Kesi ya Mnyika hukumu ni Leo

Status
Not open for further replies.
MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika, amemuudhi Jaji Upendo Msuya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kiasi cha kumtaka Wakili wake amuonyeshe kile jaji huyo alichosema ni sawa na kudharau mahakama.

Jaji Msuya alieleza kuudhiwa na mbunge huyo jinsi alivyokuwa akijibu maswali mbalimbali ya Wakili wa mlalamikaji, Issa Maige, wakati akijitetea katika kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi.

Kesi hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombe wa ubunge wa jimbo kupitia CCM, Hawa Ng'humbi.

Jana, Mnyika alipanda kizimbani kujitetea huku akikana madai yote na kudai kuwa, hata kasoro zinazolalamikiwa hazikuathiri matokeo, lakini alipobanwa kwa maswali na Wakili Maige alifika mahali akamuudhi Jaji Msuya anayesikiliza kesi hiyo.

Mambo yanayodaiwa kumuudhi Jaji Msuya ni jinsi Mnyika alivyokuwa akijibu maswali hayo, wakati mwingine alikuwa akijibu kinyume na swali na wakati mwingine kutoa maelezo marefu ambayo yalikuwa hayahitajiki.

Kutokana na hali hiyo, Jaji Msuya alilazimika kuingilia kati mara kwa mara akimtaka Mnyika ajibu swali kwa kadri alivyokuwa akiulizwa, badala ya kutoa maelezo ambayo hayakuwa yakihitaji. Hata hivyo, Mnyika aliendelea kupiga chenga.

Hali hiyo ilimuudhi Jaji Msuya na Wakili wake, Edson Mbogoro alisimama na kumnong'oneza Mnyika mambo kadhaa.

"Nafikiri wakili ni vyema pia umemwelewesha kuwa majibu mengine anavyojibu si sawa, na hii inaweza kutafsiriwa kuwa ni dharau kwa mahakama maana nimeshamuonya na kumuonya lakini bado tu," alisema Jaji Msuya.

Baada ya onyo hilo, Mnyika alionekana kutulia na kujibu maswali kadhaa ya Wakili Maige kwa utulivu na kwa kadri swali lilivyokuwa likiulizwa.

Katika hatua nyingine, Mnyika alipingana na aliyekuwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Gaudence Kadiarara, kuhusu madai ya matumizi ya kompyuta zake (Mnyika) kuhesabia kura.

Majibu ya swali hilo ni miongoni mwa majibu yaliyoonesha kumuudhi Jaji Msuya kwa jinsi Mnyika alivyokuwa akijibu.

Wakili Maige: Kwa hiyo DW1 ni muongo?

Mnyika: Nimesema maelezo yake siyo ya kweli

Wakili Maige: Sawa, siyo sahihi kwa hiyo ni muongo, kweli au si kweli?

Mnyika: Nimesema maelezo yake siyo ya kweli.

Katika kujibu maswali ya Wakili Maige, Mnyika likiri kuwapo kwa dosari katika matokeo yaliyorekodiwa katika fomu ya matokeo ya jumla na kwamba, kwa jinsi yalivyorekodiwa siyo sahahi wala halali.

Pia, alikubali kuwa kama angeyabaini mapema asingesaini mpaka yangerekebishwa huku akikiri pia kuwa katika hali hiyo mwenye mamlaka ya kurekebisha dosari hizo kwa sasa ni Mahakama.

Mnyima pia alikiri tofauti ya kura zaidi ya 14,000 inayoonekana katika fomu hiyo yeye binafsi hawezi kuielezea.

Lakini katika awali katika ushahidi wake wakati akongozwa na wakili wake, Mbogoro Mnyika alidai kuwa dosari hizo haziathiri matokeo hayo na kwamba, hata kama ikithibitika kuwa tofauti ya kura hizo ni za Ng'humbi, bado hawezi kushinda.
 
Mahakama itatengua ushindi wa Mnyika habari toka ndani.
wakitengua watakuwa wamewadhulumu wapiga kura elfu 66 hawatakuwa wamemuathiri Mnyika au Chadema, kwa upande wa chadema watamtumia Mnyika kujenga chama na italeta tija zaidi 2015, unaona Arusha? Lema anakubalika, na walivyomtoa ubunge sasa anawapigisha kwata, anawavua mashati ya kijani anawavalisha kombati na imeongeza chachu ya mabadiliko imeleta ladha kwenye M4C
 
Lazima msifiane kwasababu mpo kampuni Moja ya NAPECCM na payroll yenu inatoka kapu moja

Wewe kila post yako lazima umtaje Nape, kwenye siasa za Tanzania Nape ni mtu mdogo sana..nadhani umri wako na Nape mnafafana ndio maaana unamtaja sana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom