Kesi ya Lissu- msimamizi wa uchaguzi (mkurungenzi wa wilaya) apanda kizimbani

Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
450
Msimamizi wa uchaguzi, na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Singida, Bi. Illuminata Leornard Mwenda, amepanda kizimbani katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Singida mashariki, Yeye anakuwa shahidi wa pili, baada ya Jana Tundu Lissu kujitetea kwa siku nzima. Mahojiano yake na wakili wa serikali, wakili msomi Tango yanaendelea tutaendelea kuwapa kwa urefu
 
Naona kesi hii imeanza kuwa na mvuto, kulikoni? Ule mkakati wa kimagamba upo kazini nini?

Na mwamini Mh Lissu atashinda tu!
 
Magamba at work, wamepanda kumtengua lakini watakiona ngoja wajaribu, Lissu Moto wa kuotea mbali.
 
Msimamizi wa uchaguzi, na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Singida, Bi. Illuminata Leornard Mwenda, amepanda kizimbani katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Singida mashariki, Yeye anakuwa shahidi wa pili, baada ya Jana Tundu Lissu kujitetea kwa siku nzima. Mahojiano yake na wakili wa serikali, wakili msomi Tango yanaendelea tutaendelea kuwapa kwa urefu

wewe nawe sometimes riport zako zina mning'inio sana. updates hutoi kwa mtiririko unaoendana na muda. kama si kujirekebisha, tueleze sababu ya kuchelewa ku-pdate.
 
Watu wa Singida Mashariki lazima waichukie CCM kama ilivyo kwa Watu wa Arusha... Serikali ya Magamba imekuwa inatumia Nguvu nyingi sana kupinga viongozi wa waliochaguliwa na wananchi kupitia Upinzani kama ambavyo tunaona.

Wanawadumaza kimaendeleo kwani CCM inafahamu kabisa hawa kina TL walishinda na sasa alitakiwa kuwa Bungeni lakini kama si kosei hii ni wiki ya Tatu yuko mahakamani eti kwa sababu TLP haikuwaweka mawakala huu ni uhuni dhidi ya wananchi wa Singida Mashari na sehemu zote ambazo wameichagua CDM...
 
[h=2]Mimi kama msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Singida mashariki, nasema uchaguzi ulisimamiwa kwa kanuni, sheria na taratibu, hivyo ulikuwa huru na wa haki.[/h][h=2]Msimamizi wa uchaguzi, na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Singida, Bi. Illuminata Leornard Mwenda, amemaliza kuhojiwa na wakili wa serikali katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Singida mashariki.[/h][h=2] [/h][h=2]Akiongozwa na Wakili Msomi Tango haya ni mahojiano ya leo.[/h][h=2]Wakili: Kazi yako nini?[/h][h=2]WP: Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Singida[/h][h=2]Wakili: Tangu lini?[/h][h=2]WP: Mwezi Agosti 2008.[/h][h=2]WAKILI: Mwaka 2010 ulipewa wajibu mwingine wowote?[/h][h=2]WP: NDIYO[/h][h=2]Wakili: kazi gani?[/h][h=2]WP: Nilichaguliwa kuwa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Singida kaskazini, Magharibi, na Singida mashariki. Majimbo matatu[/h][h=2]WAKILI: Kama msimamizi wa uchaguzi, wajibu wako ulikuwa upi?[/h][h=2]WP: Kwa ujumla, ilikuwa ni kushughulikia utawala, mikutano ya watendaji na vyama vya siasa na kuratibu masuala ya uchaguzi. Pia nilikuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa nimepokea vifaa toka tume ya uchaguzi na kuvisambaza, na uhifadhi wa kura baada ya uchaguzi.[/h][h=2]WAKILI: Taratibu za awali za mgombea, na mawakala wake ulihusika vipi?[/h][h=2]WP: Nilishughulikia kutoa barua kwa wagombea wa Ubunge, yaani kwa kuwapa fomu namba 8 b ya uteuzi wa Ubunge, tuliwapa wagombea ambao wametambulishwa na vyama vyao vya siasa.[/h][h=2]WAKILI: Tusaidie kuhusu Jimbo la singida mashariki. Wagombea walikuwa ni akina nani?[/h][h=2]WP: Kulikuwa na Mgombea toka CCM, CHADEMA, NA CUF.[/h][h=2]WAKILI: Je kama msimamizi, je ulikuwa na wasimamizi wasaidizi katika vituo?[/h][h=2]WP: Ni kweli, kulikuwa na msimamizi mkuu mmoja, wasaidizi wawili, karani mwongozaji mmoja.[/h][h=2]WAKILI: chini yako nani alikuwa anakusaidia? [/h][h=2]WP:Walikuwepo wasimamizi wasaidizi katika kila ngazi, na afisa wa uchaguzi[/h][h=2]Wakili: zoezi la kampeni ziliratibiwa vipi?[/h][h=2]WP: tuliomba vyama vya vya siasa walete ratiba zao, na tukakaa nao kuhakikisha kuwa hakukuwa na mgongano.[/h][h=2]Wakili: katika Jimbo la Singida mashariki, zoezi la kupiga kura lilikuwaje?[/h][h=2]WP: Tulifanya maandalizi kabla, tuliwapata wasimamizi, na wasaidizi. Siku ya uchaguzi vituo vilifunguliwa saa 1 asb na kufungwa saa 10 Jioni. Wapiga kura walifika na kupanga mistari na kupiga kura kule walipojiandikisha. Wasimamizi walifika mapema kuangalia mpangilio wa vyumba vya kupigia kura mapema[/h][h=2]WAKILI: Ni vyama vingapi vilileta orodha ya mawakala kulingana na kielelezo nilichokupa[/h][h=2]WP: CHADEMA, CUF,APPT MAENDELEO,TLP, NCCR MAGEUZI.[/h][h=2]WAKILI: Kwa ufahamu wako, baada ya kupokea hayo majina kwa utaratibu huwa mnafanya nini?[/h][h=2]WP: Huwa tunapeleka orodha kwa wasimimazi wakuu, na kufanya utaratibu wa kuwaapisha kabla ya siku ya uchaguzi.[/h][h=2]WAKILI: Nini kinafuata baada yakuapishwa?[/h][h=2]WP: Hupewa barua ya kiapo itakayomtambulisha katika anapoenda kuwa wakala[/h][h=2]WAKILI: Singida mashariki zoezi liliendaje?[/h][h=2]WP, Zoezi lilienda vema, vituo vilifunguliwa mapema, na mawakala walipewa fomu kujaza kuona kuwa wameridhika na zoezi la kufungua vituo. Na jioni [/h][h=2]WAKILI: Baada ya kupiga kura zoezi gani hufuata?[/h][h=2]WP: Zoezi la kuhesabu kura hufanyika mbele ya mawakala wote, wakimaliza kuhesabu wote wanajaza fomu ya matokeo[/h][h=2] [/h][h=2]WAKILI: Fomu za matokeo hujazwa na nani?[/h][h=1]WP: Fomu hujazwa na msimamizi, nakala ya kwanza anapeleka kwa msimamizi Mkuu, fomu nyingine hubandika nje, na nyingine hupewa mawakala. Na mawakala huwa wanasaini[/h][h=2]WAKILI:Ujumlishaji wa matokeo kwa jimbo la Singida mashariki ulifanyikaje?[/h][h=1]WP: Tuliwaarifu Vyama wagombea wao wafike au mawakala wao[/h][h=2]Wakili: Baada ya kujumlisha matokeo, nini kazi ya mawakala au wagombea[/h][h=2]WP; Wanashuhudia zoezi lilivyoenda.[/h][h=2]WAKILI: Baada ya kushuhudia nini kinafuata?[/h][h=2]WP: Tunajaza fomu namba 24, ambayo wagombea wanasaini[/h][h=2]Wakili: Wakati wa kusaini fomu namba 24, mgombea wa CCM alikuwepo?[/h][h=2]WP: HAKUWEPO[/h][h=2]WAKILI: Kuna tuhuma zinasema kuwa uchaguzi wa Jimbo la Singida mashariki haukuwa huru na wa haki, wewe kama msimamizi unasemaje?[/h][h=2]WP: Mimi kama msimamizi, nasema uchaguzi katika jimbo la Singida mashariki ulisimamiwa kwa kanuni, sheria na taratibu, hivyo ulikuwa huru na wa haki.[/h][h=2] [/h]

Kila la heri Tundu Lissu mungu atakusaidia , tunaamini kua sauti ya wengi ni ya mungu mwenyewe
 
Msimamizi wa uchaguzi, na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Singida, Bi. Illuminata Leornard Mwenda, amepanda kizimbani katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Singida mashariki, Yeye anakuwa shahidi wa pili, baada ya Jana Tundu Lissu kujitetea kwa siku nzima. Mahojiano yake na wakili wa serikali, wakili msomi Tango yanaendelea tutaendelea kuwapa kwa urefu

tatizo lako Isanga, unaishiaga mitini baada ya kutoa nusu habari. Bora uwe unaacha, tulio mbali na Singida tunahamu ya kujua kinachoendelea.
 
