Kesi ya Saileth Vithlani wa kashfa ya Rada

Status
Not open for further replies.
Mh!.. Tatizo letu watanzania kila kitu tunawaza siasa na 2015. Kwa upande wangu sijaiona connection yoyote kati ya Rada issue na 2015 presidential candidate.
Suala kuhusiana na watu walio cheza hilo dili la mabilioni ndio la msingi kuhoji. Ila tukikaa tunaangalia 2015 tutabaki hapahapa na fikra zetu mgando!
 
Huu ni ukweli usiopingika kuwa kitendo cha kutowawajibisha au kuwafikisha mahakamani wahusika wa rada kwa upande wa Tanzania, kinatuondolea heshima kwenye jumuiya ya kimataifa. SFO walitaja baadhi ya watuhumiwa wa sakata hili la lada, taasis zetu za serikali zikawasafisha, pasipo kutaja majina mbadala. Yaani kama ni kweli tumeibiwa, na tumeweza kudhibitisha somebody 'A' hausiki, lazima tuseme tumegundua somebody 'B' ndo katuibia. Hivyo mheshimiwa waziri wa mambo ya nje inabidi atufafanulie zaidi kwa nini anafikiri tunadharauliwa
 
Mh!.. Tatizo letu watanzania kila kitu tunawaza siasa na 2015. Kwa upande wangu sijaiona connection yoyote kati ya Rada issue na 2015 presidential candidate.
Suala kuhusiana na watu walio cheza hilo dili la mabilioni ndio la msingi kuhoji. Ila tukikaa tunaangalia 2015 tutabaki hapahapa na fikra zetu mgando!

@Avatar, inawezekena uhusiano wa rada na 2015 usiwe very obvious - na hapo ndipo wakubwa wanafaidi. Lakini nakuhakikishia ndani ya ccm sasa hivi 99.9% ya maamuzi na mikakati yako proportionally linked na 2015. Kasheshe ni kuwa wadau wako kwenye makundi na kwa sasa ni minyukano mtindo mmoja only the strongest will survive. Hiyo 0.1% niliyoacha ni mahususi kwa Mzee wetu Mukama ambae maskini ya mungu anafanya kazi kusafisha chama kumbe asijue wenzie wanasafisha njia.
 
BAADA ya kutulia kwa muda, sakata la ununuzi wa rada, limeibuka tena na safari hii kwa sura tofauti, baada ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuazimia kulijadili bungeni katika moja ya vikao vyake vinavyoendelea.Hoja hiyo jana ilifikishwa bungeni na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ambaye alisoma kauli ya serikali dhidi ya hatua ya Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza kutoa fedha za tozo ya rada kwa asasi za kiraia.

"Tanzania ni nchi maskini, lakini haiko tayari kudharauliwa kiasi hicho kwa serikali yake, tasisi zake na asasi zake kutoaminiwa. kuruhusu hilo lifanyike ni kuruhusu kuibiwa kwa mara ya pili,"alisema Membe.Membe alisema kitendo cha BAE kutaka kuzipeleka fedha hizo kwenye asasi za kiraia nchini Uingereza ili zije kufanyia shughuli hapa nchini ni kinyume na makubaliano yaliyofikia kati ya Serikali ya Tanzania, SFO na serikali ya Uingereza.

Baada ya taarifa hiyo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alisimama na kuomba mwongozo wa spika na kusema," Mheshimiwa Spika, tunaomba taarifa hiyo ya serikali ijadiliwe bungeni."Baada ya kusema hivyo takriban wabunge wote walisisimama kuuuga mkono kitendo kilichomfanya Spika Anne Makinda kusema atatafuta fursa kwa ajili ya kujadili suala hilo bungeni.

Source: Mwananchi

My take:
This radar change has absolutely nothing to do with recovering the money on behalf of ordinary Tanzanians, but has everything to do with 2015. Membe alikuwa wapi siku zote asiseme uchunguzi ufanyike ili washiri kwa upande wa Tanzania wachukuliwe hatua. Mbona ang'ang'ania hela bila uwajibikaji wa wale wote waliofanikisha dili? Na hao wabunge waliounga mkono hoja kwa kishindo wamejuwa lini Tanzania imelanguliwa kwenye ununuzi wa Radar? Na wamefanya nini tangu walipogunduwa ulanguzi huo?

Kwa upande mwingine nahisi fitna za kuwatoa kafara mapacha watatu zimekuwa ngumu hivyo wazee wa ‘kuzunguka mbuyu' wamepata kona nyingine. Wataanza na rada kujadiliwa bungeni na baadae tunaweza kuona mizimu mingine ikifufuliwa lengo likiwa kupata mtaji wa kumtoa mtu kwenye matumaini ya 2015!

serikali kupitia kwa membe bado inajikanyaga kanyaga kusema ukweli,
hao BAE wanataka kuakikisha ili suhala linakwisha kabisa katika media na sio kujirudi rudia na kwa
kuwa hawa jamaa walishawahi kuiweka serikali yetu mifukoni mwao wanajua uwezo wa serikali yetu na
unyama wake
jamaa wanajua hii hela italiwa na hivyo kuendelea kusemwa semwa kwa vyombo vya habari na hii inaathiri biashara zao kwa kuwwa kila ili sakata litakapoibuka wao wakiendelea kutajwa,
sio sisi tu tunaorudishiwa change ni karibu nchi 3 moja ni USA mbona huko wanapewa hela yao bila mashaka na lakini sisi wanatugomea?

swali gumu kwa serikali mwandosya bado ni waziri kwa misingi ipi hata baada ya ili suhala kujulika ukweli wake? kwa nini asiwajibike hata kwa uzembe maana yeye alikuwa ni waziri mwenye dhamana wakati wa tukio

tusifanyane watoto serikali inaogopa kuchukua hatua kwa nini? au kiranja mkuu alipata mgao
 
BAADA ya kutulia kwa muda, sakata la ununuzi wa rada, limeibuka tena na safari hii kwa sura tofauti, baada ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuazimia kulijadili bungeni katika moja ya vikao vyake vinavyoendelea.Hoja hiyo jana ilifikishwa bungeni na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ambaye alisoma kauli ya serikali dhidi ya hatua ya Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza kutoa fedha za tozo ya rada kwa asasi za kiraia."Tanzania ni nchi maskini, lakini haiko tayari kudharauliwa kiasi hicho kwa serikali yake, tasisi zake na asasi zake kutoaminiwa. kuruhusu hilo lifanyike ni kuruhusu kuibiwa kwa mara ya pili,"alisema Membe.Membe alisema kitendo cha BAE kutaka kuzipeleka fedha hizo kwenye asasi za kiraia nchini Uingereza ili zije kufanyia shughuli hapa nchini ni kinyume na makubaliano yaliyofikia kati ya Serikali ya Tanzania, SFO na serikali ya Uingereza.Baada ya taarifa hiyo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alisimama na kuomba mwongozo wa spika na kusema," Mheshimiwa Spika, tunaomba taarifa hiyo ya serikali ijadiliwe bungeni."Baada ya kusema hivyo takriban wabunge wote walisisimama kuuuga mkono kitendo kilichomfanya Spika Anne Makinda kusema atatafuta fursa kwa ajili ya kujadili suala hilo bungeni.Source: MwananchiMy take: This radar change has absolutely nothing to do with recovering the money on behalf of ordinary Tanzanians, but has everything to do with 2015. Membe alikuwa wapi siku zote asiseme uchunguzi ufanyike ili washiri kwa upande wa Tanzania wachukuliwe hatua. Mbona ang'ang'ania hela bila uwajibikaji wa wale wote waliofanikisha dili? Na hao wabunge waliounga mkono hoja kwa kishindo wamejuwa lini Tanzania imelanguliwa kwenye ununuzi wa Radar? Na wamefanya nini tangu walipogunduwa ulanguzi huo?Kwa upande mwingine nahisi fitna za kuwatoa kafara mapacha watatu zimekuwa ngumu hivyo wazee wa ‘kuzunguka mbuyu' wamepata kona nyingine. Wataanza na rada kujadiliwa bungeni na baadae tunaweza kuona mizimu mingine ikifufuliwa lengo likiwa kupata mtaji wa kumtoa mtu kwenye matumaini ya 2015!
Inafaa tudharauliwe tu! Maana hatushauliki! Wao ndo wamewezesha fedha kupatikana. Sie tulishakubali yaishe.tena na mhusika katajwa .Iv m2 akushikie mwizi anaiba chakula cha watoto wako na kusababisha wafe njaa. Anakwambia anayeua wanao ni huyu hapa. Ucpochukua hatua atakudharau. Atamnyang'anya mwizi chakula na kuamua kuwagawia watoto kwa usimamizi wake!
 
Tatizo tunakataa au hatutaki kujijua tulivyo. Kibaya zaidi hatutaki kuukubali ukweli wa jinsi watu wanavyotujua. Tuko hard hearted kwa wananchi wetu kwa kuendeleza udhalimu wetu bila kujali umskini wao. Wacha waingereza, pamoja na ukatili wao wa kikoloni wa hapo awali, tuwaachie watupangie matumizi hela hizo za rada. Mpaka leo watu wanahoji hela za EPA zilizorudishwa na mafisadi zilikoenda. Zilikotarajiwa kwenda bado kizungumkuti!!!!!! Tunaonyesha miare ya hasira kwa matumizi ya hizi hela za rada kuliko kwa waliosababisha ubaradhuli huu wa kuwanyang'anya wa Tz fedha zao - SHI SHAWA!!!!!!!
 
Hivi ni lini hii serikali yatu ilishakubali kwamba tumelanguliwa kwenye sakata la rada?

Hii ni aibu kubwa kwa Membe na kwa CCM kwa ujumla na aliekua mgombea wao wa uspika.

Kama Membe anafanya hivi akidhani anajisafishia njia ya 2015, ninaamini matokeo yatakua kinyume chake maana tunakumbuka kabisa serikali ilishikia bango suala hili kwamba halikua na matatizo yoyote, kuanza ghafla kuona kwamba tumeibiwa hasa baada ya kuona mshiko kunawashushua na kuwashushia heshma zaidi.

Ikiwa wanafanya hivyo kuwaweka mapacha watatu kwenye hali ngumu, I think wanapoteza muda maana sie wananchi tulisha wadelete na kuwa-empty kwenye recycle bin ...

Sijui tunaelekea wapi wajameni ...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom