Kesi ubunge wa Lema: Hukumu tar 5 April...

bibikuku

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
832
495
Swali ni kwamba, Lema atashiriki mkutano ujao wa bunge mwezi April Dodoma ama ndio mwisho wa safari na tujiandae tena kwa uchaguzi mdogo? Hukumu ya kesi yake sasa inatolewa Tarehe 5 mwezi ujao. Pande zote mbili zimemaliza kutoa ushahidi wake na kila upande umemaliza kutoa maelezo ya mwisho ya kesi.
 
Sijui kama kunakuwa na uchaguzi mwingine mdogo nadhani sheria ilibadirika katika hilo; sina uhakika sana.
 
Kwa hali ilivyo..... Uje uchaguzi mdogo mwingine, Lema ataongeza margin ya ushindi alokuwa ameupata 2010.
 
Mlalamikaji anatafuta kujikosha tu wakati maji yalimfika shingoni ngoja tuone
 
Kwa hali ilivyo..... Uje uchaguzi mdogo mwingine, Lema ataongeza margin ya ushindi alokuwa ameupata 2010.

mara nyingi mlalamikiwa huzuiwa asishiriki uchaguzi mdogo,itabidi awekwe cdm mwingine
 
Naunga mkono.
Hii kesi ni ya kipumbavu, Lema kalichukua lile jimbo kiulaini mno na mashahidi wa hii kesi walitia aibu!!


Hakuna kesi pale ni mbwembwe tu. walikuwa wanatafuta jinsi ya kula pesa ya CCM na mbunge mwenyewe na isitoshe kuna baadhi ya mashahidi hakutokea upande wa walalamikaji.

Hata wakiludia tena CCM hawawezi kushinda na sanasana ni aibu kubwa zaidi ya 2010
 
Wamwambie hakimu atengeue ubunge wa Lema kisha waone jinsi hli itavyokuwa mbaya.
 
Hukumu itakapotoka Lema anapigwa ban kugombea tena CCM wanashinda kiulaiiiniii!!
 
Navutiwa xana na ushahidi unaotolewa kwenye kesi ya MPENDAZOE Vs MAK0NGORO
Segerea Uchaguzi mdogo ni kitu ambacho kakihepukiki na nitashangaa sana kama CHAADEMA mpaka sasa watakuwa hawajaanza maandalizi ya kulichuwa rasmi jimbo hili.
 
Segerea Uchaguzi mdogo ni kitu ambacho kakihepukiki na nitashangaa sana kama CHAADEMA mpaka sasa watakuwa hawajaanza maandalizi ya kulichuwa rasmi jimbo hili.

yaani,japo sijaenda mahakaman,lakin kwa jins inavyoripotiwa,ile kesi ni ngumu kwakweli,any way tusubiri!
NILISHTUKA NILIPOSKIA MAK0NGORO ALIKUTWA NA MASANDUKU.TABATA
 
Kama umefuatilia kesi ya msingi sijaona mahali lema kapatikana na hatia labda kama ccm watatumia mahakama vibaya na hili linaweza kuwa hatari zaidi kwao
 
Back
Top Bottom