Kesi ya Kiongozi Uamsho: Mawakili watishia kujitoa, Sheikh Farid anyolewa ndevu...

Pasco

Natumaini hujambo. Hongera kwa ushindi mnaoendelea kuupata EL & Co.

By the way. Kumbuka Sheikh Farid amewekwa katika mahabusu ambayo Zenj inaitwa Chuo cha Mafunzo. Hili si jambo la muungano na hata mfumo wa mahakama si jambo la muungano, taratibu za wafungwa na mahabusu wa Bara ni tofauti na visiwani. Tanbua hilo mkuu.

Pili, jambo la Sheikh Farid kunyolewa limewasikitisha sana wafuasi wake waliokuwepo mahakamani leo maana kwa watu wenye IMANI kali (Sio waislamu wote naomba nieleweke vema hapa) kama Farid (Fundamentalists), kunyoa ndevu zote namna hiyo ni jambo lisilokubalika na linalochukuliwa kama usaliti kwa imani.

Sina sababu ya kuwa mshabiki katika hili kaka
Mkuu wangu tafadhali wala usiende Huko.. Kufuga ndevu lini ikiwa Uislaam au unazungumzia Culture ya waarabu. Kwa nini mnataka sana kupindisha dini ya watu kwa fikra zenu wenyewe.. Waarabu na wayahudi walifuga ndevu hata kabla mtume hajazaliwa. Infact ilikuwa fashion kwao hata Ulaya watu walikuwa wakifuga ndevu na pengine hata vifaa vya kunyolea wakati huo vilikuwa havipo, isipokuwa walichopishana ni usafi wa ndevu hizo. Tazama picha za watu na hata maprofesa wote wa zamani utaona ufugaji ndevu ni jambo la utashi wa mtu..

Mbali na hilo, afadhali ungesema bara inawezekana mtu akanyolewa kuliko Zanzibar maana wao bado wanaheshimu mila na tamaduni za watu hasa waarabu na zinaenziwa. Mkuu please Uslaam sio ndevu wala sunna ya Mtume. Ni uzushi wa watu wanaoandika vijitabu vyao kuimarisha mila zao ndani ya dini sasa wanataka hata kuubadilisha Uislaam..
 
Mkuu wangu tafadhali wala usiende Huko.. Kufuga ndevu lini ikiwa Uislaam au unazungumzia Culture ya waarabu. Kwa nini mnataka sana kupindisha dini ya watu kwa fikra zenu wenyewe.. Waarabu na wayahudi walifuga ndevu hata kabla mtume hajazaliwa. Infact ilikuwa fashion kwao hata Ulaya watu walikuwa wakifuga ndevu na pengine hata vifaa k vya kunyolea wakait huo vilikuwa havipo, isipokuwa walichopishana ni usafi wa ndevu hizo..

Mbali na hilo, afadhali ungesema bara inawezekana mtu akanyolewa kuliko Zanzibar maana wao bado wanaheshimu mila na tamaduni za watu hasa waarabu na zinaenziwa. Mkuu please Uslaam sio ndevu wala sunna ya Mtume. NI uzushi wa watu wanaoandika vijitabu vyao kuimarisha mila zao ndani ya dini.

Naomba urudie upya kusoma post yangu uelewe vizuri. Soma kwa kituo tafadhali.
SIJASEMA WAISLAMU WANA TABIA YA KUFUGA NDEVU
 
Mkuu wangu tafadhali wala usiende Huko.. Kufuga ndevu lini ikiwa Uislaam au unazungumzia Culture ya waarabu. Kwa nini mnataka sana kupindisha dini ya watu kwa fikra zenu wenyewe.. Waarabu na wayahudi walifuga ndevu hata kabla mtume hajazaliwa. Infact ilikuwa fashion kwao hata Ulaya watu walikuwa wakifuga ndevu na pengine hata vifaa vya kunyolea wakati huo vilikuwa havipo, isipokuwa walichopishana ni usafi wa ndevu hizo. Tazama picha za watu na hata maprofesa wote wa zamani utaona ufugaji ndevu ni jambo la utashi wa mtu..

Mbali na hilo, afadhali ungesema bara inawezekana mtu akanyolewa kuliko Zanzibar maana wao bado wanaheshimu mila na tamaduni za watu hasa waarabu na zinaenziwa. Mkuu please Uslaam sio ndevu wala sunna ya Mtume. Ni uzushi wa watu wanaoandika vijitabu vyao kuimarisha mila zao ndani ya dini sasa wanataka hata kuubadilisha Uislaam..
Mkuu Mkandara mimi nimekuwa nikiamini kwamba kufuga ndevu ni miongoni mwa sunna za Mtume SAW kumbe sivyo! Naona hata wachina walislimu wanafuga ndevu japo za kwao hazina mbolea! Akina Dr. Naik Zakir anafuga japo na za kwake hazina rutuba!
 
Kesi imetajwa leo katika mahakama ya Mwanakwerekwe na kisha ikahamishiwa katika mahakama ya Vuga.

Mawakili wametishia kujitoa katika kesi hyo kwa madai ya usumbufu wanaoupata wateja wao. Mawakili hao ni Salim Tawfik na Abdallah Juma wanaowawakilisha Sheikh Farid Hadi Ahmed na wenzake sita. Leo hii wamesusa kabisa kuingia mahakamani na wamesema wanakusudia kujitoa kutokana na uusmbufu wanaofanyiwa wateja wao wa kuhawangaisha.

Na sasa hivi mawakili hao wameshaondoka na watuhumiwa ndio wanafikishwa mahakamani wakiwa wamenyolewa ndevu zote wakiwa mahabusu. Kesi leo inatarajiwa kutolewa maamuzi ya masharti ya dhamana yaliyokuwa yanapingwa na mawakili wa utetezi ambao wameshaondoka mahakamani hapa.

Hatujui nini kitaendelea tena maana watu wamezuiliwa kuingia katika eneo la mahakamani. Nikipata updates nitawajulisha

Updates:
406877_300222736744489_1479620875_n.jpg

Mawakili wakisoma tamko la kutaka kujitoa kabla hawajaondoka mahakamani hapo.

293737_300224926744270_948112269_n.jpg

Sheikh Farid akiwa kanyolewa ndevu akiwasili mahakama ya Vuga leo.

MORE UPDATES:

Sheikh Farid na wenzake wasomewa mashtaka mapya:
1) Kusababisha uvinjifu wa amani zanziba
2) Kusababisha uharibifu wa mali kisiwani zanzibar kutokana na vurugu
3) Kushawishi na kuchochea vurugu zilizosababisha kuhatarisha maisha ya watu na serikali kuingia hasaraK

Aidha mtuhumiwa mmoja anatuhumiwa kumtukana Kamishna wa Polisi Zanzibar Musa Ally Musa

washtakiwa wote wamenyimwa dhamana kwani ni Jaji pekee ndie anayeweza kutoa dhamana kwa makosa yao lakini wana haki ya kukata rufaa kudai dhamana katika mahakama ya juu.

Naona kama alama ya V !! Ni mwana CDM?
 
Naomba urudie upya kusoma post yangu uelewe vizuri. Soma kwa kituo tafadhali.
SIJASEMA WAISLAMU WANA TABIA YA KUFUGA NDEVU
Pili, jambo la Sheikh Farid kunyolewa limewasikitisha sana wafuasi wake waliokuwepo mahakamani leo maana kwa watu wenye IMANI kali (Sio waislamu wote naomba nieleweke vema hapa) kama Farid (Fundamentalists), kunyoa ndevu zote namna hiyo ni jambo lisilokubalika na linalochukuliwa kama usaliti kwa imani.
Nachokwambia hakuna mahusiano baina ya ndevu na Uislaam wala Ufundamentalist mbona wapo wengi tu wasiokuwa waarabu hawafugi ndevu...Yeye ni Mwarabnu na anafuga ndefu kwa sababu ni culture yake..Kwanza ktk Uislaam unatakiwa kila mtu kuwa fundamentalist ambalo kwa kikristu tunawaita walokole. Hawa watu kina Farid ni revolutionalist ni watu wanaopenda kuitumia dini kufikisha ujumbe wao hivyo tusiuhukumu Uislaam kwa watu kama hawa.