Niay yao kuu ni kumfanya Lisu atumie mda mwingi kuhangaikia masuala ya Kesi badala ya kuwatumikia wananchi Bungeni, lakini CCM hawajui kwamba kila mtanzania mwenye akili timamu anajua dhamira yao na ndivyo wanavyozidi kukichukia hiki chama. CCM fahamuni kwamba wakati wa kuendesha siasa za fitna umekwisha Watanzania wa leo sio wale mliozoea kuwaburuza mupendavyo miaka ya 90
 
Watu wa Singida Mashariki lazima waichukie CCM kama ilivyo kwa Watu wa Arusha... Serikali ya Magamba imekuwa inatumia Nguvu nyingi sana kupinga viongozi wa waliochaguliwa na wananchi kupitia Upinzani kama ambavyo tunaona.

Wanawadumaza kimaendeleo kwani CCM inafahamu kabisa hawa kina TL walishinda na sasa alitakiwa kuwa Bungeni lakini kama si kosei hii ni wiki ya Tatu yuko mahakamani eti kwa sababu TLP haikuwaweka mawakala huu ni uhuni dhidi ya wananchi wa Singida Mashari na sehemu zote ambazo wameichagua CDM...

Nimependa maelezo ya Msimamizi wa uchaguzi hebu cheki hapa

WAKILI:Ujumlishaji wa matokeo kwa jimbo la Singida mashariki ulifanyikaje?

WP: Tuliwaarifu Vyama wagombea wao wafike au mawakala wao

Sasa kama CCM wanalalmika kwamba TLP hawakuwa na mawakala tatizo ni lao wenyewe na Magamba wameng'ang'ana yaani hawana hata aibu
 
