Kesi ya Liyumba: Naibu Gavana aibua mambo mazito

Tanzania yetu Inateketea...Hivi unawezaje kumuajiri Naibu Gavana Mbumbumbu kama Reli kwenye kitengo muhimu kama hiki? yani ni kama pale BOT haelewi chochote kinachoendelea.....Tusisahau Mtu huyo huyo ndiyo mmojawapo wa magavana waliojengewa majumba ya mabilioni. Je, msaada wake katika kulijenga taifa uko wapi? mtu kama huyo ni wa kumstahafisha kwa maslahi ya Taifa. Na kesi hii ya Liumba mwisho wake naanza kuuona, Hii kesi imegeuzwa kabisa na kuimaliza kwa kutumia kivuli cha Gavana ambaye ni marehemu na idhinisho zote zilizopitishwa zitatupiwa kwake...By the end of time LIUMBA will be Free kwakuwa mabadiliko ya project hiyo yaliidhinishwa na Marehemu Gavana.

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu ibariki Africa.
Kesi hii ilifunguliwa baada ya kifo cha Gavana. Halafu Reli si mbumbu anasema anachokielewa, ujue kuwa yupo mahakamani na anatakiwa aseme ukweli na ambao anaweza kuutetea akiwekwa kwenye kona. Ukweli ni kwamba bodi ilipitisha mabadiliko na ndiyo maana yaliendelea. Kama bado haikuridhika basi aliyeruhsu matumizi bila adhini angechukuliwa hatua. inaonekana kila kitu hapo BoT kilfuata process na hat TZS1.2billion za nyumba ya gavana ilifuata process hiyo hiyo....Hapa tunachezewa kiini macho na serikali yetu..wanafungua kesi zisizo na ushahidi wa kutosha ili mradi tu donors waone kwamba wanachukua hatua, hata kama kesi itatupiliwa mbali na mahakama baadaye... in short wanaendelea ku-misues resources zetu!!!
 
Obi said:
Hapa kuna changa la macho. Kama ripoti ya ujenzi wa majengo pacha haijakamilika je hiyo hasara ambayo serikali inadai imepata ilikokotolewa kwa njia gani na kutoka wapi? Na je Liyumba anashitakiwa kwa kosa gani wakati BOT wenyewe kupitia kwa Naibu Gavana Juma Reli wamesema BOT haikupata hasara kwa sasa kwa sababu final financial report haijakamilika. Ieleweke kwamba simtetei mtu hapa. Nashindwa kuelewa credibility ya serikali mpaka inapeleka kesi mahakamani bila kuwa na ushahidi wa kutosha. Ikumbukwe kuwa fedha zinazotumiwa kuendesha hiyo kesi ni ya walipa kodi wa Tanzania, ilitokea Liyumba kweli hana kosa serikali itatuambia nini? Kwamba wametumia mamilioni ya walipa kodi kuendesha kesi isiyo na ushahidi uliojitosheleza na hatimaye kushindwa?


Obi,

..naunga mkono hoja zako 100%.

..mawakili wanapaswa kuwaandaa mashahidi wao kabla hawajawapeleka mahakamani.

..kama wakili anaona shahidi hayuko tayari, au ushahidi wake hauwezi kumsaidia kupata hakumu anayoitarajia, basi wakili anapaswa kuachana na shahidi huyo.

..nimeshangazwa sana na ushahidi wa Naibu Gavana Juma Reli, ukizingatia kwamba ni shahidi wa upande wa mashtaka.
 



Obi,

..naunga mkono hoja zako 100%.

..mawakili wanapaswa kuwaandaa mashahidi wao kabla hawajawapeleka mahakamani.

..kama wakili anaona shahidi hayuko tayari, au ushahidi wake hauwezi kumsaidia kupata hakumu anayoitarajia, basi wakili anapaswa kuachana na shahidi huyo.

..nimeshangazwa sana na ushahidi wa Naibu Gavana Juma Reli, ukizingatia kwamba ni shahidi wa upande wa mashtaka.
Kesi zote za ufisadi zilizo mahakamani ni changa la macho tu! Kwani hamfahamu enyi wadanganyika?
 
mlitegemea nini kama naibu gavana ni kilaza....kwa credential zake ..advance diploma na MBA ....hazitoshi kumfanya awe naibu gavana..ni AHSANTE MUUNGANO!!!...ilibidi naibu gavana atoke zanzibar....walipochagua BOT walimtaka jamaa mmoja anatoka PEMBA ...ni Phd holder...serikali ya zanzibar ikamkataa....wakampendekeza RELI

Ndo swali langu kila siku.
BOT ni Nerve centre ya financial institutions nchini. Je, wakuu ni watu wa aina gani? BNest trained we have? Au maficho ya watoto wao waliokosa ajira za maana na hapo ndo kuna pesa ya bure.

Wamesoma kwa kuunga-unga halafu unawapa Ukurugenzi.

Hivi Gavana ana u-profesa wa nini na wapi? Chuo kipi kilimpa u-profesa?
 
Yaaani mie nimeangalia jana nikabakia kushangaa ..kama Gavana hajui lolote huyo Liumba wamemuweka ndani kwa nini??
Nasikia kawekwa ndani kwa shinikizo ya mkulu. Inahusu yule kisura aliyehitimu London aliyeonekana Michuzi akivaa gauni jekundu.
 
Nimemkumbuka Askofu Valentino Mokiwa alisema hizi kesi ni za visasi sasa tunaona kumbe ni majungu tu duh sasa hizi siasa
 
Hivi katika zile nyumba mbili za mabilioni moja ni kwa ajili ya huyu Bwana Reli ? It is only in Tanzania where a person can be less than a mediocre , and be awarded a prestige position as well as a mansion. This guy is too shallow and to put it bluntly ......He is an empty suit.
 
ukurupukaji wa pccb tu kupeleka watu mahakamani bili vigezo na ushahidi liyumba the former great seminarian will be released soon,
 
Mundele,

Thank you for your comment that this Deputy Governor Reli is "Mbumbumbu". This country of ours is going down the drain because of the mediocre peolpe we have put in charge of crucial institutions like BoT.

First of all, it should be understood that the Twin Towers of BoT are there and that they belong to the People of Tanzania. Liyumba cannot therefore be accused of stealing the whole value of the Towers.

It should also be understood that as a public building, it ought to have been the subject of a public tender and that the cost of its construction should have been known (presumably the lowest tenderer) and fixed before construction started.

During the construction it is possible for variations to be proposed either by the BoT or by the contractor; but such variations would have been the subject of discussion and approval of the Board under the Chairmanship of the Governor; and additional costs or even reduced costs would known and be recorded. Under no circumstances would such approval be approved by a Manager like Liyumba.

The difference between the agreed tender price and what was actually paid, if payment was improperly effected by Liyumba, would then be the amount of loss caused by Liyumba. This should be known now; and it should not await the completion of accounts as iimplied by this naive Deputy Governor Reli.

It is a shame that the most prestigious financial institution of Tanzania is run (or rather is being ruined) by the likes of Reli.
 
Hivi kweli naibu gavana wa benki kuu, maswali ya msingi kabisaaa ya utendaji wake wa kila siku...majibu yanakuwa "sikumbuki/sikumbuki sawa sawa", huu ni utani mahakamani/kazini. ". HERI KUJIKWAA KIDOLE KULIKO ULIMI"

Ama kweli hii kesi ina mkono wa mtu, Naibu Gavana mbele ya majaji anasema mradi huo hauna madhara yeyote kwa BOT...so tunaposema Liyumba ana kesi ya kuitia hasara serikali tunapatia au ndio kusema MAITI HAULIZWI SANDA?
 
Mundele,

Thank you for your comment that this Deputy Governor Reli is "Mbumbumbu". This country of ours is going down the drain because of the mediocre peolpe we have put in charge of crucial institutions like BoT.

First of all, it should be understood that the Twin Towers of BoT are there and that they belong to the People of Tanzania. Liyumba cannot therefore be accused of stealing the whole value of the Towers.

It should also be understood that as a public building, it ought to have been the subject of a public tender and that the cost of its construction should have been known (presumably the lowest tenderer) and fixed before construction started.

During the construction it is possible for variations to be proposed either by the BoT or by the contractor; but such variations would have been the subject of discussion and approval of the Board under the Chairmanship of the Governor; and additional costs or even reduced costs would known and be recorded. Under no circumstances would such approval be approved by a Manager like Liyumba.

The difference between the agreed tender price and what was actually paid, if payment was improperly effected by Liyumba, would then be the amount of loss caused by Liyumba. This should be known now; and it should not await the completion of accounts as iimplied by this naive Deputy Governor Reli.

It is a shame that the most prestigious financial institution of Tanzania is run (or rather is being ruined) by the likes of Reli.
Kilasara,
you are right. The straight answer here is that Reli has talked the truth. PCCB has not established the truth before taking the case to court and that is why Reli couldn't admit that there is "hasara" caused by Liyumba. To me he is a man who stayed to the truth. he has not either said that Liyumba or governor or board had unlawfully approved expenditure regarding to the building-meaning that all the variations and expenditure were approved as required. When people wants him to say the amount that BoT has lost, he cannot as no money BoT has lost as they have the building and they did allow the variations.
To me Reli is right and to this, he has stood to say the truth. We shouldn't be angry if we hear what we did not expect to hear so long it is a truth. To me this is a big up to Reli and shame to PCCB and the govt for trying to politicise the BoT issue.
JK and his Mkullo are using this case as the bridge of continuing getting support from EU and US. If you have been following the episodes and events, when you read about EU making some noise you will hear of a case being taken to court just to show that they are doing something on scandelous spending of public and donors funds. Shame to all who mislead the public.
Hii serikali iache VISASI!!!!!! It should stop its Retaliation politics!!!!
 
mtu mmoja kusema amekula bil 200 peke yake ni kitu cha kushangaza sana

hata rostam akula bil 40 peke yake
 

Wakili: Ni nani alikuwa na maamuzi ya mwisho ya hili lifanyike au hili lisifanyike?

Shahidi: Gavana.

Wakili: Nani alikuwa na maamuzi ya mwisho ya kuidhinisha mabadiliko ya mradi na fedha?

Shahidi: Ni bodi ya wakurugenzi ambayo mwenyekiti wake ni gavana.

Wakili: Je, mkurugenzi wa idara zozote pale BoT anaweza kutoa maamuzi bila gavana na bodi kujua?

Shahidi: Hapana.



...Hapa ndio patamu...
 
Kuhusu duality ndani ya board nilikuwa napiga kelele hilo jambo kila siku nikisema hakuna accountability ndani ya board kwasababu gavana has to many power kiasi kwamba hakuna mtu anayemzuia kufanya analolitaka and that is why marais toka zamani wanateua washkaji zao kushika nafasi hizo kwasababu hata akivurunda hakuna wa kuuliza hili jambo ni hatari kwa institution kama BOT kwasababu ndio moyo ya financial system ya Tanzania.

Pili mkitizama katika thread zangu nyuma niliwahi kuwaambia na narudia kuwa huu ni usanii unaondelea ili Kikwete aonekane yupo accountable na kuwafurahisha wafadhili sasa kinachotokea sasa hivi ndio yale niliyoyasema walipomkamata Liyumba kuwa hii ni kesi ya usanii kwasababu Liyumba hana kosa katika hilo. Utamhukumu vp mtu kwa ubadhirifu wa Billioni 200 yeye na Kweka kwani wao ndio benki kuu. Haingii akilini kabisa. Hizo pesa must have come from a system iliyooza ambayo inajifanyia tu maamuzi bila ya kujali impact yake kwajamii.