Hivi nikuulize:- Mtu anapokwenda mahakamani akavikwa suti huwa ina maana ana uzungu sana, na hata watu wanapochukia hakuvikwa suti ni kwa saabu ya Uzungu?.. acheni hizi jamani msiwe na akili zilizofungwa kufikiri mbali zaidi.
 
Wewe ukiwa mmojawao, umenyimwa/umepoteza haki yako ipi??? Be honest, zungumzia nafsi yako wewe peke yako.

Katika uislamu haipendezi kila muumini kujali nafsi yake...Tunatakiwa tuangaliane kama ndugu wa famila moja katika imani...Mfumo kristo unaendela kukandamiza haki za waislamu ndani ya tz. Zanzibar imelazimishwa kujitoa katika OIC na wasimamizi wa mfumo kristo. Kwanini Uganda na Msumbiji wawe wanachama wa OIC , Zanzibar isiwe?
 
Hivi wakili akijitoa kwenye kesi atakua anakomoa mahakama au client wake??
All in all kumbe jamaa toto zuri tu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Katika uislamu haipendezi kila muumini kujali nafsi yake...Tunatakiwa tuangaliane kama ndugu wa famila moja katika imani...Mfumo kristo unaendela kukandamiza haki za waislamu ndani ya tz. Zanzibar imelazimishwa kujitoa katika OIC na wasimamizi wa mfumo kristo. Kwanini Uganda na Msumbiji wawe wanachama wa OIC , Zanzibar isiwe?

Umekwepa swali, unajibu siasa. Ponda kawalisha sumu hata hamuwezi kufikiria na kujenga hoja zenye mashiko. Nini maana ya mfumo kristo?? Msumbiji kwa kuwa member wa OIC wamepata faida gani kuwazidi nyie Tz?? Umaskini wa Zanzibar toka mwaka 1964 umetokana na kutokuwa kwake member wa OIC?? Wewe huo unaouita mfumo kristo umekuathiri vipi??
 
Mkuu Mkandara mimi nimekuwa nikiamini kwamba kufuga ndevu ni miongoni mwa sunna za Mtume SAW kumbe sivyo! Naona hata wachina walislimu wanafuga ndevu japo za kwao hazina mbolea! Akina Dr. Naik Zakir anafuga japo na za kwake hazina rutuba!
Sunna za mtume ni mambo ambayo ameyafanya ktk maisha yake kwa nia njema. Ni mifano bora ya kitabia kwa wanadamu wote hivyo huwezi kusema kufuga ndefu ni Sunna wakati sii watu wote wanaota ndevu wala kuwafanya wawe binadamu bora ktk matendo na maneno yao. Baba yake mtume alokufa kabla hata ya hajaanza utume alifuga ndevu na hata mjomba wake aliyekataa Uislaam alifuga ndevu. Sasa sunaa hiyo iko wapi? na Wanawake je wao watafuata sunna hiyo kivipi?..
 
http://2.bp.blogspot.com/-viuqgw61AbU/UIk-TNz4p0I/AAAAAAAByKo/dT8t9M7BnPU/s1600/DSC03103.JPG
Baadhi ya Askari wa kutuliza fujo wakiwa Mahakama kuu Zanzibar Vuga kwa lengo la kutuliza amani Mahakamani hapo.. Picha na MakameMshenga-Maelezo Zanzibar.Viongozi hao wote wamerudishwa Rumande.Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

Waziri wa Sheria na Katiba Zanzibar awe anakumbuka kutenga fedha kwa ajili ya jengo la mahakama kuu. Hata rangi imeshindikana jamani? Jengo zuri lakini maintanance hakuna.
 
Back
Top Bottom