Kesi ya kupinga matokeo Arusha mjini inaendelea

Yeye Batilda anakula kuku kwa Kibaki huku wachovu wamejivalisha kesi kwa kisingizio cha 'kuchukizwa' na kauli za watu wakati wa campaign! very strange!
 
Tunashukuru Mkuu kwa kutupa updates kutoka mahamakani.

Kuwa fair mkuu kwenye kuripoti upande wa pili usiripoti nagative!

Ritz,mbona wewe ni mlalamishi tu muda wote?leo nimeripoti mahojiana kati ya wakili wa upande wa wadai(Musa Mkanga na wenzake)bado unalalamika,lazima utakuwa na matatizo wewe
 
Ritz,mbona wewe ni mlalamishi tu muda wote?leo nimeripoti mahojiana kati ya wakili wa upande wa wadai(Musa Mkanga na wenzake)bado unalalamika,lazima utakuwa na matatizo wewe

Mkuu Nanyaro Ephata,
Hakuna sehemu yoyote niliolalamika, kukwambia uwe fair ndio kulalamika? Niwe radhi mkuu kama nimekukwaza na swali langu.
 
Hii kesi ikiamuliwa kwa shinikizo za wanasiasa wa CCM kama inavyosemekana si tu itaweka precedence ambayo itawageukia CCM wenyewe 2015 bali itaonesha kuwa mahakama si mahala pa kupatia haki bali pa kuchezea siasa. Ninachokiona kwenye kesi hii ni SIASA KUHAMIA MAHAKAMANI PERIOD.
 
Let us wait...Kwa taarifa za kweli kabisa nilizozipata kutoka kwa mmoja aliyekuwa NEC ya Magamba alisema Chama sasa kinatetemeka kwa Chadema na kanipa 100% infomation za ushindi wa Igunga kuwa CCM ilikuwa Chali, Sasa wana Mchakato wa kumweka mtoto wa Marehemu awanie Ubunge hapo Arusha. Zaidi mtaamini haya tar 27 feb. Chadema ushindi ni lazima na CCM wanajimaliza wenyewe.
 
Baada ya wakili wa wadai kumaliza mhaojiano,alifuata wakili wa utetezi Kimomogoro,
1.Wakili wa utetezi.ulijiunga lini na jeshi?
2.shahidi.1973
3.Wakili wa utetezi.Elimu yako ni ipi?
4.Shahidi.Kidato cha nne,nilihitimu Mzumbe mwaka 1974
5.Wakili wa utetezi.Eleza mahakama nafasi zako kwenye chama chako
6.Shahidi.Mwaka 1991,niliteuliwa kuwa katibu wa uvccm wilaya ya mpwapwa.2005 katibu wa ccm wilaya ya kishapu,na mwaka 2009 katibu wa ccm wilaya ya Arusha mjini,na kwa sasa nipo Kyela
7.Wakili wa utetezi.Kuna tuhuma nzito kuwa ulimhujumu Batilda kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010
8.Si kweli
9.wakili wa utetezi.Rejea gazeti la mwananchi la Mei 21 mwaka 2010(hapa wakili akamwonysha picha ya Mary Chatanda)unaitambua hii sura?
10.Simtambui
11.wakili wa utetezi.Unamfahamu Mary Chatanda,katibu wa ccm mkoa?
12.Shahidi.Sioni vizuri
13.Wakili wa utetezi.Angalia vizuri picha
14.Shahidi.Ni katibu wa ccm mkoa,Mary Chatanda
15.wakili wa utetezi.Soma vizuri alichokutuhumu nacho
16.shahidi.Chatanda alidai kuwa Salim Mpande alichangia kupoteza jimbo,pamoja na Mkurugenzi wa uchaguzi
17.Wakili wa utetezi.Una kosa lolote
18.Shahidi .sina kosa lolote
19.Wakili.Unafahamu kuwa polisi wanafundishwa kuwa ni hatari ubaguzi wa dini,kabila,rangi,au jinsia?
20.Shahidi.Ndio
21.Wakili wa utetezi.askari polisi akisikia mtu akisema usichague mtu kwa kabila,dini,au ubaguzi mwingine anatakiwa kufanya nini?
22.Shahidi.Aripoti kwa bosi wake,au pia amkamate huyo mbaguzi
23.Wakili.Kuna watu wametoa ushahidi mahakamani kuwa Mh Lema alitoa maneno ya ubaguzi,je wewe unazo hizo taarifa?
24.Shahidi.Ninazo,nilizipata kwa Aliyekuwa mgombe wa ccm Dr Batilda
25.Wakili wa utetezi.Ju huyu Musa Mkanga unafahamu alikuwa meneja kampeni wa Batilda
26.Hapana sifahamu
27.Wakili wa utetezi.Je Happy Kivuyo,na Agness walikuwa kwenye timu ya kampeni ya Dr Batilda
28.Shahidi.Hapana
29.Wakili wa utetezi.Baada ya matokeo,ulikaa na Batilda,kutafakari au kupanga kufungua kesi?
30.shahidi hapana
Baada ya hapo kesi imeahirishwa hadi kesho
 
Ivi kabla ya kuingia hapo hawa jamaa wanatumia vilevi? Eti hamjui musa mkanga.tehe tehe tehe
 
Back
Top Bottom