki baadhi ya tuhuma. Lissu anasimama kuanza kuhoji, nitaendelea kuwaletea
 
Back
Top Bottom