Kesi ya Mahalu: Nani kilaza hapa?

Duh JF bwana, sasa kweli tumepanda kichwa, yaaani hata mahakama haijaaamua sisi tumesha iamulia hukumu, duh ukisikia masikio kupita kichwa ndio hii wakuu,

Duh tuiachieni mhakama kwanza iamue wakuu!

Mambo yanayo fanywa na JF kuanza kuangalia mambo kwa umbali na hata kutabili hufanywa sana na media na hasa US na nadhani watu kuelezea wanalo liona kutokana na mauza uza na ya kesi yenyewe inavyo pelekwa.

Sijaona watu wamesema wote kwamba Kesi imeisha ila mwekeleo ni sawa na ule wa mafisadi na EPA na madawa ya kulevya then people do connect events na kupata what they are saying now .Je ni mbaya ?
 
Mkuu ninakusikia, lakini kesi zetu zinatofautiana, Mahalu ni balozi wa kwanza nchini kurudishwa kwa kufukuzwa kazi na sababu kutolewa kuwa ni kutokana na wizi, sasa hii serikali jamani itakuwa ni ya namna gani, ambayo imekubali ku-act kutokana na ripoti ya wakaguzi wa hesabu, halafu isim-prosecute tena Mahalu kisheria baada ya kututangazia umma habari zake zote ambazo kama wangekuwa na nia ya kumuachia basi wasingezitoa hizo habari,

I mean ni kweli Jf siku zote tuko one step ahead, lakini sometimes pia ni vyema kuiheshimu inapojaribu kutumia haki, pale ni mahakamani Mahalu, ni professor wa sheria tena wa kuaminika sana, sasa mlitegemea nini kwamba atakuja kwenye kesi bila defense?

Ndio maana ya dual process, na advesarial process pande mbili zinatupiana mawe, ili apatikane mshindi kwa haki, mimi ninaaamini kuwa Mahalu hawezi kushinda hii kesi, kwa sababu muungwana, alikuwa akiijua toka akiwa waziri wa nj na ushahidi upo, Mahalu angekuwa anaamini ameonewa na serikali angekuwa ameshaenda kwenye sheria kuishitaki serikali.

Hapa panahitaji subira wakuu!
 
Mkuu ninakusikia, lakini kesi zetu zinatofautiana, Mahalu ni balozi wa kwanza nchini kurudishwa kwa kufukuzwa kazi na sababu kutolewa kuwa ni kutokana na wizi, sasa hii serikali jamani itakuwa ni ya namna gani, ambayo imekubali ku-act kutokana na ripoti ya wakaguzi wa hesabu, halafu isim-prosecute tena Mahalu kisheria baada ya kututangazia umma habari zake zote ambazo kama wangekuwa na nia ya kumuachia basi wasingezitoa hizo habari,

I mean ni kweli Jf siku zote tuko one step ahead, lakini sometimes pia ni vyema kuiheshimu inapojaribu kutumia haki, pale ni mahakamani Mahalu, ni professor wa sheria tena wa kuaminika sana, sasa mlitegemea nini kwamba atakuja kwenye kesi bila defense? Ndio maana ya dual process, na advesarial process pande mbili zinatupiana mawe, ili apatikane mshindi kwa haki, mimi ninaaamini kuwa Mahalu hawezi kushinda hii kesi, kwa sababu muungwana, alikuwa akiijua toka akiwa waziri wa nj na ushahidi upo, Mahalu angekuwa anaamini ameonewa na serikali angekuwa ameshaenda kwenye sheria kuishitaki serikali.

Hapa panahitaji subira wakuu!


Es kuna reports kama za EPA bado zina hang hakuna aliyechukuliwa hatua na siamini kama wanategemea kuchukua hatua .Je unasemaje kuhusu hili mkulu ?Nini tofauti ya kesi ya Mahalu na EPA ambayo inapigwa dana dana ?
 
Mhhhh Mkuu mbona una mbio sana, kwanza hapa tuongee Mahalu, EPA si inayo thread yake mkuu hapa JF, anyways mkuu sina sana dataz za EPA, ndio maana hujaniona sana kwenye hilo lakini ninazitafuta mkuu.
 
Takukuru wanaweza kushindwa hii kesi kwa uzembe au kwa makusudio.

Tukumbuke Mahalu hana hatia mpaka atiwe hatiani. Aliyeuza nyumba ataletwa kama shahidi wa Mahalu? Nadhani hataletwa kama shahidi wa mashtaka. Angekuwa upande wao basi wangemsimamisha kabla ya huyo Marco Papi (Notary Public). Tungojee ushahidi wa auditors.

Zingatia kwamba ushahidi wa Marco Papi umeonyesha kulikuweko na mkataba wa viuro milioni na ushee, lakini haukuonyesha kwamba haukuwepo mkataba wa pili (ambao utakuwa umeshuhudiwa na Notary Public mwingine). Mahalu hana jukumu la kuonyesha kulikuweko na mkataba wa pili. The onus is on the prosecution to prove that there was no other contract. Do they know that?

Takuru na Takukuru walishapoteza makesi huko nyuma, kutokana na uwezo mdogo. I doubt that they have the cranial capacity to win this case either. I'd be happy to be proved wrong.

Augustine Moshi
 
Mkuu Moshi,

Busara ni kuiachia mahakama iamue, ndio tulijadili otherwise ni kuingilia utaratibu wake na kujaribu ku-influence matokeo hiyo siyo haki kwa pande zote mbili, kuanzia jamhuri na mshitakiwa.
 
Mkuu ES,
Heshima mbele Mkuu!

We are certainly free to discuss an ongoing case. We are neither the judge nor the jury. We have freely discussed the cases of Ditto and Justine Nyari. Why must Mahalu be treated differently? We are not alone in this. In the US, they discussed OJ's case ad nauseam!

Journalists wouldn't bother to write about court cases if these could not be discussed. Let the powers that be sequester the poor witnesses and magistrates if they do not want them to hear what we have to say.

Remember that we are not a disinterested party. It is our money that they have stolen (and are still stealing). It is our poor brothers and sisters that Ditto and company shoot, for fun, on the streets. It is diamonds that should rightly belong to us that Justin Nyari and other armed leaders hijack on our roads.

We can't just keep quiet while they go thorough the motions of a court case. We will say what we think, anytime and every time we wish to do so.
 
Augustoons said:
Kesi ya mahalu si rahisi kama wengi wanavyofikiri hapa.

Kesi hii ndani yake kwa habari za kusadikika toka kwa watu waliokaribu na mahalu na serikalini inahusu mapenzi, siasa na kukosekana kwa mgao ndani ya pesa za kununulia jengo.

Kwa ufupi tu Rostam pia anahusika, balozi aliwahi kupitisha pesa fulani za uchaguzi kupitia embassy Italy, lakini baadaye alikataa kupitisha hela chafu za uchaguzi wa Rais 2005 kwaajili ya Rostam na kundi lake akiwamo Prezidar, kukataa huku kulimjengea chuki na kundi hilo lililoapa kulipa kisasi.

Stori ya pili, balozi alikuwa na mahusiano na Grace wakati Rais pia akiwa waziri alikuwa na mahusiano naye,aidha katika mgao wa pesa hizo inasadikika lumbanga alikosa mgao kwa kuwa walikubaliana kuhusu hizo dili balozi alichofanya alishtuka na kuamua kumlipa huyo mama moja kwa moja kupitia akaunti yake yaani bank to bank transfer ili anayetaka mgao amfuate huyo mama ndio amgawie, kwa hali hii wengi walikosa walichotegemea.

Hivyo bilioni tatu zote ziliingia kwenye akaunti ya huyo mwenye nyumba, kama Mahalu alipata basi ni kwa huyo mama kutoa hela benki na kumpa mshiko wake akafie mbele. Hapa ndio ugumu unapokuja. Wakati huohuo inasemekana mahalu hana akaunti popote nje ya nchi, akaunti anayotumia siku zote ni ya mke wake hapa na yake binafsi ni ile iliyopo hapa nchini. So which is which yetu masikio ngoja tusubiri.

