Mwanakijiji,
Mimi hata sielewi kinachoendelea huko Arusha, hata nikisoma kilichoandikwa hapa natoka mtupu. Mara namsoma huyo Agness Gideon Mollel kama shahidi wa kesi, halafu ghafla anabadilika na kuwa mshitaka aliyefungua kesi..darasa la saba sijui hiyo elimu ndio inaweza fungua kesi au ndio kujua zaidi haki yake.
Halafu utangulizi unaonyesha ni kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema), sasa sielewi ni nani anayeweza kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo hilo zaidi ya Batilda mwenyewe..Mwenye kuelewa zadi kinachoendelea atujuze maana vitu kibao vinajichanganya hapa.
Nafikiri hii case itakuwa ni ya kujionesha nani mkereketwa wa CCM zaidi. Ninachokiona kwenye kesi hii ni sawa na kuhamishia jukwaa la siasa mahakamani. Nina wasiwasi na unpartiality ya jaji Mujuluzi aliyekubali kusikiliza kesi hii hapo awali kabla ya kujitoa. Hapo hakuna kesi ya kupinga matokeo bali kuna kesi ya madai ya kashfa. Kinachotakiwa kuoneshwa katika kesi ya kupinda matokea ni jinsi gani uchaguzi kam process uliharibiwa na kashfa dhidi ya Batilda eg.
- Kuna watu walikosa haki ya kupiga kura
- Matokeo ya kura yaliharibishwa kwa kuwa contaminated
- Mgombea aliyeshinda hakuwa na sifa za kugombea(eg si raia wa nchi au below 18 years)
- Matokeo yalichakachuliwa na hayaonesha uhalisia wa wapiga kura
Ushauri wa Yussuf Makamba mwaka 2010 kuwa CCM wafungue kesi sehemu zote walizoshindwa na wapinzani was a total waste of resources and time. Inawezekana ilikuwa strategy ya kulinda majimbo waliyojitangaza washindi bila ridhaa ya wananchi ila kesi ya Arusha is as good as ze comedi.