Kesi ya serikali dhidi ya dkt Namala Mkopi

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya kudharau amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi inayomkabili Rais wa Chama cha Madaktari nchini (MAT), Dkt. Namala Mkopi, Septemba 26, 2012 ulimsomea maelezo ya awali mshitakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka mbele ya Hakimu Mkazi, Faisal Kahamba aliikumbusha mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya upande wa Jamhuri kumsomea maelezo ya awali mshitakiwa huyo anayekabiliwa na makosa mawili ya kudharau amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi kinyume na kifungu cha 124 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, na kosa la pili ni kuwashawishi madaktari wagome.

Wakili Kweka alianza kumsomea maelezo ya awali mshitakiwa huyo na kudai kuwa Dkt. Mkopi, ni daktari wa binadamu aliyeajiliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili.

Alidai kuwa Dkt. Mkopi ni mwanachama wa MAT, chama ambacho kimeanzishwa na madaktari ambacho pia kinaishauri serikali katika mambo ya afya na utabibu na kusimamia na kulinda maadili ya wanachama wake.

Kwamba mwaka 2011 mshitakiwa huyo alichaguliwa kuwa rais wa chama hicho.

“Juni 2012 madaktari wanaofanya kazi katika hospitali za serikali waliingia kwenye mgomo dhidi ya mwajiri wao ambaye ni serikali na mgomo huo uliandaliwa na MAT na madaktari hao waligoma kuwahudumia wagonjwa wakati wakati mkataba wao wa ajira waliongia na serikali ni kuwatibia wagonjwa” alidai Kweka.

Wakili Kweka alidai kuwa wakati mgomo huo ukiendelea, serikali ilipeleka maombi No.73 ya mwaka 2012 katika Mahakama Kuu Diveshini ya Kazi yaliyokuwa yakiomba mahakama hiyo itoe amri ya kuzuia mgomo huo usiendelee hadi pale ule mgogoro baina ya MAT na serikali uliofunguliwa katika Tume ya Usuluhishi wa migogoro (CMA) uliosajiliwa kwa namba CMA/DSM/ILA/145/12 mbele ya Jaji Moshi utakapomalizika.

Aidha, Kweka alidai kuwa Juni 22 mwaka huu, Mahakama Kuu ilitoa amri ya kuwataka madaktari waliogoma nchi nzima wasitishe mgomo na mahakama hiyo ikampatia nakala ya amri hiyo mshitakiwa (Dkt. Mkopi), Juni 25 mwaka huu.

“Kwa kuwa mgomo huo ulikuwa ni batili, Serikali ilifungua maombi (namba 73 ya mwaka 2012), Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi, dhidi ya Chama cha Madaktari,” alidai Wakili Kweka na kuongeza: “Katika maombi hayo, pamoja na mambo mengine iliomba mahakama itoa zuio la muda dhidi ya MAT na wanachama wake kutokuitisha wala kushiriki katika mgomo, kusubiri uamuzi wa mgogoro uliowasilishwa Mahakama Kuu na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).”

Wakili Kweka alidai kuwa Juni 22, 2012, mahakama ilisikiliza maombi hayo ya Serikali na kuamuru kwamba MAT na wanchama wake nchini kote kutokuitisha wala kushiriki katika mgomo kusubiri usikilizwaji wa maombi hayo pande zote, “Amri ya mahakama iliwasilishwa kwa mshtakiwa tarehe 25.06.2012. Bila kujali amri ya mahakama, mshtakiwa na wanachama wake waliendela na mgomo.Tarehe 26.06.2012, mbele ya mshtakiwa, mahakama ilitoa amri nyingine ikiiamuru MAT kutekeleza amri yake ya awali.”, alidai Kweka na kuongeza: “Pia mahakama ilimwamuru mshtakiwa kama rais wa MAT kutekeleza amri hiyo kupitia katika vyombo vya habari. Mshtakiwa hakutekeleza amri hiyo na aliendelea na mgomo akihamasisha wanachama wake kugoma,” aliongeza Wakili Kweka; “Licha ya mshitakiwa kupatia amri hiyo ya mahakama ambayo aliipokea, yeye na madaktari wenzake waliendeleza mgomo huo na Juni 26 mwaka huu, Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi ilitoa amri nyingine kwa MAT iliyokuwa ikikitaka chama hicho kutekeleza kwa vitendo amri ya mahakama iliyotolewa Juni 22 mwaka huu ambayo ilimtaka Dkt. Mkopi kwenda kwenye vyombo vya habari kuwatangazia madaktari wote waliogoma wasitishe mgomo huo; Lakini Dkt. Mkopi alishindwa kutekeleza amri hizo mbili za Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi na matokeo yake yeye na madaktari wenzake wakaendelea na mgomo. Julai 9 mwaka huu, mshitakiwa alikamatwa na kufikishwa mahakamani hapa. Julai 10 mwaka huu alifunguliwa kesi hii iliyopo mbele yako Mheshimiwa Hakimu,” alidai Kweka.

Kwa upande wake, Dkt. Mkopi alidai ameyasikia maelezo hayo aliyosomewa wakili Kweka ila anakanusha kuwa yeye ni Daktari wa Hospitali ya Taifa ya Mhimbili ila akakubali kuwa ni kweli yeye ni daktari wa binadamu. Akakataa kuwa madaktari waligoma kuwatibia wagonjwa. Kwamba si kweli kuwa alidharau amri ya mahakama ya Juni 22 mwaka huu iliyomtaka aende kwenye vyombo vya habari kuwatangazia madaktari waache kugoma.

Hakimu Kahamba aliarisha kesi hiyo hadi Oktoba 23 mwaka huu, ambapo siku hiyo kesi itakuja kwa ajili ya mashahidi wa upande wa Jamhuri kuanza kutoa ushahidi wao.

Julai 10 mwaka huu, ilidaiwa na wakili wa serikali Lasdilaus Komanya kuwa kati ya Juni 26 na 28 mwaka huu, Dkt. Mkopi akiwa ni Rais wa MAT alidharau amri halali ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi ya Juni 26 mwaka huu, ambayo ilimtaka mshitakiwa huyo kwenda kwenye vyombo vya habari kuwatangazia wanachama wa chama hicho wasitishe mgomo kwani mgomo ule waliokuwa wakitaka kuufanya ni batili kama ambayo mahakama hiyo ya Divisheni ya Kazi, Juni 22 mwaka huu, ilitoa amri kama hiyo ya kuubatilisha mgomo huo, lakini mshitakiwa huyo hakufanya hivyo.

Wakili Kweka pia alidai kosa la pili ni kuwashawishi madaktari wagome kinyume na kifungu 390 na 35 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, kuwa Juni 27 mwaka huu, mshitakiwa huyo akiwa rais wa chama hicho aliwashawishi madaktari wasitekeleze amri hiyo ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi ya Juni 22 mwaka huu, na matokeo yake madaktari hao wakagoma.
 
"Juni 2012 madaktari wanaofanya kazi katika hospitali za serikali waliingia kwenye mgomo dhidi ya mwajiri wao ambaye ni serikali na mgomo huo uliandaliwa na MAT na madaktari hao waligoma kuwahudumia wagonjwa wakati wakati mkataba wao wa ajira waliongia na serikali ni kuwatibia wagonjwa" alidai Kweka.


Serikali inajitafutia kushindwa tu kesi hii, mgomo haukuandaliwa na MAT bali uliandaliwa na Jumuia ya Madaktari inayoongozwa na Dr Ulimboka. Wanasheria wa serikali kweli VIHIYO!
 
Serikali yetu ni ya wendawazimu kabisa.

Mgomo ulianzishwa na jumuia za madaktari, sasa MAT inahusukaje hapa.

Yaani serikali imezoea kubambikizia kesi watu bila aibu. Halafu mwisho wa siku serikali inashindwa mahakamani tena kwa aibu.
 
Serikali inajitafutia kushindwa tu kesi hii, mgomo haukuandaliwa na MAT bali uliandaliwa na Jumuia ya Madaktari inayoongozwa na Dr Ulimboka. Wanasheria wa serikali kweli VIHIYO!
Umeona eeh!
Hii ndio serikali yetu na hao ndio mawakili wa serikali yaani wote vilaza.
 
Mgomo unaendelea mpaka leo ukienda hospitali za serikali mawili kufa au kupona wa mwache Mkopi
 
Mgomo unaendelea mpaka leo ukienda hospitali za serikali mawili kufa au kupona wa mwache Mkopi

nakubaliana nawe kabisaaaa,,,,case study ni mhimbili,,,,nilikua na mgonjwa pale mwaisela,aisee usipojiweka mguu sawa ANACHINA,kuna watu wana zaid ya miez MI 3 LAKINI WAPI HAWAFANYIWI UPASUAJI
 
Back
Top Bottom