Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Status
Not open for further replies.
Taarifa nyingine toka Bongo (bado sijaithibitisha), ni kwamba Bw. Liyumba amelazwa hospitali (sijajua hospitali gani) akiwa hoi baada ya blood pressure kupanda.
 
Mawakili wa Liyumba pia waliwasilisha hati ya kusafiria ya mshitakiwa huyo yenye namba A0320091 ambayo muda wake wa kutumika ulimalizika tangu Februari 12, mwaka juzi. Baada ya mahakama kutoa dhamana hiyo, waendesha mashitaka ambao hawakuridhika na uamuzi huo, waliahidi kufanya kikao ili kujadili mwenendo wa suala hilo. Liyumba ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, katika kesi hiyo anashitakiwa pamoja na Deogratius Kweka ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Miradi BoT.

duh kumbe hiyo hata iliisha muda tu, tangu Feb mwaka juzi... kweli hili movie
 
Ndugu wananchi msiwe na wasiwasi mkuu AL atarudi tu, kuna ka-prosidya kadogo ka-tiba kanafanyika... kwani HEAMODIALYSIS huwa inachukua muda gani, nafikiri wataalam wa afya watatusaidia hapa!
 
Kama ni kweli itathibitishwa Liyumba ametoroka, kwa mujibu wa mwenendo wa kesi za jinai, kesi hiyo kesho inafutwa rasmi na mtuhumiwa anaachiwa huru.
Hivi ndivyo ilivyofanyika wakati wa Kesi ya Pili ya Uhaini Tanzania, Mwaka 1983, baada ya kutoroka gereza la Ukonga, Mshtakiwa wa kwanza, Father Tom na mshtakiwa wa pili, Hatty McGhee, kesi hiyo ilifutwa rasmi na washtakiwa wengine wote 29 waliachiwa huru. Hata hivyo, washtakiwa wote walikamatwa mara tuu baada ya kutoka mahakani na kesho yake walifikishwa tena mahakamani kusomewa mashitaka mapya.
Kwa hiyo kesi ya Liyumba itafutwa kesho, mshtakiwa mwenza ataachiwa huru, labda serikali ikiamua kumkamata tena na kumfungulia kesi mpya.

Pamoja na jamaa kutoroka, serikali ilikurupuka kufungua mashtaka ya thamani yote ya majengo pacha kana kwamba mradi mzima ni mradi batili.
Angetokea mwanasheria wa John Cochram type, angemwambia Liyummba na mwenzake wakubali kosa, wairudishie serikali hizo
Bilioni 200 na majengo pacha yawe ya mwekezaji mpya.

The-proper charge ya kuitia hasara serikali, ilikuwa ifanyike baada ya valuation ya Twin Towers. Then unacompare value halisi na value iliyozidishwa, ndipo unawafungulia kesi ya kusababisha hasara ya kile kiasi tuu kilichozidi.

Pamoja na hasira zetu zote kuhusiana na hivi vitendo vya ufisadi,
Waliovitenda ni binadamu, hivyo ubinadamu uko pale pale kama Mkapa anavyoheshimiwa pamoja na madudu yote yaliyofanyika wakati wa utawala wake.

are you serious Mkapa anaheshimiwa, na nani ? nnavyo jua mimi anazomewa kila anapokwenda ama kama unamchanganya na Mzee Mwinyi,

SAHIBA,
 
Yupo dar wakuu ila ni kweli afya na mshituko vyaweza kutupatia sura mpya juu ya hatima ya maisha yake na mwenendo mzima wa kesi, tumuombee mungu amponye ktk kipindi kizito cha maisha yake.

Lakini naamini hakimu mama hadija msongo naye yuko matatani ktk hili.
 
are you serious Mkapa anaheshimiwa, na nani ? nnavyo jua mimi anazomewa kila anapokwenda ama kama unamchanganya na Mzee Mwinyi,

SAHIBA,

Tupo ambao bado tunampa heshima yake kwa yale mazuri aliyojitahidi kuyafanya ingawa tunatatizwa sana na mabaya anayosemekana kuyafanya yeye kama mtu binafsi na yale kama kiongozi wa CCM.

Omarilyas
 
Ndugu wananchi msiwe na wasiwasi mkuu AL atarudi tu, kuna ka-prosidya kadogo ka-tiba kanafanyika... kwani HEAMODIALYSIS huwa inachukua muda gani, nafikiri wataalam wa afya watatusaidia hapa!

inaweza ikamchukua wiki kadha ila itategea na maelezo ya daktari(nephrologist) wake.
 
Ndugu wananchi msiwe na wasiwasi mkuu AL atarudi tu, kuna ka-prosidya kadogo ka-tiba kanafanyika... kwani HEAMODIALYSIS huwa inachukua muda gani, nafikiri wataalam wa afya watatusaidia hapa!

Hapana, wala tatizo si hilo. Baada ya kutoka alikwenda kwa mganga wake bagamoyo, akaambiwa kuna shari la kuwekwa ndani kwa siku kadhaa, akakubali. Hivyo siku akiachiwa na mganga wake mtamuona na hiyo itakuwa kabla ya Feb 24
 
Ndugu wananchi msiwe na wasiwasi mkuu AL atarudi tu, kuna ka-prosidya kadogo ka-tiba kanafanyika... kwani HEAMODIALYSIS huwa inachukua muda gani, nafikiri wataalam wa afya watatusaidia hapa!

...ndio kusema, mzee wa mahenge yupo kwenye Dializer, ambayo huchukua kati ya masaa mawili mpaka manne kwa session moja ya Hemodialysis. inategemeana na dakitari kashauri afanyiwe ngapi wiki hii... fingers crossed!
 
Nasikia kichefu chefu..... Yaani kweli nikasikia wadhamini wameshikiliwa wanaweza kushitakiwa, sasa naambiwa wameachiwa tena!!!!!Hii picha ina wachezaji wengi sisi tutaendeela kuwa Watazamaji, na ndio maana leo Peter Noni ni shahidi na mshitakiwa wa kesi za EPA. Na Noni kuwa shahidiwahandishi wa abari wanaandika (tunaandika) na wako wanaomjuita Peter .... na si Peter Noni yule ambaye ana ukwasi wa kutisha mwenye mapesa mengi ya Vodacom aloyomuuzia Rostam hisa

tuache majungu,mtu kuwa na pesa haina maana kaiba....umaskini wetu usitufikishe mahali tukawa na mawazo kuwa kila mtanzania mwenye pesa basi amefanya ufisadi,ulitaka noni ashitakiwe kwa kosa lipi?...kuuza hisa zake kwa rostam?....usikurupuke kuhukumu watu bila kujua utajiri wameupata vipi,....!
 
Ndugu wananchi msiwe na wasiwasi mkuu AL atarudi tu, kuna ka-prosidya kadogo ka-tiba kanafanyika... kwani HEAMODIALYSIS huwa inachukua muda gani, nafikiri wataalam wa afya watatusaidia hapa!
Kwa ni kweli yuko Dialysis then yuko Regency Hospital, by the way asilimia kubwa ya wagonjwa wanaofanyiwa Dialysis hapo Regency hatima yao huwa siyo nzuri. Wagonjwa wengi wa figo huenda India na huko ndiko matatizo hayo huonekana. Full circle ni masaa 4. Kwa vile Liyumba hajafanya siku nyingi hiyo Dialysis, hawezi kuanza na ful session, lazima aanze na masaa 2 next round ndio full circle. Watu wa dialysis ya HIV ya ukweli huifanyia London, hata hivyo afya zao bado zinatetereka kwa miili yao kupoteza nuru ya maisha (life force).
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom