Kesi ya Mengi yapigwa kalenda

Status
Not open for further replies.

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Kesi ya Mengi yapigwa kalenda


na Happiness Katabazi


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, jana ilishindwa kuanza kusikiliza kesi ya kashfa ya madai iliyomkabili Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Reginald Mengi, kutokana na mawakili wa mlalamikaji, Yusuf Manji, kutojiandaa.

Hakimu Aloyce Katemana alisema anakubaliana na hoja ya kuahirishwa usikilizwaji wa kesi hiyo ambayo ilipangwa kuanza kusikilizwa jana. Katika kesi hiyo Manji anawakilishwa na mawakili Mabere Marando, Beatus Malima, Dk. Ringo Tenga na Richard Rweyongeza.

"Nakubaliana na hoja ya mawakili wa mlalamikaji kwamba leo tusianze kusikiliza kesi hii hivyo naiahirisha hadi Februali 3-4 mwaka huu, kwani licha ya mawakili hao kutojiandaa pia mimi ni mgeni na kesi hii na jalada lake bado sijalipitia," alisema Hakimu Mkazi Katemana.

Awali akijibu hoja ya Wakili Marando ya kutaka kesi hiyo isianze kusikilizwa jana kwa madai upande wa madai haukujiandaa, wakili wa Mengi, Michael Ngaro, alielezwa kushangazwa na ombi hilo kwa sababu mawakili wa mlalamikaji ndiyo waliifungua kesi hiyo Na.85/2009 na kuhoji ni kwa nini hawakuwa wamejiandaa.

"Sisi tunashangazwa na ombi la hawa wenzetu wa upande wa mlalamikaji la kutaka usikilizwaji usiendelee…sisi upande wa mdaiwa tuko tayari kuendelea na usikilizwaji wa kesi hii," alisema Ngaro.

Mapema mwaka juzi, Yusuf Manji alimfungulia kesi ya madai ya kashfa Mengi na kituo cha televisheni cha ITV akitaka amlipe fidia ya SHILINGI MOJA kwa madai kuwa Mengi alitumia televisheni yake kumkashifu kwa kumuita ‘Fisadi Papa' na kwamba mmoja wa watu wanaopora rasilimali za Tanzania.
 
Mafisadi wanatumia mahakama kama nafasi ya kutisha jamii isitamke ukweli.............................
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom