Kesi ya kupinga matokeo ushindi wa mbunge wa Ilemela, Tundu Lissu awa mbogo

don-oba

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
1,387
677
Katika kesi iliyoanza jana kupinga matokeo ya ushindi wa mbunge wa ilemela, mahakama kuu ya kanda ya mwanza imeanza kumsikiliza shahidi Beatus Martin Madenge wa upande wa walalamikaji. Shahidi huyo aliyakataa maelezo aliyoyatoa katika hati ya mashtaka.

LISSU: Tuthibitishie hii ni sahihi yako-anamwonesha hati ya mashtaka.

SHAHIDI: ndio.

WAKILI: Sasa kwanini unayakataa maelezo uliyoyatoa?

SHAHIDI: kimya.

LISSU: Hati hii inaonesha ulikiri kupiga kura oct 31 2010 hapa unakataa.

SHAHIDI: sikupiga kura, nilizuiwa na vijana km 200 wa chadema.

LISSU: Kwanini Diallo hajafungua kesi, eleza endapo umepewa pesa au ulikua mgombea mwenza?.

SHAHIDI: Sikupewa pesa wala sikuwa mgombea mwenza.

LISSU: unaufahamu usemi, pilipili usiyoila wewe ikuwashie nini?.

SHAHIDI: kimya.
 
laiti chadema ingekua na majembe matatu dizaini ya lisu tungekua mbali sana.nawaomba chadema watafute mejembe mengine dizaini ya lisu .bravo lisu
 
Don-Oba asante kwa taarifa uliyotupa. Uko makini, pia inapenfza ku-share nasi kile ulichosikia.

Nasubiri sehemu iliyobaki... inanikumbusha maswali ya Advoc. Lakha
 
Hakunaga kama lissu.....! Magambani kumpata wa aina ya lissu ni mpaka tondogo...! Bg up kamanda TL.
 
jitahidi umalizie kwani kuna vitu tumevikosa Du! shahidi kapiga kura kwenye hati ya kiapo, mahakamani anatosa!
 
Don-Oba asante kwa taarifa uliyotupa. Uko makini, pia inapenfza ku-share nasi kile ulichosikia.

Nasubiri sehemu iliyobaki... inanikumbusha maswali ya Advoc. Lakha

Dah, umenikumbusha mbali advoc. lakha kwenye kesi ya uhaini. ilikuwa burdani sana kuisoma.
 
Hatakimbia sasa hivi huyu kimbelembele tu wewe hayakuhusu dialo ana
watoto wake akipokea mshahara ni wake wewe inakuhusu nini ????????
 
Kina Hamza,Michael,Ben wako busy na kusimamia mali za baba yao(Diallo) na kupata elimu pia wewe unahangaika na mahakama
 
Mh!! Ni kama mleta thread umekuza jambo saaaaanaaa wakti haliko hivyo...sasa hapo umbogo upo wapi? Mbona haya ni maswali ya kawaida sana kwa wanasheria? Labda kama ulikuwepo mahakamani kwa hiyo uliona emotional feeling za Tundu Lissu...otherwise sioni huo umbogo hapo...
 
Back
Top Bottom