Kesi ya kupinga matokeo Arusha mjini, yaendelea

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,221
1,788
Wakuu
Kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Arusha mjini imeanza kusikilizwa,baada ya kujitoa kwa Jaji Aloyce Mujuluzi.Jana upande wa mashtaka ulianza kutoa ushahidi,ambapo shahidi wa kwanza Musa Nkangaa,aliieleza Mahakama kuwa Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema,aliwataka wapiga kura kutomchagua Batilda Burian,kwa kuwa eti ni Al qaeda.
Mahojiano yalikuwa hivi..
1.shahidi.Mh Mbunge wakati wa kampeni kwenye mkutano Terat,aliwaambia wapiga kura wasimchague Batilda Burian,maana ni Al qaeda
2.Wakili wa utetezi..Unawafahamu Al qaeda?
3.Shahidi.Ndio nawafahamu,ni Mtu yeyote anayefunga kitambaa kichwani
4.Wakili wa utetezi..Je masista nao ni Al qaeda?
5.Shahidi.Ndio ni Al qaeda,kwa kuwa nao masista wanafunga vitambaa kichwani
Shahidi Musa Nkangaa ataendelea na ushahidi wake leo,nitaendelea kuwajuza kitakachojiri
 
hahahahaaaaah AlQuada huyu hapa

Batilda-Burian.jpg
 
Kazi kweli kweli yaani kumtambua al quida ni kwa kuvaa kitambaa kichwani? Na sio kwa kufanya ugaidi? Basi naona uelewa wake ni finyu hastahili kuwa shahidi kwa sababu namharibia anaye mtetea.
 
Sasa kama Al-qaida wanafunga vitambaa kichwani anachompinga Lema ni nini?
manake Batilda Burian hufunga kitambaa kichwani.Hivyo ni al-qaida.
 
Ahsante Nanyaro endelea kutuupdate tulio mbali na mahakama, ila shahidi huyu uelewa wake ni mdogo sana sijui anamsaidia vipi anaemshuhudia.
 
Sasa huyo ndio shaidi gani?ni timamu kweli huyo?serikali ndio maana uwa wanashindwa kesi nyingi sana!yaani nafikiri hata wakili mwenyewe alikua anajichekea kimoyomoyo tu
 
Upande wa uteteze wamuulize huyo shahidi yafuatayo:
- je wananchi wa Arusha hasa wapiga kura wana akili timamu?
- Je wapiga kura wa Arusha wana uwezo wa kuamua kumchagua mtu bila ya kufuata maelekezo ya mtu yoyote?
- Je, ni kweli wananchi wa Arusha walimchagua Lema kwa sababu tu waliambiwa kuwa Batilta ni Al-Qaeda?
 
huyu mshahidi anatokea wapi hembu jaribu kuuliza au kabla hajafika hapo alipitia Matejoo kunywa kachasu(gongo)
Wakuu
Kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Arusha mjini imeanza kusikilizwa,baada ya kujitoa kwa Jaji Aloyce Mujuluzi.Jana upande wa mashtaka ulianza kutoa ushahidi,ambapo shahidi wa kwanza Musa Nkangaa,aliieleza Mahakama kuwa Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema,aliwataka wapiga kura kutomchagua Batilda Burian,kwa kuwa eti ni Al qaeda.
Mahojiano yalikuwa hivi..
1.shahidi.Mh Mbunge wakati wa kampeni kwenye mkutano Terat,aliwaambia wapiga kura wasimchague Batilda Burian,maana ni Al qaeda
2.Wakili wa utetezi..Unawafahamu Al qaeda?
3.Shahidi.Ndio nawafahamu,ni Mtu yeyote anayefunga kitambaa kichwani
4.Wakili wa utetezi..Je masista nao ni Al qaeda?
5.Shahidi.Ndio ni Al qaeda,kwa kuwa nao masista wanafunga vitambaa kichwani
Shahidi Musa Nkangaa ataendelea na ushahidi wake leo,nitaendelea kuwajuza kitakachojiri
 
Heshima kwako E Nanyaro.

Tafadhali wakati wa kutujuza kinachoendelea mahakamani weka ushabiki pembeni usiwe kama yule rafiki yako Lema akibanwa we sema tu.Nje ya kesi ya Lema vipi mbona mgogoro wa mtaro wa maji Makao mapya umekushinda unajua hicho ndiyo kipimo cha uongozi wako ?.
 
Ngongo,naripoti kile kinachojiri mahakamani,ukiona ni ushabiki shauri yako,ila niliyoeleza ndio shahidi Musa Nkanga kaeleza mahakama
Swala la mtaro wa maji machafu,makao mapya sehemu gani?
Heshima kwako E Nanyaro.

Tafadhali wakati wa kutujuza kinachoendelea mahakamani weka ushabiki pembeni usiwe kama yule rafiki yako Lema akibanwa we sema tu.Nje ya kesi ya Lema vipi mbona mgogoro wa mtaro wa maji Makao mapya umekushinda unajua hicho ndiyo kipimo cha uongozi wako ?.
 
Heshima kwako E Nanyaro.

Tafadhali wakati wa kutujuza kinachoendelea mahakamani weka ushabiki pembeni usiwe kama yule rafiki yako Lema akibanwa we sema tu.Nje ya kesi ya Lema vipi mbona mgogoro wa mtaro wa maji Makao mapya umekushinda unajua hicho ndiyo kipimo cha uongozi wako ?.

Mbona unachanganya mambo mara kesi mara mtaro? Mtu mzima ovyooo.
 
Kesi imeanza,na Jaji amemkumbusha shahidi kuhusu kiapo alichokula cha kusema kweli,na sasa wakili wa utetezi,anamwuliza shahidi kuhusu ushahidi wake alioutoa jana,hivyo anatakiwa athibitishe,
 
Tupo standby tunakusubiri utuletee taarifa ambazo hazina upendeleo
 
Back
Top Bottom