Likewise ninamshangaa Reli anaposema kuwa Liyumba alishatumia hizo pesa wakati in any organisation navyofahamu mie kuna limitation katika maamuzi. Anataka kutwambia eti Liyumba aliamua billioni 200 peke yake thubutu itakuwa the biggest scandal in the world banking history. Hivyo basi kuna internal auditors, chief accountants, directors of operations and board members wameyaona haya kwanini wasiyazuie unakuta the whole system ya BOT imeoza. Internal auditor ana panga lake hivyo hawezi kuquery hayo madudu, directors wana mapanga yao (yaani fungu lao) ndio kwanza wanaifagilia hiyo project even may have no benefits to BOT. Board members wana mafungu yao wakienda pale wanajifanya wanaquestion but at the end of the day wanapitisha ili isionekane obvious. So kimsingi they whole management system imekalia kula tu hamna jengine.

Sasa tuje katika kesi ya Liyumba kimsingi hii ni kesi geresha ukitazama maelezo hapo juu utaona Liyumba hana kesi ya kujibu. Na sitoshangaa akalipwa fidia ya usumbufu na kurejeshwa kazini basi end of story. vile vile kesi ya mgonja, yona na mramba ni hivyo hivyo hamna lengine isipokuwa ni changa la macho tu. BOT bwana ili isafishike wamteue gavana mpya na manaibu wapya na bodi ivunjwe. Halafu waseparate hizo post mbili za uchairman na gavana kama ilivyo Uingereza (hasa ukichukulia our laws are mostly common laws). Pili isafishwe BOT kuna vijana wako bright humo ndani but wanaharibiwa na vijana wengine majizi ambao kazi yao kulinda maslahi ya baba zao au wazee (godfather wao) ambao hawa wana nguvu. Tatu Kikwete awe mkweli asidhani sie watanzania tunadanganyika kirahisi kihivyo awashughulikie mafisadi kiukweli na sio usanii. wakifungwa watu watatu miaka mingi au maisha ufisadi utapungua but kesi za kiusanii kama hizi hamna kitu
 
Kwani angekuwa huyo mwenye PhD ndiye deputy gavana hiyo hasara angeijuaje wakati ripoti bado haijakamilika?

Hiki kitu gani haswa? Wanataka kumuachia kama Zombe? Uwezo mdogo wa upande wa mashitaka? nini kiki jamani? ama ni kampeni za kutumia media? Jamani au ni uzembe? MASWALI NI MENGI.

Lakini, nashangazwa na jinsi kesi inavyoendeshwa/inavyoripotiwa maana hata hizo Q&A za magazeti zinatofautiana, inakuaje?

Kesi ya mahakamani inahusu uchunguzi wa PCCB, unamuuliza Gavana hasara wakati yeye anasubiri ripoti ya wakaguzi wa nje kukagua twin tower sasa anaulizwa atasemaje?
 
..hiyo hasara imepatikana vipi?

..je, mkandarasi amejenga jengo sub-standard?

..je, mkandarasi,Quantity Surveyor, Project Manager,Project Consultant, wame-inflate gharama za ujenzi?

..ukitaka ku-prove hasara ktk ujenzi huna ujanja bali kupitia njia hizo mbili hapo juu.

NB:

..Juma Reli pia hawezi kumtupia lawama zote Gavana wa Benki Kuu kwa kisingizio kwamba ndiye mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi.

..Wajumbe wa Bodi hawalazimiki kukubaliana na kila anachopendekeza gavana. mara nyingine maamuzi ya bodi hufanyika kwa kupiga kura.

..hakuna wakati wowote ule ambapo Gavana hutoa uamuzi kama mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa BOT bila kushirikisha idadi fulani ya wajumbe wa bodi hiyo.
 
Hivi matumizi mabaya ya fedha lazima yalete hasara? Nadhani hapa issue si hasara (ambayo itakuwa ni vigumu ku-prove maana si jengo la biashara) bali matumizi ya fedha nje ya matarajio. Mategemeo yalikuwa kupata jengo kwa kiasi fulani badala yake wamelipata kwa mara nyingi zaidi. Atafutwe nani amesababisha ongezeko hilo. Ni wabunifu majengo na wenzao? Ni mkandarasi? Au ni mshitiri? Kuwa jengo limegharimu zaidi ya bajeti halina ubishi. Sasa tuambiwe kwa nini imekuwa hivyo.

Amandla..........
 
Back
Top Bottom