Kesi ya kupinga matokeo Arusha mjini, yaendelea

Na Queen Lema, Arusha

KESI ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa Arusha Mjini, Bw. Godbless Lema, imeanza kusikilizwa jana.

Shahidi wa kwanza katika kesi hiyo upande wa mlalamikaji, Bw. Musa Mkangaa, aliieleza Mahakama jinsi Bw. Lema alivyotumia maneno kumdharirisha aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Batilda Buriani.

Kesi hiyo namba 13 ya mwaka 2010, inasikilizwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na Jaji Mfawidhi, Gabriel Rwakibarila, kutoka Mahakama ya Sumbawanga.

Bw. Mkangaa alidai kuwa yeye binafsi alifanikiwa kutembelea sehemu nne za mikutano ya kampeni ya Bw. Lema, ambapo mbali na kutoa ahadi, mbunge huyo alimkashifu Dkt. Buriani.

Alidai kuwa Agosti 312010, katika eneo la Kwa Muorombo, Kata ya Terrat, Bw. Lema aliwaeleza wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni kuwa wanaume katika makabila ya Wachaga na Waarusha, hawawezi kutawaliwa na mwanamke.

Alisema kauli hiyo kwa mujibu wa sheria ni kinyume cha taratibu na kudai kuwa, mbali ya kuwakataza wananchi kutompa kura Bi. Buriani pia aliwataka kujiadhari na watu wanaovaa vitambaa katika vichwa vyao, kwani huenda ni miongoni mwa makundi ya kigaidi.

“Mimi nilimsikia Bw. Lema akiwaambia wananchi wasimchague Dkt. Buriani kwa kuwa anavaa vitambaa na kufunika kichwa kila mara hivyo si kiongozi bora,” alisema.

Katika hatua nyingine, shahidi huyo alisema Septembe 18,2010, saa sita mchana katika eneo la Mbauda, Bw. Lema, akiwa na viongozi wa chama chake waliendelea kurudia maneno hayo.
:A S 465:
 
Huyu jamaa ni kesi kila siku! Hivi ana muda wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi? Uwakilishi wake una mashaka sana.
 
haki ni gharama, ila tunaamin hakuna dhuluma na uongo iliyowahi kushindana na ukweli ukashinda! ccmagamba watashindwa tu!cjui itachukua muda gani, ila imani yangu ni kuwa lazima watashindwa tu . . . '*******_'yako icu now!?!
 
anaitwa kiusahihi Musa Hamis Mkanga, sio Nkangaa; aliwahi kuwa diwani wa kata ya Sombetini akafukuzwa kwa kashfa ya ubadhirifu!
Utakuwa sahihi. Hata mimi nilianza kushangaa kama Musa Nkangaa ninayemfahamu (Aliyewahi kuwa waziri na mkuu wa mkoa) ndiye katoa tafsiri hiyo kituko ya Al Qaeda.
 
Hivi huyu bwana Mkangaa katika uko kina mama ndio wanaongoza familia? Vitabu vya Mungu vimeandika "mwanaume ni kichwa cha nyumba". Nyumba ambazo wanaume wameproof failure ndiyo wanawake wanalazimika kuwa wasemaji wa familia hata ukoo.

Sina hakika kama Arusha imekosa mtu kuiongoza. Lema amesema, hajasema nina hakika watu wa Arusha kwa kipindi hiki hawawezi kumchagua huyu mama.

Kwani adha wanazopata watu wa Hanang ndiyo ingewapata, mtu mnampa ubunge baada ya uchaguzi anakwenda kuishi na familia yake nje ya wilaya kufurahia posho na mshahara ambao hajaufanyia kazi wananchi tukaridhika kwa kutokuwepo kwake wilayani.
 
Sasa mbona si elewi ana pinga matokeo gani huyu ....dkt batilda ....kwani lema ameshinda kwa kuchaguliwa na idadi kubwa ya wanachi.......sasa haya mengine yanatokea wapi.....
 