Ila kweli haowaandishi vilaza, ndio maana beni alikuwa akiwapaka. Aiiiiiiiiiibu

Jamani kwanza Augustoons na yeyote aliyekuunga mkono maelezo yako hayana mashiko na yanaelemea katika majungu yasiyo na ukweli wowote. Labda ungesema kwamba Bi Grace ni mke wa mtu (which is fact) na kwamba mume wake walitengana na sababu ni Mahalu (which is fact) na kwamba upo uwezekano kwamba mumewe Grace (Martin) alishiriki ununuzi wa nyumba awamu ya kwanza waliyolipa Euro milioni moja (which is fact) na baadaye Grace na hawara yake (Mahalu) wakafanya deal baada ya kuona fedha walizopewa na serikali kwa idhini ya Kikwete (Waziri wa Mambo ya nje) zilikua zimebaki kama Euro milioni mbili hivi, wakaamua kucheza dili.

Kuna maneno (hakuna ushahidi) kwamba Mkapa na alimpa idhini Mahalu kuchota kiasi kilichosalia (Hakuna Ushahidi).

Sasa kwa wale wanaosema Mahalu atashinda sina hakika wana kigezo gani. Kwanza kabisa Kikwete alikua hapendezwi na dharau ya Mahalu kwake kwani alikua akiwasiliana moja kwa moja na Mkapa na si Waziri na alimdharau sana kwa kusema kwamba wote ni wateule wa Rais.

Na kwa hili alikua akiwasiliana mara kwa mara na Mkapa kwa hiyo JK analijua sana suala hilo na ndio maana THISDAY walipoandika kuhusu Mahalu, JK aliwasifu alipotembelea Wizara ya Habari katika ziara zake za mwanzo katika wizara

Ama kuhusu waandishi kukosea title ya huyu Mtaliano (Marco Papi) aliyetoa ushahidi, tatizo kubwa lilikua la Mkalimani (Padri wa Boko) ambaye alitafsiri kwa mara ya kwanza kama Papi alikua Mwanasheria Mkuu wa Italia, lakini kwa waliofuatilia na kupata ufafanuzi waliopatia

Lakini hata mawakili wa utetezi kama baadhi ya watu hapa wanavyosema ni kwamba Mahalu alikua anao mkataba wa pili lakini Papi aliiambia Mahakama ya Kisutu kwamba KISHERIA hakuna mkataba wa pili na ofisi yake ndio pekee inayosajili mikataba HALALI. Sasa Mahalu na mawakili wake wanayo mikataba miwili, mmoja ukiwa uliosainiwa kuhalalisha malipo na kwamba alifanya hivyo na kupeleka nyaraka zote serikalini (Ikulu) akielezea kwamba alilazimika kufuata "desturi" ya watu wa Italia kuwa na mikataba miwili, mainly kukwepa kodi, lakini je, serikali inaweza kukwepa kodi ya nchi nyingine?

Ni halali kisheria kuwa na mikataba miwili? Je, ubalozi (Viena Conv) si huwa wanasamehewa kodi? Ina maana Serikali ya Italia ilikataa kusamehe kodi? Si kweli, Ubalozi ulisamehewa.

Jambo la msingi hapa ni kuangalia mwenendo wa kesi kwani Mahalu na Grace wanatetewa na Mawakili makini sana na PCCB wana wanasheria dhaifu sana japo sasa wameanza kuamka na kupata msaada wa wanasheria wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu. HAKUNA AJABU kwa Mahalu kushinda japo itakua ni AIBU.
 
Kwanza kabisa Kikwete alikua hapendezwi na dharau ya Mahalu kwake kwani alikua akiwasiliana moja kwa moja na Mkapa na si Waziri na alimdharau sana kwa kusema kwamba wote ni wateule wa Rais. Na kwa hili alikua akiwasiliana mara kwa mara na Mkapa kwa hiyo JK analijua sana suala hilo na ndio maana THISDAY walipoandika kuhusu Mahalu, JK aliwasifu alipotembelea Wizara ya Habari katika ziara zake za mwanzo katika wizara

ACTUALLY MAHALU NA MKAPA NI MASHEMEJI. MKE WA MKAPA MAMA ANNA NA MKE WA MAHALU WANA UNDUGU NA NI MAJIRANI KULE KIJIJINI. WAMECHEZA WOTE TOKA UTOTONI MPAKA UKUBWANI WANAIBA PAMOJA.

