Kesi ya Mramba yafikia patamu...

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Shahidi abanwa kesi ya kina Mramba


Na Gladness Mboma

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtaka shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka Bw. Godwin Nyelo, kuwasilisha barua iliyokuwa ikitoka benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwenda Kampuni ya
M/S Alex Stewart Government Bussines Cooparation kama kielelezo cha ushahidi kwa upande wa utetezi.

Agizo hilo lilitolewa jana katika kesi inayomkabili Waziri wa zamani wa Fedha, Bw. Basil Mramba aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Daniel Yona na aliyekuwa Katibu Mkuu Hazina, Bw. Grey Mgonja.

Hakimu Saul Kinemela alitoa agizo hilo baada ya Wakili Bw. Eliasa Msuya anayemtetea Bw. Yona, kuitaka mahakama imlazimishe shahidi huyo kutoa barua hiyo kama sehemu ya ushahidi wao.

Awali, Bw. Nyelo alidai kuwa anaikumbuka barua hiyo, lakini hawezi kuiongelea wala kuitoa kama kielelezo cha ushahidi kwa upande wa utetezi mahakamani hapo, kwa sababu siyo yake wala hakuwa hakuwa anafanyia kazi taasisi iliyohusika.

Akitoa uamuzi juu ya hoja hiyo, Hakimu Kinemela alisema ili kutenda haki, mahakama inamlazimisha shahidi kutoa barua hiyo kama kielelezo cha ushahidi kwa upande wa utetezi.

Barua hiyo inadaiwa kuandikwa na aliyekuwa Msaidizi wa Gavana wa BoT, Bibi. Kesisia Mbatia Novemba 28, 2002 akiitaka kampuni ya M/S Alex Stewart Government Bussines Cooparation kuwasilisha mchanganuo uliosaidia kuingiwa kwa mkataba kati ya kampuni hiyo na BOT.

Mawaziri hao na katibu mkuu kwa pamoja wanatuhumiwa kuingia mkataba na kuisamehe kodi kinyume cha sheria kampuni ya M/S Alex Stewart Government Bussines Cooparation, jambo linalodaiwa kuwa lilisababisha serikali kupata hasara ya sh.bilioni 11.7.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14 mwaka 2004 .

 
Kesi ya Mramba yaendelea kunguruma


na Happiness Katabazi


amka2.gif
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, jana ilimtaka shahidi wa upande wa mashitaka, Godfrey Nyero, katika kesi ya matumuzi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.7 inayomkabili aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba, na wenzake kutoa ushahidi kwa kutumia kielelezo kilichowasilishwa na mawakili wa upande wa utetezi.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi, Saul Kinemela, aliyekuwa akisaidiana na Jaji John Utamwa na Sam Rumanyika, ikiwa ni muda mfupi baada ya shahidi huyo ambaye ni wa kwanza wa upande wa mashitaka kutakiwa na wakili wa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona, Elisa Msuya, kutumia kielelezo cha pili kujibu maswali atakayomuuliza.
Awali shahidi huyo alidai kuwa hawezi kukitumia kielelezo hicho ambacho ni barua ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) waliyokuwa wameiandikia Kampuni ya Alex Stewart na shahidi huyo akamwomba wakili Msuya kwamba awatafute watu wa BoT ndio waje mahakamani kuizungumzia barua hiyo.
Hoja hiyo iliungwa mkono na Wakili Mkuu wa Serikali, Fredrick Manyanda, aliyekuwa akisaidiana na Ben Lincol na Shadrack Kimaro.
Hata hivyo, Jaji Utamwa aliuuliza upande wa Jamhuri endapo shahidi huyo akitumia kielelezo hicho kukitolea ushahidi kutakuwa na madhara yoyote na Manyanda kueleza hakutakuwa na madhara.
Kutokana na hoja hiyo, mahakama ilimtaka shahidi huyo atoe ushahidi kwa kutumia kielelezo hicho.
Mbali na Mramba, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona na Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja. Kesi hiyo itaendelea leo.
 
Wanatuadaa hamna kitu, utasikia kesi imefutwa ushahidi hautosherezi
 
Hivi huyu Jamaa mali zake hazitoshi hata robo ya alizofuja ili tuzirejeshe mikononi mwetu......, huyu jamaa anayo hatia kama sio yeye aliyeiba basi ni uzembe wake ndio ulisababisha... kwahiyo kwa njia yoyote ile anayo kesi ya kujibu..... huku kusikiliza hizi kesi ni kuendelea kupoteza pesa za mlipa kodi.... Asifungwe bali mali zake zote zichukuliwe na ahukumiwe kufanya kazi bure kama community service.... hata kuuza magazeti....
 
