Kesi ya IGP Mahita na tuhuma za kuzaa na mtumishi wake wa ndani

Sidhani kama Mungu anafanya kazi ya kuumbua watu. Tunajiumbua wenyewe kwa matendo yetu. Kama angekuwa anaumbua watu, mbona tungekuwa tunaishi na wasiwasi mwingi, kutokana na maovu mengi tutendayo tukidhani tumejificha? Niliona tu nisahihishe hii statement yako iliyomongelea Mungu maana umeirudia mara mbili, ikimaanisha hukuandika kimakosa bali ni mawazo yako.
Mkuu asante kwa kunirekebisha but nadhani na wewe unanirekebisha kutokana na imani yako tu, so asante. ila kwa imani yangu Mungu anaumbua wale madhalimu anaowataka kuwaumbua mbele ya binadamu wenzio, japo ni kweli kuna wengine wataumbuka siku ya mwisho.
 
Labda tujue mke wa Mahita anasemaje juu ya hili maana watoto wake anawajua vizuri; je huyu anafanana na wake?
 
hii habari ilitoka kwenye gazeti 28 Sep 2006http://www.habaritanzania.com/articles/1135/1/Kesi-ya-Mkuu-wa-polisi-mstaafu-yaanza-Dar
KESI ya madai ya kutelekeza mtoto inayomkabili Mkuu wa zamani wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Omar Mahita, ilianza kuunguruma jana katika Mahakamani ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Wakati kesi hiyo ikiendelea bila Mahita mwenyewe kuwepo, kivutio kikubwa alikuwa ni mtoto Juma Omar Mahita (8), anayedaiwa kuzaliwa IGP huyo mstaafu pamoja na mama yake, Rehema Shaaban.
Baada ya kesi hiyo iliyochukua dakika saba kumalizika, watu waliokuwepo mahakamani hapo walimfuata Rehema kwa lengo la kumuona mtoto wake.
Wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari nao walikuwa miongoni mwa waliofurika kumuona mtoto huyo na walipokuwa wanampiga picha mtoto, kwanza alipigwa na butwaa na baadaye akaanza kububujikwa na machozi.
Kipindi chote alichokaa mahakamani hapo, mwanamke huyo alikuwa akifuatwa na watu waliofurika mahakamani, hadi saa 4:00 asubuhi mwanamke huyo alipoondoka na mwanawe.
Shauri hilo la madai lilisomwa saa 2.30 asubuhi mbele ya Hakimu Mkazi Pellagia Khaday huku mdaiwa, Mahita akiwakilishwa na wakili wake, Charles Semgalawa.
Kupitia wakili huyo, Mahita aliieleza mahakama kuwa atawasilisha utetezi wake wa maandishi mahakamani Oktoba 16, mwaka huu na siku inayofuata, Oktoba 17 utetezi huo utasikilizwa.
"Mheshimiwa hakimu nitaleta utetezi wa mteja wangu kimaandishi Oktoba 16 ili kuweza kuendelea na shauri hili," alidai Semgalawa na kujibiwa na Hakimu Khaday: "Kwa kuwa utetezi utakuja Oktoba 16 kesi hiyo itaendelea Oktoba 17."
Mahita amefikishwa mahakamani kwa madai matatu yanayohusiana na kumtelekeza mtoto huyo bila tangu mwaka 1997 alipozaliwa.
Kesi hiyo ya madai yenye namba 02/06 ilifunguliwa mahakamani hapo Agosti 28, mwaka huu na Rehema akisaidiwa na kituo cha haki za binadamu.
Mbali na matunzo ya mtoto ambaye anasoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Mwongozo, Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es Salaam, mdai anaiomba mahakama hiyo itamke kuwa Mahita ndiye baba wa mtoto huyo.
Pia anataka itolewe amri ya kumtaka Mahita kulipa Sh100,000 kila mwezi hadi mtoto huyo atakapokua na kulipa gharama za matuzo ya mtoto huyo tangu mwaka 1997.
Madai hayo yameambatanishwa na hati ya kiapo ya Rehema ambapo anaelezea uhusiano wake na Mahita tangu Mei 1996 hadi Oktoba 1996 wakati akiwa mfanyakazi wa ndani wa Mahita huko Moshi, mkoani Kilimanjaro ambapo kiongozi huyo alikuwa Kamanda wa Polisi (RPC) mkoa wa Kilimanjaro.
Kufuatia mahusiano msichana huyo alipata ujauzito na hatimaye Mahita kumshauri kurudi kwao Kondoa mkoani Dodoma, ili mkewe asijue kinachoendelea kati yao.
Katika kiapo hicho binti huyo anaeleza alivyokubali kuondoka, na Mahita alivyompatia Sh 40,000 za matumizi katika kipindi hicho cha ujauzito na ahadi kumtuza bila mkewe kujua.
Baada ya mtoto kuzaliwa aliahidi kumtunza lakini alimkataza msichana huyo kufika ofisini wala nyumbani kwa kuhofia mkewe kujua siri hiyo.
 
Kesi ya Mahita, yaya:Waandishi watimuliwa mahakamani KinondoniNa Kulthum Ahmed

WAANDISHI wa habari wametimuliwa nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, wakati wa utetezi wa kesi ya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Omary Mahita ya madai ya matunzo ya mtoto.

Waandishi hao, walitolewa nje baada ya wakili wa Mtuhumiwa Charles Semgalawa kuiambia mahakama kwamba waandishi wa habari, hawaruhusiwi kuisikiliza kesi hiyo baada Hakimu Stamili Ngwawasya kutoa tamko hilo, awali.

Semgalawa alifafanua kwamba Hakimu Ngwawasya aliagiza wakati wa kuisikiliza kesi hiyo,waandishi wa habari wasiruhisiwe kuisikiliza.

Maamuzi hayo ya hakimu huyo yalikuja baada ya pande zote mbili kukubaliana kuwa kesi hiyo iwe ya siri baina yao.

"Julai Mosi 2008 Hakimu Ngwawasya, alitoa tamko kwamba waandishi wa habari wasisikilize kesi hii," alidai Semgalawa.

Hakimu Suzan Kihawa aliiambia Mahakama kuwa hakuona maelezo hayo, lakini wakati Hakimu huyo akisema hivyo, wakili Semgalawa alimtaka Hakimu asome kumbukumbu za kesi hiyo za Julai Mosi 2008.

Baada ya Hakimu Kihawa kusoma maelezo ya tarehe hiyo, alisema kesi hiyo, itaendeshwa faragha na kwamba waandishi wa habari, hawaruhusiwi kuisikiliza na hivyo watoke nje.

"Kwa kuwa tupo chemba court (Mahakama ya faragha), waandishi mnatakiwa mkae nje na mlango ufungwe ili tuweze kuendelea na mahakama,"alisema Kihawa.

Mahita anakabiliwa na shtaka la madai ya matunzo ya mtoto wa aliyekuwa mfanyakazi wake wa ndani (housegirl), Rehema Shabani. Kesi hiyo, inatarajiwa kuendelea Septemba 10, mwaka huu kwa ajili ya kutolewa maamuzi.
 
Kesi ya Mahita, yaya:Waandishi watimuliwa mahakamani KinondoniNa Kulthum Ahmed

WAANDISHI wa habari wametimuliwa nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, wakati wa utetezi wa kesi ya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Omary Mahita ya madai ya matunzo ya mtoto.

Waandishi hao, walitolewa nje baada ya wakili wa Mtuhumiwa Charles Semgalawa kuiambia mahakama kwamba waandishi wa habari, hawaruhusiwi kuisikiliza kesi hiyo baada Hakimu Stamili Ngwawasya kutoa tamko hilo, awali.

Semgalawa alifafanua kwamba Hakimu Ngwawasya aliagiza wakati wa kuisikiliza kesi hiyo,waandishi wa habari wasiruhisiwe kuisikiliza.

Maamuzi hayo ya hakimu huyo yalikuja baada ya pande zote mbili kukubaliana kuwa kesi hiyo iwe ya siri baina yao.

kwa nini hii kesi iwe ya siri? Naelewa kuwa kuna kesi ambapo majina yanaweza kuminywa, lakini kesi kuwa siri kweli? Moja ya nguzo zinazojenga mahakama sio uwazi kwa kila mtu?
 
kwa nini hii kesi iwe ya siri? Naelewa kuwa kuna kesi ambapo majina yanaweza kuminywa, lakini kesi kuwa siri kweli? Moja ya nguzo zinazojenga mahakama sio uwazi kwa kila mtu?
lakini mbona inaoneshwa kana kwamba walikubaliana kesi iwe ya siri! kama walikubaliana hivi ni kwa nini mdai alikubali? Na kwa nini upande wa tatu-yaani waandishi-hawakushirikishwa kwenye maamuzi ya kuifanya kesi isikilizwe kwa siri?
 
WAANDISHI wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari jana walijikuta wakitolewa ndani ya Mahakama na kudaiwa hawaruhusiwi kusikiliza kesi hiyo inayomkalibili aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Omari Mahita
Hatua hiyo imekuja baada ya wakili wa mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina la Charles Semgalawa kutaka waandishi watokea nje na hawaruhusiwi kusikiliza kesi hiyo kwa kuwa ilitakiwa iendeshwe faragha.

Waandishi hawakuridhika na maamuzi hayo na wakili huyo kumwambia Hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo kusoma maagizo yaliyotolewa awali na Hakimu Ngwawasya mahakamani hapo.

Hivyo Hakimu Suzan alisoma maelezo hayo yaliyotolewa na Hakimu huyo na kuwaambia wandishi hao kuwa watoke nje kwa kuwa kesi hiyo ilitakiwa isikilizwe faragha.

Hakimu aliwaambia waandishi hao kuwa kulitolewa maelezo ya kuwa kesi hiyo haitaendeshwa Open Courty na kuwataka waandishi hao watoke nje.

Hivyo kutokana na maelezo hayo ya Hakimu waandishi wa habari walilazimika kutoka nje ya mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi Kinondoni na kuacha kesi hiyo kwa siku hiyo ikiendelea faragha.

Mahita anakabiliwa na mashitaka ya kumtelekeza mtoto wake wa kiume aliyezaa na aliyekuwa msichana wake wa kazi za ndani.

Ilidaiwa Mahita kuwa alimtelekeza msichana huyo na mtoto wake bila kumpa huduma muhimu stahili na msichana huyo kwenda kumfungulia mashitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo kesi hiyo inaendeshwa.

Kesi hiyo iliahirishwa na itarudi tena Mahakamani hapo Septemba 10, mwaka huu kwa kutolewa maamuzi.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2675102&&Cat=1
 
Mimi naona poa tu mwishoni si tutajua tu, kwani kuna siri gani hapo? Hawataki mzee mzima aumbuke. Alikua anapambana na majambazi wakati alikua katika harakati kwa kumtengeneza - the could-be Jambazi. Manake wanaotelekeza kama yeye ndio hao wako barabarani, wengine wala unga, machangudoa. Ukiwauliza baba yuko wapi wanakwambia - hata sijui au alitukimbia. Very stupid indeed!
 
Mahita atakuwa ameshatumia gharama kubwa sana katika hiyi kesi kuliko hata gharama ya kumtunza huyo mtoto. Labda angetakiwa awe analipa laki moja kwa mwezi na siyo hela ya ajabu kwake. Sasa katika kesi anamlipa wakili, anatumia mafuta yake kutoka morogoro kuja kwenye kesi kila wiki, anatumia air time ya kutosha kujibu sms za pole na simu kutoka kwa rafiki zake, na kibaya zaidi, anaanikwa kwenye magazeti kila kesi inapokuja. Nafikiri kuandikwa andikwa na kusemwa semwa negatively ni costly hata zaidi ya kutumia hela kidogo kumtunza mtoto. After all, kwa sisi waafrika, or rather watanzania hatuna utaratibu wa kutunza biological kids pekee hata watoto wa ndugu huwa tunawatunza tu kama kawaida
 
Nasikia sheria za nchi za kutunza mtoto kama hii kesi ni shs. 10,000 kwa mwezi, nadhani mtoto huyu siyo wake wangeshayamaliza kwa faragha, ila atakuwa alitembea na huyo binti.
 
lakini mbona inaoneshwa kana kwamba walikubaliana kesi iwe ya siri! kama walikubaliana hivi ni kwa nini mdai alikubali? Na kwa nini upande wa tatu-yaani waandishi-hawakushirikishwa kwenye maamuzi ya kuifanya kesi isikilizwe kwa siri?

Waandishi hawawezi kusikilizwa as a third party maana kesi haiwahusu wao. Nimesoma katika jurisdiction nyingine, kuna kesi unaweza kuomba kukawa na closed court.
Kwa mfano australia unaweza kupata details zake hapa:http://www.courts.qld.gov.au/Benchbook/SD-61-ClosedCourtExceptionsToTheGeneralRuleOfOpenness.pdf
Kwa kesi kama za sexual assaults, nk
 
Yawezekana housegirl alikuwa pia anatembea na houseboy na pia kijana wa ng'ombe..sasa je Mahita ana uhakika mimba yake?

Kiubinadamu amlee tu huyu mtoto malaika!
 
Si akubaliii amtunze??kuna haja gani kuvuliwa nguo na huyo dada........
 
Amlipe fidia huyo kimada wake kwa kuwa yeye ndio aliyetaka makubwa kwani alikuwa na uwezo kumpa fedha za matumizi na kuzuia kesi.Au alitaka kuumbuka nini?
 
Nasikia sheria za nchi za kutunza mtoto kama hii kesi ni shs. 10,000 kwa mwezi, nadhani mtoto huyu siyo wake wangeshayamaliza kwa faragha, ila atakuwa alitembea na huyo binti.

Ka nini anakataa kufanya DNA test sasa? DNA inaweza ku settle the issue squarely.
 
On the Complainant: it is all about being a needy person:

Plaintiff in Mahita paternity case seeks financial aid for DNA testing

2008-07-12 09:59:49
By Lydia Shekighenda


A woman who claims to have had a child with former Inspector General of Police Omary Mahita, Rehema Shabani, is seeking help from good Samaritans to raise money for performing DNA test that will prove that the retired police chief is the biological father of her child.

Speaking to journalists at the Tanzania Labour Party head office in Dar es Salaam where she went to ask for assistance from the party`s women wing chairperson, Rehema said the test, known as deoxyribonucleic acid (DNA) , is very expensive and she cannot afford it.

Rehema, who has filed a case in the Kinondoni district court to seek maintenance for the child, said hearing of the case had begun and what was needed now was the DNA evidence to prove that Mahita is the biological father of the boy.

``Since I am the one who went to court, I am supposed to pay for the DNA test, which is 300,000/-,`` she said.

She said her decision to go for the DNA test was because the ex-police chief does not want to acknowledge the boy as his. The child is called Juma Omari Mahita.

``The only evidence which I believe would work and prove the truth about the father of this baby is the DNA test,`` she said.

Rehema claims that she had a love affair with the respondent from May 1996 to October 1996 while she was working at the respondent`s house as a house girl in Moshi when Mahita was Regional Police Commander there.

She further claims that she conceived in 1996 in the course of their amorous relationship and informed the respondent of the pregnancy, who allegedly advised her to go and settle in Kondoa as she prepared for delivery.

Rehema further claims that at no material time did the respondent challenge her pregnancy, meaning he had not objected to being the putative father of the baby boy, Juma Omari Mahita, born in March 1997.

TLP Women Wing Disciplinary Chairperson Rose Mrema said the government should review the charges for DNA tests because most people could not afford them.

``There are women who could wish to go for DNA test but they failed because the service is too expensive and not available in many areas.`` She said.

She however said the government should consider this service as crucial and minimize the costs so that many people could afford and it will help to reduce the number of children abandoned by their fathers.
 
Back
Top Bottom