UGOMVI WA WAZIRI WA ZAMANI WA MAMBO YA NJE NA MAHALU UNAHUSISHWA NA SHAMBA LA NAFCO LILILOKO BAGAMOYO(KWA WALE MNAOENDAGA BAGAMOYO MTAKUWA MMELIONA SHAMBA LILILOJAA MINAZI MINGI BARABARANI). LILE SHAMBA LILINUNULIWA KWA BEI YA KUTUPA NA MAHALU KWA KUKINGIWA KIFUA NA MKAPA NA HILI LIMUUDHI SANA WAZIRI WA ZAMANI(SASA NI MKUU WA KAYA) KWA SABABU YEYE ALITAKA WAPEWE WATU WA BAGAMOYO(AU NDUGU ZAKE).

KAMA MAHALU ATASHINDWA KESI NA MALI ZAKE KUTAIFISHWA LILE SHAMBA LITAKUWA MALI MOJAWAPO. SIDHANI KAMA WATASHINDA KESI WAKATI MZEE WA KAYA YUKO NYUMA YA KESI.
 
Maoni yangu ni kuwa PW wa kwanza wa PCCB angekuwa owner/administrator wa hiyo nyumba. Huyu ndiye anayejua bei halisi ya hiyo nyumba. Hawa wengine wangejazia jazia mapungufu .
 
Maoni yangu ni kuwa PW wa kwanza wa PCCB angekuwa owner/administrator wa hiyo nyumba. Huyu ndiye anayejua bei halisi ya hiyo nyumba. Hawa wengine wangejazia jazia mapungufu .
Heri, kwanza soma story nilizoweka link hapo juu utapata jibu. ukweli huyo unayesema mmiliki alikwishatoa maelezo lakini amekataa kuja Tanzania, amesema yeye alikwishamaliza deal na kwamba hawezi tena kupoteza muda wa biashara zake.


Katika mazingira ya kawaida, hakuna mfanyabiashara kutoka nchi ya Ulaya anayeweza kukubali kuhusishwa na ukwepaji kodi wa serikali yake na hilo ndilo linaloweza kumfanya huyo mama mmiliki 'kumkana' MAhalu kama kweli walicheza wote hilo dili kama anavyokiri Mahalu mwenyewe ambaye sasa amekua MLOKOLE na kila kitu sasa anamtaja MUNGU. Suala la "BEI HALISI" halihitaji PW wala DW. Linahitaji ushahidi wa maandishi na taratibu kufuatwa.

Hata kama Mahalu na wenzake wana ripoti ya mthamini kwamba bei ni EURO milioni 3, bado hana ushahidi wa kisheria wa mkataba wa bei hiyo mbali ya ule wa Euro milioni moja. Kwa hiyo mwalimu wa wanasheria (Mahalu) anahitaji msaada mkubwa kuweza kujinasua.
 
ACTUALLY MAHALU NA MKAPA NI MASHEMEJI. MKE WA MKAPA MAMA ANNA NA MKE WA MAHALU WANA UNDUGU NA NI MAJIRANI KULE KIJIJINI. WAMECHEZA WOTE TOKA UTOTONI MPAKA UKUBWANI WANAIBA PAMOJA.

UGOMVI WA WAZIRI WA ZAMANI WA MAMBO YA NJE NA MAHALU UNAHUSISHWA NA SHAMBA LA NAFCO LILILOKO BAGAMOYO(KWA WALE MNAOENDAGA BAGAMOYO MTAKUWA MMELIONA SHAMBA LILILOJAA MINAZI MINGI BARABARANI). LILE SHAMBA LILINUNULIWA KWA BEI YA KUTUPA NA MAHALU KWA KUKINGIWA KIFUA NA MKAPA NA HILI LIMUUDHI SANA WAZIRI WA ZAMANI(SASA NI MKUU WA KAYA) KWA SABABU YEYE ALITAKA WAPEWE WATU WA BAGAMOYO(AU NDUGU ZAKE).

KAMA MAHALU ATASHINDWA KESI NA MALI ZAKE KUTAIFISHWA LILE SHAMBA LITAKUWA MALI MOJAWAPO. SIDHANI KAMA WATASHINDA KESI WAKATI MZEE WA KAYA YUKO NYUMA YA KESI.


Zaidi ya hayo, urafiki wa Mkapa na Mahalu ulitokana na wote wawiili kusota pamoja pale wizara ya elimu ya juu. Wakati Mkapa ni waziri wa elimu ya juu, Mahalu alikuwa mkurugenzi wa elimu ya juu. Walikuwa wananyanyaswa na Bilali
(huwa nachanganya haya majina na Balali), yule aliyekuwa katibu mkuu wa wizara na ambaye alikuwa karibu sana na Mwinyi.

Mkapa alipopata urais basi ikabidi amnyanyue na mshikaji wake. Bahati Bilali akaokolewa na Komandoo na kurudishwa Zanzibar.

Ufisadi wa hawa jamaa unajulikana tokea alipokuwa pale wizarani. Zile posho za wanafunzi wa USA, scholarship za chupi nk.

Labda sasa ni muda wa yeye kulipa makosa yake ya muda mrefu.
 
hilo halina mpinzani, waandishi wa habari wa kibongo wengi wanachosha. habari haiandikwi kwa kituo. sijui hata kama yeye mwenyewe anaisoma mara mbili kabla ya kuifikisha kwa editor.
Ma-editor wenyewe kama wanapokea tu story bila kuzipitia basi nao bila shaka watakuwa vilaza.
 
Waheshimiwa,

Kama msingi wa utetezi wa Mahalu ni kuweko mkataba wa pili ambao sababu zake ni kukwepa kodi kwa muuzaji, basi atashindwa. Ataweza kweli balozi mzima kusimama mahakamani na kusema alishirikiana, kama balozi, kudanganya serikali ya Italia kuhusu kiasi cha fedha alicholipwa muuzaji, ili muuzaji ailipe kodi ndogo? Hilo litakuwa kukubali kwamba yeye Mahalu ana kosa la jinai la FRAUD huko Italia, na alilifanya kama Balozi wa Tanzania.

Ushahidi wa Marco Papi ni mzito sana. Mkataba wa pili (ambao inadhaniwa Mahalu anao), kama si wa kisheria, hauwezi kukubalika mahakamani kama ni mkataba. Bila shaka Mahalu alijua kwamba mkataba hauwi wa kisheria Italia mpaka utiwe sahihi na Notary Public (kama Marco Papi).

Ndiyo maana wa kwanza aliupeleka kwa Marco Papi. Kama huo wa pili hauna sahihi ya Notary Public basi wala asihangaike kuuleta mahakamani kwani si wa kisheria (na kwa hivyo si mktaba).
 
The presiding magistrate has already opened an avenue for appeal. He has agreed, in court, that he privately discussed the selection of an interpreter with the Prosecutor. When the defense raised an objection on the selection, he simply overruled them. This can be grounds for appeal later (if Mahalu loses). Why was the learned magistrate not aware that he ought to have held a meeting with both the prosecution and the defense side to decide on the interpreter?

We must keep in mind that Mahalu does not have to prove that he is innocent. It is up to the prosecution to prove him guilty. If he can cast some reasonable doubt on the evidence adduced, such as that the interpreter may have been biased, incompetent, or both, then Marco Papi's appearance will have been for nought.

If Mahalu is found to not be guilty, it will not follow that he is innocent. The court does not have to find him innocent in order to clear him. In fact it is almost impossible for a court to find someone innocent. Courts clear people when they do not find them guilty, not when they find them innocent. They simply do not have this latter task.
 
Mhasibu amkandamiza Prof Mahalu mahakamani (Mwananchi)

Na Tausi Ally

ALIYEKUWA Mhasibu katika Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Stewart Migwano (47), ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam namna alivyoandaa hati ya Euro 3,098,741.40 kwa ajili ya maalipo ya ununuzi wa Jengo la Ubalozi nchini humo.

Hayo aliyasema jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi, Sivangilwa Mwangesi wakati akitoa ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na aliyekuwa Afisa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania uliopo nchini Itali, Grace Martin.

Akitoa ushahidi huo, Migwano alidai kuwa alipokuwa Mhasibu nchini Italia kuanzia Julai 2001 hadi Januari 2007, alikuwa akifanya kazi ya kuandaa maalipo na kupokea fedha zote za maduhuli (mapato) na kwamba alikuwa akifanya kazi hizo kupitia maelekezo aliyokuwa akipewa na aliyekuwa Grace Martin.

Alidai kuwa anafahamu kuwa jengo hilo lilinunuliwa kwa Euro 3,098,741.40 na kwamba aliandaa hati ya maalipo ya ununuji wa Jengo hilo la Ubalozi nchini Italia na kuisaini baada ya kupata barua iliyomuelekeza kufanya hivyo.

Alidai kuwa fedha hizo za ununuzi wa jengo hilo zilitumwa kwa awamu tatu tofauti, za awamu ya kwanza zilitumwa Machi 2002, awamu ya pili Julai 2002 na za awamu ya tatu zilitumwa Agosti 2002.

Alidai zaidi kuwa Septemba 24, 200, Serikali ya Tanzania ilituma Euro 2,065,827.60 kwenda Monaco na Euro 1, 320,913.80 kwenda kampuni ya Ceres inayoendeshwa na Fioreolla Pegliuca kwa ajili ya ununuzi wa jengo hilo na kwamba zote zilifika katika kampuni husika.

Baada ya maelezo hayo, Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB), Abubakar Msangi alimhoji Migwano kuwa wakati wanafanya mauziano ya jengo hilo kuna mkataba wowote aliyowahi kuuona.

Migwano alijibu kuwa mpaka wanafanya maalipo ya ununuzi wa jengo hilo hakuwahi kuuona mkataba wowote bali ulikuwa unashughulikiwa.

Msangi alimhoji shahidi huyo, kuwa kulikuwa na haraka gani ya kufanya maalipo ya ununuzi kabla ya mkataba.

Naye alisema hafahamu kwanini ilikuwa hivyo na kuongeza kwamba aliwahi kuona barua kwenye mafaili ikidai kuwa taratibu zote za ununuzi wa jengo hilo zimekwisha kamilika bado kusaini mkataba.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuhujumu uchumi kwa kuisababishia hasara serikali ya Euro 2,065,827.60 wakati wakiwa maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Itali.

Ilidai kuwa Septemba 23 mwaka 2002 katika ubalozi wa Italia jijini Roma, washitakiwa wakiwa waajiriwa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, walisaini vocha yenye namba D2/9/23/9/02 ikionyesha kuwa bei ya ununuzi wa jengo hilo kuwa ni Euro 3,098,741.58 maelezo ambayo yanadaiwa kuwa ni ya uongo na yenye nia ya kumdanganya mwajiri wao.

Katika shtaka la tatu wanadaiwa kuwa Oktoba Mosi, 2002 washitakiwa hao kwa pamoja wakiwa waajiriwa wa serikali kwa pamoja walisaini mkataba wa mauzo na shitaka la nne, wanadaiwa kuwa Oktoba Mosi, 2002, walitumia hati ya malipo ya Euro 3,098,741.58 kwa maelezo kuwa muuzaji wa jengo la ubalozi mjini Rome alipokea fedha hizo huku wakijua kwamba ni uongo.

Katika shitaka la tano, wanadaiwa kuwa Oktoba Mosi, 2002 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, washitakiwa hao kwa pamoja waliiba euro 2,065,827.60 ambazo zilikuwa mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Mhasibu 'amtosa' Balozi Mahalu

Shadrack Sagati
Daily News;
Thursday,April 24, 2008

ALIYEKUWA Mhasibu katika Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Steward Migwano, amedai alielekezwa na Balozi Costa Mahalu kuandaa malipo ya Euro milioni tatu kwa ajili ya ununuzi wa jengo la ubalozi bila ya yeye kuona mkataba wa mauzo.

Migwano aliyefanya kazi Ubalozi wa Tanzania nchini Italia kuanzia Januari 2001 hadi Januari 2007 kama mhasibu, alisema alipojaribu kuhoji juu ya mkataba wa mauzo wa jengo hilo, alielezwa na Profesa Mahalu kuwa mkataba huo ulikuwa bado uko kwenye mchakato wa kuandaliwa.

Migwano, ambaye kwa sasa anafanya kazi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, aliiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kuwa aliandaa malipo ya Euro 3,098,741 kama alivyoelekezwa na Balozi Mahalu pamoja na Ofisa Utawala wa ubalozi huo, Grace Martin, ya ununuzi ya jengo hilo.

"Balozi aliniambia kwa kuwa mkataba unahusisha nchi mbili bado ulikuwa kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Italia kwa kukamilisha taratibu mbalimbali…hivyo nikafanya malipo yake kutokana na barua alizokuwa anafanya balozi na wizara," alisema shahidi huyo aliyekuwa anaongozwa na Wakili wa Serikali, Ponsiano Lukonsi.

Migwano alisema hata hivyo baada ya kufanya malipo hayo, alikuja kuona mkataba uliosajiliwa kwenye mamlaka za Italia ambao ulieleza kwa uwazi kuwa ununuzi wa jengo hilo ulifanywa kwa Euro 1,032,912 na siyo Euro 3,098,741 kama alivyoelekezwa na maofisa hao waandamizi wa ubalozi.

Mahalu na Grace wote wanashitakiwa kwa kula njama na kuisababishia hasara Serikali ya Tanzania ya Euro 2,065,827.60. Wanadaiwa kutenda kosa hilo mjini Rome, Italia wakati wakiwa watumishi kwenye ubalozi huo mwaka 2002.

Mbele ya Hakimu Sivangilwa Mwangesi, shahidi huyo alisema yeye alijiridhisha na kuidhinisha malipo hayo kwa vile aliona barua ambayo iliandikwa na Balozi Mahalu kwenda Wizara ya Mambo ya Nje ikieleza kuwa tayari alishakamilisha taratibu zote za manunuzi ya jengo hilo.

Alisema baada ya kufanya malipo hayo alipata taarifa kutoka benki ambako walikuwa wanahifadhi fedha za ubalozi kuwa, malipo aliyofanya yalipelekwa kwenye akaunti mbili zilizoko benki mbili.

Alifafanua kuwa kwa mujibu wa ripoti ya benki hiyo, Euro 1,032,912 zilipelekwa kwenye benki moja mjini Rome na Euro 2,065,839.60 zilipelekwa katika benki iliyoko Monaco.

Akihojiwa na wakili wa utetezi Bob Makani, shahidi huyo alisema hakuwahi kushirikishwa katika maandalizi ya ununuzi wa jengo hilo zaidi ya kuelezwa na wakubwa wake kuandaa malipo ya ununuzi.

Pia alikana kuona tathmini inayodaiwa kufanywa na mtathmini wa serikali iliyothibitisha kuwa jengo hilo thamani yake ilikuwa ni Euro milioni tatu. "Nakumbuka nilimwona Kimweri lakini sikujua kama alikuja kufanya kazi hiyo." Kesi hiyo itaendelea tena Aprili 27, mwaka huu.
 
na wewe mhasibu gani unatoa tu pesa bila kuona unadaiwa kiasi gani!
mtatajana mwaka huu mpaka mmalizane.....
na moto umeanza huo hauzimi leo wala kesho, mpaka wote wamalizike
 
Hivi mume wake Grace alikuwa anaitwa nani? Je huyu mhasibu ndiye alikuwa bwanake Grace?

Inaelekea nchi inapoteza/imepoteza pesa nyingi sana kwenye hizi dodgy deals.
 
Back
Top Bottom