Kesi ya samaki wa magufuli ikoje?

Mongoiwe

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
524
263
Mahakamani kuna Raia 32 kama washitakiwa wa kesi ya kukamatwa wakifanya uvuvi kwenye pwani ya ya Tanzania ya Bahari Hindi bila ya kuwa na leseni.

Washitakiwa hao wanadaiwa kukutwa na tani 296 za samaki waliokuwa wamehifadhiwa ndani ya meli ya Tawaliq 1. Samaki hao wana thamani ya jumla ya Sh2.7 bilioni.

Ninataka kujua kwa wale wenye kufahamu;
a). Washitakiwa wameshitakiwa kwa kosa/makosa gani mahakamani?,
b). Pia wanashitakiwa kwa sheria ipi
c). Wanashitakiwa kwa makosa mangapi?
d). Sheria wanayoshitakiwa ni ya mwaka gani?
Nitashukuru sana iwapo nitasaidiwa kwa hayo maswali yangu machache, kwani nimeona ni vyma nikaelewa hayo kabla sijaingia katika mjadala kwani nimesoma sana katika magazeti na sijajua makosa na sheria wanakabiliwa nayo.
 
Back
Top Bottom