Hivi huyu bwana Mkangaa katika uko kina mama ndio wanaongoza familia? Vitabu vya Mungu vimeandika "mwanaume ni kichwa cha nyumba". Nyumba ambazo wanaume wameproof failure ndiyo wanawake wanalazimika kuwa wasemaji wa familia hata ukoo. Sina hakika kama Arusha imekosa mtu kuiongoza. Lema amesema, hajasema nina hakika watu wa Arusha kwa kipindi hiki hawawezi kumchagua huyu mama. Kwani adha wanazopata watu wa Hanang ndiyo ingewapata, mtu mnampa ubunge baada ya uchaguzi anakwenda kuishi na familia yake nje ya wilaya kufurahia posho na mshahara ambao hajaufanyia kazi wananchi tukaridhika kwa kutokuwepo kwake wilayani.

Huyu Juma MKangaa ni mnafiki tu,
aliwahi kupigwa chini udiwani wa CCM kwa kashfa ya kuuza kiwanja pale soko la KIlombero,
hivyo nina wasiwasi na uadilifu wake
 
Wakuu
Kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Arusha mjini imeanza kusikilizwa,baada ya kujitoa kwa Jaji Aloyce Mujuluzi.Jana upande wa mashtaka ulianza kutoa ushahidi,ambapo shahidi wa kwanza Musa Nkangaa,aliieleza Mahakama kuwa Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema,aliwataka wapiga kura kutomchagua Batilda Burian,kwa kuwa eti ni Al qaeda.
Mahojiano yalikuwa hivi..
1.shahidi.Mh Mbunge wakati wa kampeni kwenye mkutano Terat,aliwaambia wapiga kura wasimchague Batilda Burian,maana ni Al qaeda
2.Wakili wa utetezi..Unawafahamu Al qaeda?
3.Shahidi.Ndio nawafahamu,ni Mtu yeyote anayefunga kitambaa kichwani
4.Wakili wa utetezi..Je masista nao ni Al qaeda?
5.Shahidi.Ndio ni Al qaeda,kwa kuwa nao masista wanafunga vitambaa kichwani
Shahidi Musa Nkangaa ataendelea na ushahidi wake leo,nitaendelea kuwajuza kitakachojiri

Mkuu mbona unapotosha wewe ni kiongozi weka ushabiki wa kisiasa mbali..

Alichosema Mkanga, aliileza mahakama kuwa alimsikia Lema, akiwaonya wananchi kuwa makini na watu wanaovaa hijabu na ushungi ili wasije kuchagua Al-Qaida.

Lema, pia alihoji mila na desturi za makabila ya Wamasai na Wachaga, aziruhusu mwanamke kuwa kiongozi wa wazee wa kimila.

Mkanga, alisema Lema, alimchonganisha Dk Burian na wapiga kura kwa kutumia udini, Lema alisema Dk Burian, akishinda atakifunga kituo cha Radio cha Safina kinachomilikiwa na madhehebu ya Kikiristo kwa madai kinasaidia upinzani.

Haya sio maneno yangu ni maneno ya Mussa Mkanga.
 
Huyu Juma MKangaa ni mnafiki tu,
aliwahi kupigwa chini udiwani wa CCM kwa kashfa ya kuuza kiwanja pale soko la KIlombero,
hivyo nina wasiwasi na uadilifu wake

Yawezekana kapewa takrima kidogo kakubali kumchafulia Mh. Mbunge
 
Heshima kwanu wanajamvi,

Nilisema mara baada ya matokeo ya uchaguzi yalipotangazwa kwamba ushindi wa Mheshimiwa Lema ukitinga mahakamani lazima atapigwa chini kwasababu yapo matamko mengi ambayo hakupaswa kutamka hadharani.Huo ndiyo ukweli wa mambo lipo suala la Redio Safina likifikishwa mbele ya Jaji hakika lazima maandalizi ya uchaguzi mwingine yafanyike.

Mheshimiwa Lema bado ana nafasi ya kushinda tena uchaguzi mwingines si kwasababu kafanya mambo mazuri lahasha atashinda kwakuwa bado siasa za kishabiki zitachukua nafasi yake.
 
Huyu jamaa ni kesi kila siku! Hivi ana muda wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi? Uwakilishi wake una mashaka sana.

Hivi kweli Rejao kuna siku uliwahi kula chochote ulichotafuna? huenda hujawahi kupata utamu kwani vya kutafuniwa vitakuwa na mate na harufu mbaya ya mdomo usio kuwa wako, na hivyo kutokuambulia utamu. Sijui usaidiwe je?
 
Huyu Juma MKangaa ni mnafiki tu,
aliwahi kupigwa chini udiwani wa CCM kwa kashfa ya kuuza kiwanja pale soko la KIlombero,
hivyo nina wasiwasi na uadilifu wake

Yawezekana kapewa takrima kidogo kakubali kumchafulia Mh. Mbunge na kumpotezea muda maana hizi mbinu zinazotumiwa sana na vyama vya siasa hasa vile vyenye hofu na CDM. Na kumbe mtu mwenye njaa hata anathubutu kuuza rasilimali za nchi kwa kukidhi njaa yake, Halafu anatudanganya ana uchungu kuliko hata familia ya mhusika kama siyo unafiki ni nini? Tuna wasiwasi pengine kaahidiwa donge ikiwa mama angepata ubunge maana ni kawaida ya watawala wetu hasa wanapoomba kura.
 
Ritz,nimeripoti mtiririko wa maswali ya wakili wa utetezi,na shahidi wa mashitaka,kama na wewe una ya nyongeza ongezea sio kuanza kushtumu,
 
Ritz,nimeripoti mtiririko wa maswali ya wakili wa utetezi,na shahidi wa mashitaka,kama na wewe una ya nyongeza ongezea sio kuanza kushtumu,

Nanyaro,
wala mie sijakushutumu jinsi ulivyoripoti ki ukweli umeweka ushabiki wa kisiasa mbele.

Umechukuwa maneno yaliokufurahisha na kuyaweka jamvini, mtu ambae akuwepo lazima ataona hiyo kesi ni kituko mkuu najua unaipenda sana Chadema. Weka ulingo wa habari sawa.

Ungeweka basi hata maelezo kidogo ya Wakili Alute Mugwai, na Modest Akida.
 
Nadhani ata wewe umeshindwa kujua Al-Qaida ni nani, sio magaidi wote ni wanaitwa Al-Qaida, ina wezekana huyo shahidi yupo right kwenye ya tafsiri ya Al-Qaida..

Lema, yeye alivyosema Al-Qaida alikuwa anajua ni kina nani?

Shahidi ukishindwa kuthibitisha katika kesi, ina maana hiyo kesi ni batili. Kwamtazamo wangu ingawa sikuwa ARUSHA kipindi cha kampeni lakini naona kuwa ni kesi ya kutengenezwa, sasa watengenezaji wamewachukua MBULULA kufungua kesi na hawakuwajaza maneno ya kuongea.

Wanafikiri ubishi wa kwenye vijiwe vya kunywa kahawa na kucheza draft ni sawa na mahakamani!!!!

Pale ni mambo ya sheria na kutoa jibu lenye usahihi. siyo kupeleka ubishi wa kwenye vijiwe. Au huyu bwana alikuwa anataka kupanda chat kwa kuandikwa katika magazeti?????????????

Ndio hawa mambumbumbu wanaongangania CHAMA CHA MAJAMBAZI (CCM) kwa zawadi ya tshirt na khanga.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!
 
Heshima kwanu wanajamvi,

Nilisema mara baada ya matokeo ya uchaguzi yalipotangazwa kwamba ushindi wa Mheshimiwa Lema ukitinga mahakamani lazima atapigwa chini kwasababu yapo matamko mengi ambayo hakupaswa kutamka hadharani.Huo ndiyo ukweli wa mambo lipo suala la Redio Safina likifikishwa mbele ya Jaji hakika lazima maandalizi ya uchaguzi mwingine yafanyike.

Mheshimiwa Lema bado ana nafasi ya kushinda tena uchaguzi mwingines si kwasababu kafanya mambo mazuri lahasha atashinda kwakuwa bado siasa za kishabiki zitachukua nafasi yake.

Mkuu Ngongo.
kwenye kesi hiyo Lema akifanya mchezo itamtupa kwenye ulingo wa siasa..

Mkanga, aliezea mahakama mbele ya Jaji Gabriel Rwakibarila kuwa Lema, alitumia mikutano aliyofanya katika kata za Sombetini, Terat na Elerai, akiwataka wananchi wasimchague Dk Burian kwa madai ni mwanamke aliyeolewa Zanzibar na kwamba angerejeshwa visiwani humu mara baada ya uchaguzi ili kuhudumia familia yake.

kesi ngumu sana hii kwa Lema.
 
Back
Top Bottom