Hivi huyu Jamaa mali zake hazitoshi hata robo ya alizofuja ili tuzirejeshe mikononi mwetu......, huyu jamaa anayo hatia kama sio yeye aliyeiba basi ni uzembe wake ndio ulisababisha... kwahiyo kwa njia yoyote ile anayo kesi ya kujibu..... huku kusikiliza hizi kesi ni kuendelea kupoteza pesa za mlipa kodi.... Asifungwe bali mali zake zote zichukuliwe na ahukumiwe kufanya kazi bure kama community service.... hata kuuza magazeti....

..ktk RED; inawezekana wewe ni mmoja kati ya Watanzania wanaodai katiba mpya ili hali hii iliyopo sa hivi huijui na wala hujawahi kuiona sembuse kuisoma.
 
[/COLOR]
..ktk RED; inawezekana wewe ni mmoja kati ya Watanzania wanaodai katiba mpya ili hali hii iliyopo sa hivi huijui na wala hujawahi kuiona sembuse kuisoma.

Nani anaongelea katiba hapa ? its just common sence hizi kesi zitasikilizwa lakini mwisho wa siku we know kwamba jamaa atashinda.., popote pale with good lawyers and money hushindwi kesi (ask O. J. Simpson)..., sasa cha maana kuliko kesi kuendelea kupigwa tarehe kiwepo kifungu kuhujumu mali ya umma ni kufilisiwa... na kwanini uende gerezani uendelee kula kodi zetu... since sio menace to society in terms of kuua watu, basi uendelee kuchangia jamii, ku-serve community.... hivi hujui wachina wengi wanaokuja huku kujenga mabarabara wengine ni wafungwa kwao?
 
Kichwa cha post nafikiri hakiendani na content! Unaposema kesi imefikia patamu kwa shahidi kuagizwa alete kielelezo tu, sasa kwa kweli mimi sioni utamu wowote hapo kwa kuwa hatujui kielelezo kimeandikwa nini na kinasaidiaje kesi!
 
MH hii kesi bado ipo kweli, si imefungwa rasmi leo? sasa hapo patamu pamefikiwa ni wapi?
 
Maskini mramba hata kama alikuwa ahukumiwe miaka 5 sasa watamuhukumu miaka 20 huku wakimuongezea miaka mingine ili kupunguza hasira za wanachi juu y dowans.

Bila ya dowans mramba angeshinda kesi ila sasa hata kama kisheria atashinda itabidi iashindwe tu maana kushinda kwake ndio kaburi zaidi kwa serikali ya JK.
 
hata mimi nimejaribu kufatilia huo utamu lakini sijauona kabisa
Kichwa cha post nafikiri hakiendani na content! Unaposema kesi imefikia patamu kwa shahidi kuagizwa alete kielelezo tu, sasa kwa kweli mimi sioni utamu wowote hapo kwa kuwa hatujui kielelezo kimeandikwa nini na kinasaidiaje kesi!
 
Kesi ya akina Mramba yakwama tena

Imeandikwa na Regina Kumba; Tarehe: 18th April 2011 @ 23:20 Imesomwa na watu: 48; Jumla ya maoni: 0








MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imezidi kukwamisha kesi inayomkabili waziri wa zamani wa fedha, Basil Mramba, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hazina, Gray Mgonja.

Kesi hiyo iliahirishwa kwa mara nyingine katika mahakama hiyo na Hakimu Mfawidhi, Ilvin Mgeta, baada ya kusema mwenendo wa kesi hiyo haujawa tayari kwa ajili ya kupewa mawakili wa pande zote mbili, ili kujiandaa kuwasilisha majumuisho.


Hakimu Mgeta alisema mwenendo huo uko katika hatua ya mapitio na hivyo kupanga kesi hiyo kuja kuangalia kama itakuwa tayari Mei 6 mwaka huu.


Mara ya mwisho kesi hiyo iliahirishwa na Hakimu Mustapher Siyani, akisema mahakama imekwama kuchapisha mwenendo wa kesi hiyo, kutokana na tatizo la umeme linaloendelea, alisema pamoja na tatizo hilo, mahakama inafanya jitihada kuhakikisha unakamilika.


Kesi hiyo ni ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia hasara Serikali.


Wanatuhumiwa wanadaiwa kuisamehe kodi kinyume cha sheria, kampuni ya M/S Alex Stewart Government Business Corporation na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 11.


Washitakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14 mwaka 2004 na wako nje kwa dhamana.

 
Back
Top Bottom