Kesi ya mbunge Lema: Jaji Mujulizi ametumwa na nani?

Kama kweli hayo yalitamkwa kweli ni makosa, lkn nini hatma ya kesi na jimbo? Endapo Mh. Godbless Lema atashindwa na kuvuliwa ubunge, ninachokiona mimi hapo ni kujitia gharama za kurudia uchaguzi kwa sababu za k i p u u z i. Hata uchaguzi ukirudiwa Buriani hana ubavu wa kushinda kutokana na namna alivyobwagwa.

Na pia izingatiwe kuwa Mh. Lema ameshaijengea CHADEMA jina kubwa bungeni kwa kuwa mmoja kati ya wachangiaji wazuri ndani na nje ya bunge. CCM iache kupoteza muda na Arusha mjini, badala yake ijiandae kwa uchaguzi wa Monduli kwani Nepi Naehuyu ametuahidi kuwa baada ya uchaguzi wa Igunga, magamba mengine yaliyobaki yatang'olewa kwa nguvu.
 
Kwa majira haya ya baridi ikitanda hp kama vile tupo majira ya mwezi wa 6 nipo ndani ya Mahakama Kuu Arusha na hapa namwona (MB) Lema ameshawasili tayari kukabiliana na kesi tajwa hapo juu na bila kuwakosa Wanachama wake wa CDM waliofurika hp kama kawa,na hp vile vile naona Landcruiser ya police imweshawasili tayari utafikiri kuna vita hapa mahakamani. WanaJF nitawajuza yote yatakayojiri hapa. Kuweni wapole!
 
Kama kweli hayo yalitamkwa kweli ni makosa, lkn nini hatma ya kesi na jimbo? Endapo Mh. Godbless Lema atashindwa na kuvuli] ametuahidi kuwa baada ya uchaguzi wa Igunga, magamba mengine yaliyobaki yatang'olewa kwa nguvu.
Mkuu! Nakwambia hw magamba wanawanga Mi cjawahi kuona ila hakika mambo yao ni magumu pasipo ya mfano. Safari hii magamba hawana chaoooo!!
 
Jaji huyu anaishi Arusha ama anakuja kwenye kesi tuu na kuondoka Arusha chini ya ulinzi??mwambieni huyu Jaji asome alama za nyakati.
 
Kwa majira haya ya baridi ikitanda hp kama vile tupo majira ya mwezi wa 6 nipo ndani ya Mahakama Kuu Arusha na hapa namwona (MB) Lema ameshawasili tayari kukabiliana na kesi tajwa hapo juu na bila kuwakosa Wanachama wake wa CDM waliofurika hp kama kawa,na hp vile vile naona Landcruiser ya police imweshawasili tayari utafikiri kuna vita hapa mahakamani. WanaJF nitawajuza yote yatakayojiri hapa. Kuweni wapole!

Polisi kufika hapo ni jambo la kawaida hasa Chadema inapokuwa hapo mahakamani,cha msingi tujuze mambo yanavyoendelea mkuu.Nnasikitika nimebanwa na kazi ningetimba hapo mahakamani Kama kawaida.
 
please hebu tueleze maamuzi ya jaji ndio nitoe maoni yangu.
Jaji Aloyce Mujuluzi alitoa uamuzi wa pingamizi zilizotaka kesi hiyo itupiliwe mbali kwa madai kuwa, walalamikaji hawakuwa na haki kisheria kulalamikia mambo ambayo yalitamkwa dhidi ya aliyekuwa mgombea
wa CCM, Dk Batilda-Salha Buriani, kuwa akichaguliwa atahamia Zanzibar alikoolewa.

Walalamikaji hao, Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo, kupitia kwa Wakili wao, Alute Mughwai na Modest Akida, walidai kuwa kwa nyakati na sehemu tofauti, Lema alitoa kauli zenye dalili ya ubaguzi dhidi ya Dk Buriani, hivyo kuomba mahakama itengue ushindi wake kutokana na ukiukaji kanuni na taratibu za uchaguzi.

Hata hivyo, mawakili wa utetezi, Kimomogoro anayemwakilisha mshtakiwa wa kwanza na Vitalis anayemwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), waliomba mahakama kutupa madai hayo, wakieleza kuwa kisheria aliyestahili kulalamikia maneno hayo ni Dk Buriani siyo wapiga kura.Jaji Mujulizi alisema baada ya kupitia madai na majibu ya upande wa utetezi, mahakama imeona walalamikaji wana haki kisheria kulalamikia taratibu, mwenendo wa kampeni na mchakato mzima wa uchaguzi, kwa sababu walikuwa wapiga kura waliojiandikisha na wenye haki ya kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Alisema mawakili wa utetezi waliingia kwenye mtego kwa kuacha kuleta pingamizi kuhusu makosa ya kisheria dhidi ya hati ya mashtaka, badala yake walijikita kutafsiri na kurekebisha madai yaliyomo kwenye hati ya mashtaka, kazi aliyosema haiwezi kufanywa na mahakama wala upande wa utetezi.
“Mahakama haiwezi kuweka vipimo vya jumla kwa wapiga kura, mambo wanayoweza kulalamikia na kupinga katika uchaguzi kwa sababu kila uchaguzi huja na mambo na mazingira tofauti. Siyo sahihi mahakama kuzuia mtu yeyote anayedhani ana ushahidi kuthibitisha madai yake kuleta maombi mahakamani," alisema Jaji Mujuluzi.

Alisema katika shauri hilo, mahakama haitachunguza wala kushughulika na ukweli wa maneno yaliyotamkwa, bali kitakachotafutwa ni iwapo maneno hayo yalitamkwa na iwapo yalistahili kutamkwa.

"Kwa maoni na uamuzi wangu, pingamizi hizi zilizowasilishwa mbele yangu hazikidhi mahitaji ya kisheria, hivyo nazitupilia mbali nawajibu ili kutoa nafasi kwa wadai kuleta ushahidi wao kuthibitisha yale waliyowasilisha mahakamani, ambayo pia yatahojiwa na upande wa utetezi," alisema Jaji Mujuluzi.
 
Kwa muda huu naona Wakereketwa wa chama wametinga ndani ya mahakama tayari kwa kusikilizwa kwa kesi. Ijapokuwa wa2 ni wengi sana nami ntajitahidi kupenya angalau nipate yote yajirio humu ndani. Aluta continue!!
 
MAELEZO YA JAJI MUJULIZI: "Mahakama haiwezi kuweka vipimo vya jumla kwa wapiga kura, mambo wanayoweza kulalamikia na kupinga katika uchaguzi kwa sababu kila uchaguzi huja na mambo na mazingira tofauti. Siyo sahihi mahakama kuzuia mtu yeyote anayedhani ana ushahidi kuthibitisha madai yake kuleta maombi mahakamani," alisema Jaji Mujuluzi.

Alisema katika shauri hilo, mahakama haitachunguza wala kushughulika na ukweli wa maneno yaliyotamkwa, bali kitakachotafutwa ni iwapo maneno hayo yalitamkwa na iwapo yalistahili kutamkwa.

"Kwa maoni na uamuzi wangu, pingamizi hizi zilizowasilishwa mbele yangu hazikidhi mahitaji ya kisheria, hivyo nazitupilia mbali nawajibu ili kutoa nafasi kwa wadai kuleta ushahidi wao kuthibitisha yale waliyowasilisha mahakamani, ambayo pia yatahojiwa na upande wa utetezi," alisema Jaji Mujuluzi.

My take: Mi nadhani mwishowe atasema maneno yaliyotamkwa hayana ushahidi kama yalitamkwa.
 
Hii kesi ni ngumu sana kwa Lema, anaweza kupoteza kiti chake cha ubunge.
 
Kila mtu mwenye akili na anayejua sheria ameshanga sana maamuzi aliyetoa Jaji Mujulizi jana katika kuhukumu pingamizi ambalo mawakili wa Mbunge Lema walikuwa wameweka dhidi ya walalamikaji , hata hivyo mbunge wa Arusha mjini amekatisha safari yake jana mjini Hanang alipofanya mkutano mmoja akiwa njiani kuelekea Igunga kushahuriana na mawakili wake ni nini cha kufanya na leo baadae ataondoka kuelekea Igunga kwenye mapambano.

Hata hivyo kwa uchache unaweza kumfahamu Jaji mujulizi historia yake kidogo ili ujiulize je haki itatendeka ?

Kabla ya kuteuliwa kuwa jaji aliikuwa na mkurugenzi katika kampuni ya sheria ya IMMA ( ambayo kirefu chake ni ISHENGOMA,MASHA, NA MUJULIZI hata mpaka leo yeye ni mbia.
Kampuni hii ya sheria ndiyo aliyomsomesha Riziwani Kikwete Uingereza wakati Rizwan alipokuwa ana practise law kwao ,
Kampuni hii mpaka leo mtoto wa Karume Fatuma Karume bado anafnya kazi na ni mwanaisa mmojawapo wa kampuni hii.
Jaji Mujulizi anasimamia kesi ya uongo uliotungwa dhidi ya Lema kuhusu madai mbali mbali ikiwemo udini , je ye mwenyewe kama alipewa nafasi ya ujaji baada ya kusilimu ( alikuwa mkiristo na akabadili dini kuwa mwisilamu)
je ataweza kusimamia haki dhidi ya uongo huu , kwani hata sasa ameanza kuonyesha mapungufu makubwa .
ebe tuangalie nini kitatokea mahakamani leo baada ya Mbunge Lema kurudi kuwasiliana na mawakili zake.

Huyu Jaji Aloysius Mujulizi hawezi kutenda haki kwa kesi inayohusu Mh. Lema - namjua alikotoka.

Kwa kuongezea tu kwenye blue, huyu jamaa alikuwa ni mwanasheria wa Jiji kabla ya kuteam up na Masha ili wasajili yale makampuni ya kitapeli: Deep Green etc na ndo yaliwapa mihela hadi wakanunua jengo Upanga. Kampuni ya IMMA Advocates pamoja na majina yaliyotajwa hapo juu kuna jina la mwanamama anaitwa Margai - hivi sasa ni balozi wetu Washington baada ya kuhama kutoka London.

Kwa kuwashukuru IMMA kumpa sponsorship Ritz JK alimpa Mujulizi Ujaji, Masha akapewa unaibu waziri na Margai akapewa ubalozi.

Yule advocate jeuri aliyewahi kumtukana Hakimu ambaye ni binti wa Karume naye anafanya kazi pale, ila nasikia Ritz hayuko nao tena kwani yuko busy na shughuli zake nyingine (hawaivi tena na Masha).
 
Nanukuu (MB) Lema! Hapa hakuna kesi bali ni kupotezeana muda tu. Hiyo alikuwa akisema na call aliyoipoke toka masafa ya mbali nafikiri ni Igunga moja. Naona bila shaka km si mahakimu wamewasili naona ni majaji na mahakama imefunguliwa rasmi.
 
Tujiandae kwa uchaguzi mdogo wa Ubunge Arusha Mjini. Kesi hii imekula kwa Lema....na kuna dalili kuwa ubunge ndo bye bye manake huenda asiruhusiwe kugombea tena kutokana na uzito wa kosa na matusi dhidi ya mgombea mwenzake. Pia iwapo atabahatika kugombea, hakika atabwagwa. Wana Arusha wameshatambua kuwa walifanya kosa kubwa kumchagua mhuni.
 
Nipo sambamba kabisa na Mahakama ila kwa uzoefu wangu hakika hakuna la maana kabisa zaidi ya kupoteana muda tu. Hebu tusubirie na tusikie hizi pumba zilizoletwa na magamba zinalenga nini. Ntawajuza!
 
Hii kesi ni ngumu sana kwa Lema, anaweza kupoteza kiti chake cha ubunge.

Si rahisi kuthibitisha kuwa maneno hayo yaliwafanya wapiga kura kubadili mawazo na kutompa kura. Kesi siyo ngumu kama unavyosema.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom