Kesi ya akina Mramba nayo yafutwa

Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,550
6,062
KESI YA AKINA MRAMBA NAYO YAFUTWA
Baada ya Serikali kuwafutia kesi waliokuwa vigogo wa (BoT) akina Liyumba na Mwenzake, Brother Deus, kwa kile ilichodai kukosea kufungua mashtaka, na kuwapa kesi nyingine kama ile ya awali, waliokuwa Mawaziri waandamizi, Basil Mramba, Danieli Yona pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja, kesi yao leo ilifutwa baada ya mashtaka kukosewa. Licha ya kesi iliyokuwa ikiwakabili kufutwa, vigogo hao wamefunguliwa kesi nyingine kama hiyo, duh! kazi ipo.

1242652768_1.jpg

Kutoka kushoto ni Basil Mramba, Danieli Yona wakiangua kicheko wakati wakishuka kizimbani na wa mwisho ni Gray Mgonja, yeye aliishia kutabasamu.

1242652876_2.jpg

Waliofika kusikiliza kesi hiyo baada ya kuahirishwa kila mmoja alitoka huku akibwabwaja lake.

1242653055_3.jpg

Huyu ndiye Profesa Leonard Shahidi, Wakili anayewapeleka puta Wanasheria wa Serikali katika kesi hiyo.

1242653327_4.jpg

Yona na Mgonja (kushoto) wakirudi uraiani kula 'bata'.
PICHA: RICHARD BUKOS NA CHRISTOPHER LISSA

Habari kutoka Global Publisher
 
Duu, Mwana Kijiji na wengine.

Mwanzo sikuamini niliposikia ni USANII. Sasa naanza kuamini kuwa hata kesi iliwekwa ili akina Mramba washinde. Sawa, wametufunga goli la Pili Mafisadi. Ila cha kufurahisha ni kuwa siku Arobaini zinazidi kusogea.

Tunawatakia maisha mema huko uraiani wakati watakuwa wanafaidi hela zetu. Hakuna ya kumtaja Mkapa wala nani yake. Kila kitu kinakufa kama maji kwenye jangwani.
 
Kesi kufutwa au ujanja wa kisheria kupoteza muda? Itapigwa tarehe weee hadi watu watasahau juu ya hizi kesi!
 
yaleyale niliyosema kwamba kesi haina mguu wala njia yametimia....

Serikali ingeweka precedent kubwa na nzito kwa wale wote walioifanya ipatae hasara akiwemo Jk, BWM na wengineo...

bora kubali yaishe, futa kesi leta nyingine ifutwe pia..
 
Tulishasema hapa kwamba hizi kesi ni ni kiinimacho. ila hawajui kwamba nafsi haichoki kuhifadhi kumbukumbu za maumivu ya sasa....

Lakini mkuu wamefutiwa kweli au??? maana.....
 
Tulishasema hapa kwamba hizi kesi ni ni kiinimacho. ila hawajui kwamba nafsi haichoki kuhifadhi kumbukumbu za maumivu ya sasa....

Lakini mkuu wamefutiwa kweli au??? maana.....

Habari imejaa tele kama pishi la .......

TOO SAD.
 
Sasa bado za EPA kufutwa ndiyo usanii wa hii serkali iliyokuwepo madarakani. Walitupa imani wananchi na wengine hata kutamka kwamba sasa "Kikwete kaamua kufanya kweli" kumbe hakuna lolote bali ni USANII NA UPUUZI MTUPU!
 
sante sana mkuu
hakuna jipya hapo ni kulindana tu.
ila nahisi kuna mkataba mzito nyuma ya pazia ndo maana walumendago wamewalk free
 
BAK,

Kuna site yenye maelezo mengi zaidi? Please ukizipata basi turushie hapa maana naona leo JF hata hii habari imetupita kushoto na wengine hadi wameshaiweka kwenye site zao.

NB: Mnyang'anyeni kisu Mwanakijiji maana nasikia anaanza KUKATA TAMAA.
 
Tulishasema hapa kwamba hizi kesi ni ni kiinimacho. ila hawajui kwamba nafsi haichoki kuhifadhi kumbukumbu za maumivu ya sasa....

Lakini mkuu wamefutiwa kweli au??? maana.....

Nachelea kukubali kwamba ni kiini macho na kama ni kweli basi ni tusi kubwa sana kwa wanasheria waadilifu nchini.... profession ya sheria imepigwa doa jesi kwenye makalio!!!!

Wanasheria tusaidie kuchambua kwa kina na kutupa moyo kwamba wanasheria wetu hawamo ndani ya kile chungu cha bibi

Kuna mtu mmoja alisema the best indicator of a corrupt legal system is the rich lawyers---- sijui ina maana gani
 
Sasa bado za EPA kufutwa ndiyo usanii wa hii serkali iliyokuwepo madarakani. Walitupa imani wananchi na wengine hata kutamka kwamba sasa "Kikwete kaamua kufanya kweli" kumbe hakuna lolote bali ni USANII NA UPUUZI MTUPU!

Baba makosa ni ya kisheria, kesi itarudi tena, kwa mawakili wa Utetezi ndio njia nzuri ya kula mshiko wa akina Yona/Mramba/Mgonja.

Tangu lini Rais alikuwa mwanasheria!

Lakini mimi kuna moja angalau naliamini, huwezi kumlipa state attorney 400,000/- ashindane na mtu anayelipwa 10,000,000/- kwa mwezi.

Ngoja tuone.
 
Ni wananchi tu ndio wanaoweza kuifuta hiyo kesi. Fikiria jinsi CCM walivyozomewa Busanda wananchi waliposikia hakimu anamdai hela Kubenea,sh. b. tatu.
 
Sikonge,

Yaani wewe uliona hawa walikuwa na kesi ya kujibu? ha ha ha, ni bora wangemuuliza Yona, wewe kama waziri wa nishati, ni vipi BMW alijiuziaje kiwanda?
 
La kufurahisha ni kwamba huo ndio utawala wa sheria, uamui tu kumshitaki mtu ukadhani atafungwa lazima uwe na ushahidi wa kutosha, kesi au mashitaka yawe ya uhakika.

Mimi nadhani ndio maana tutalia weeee lakini hakuna siku Mh. Rostam atapanda kizimbani, issue ni rahisi hakuna ushahidi wowote wa maana... kama akina Mh. Mramba wameonekana hawana issue, kwa Mh. Rostam ndio hakuna lolote kabisaaaa
 
Licha ya kesi iliyokuwa ikiwakabili kufutwa, vigogo hao wamefunguliwa kesi nyingine kama hiyo

..nadhani muendesha mashtaka atafungua kesi upya/mpya.

..haya mambo ni ya kawaida kabisa kutokea.

NB:

..mashtaka yale ya kuitia hasara serikali nadhani yangeweza kujenga precedence moja kali sana.

..kwa mfano, waziri Magufuli ambaye alitoa uamuzi wa kubomoa kituo cha mafuta Mwanza. mwenye kituo cha mafuta alishtaki na hukumu ikatolewa kwamba serikali imlipe mabilioni ya pesa. katika kesi hiyo ilibainika kwamba Magufuli alipuuza ushauri wa wataalamu.
 
Last edited:
Yombayomba,

Kwanza habari za kupotea. Nilikuandikia lakini kimya. Anyway tuwasiliane kwa kutumia PM.

Ni kweli nilijidanganya na kunywa sana siku hiyo Wanzuki kibao. Natamani niende kwa mama muuza nimrudishie wanzuki yake na mie nipate vihela vyangu. Nimeibiwa mara mbili maana hata mama muuza kaniibia.

Hawa jamaa ipo siku. Yombayomba inabidi siku moja mkono utembezwe na hapo ndipo watu watajua kula kwa kunawa. Sasa hivi acha tu watutese kwa kupita na magari yao ya bei mbaya ila kuna siku wataipata joto la Pertsovka vodka, inakuja na pilipili......
 
Baba makosa ni ya kisheria, kesi itarudi tena, kwa mawakili wa Utetezi ndio njia nzuri ya kula mshiko wa akina Yona/Mramba/Mgonja.

Tangu lini Rais alikuwa mwanasheria!

Lakini mimi kuna moja angalau naliamini, huwezi kumlipa state attorney 400,000/- ashindane na mtu anayelipwa 10,000,000/- kwa mwezi.

Ngoja tuone.

Tena nasikia wakati mwingine hawa mawakili wa pande mbili hukutana na kutambiana madau yao na wakati mwingine wenye dau kubwa huwashawishi wenye dau dogo kuegemea upande wao kwa namna wanaoijua wao na kisha anayetetewa na wenye dau dogo hushindwa kesi. Hizo ndo mahakama zetu. Haki inapatikana kwa MUNGU tu hapa duniani ni usanii mtupu.
 
Hizi kesi zote zilizopo mahakamani kwa sasa, ile ya EPA, ya akina Mramba, ya Prof. Mahalu, na ya twin tower ni uhuni mtupu!! Serikali yote imejaa wahuni watupu!!
 
Hahahaha wacha nicheke mie........... Sanaa ndo hizo zishaanza kazi yetu kubwa nikuangalia tu hao wasanii wanatuletea kiburudisho gani cha kukonga nyoyo zetu alhaula lakwata!!!!
 
Huu ni mchezo wa kuigiza, tamthilia ambayo haitaisha leo wala kesho, hao wachache waliodakwa ni mbuzi wa kafara lakini hawatachinjwa! Itapigwa danadana hadi uchaguzi mkuu ufanyike then the worst will come- ITAFUTWA!
 
Back
Top Bottom