[h=2]Mimi kama msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Singida mashariki, nasema uchaguzi ulisimamiwa kwa kanuni, sheria na taratibu, hivyo ulikuwa huru na wa haki.[/h][h=2]Msimamizi wa uchaguzi, na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Singida, Bi. Illuminata Leornard Mwenda, amemaliza kuhojiwa na wakili wa serikali katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Singida mashariki.[/h][h=2] [/h][h=2]Akiongozwa na Wakili Msomi Tango haya ni mahojiano ya leo.[/h][h=2]Wakili: Kazi yako nini?[/h][h=2]WP: Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Singida[/h][h=2]Wakili: Tangu lini?[/h][h=2]WP: Mwezi Agosti 2008.[/h][h=2]WAKILI: Mwaka 2010 ulipewa wajibu mwingine wowote?[/h][h=2]WP: NDIYO[/h][h=2]Wakili: kazi gani?[/h][h=2]WP: Nilichaguliwa kuwa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Singida kaskazini, Magharibi, na Singida mashariki. Majimbo matatu[/h][h=2]WAKILI: Kama msimamizi wa uchaguzi, wajibu wako ulikuwa upi?[/h][h=2]WP: Kwa ujumla, ilikuwa ni kushughulikia utawala, mikutano ya watendaji na vyama vya siasa na kuratibu masuala ya uchaguzi. Pia nilikuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa nimepokea vifaa toka tume ya uchaguzi na kuvisambaza, na uhifadhi wa kura baada ya uchaguzi.[/h][h=2]WAKILI: Taratibu za awali za mgombea, na mawakala wake ulihusika vipi?[/h][h=2]WP: Nilishughulikia kutoa barua kwa wagombea wa Ubunge, yaani kwa kuwapa fomu namba 8 b ya uteuzi wa Ubunge, tuliwapa wagombea ambao wametambulishwa na vyama vyao vya siasa.[/h][h=2]WAKILI: Tusaidie kuhusu Jimbo la singida mashariki. Wagombea walikuwa ni akina nani?[/h][h=2]WP: Kulikuwa na Mgombea toka CCM, CHADEMA, NA CUF.[/h][h=2]WAKILI: Je kama msimamizi, je ulikuwa na wasimamizi wasaidizi katika vituo?[/h][h=2]WP: Ni kweli, kulikuwa na msimamizi mkuu mmoja, wasaidizi wawili, karani mwongozaji mmoja.[/h][h=2]WAKILI: chini yako nani alikuwa anakusaidia? [/h][h=2]WP:Walikuwepo wasimamizi wasaidizi katika kila ngazi, na afisa wa uchaguzi[/h][h=2]Wakili: zoezi la kampeni ziliratibiwa vipi?[/h][h=2]WP: tuliomba vyama vya vya siasa walete ratiba zao, na tukakaa nao kuhakikisha kuwa hakukuwa na mgongano.[/h][h=2]Wakili: katika Jimbo la Singida mashariki, zoezi la kupiga kura lilikuwaje?[/h][h=2]WP: Tulifanya maandalizi kabla, tuliwapata wasimamizi, na wasaidizi. Siku ya uchaguzi vituo vilifunguliwa saa 1 asb na kufungwa saa 10 Jioni. Wapiga kura walifika na kupanga mistari na kupiga kura kule walipojiandikisha. Wasimamizi walifika mapema kuangalia mpangilio wa vyumba vya kupigia kura mapema[/h][h=2]WAKILI: Ni vyama vingapi vilileta orodha ya mawakala kulingana na kielelezo nilichokupa[/h][h=2]WP: CHADEMA, CUF,APPT MAENDELEO,TLP, NCCR MAGEUZI.[/h][h=2]WAKILI: Kwa ufahamu wako, baada ya kupokea hayo majina kwa utaratibu huwa mnafanya nini?[/h][h=2]WP: Huwa tunapeleka orodha kwa wasimimazi wakuu, na kufanya utaratibu wa kuwaapisha kabla ya siku ya uchaguzi.[/h][h=2]WAKILI: Nini kinafuata baada yakuapishwa?[/h][h=2]WP: Hupewa barua ya kiapo itakayomtambulisha katika anapoenda kuwa wakala[/h][h=2]WAKILI: Singida mashariki zoezi liliendaje?[/h][h=2]WP, Zoezi lilienda vema, vituo vilifunguliwa mapema, na mawakala walipewa fomu kujaza kuona kuwa wameridhika na zoezi la kufungua vituo. Na jioni [/h][h=2]WAKILI: Baada ya kupiga kura zoezi gani hufuata?[/h][h=2]WP: Zoezi la kuhesabu kura hufanyika mbele ya mawakala wote, wakimaliza kuhesabu wote wanajaza fomu ya matokeo[/h][h=2] [/h][h=2]WAKILI: Fomu za matokeo hujazwa na nani?[/h][h=1]WP: Fomu hujazwa na msimamizi, nakala ya kwanza anapeleka kwa msimamizi Mkuu, fomu nyingine hubandika nje, na nyingine hupewa mawakala. Na mawakala huwa wanasaini[/h][h=2]WAKILI:Ujumlishaji wa matokeo kwa jimbo la Singida mashariki ulifanyikaje?[/h][h=1]WP: Tuliwaarifu Vyama wagombea wao wafike au mawakala wao[/h][h=2]Wakili: Baada ya kujumlisha matokeo, nini kazi ya mawakala au wagombea[/h][h=2]WP; Wanashuhudia zoezi lilivyoenda.[/h][h=2]WAKILI: Baada ya kushuhudia nini kinafuata?[/h][h=2]WP: Tunajaza fomu namba 24, ambayo wagombea wanasaini[/h][h=2]Wakili: Wakati wa kusaini fomu namba 24, mgombea wa CCM alikuwepo?[/h][h=2]WP: HAKUWEPO[/h][h=2]WAKILI: Kuna tuhuma zinasema kuwa uchaguzi wa Jimbo la Singida mashariki haukuwa huru na wa haki, wewe kama msimamizi unasemaje?[/h][h=2]WP: Mimi kama msimamizi, nasema uchaguzi katika jimbo la Singida mashariki ulisimamiwa kwa kanuni, sheria na taratibu, hivyo ulikuwa huru na wa haki.[/h][h=2] [/h]

[FONT=
Calibri] [/FONT]

Asante sana mkuu kwa Updates za uhakika!
 
Kasi za 'kuku' kama hizi magamba wako kimbelembele sana, lakini zile za EPA wanafyata mkia kama mbwa koko. Dawa yao ni M4C. Kamanda Lema kaeleze ubaya wa hawa mafisadi na wauza madawa ya kulevya, hadi ifike wakati wawe wanapigwa mawe kila wanapoenda.
 
kila jambo lina majira yake, magamba hawatatawala milele, mimi ninasema Mene mene tekeli na peresi kwa ccm
 
Watu wamezoea kula kwa maghumashi, pesa za bure bure bila kufanya kazi halali! kwa hili watang'ang'a ili kupoteza muda tu. Lakini, maamuzi yeyote ya hii kesi yatazidi kuwaweka CCM pabaya zaidi.
 
Hata mwanangu anayesoma chekechea anajua hapo hakuna kesi ni uonevu tuu. Ngoja nianze kuwafundisha makamanda wangu kabla hawajaingia la kwanza waanze kuichukia CCM
 
Back
Top Bottom