Kesi inayowakabili Viongozi waandamizi wa CHADEMA kuendelea kusikilizwa kesho Arusha

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,221
1,788
Ile kesi ya Maandamano ya January 5,inayowakabili viongozi waandamizi wa CHADEMA,akiwepo Mwenyekiti Taifa Freeman Mbowe,katibu Mkuu Taifa,Dr Slaa, Wabunge Ndesamburo, Selasini, Lema, na viongozi wengine wa mkoa, wilaya na wanachama, itaendelea kusikilizwa tena kesho Jumatatu tarehe 28, katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha.

Juzi Ijumaa wakili wa utetezi aliweka mapingamizi kwenye mashtaka yote yanayowakabili kwa kuwa yamefunguliwa kinyume cha sheria na taratibu, hivyo akaomba hakimu aitupilie mbali.

Ndipo wakili wa serikali akaomba hadi Jumatatu ili aweze kuyapitia.
 
Mkuu! Tunamshukuru MUNGU kwa hili na bila shaka tutakuwepo hapo mahakamani bila ya kukosa! Zaidi ya yote ni tunategemea uwepo wa wanaCDM km kawa na ukizingatia hii kesi ina historia ambayo ni ngumu kuisahau ktk Taifa letu ambalo polisisiem wamelisababisha. Tupo pamoja na nyuma haturudi mpk kieleweke! Wao wana pesa sisi tuna MUNGU!
 
Hivi hizi gharama za kwenda Dar - Arusha kwa viongozi wetu vipi? Nataka fungu la kumi mwaka huu 2011 nitoe kuchangia gharama. Ukombozi hauji ivi-vi. Mkuu Ephata toa mwongozo.
 
Mkuu! Tunamshukuru MUNGU kwa hili na bila shaka tutakuwepo hapo mahakamani bila ya kukosa! Zaidi ya yote ni tunategemea uwepo wa wanaCDM km kawa na ukizingatia hii kesi ina historia ambayo ni ngumu kuisahau ktk Taifa letu ambalo polisisiem wamelisababisha. Tupo pamoja na nyuma haturudi mpk kieleweke! Wao wana pesa sisi tuna MUNGU!

Mkuu nimependa sana ulivyochangia. Kwa kifupi umeeleza vizuri niliyotaka kuchangia. Tuko pamoja!
 
Mkuu! Tunamshukuru MUNGU kwa hili na bila shaka tutakuwepo hapo mahakamani bila ya kukosa! Zaidi ya yote ni tunategemea uwepo wa wanaCDM km kawa na ukizingatia hii kesi ina historia ambayo ni ngumu kuisahau ktk Taifa letu ambalo polisisiem wamelisababisha. Tupo pamoja na nyuma haturudi mpk kieleweke! Wao wana pesa sisi tuna MUNGU!

Hapo kwenye red inanifanya nitamani kuingia msituni kwa hasira!
 
Hapo kwenye red inanifanya nitamani kuingia msituni kwa hasira!

KAMANDA! Hakika nakwambia ya kwamba,kama hakuna marekebisho yoyote yatakayofanyika hasa kuhusu mambo yanayolenga KATIBA ya Nchi hakika nakwambia hatuna budi kuzama mstuni ktk hali ya harakati ya UKOMBOZI wa vizazi vijavyo! Maana Mwenyenzi MUNGU wa rehema ametupata TANZANIA yetu yenye kila kilichomuhimu kwa mwanadamu lakini mafisadi wameikumbatia lakini watajutia nawaambia! Kwa hali ndg zetu wanachotufanyia nawambieni ya kwamba inaniumiza sana nafsi!
 
Advocate kimomogoro ametoa hoja za msingi.ni aibu polisi kushnda wanakimbizana na chadema huku wakishndwa kutekeleza mambo muhimu.hiv dege la kubeba twiga si lilitua kia?mbona kesi hiz za msingi hatuziskia bali kesi za chadema?mapolisi wenye akili ni kamanda nyakoro sillo,isutu mantage.mengine ni bongo lala.si wanajiita kuwa wameanzisha "polisi jamii".basi waombe jf apa wapewe polis forum or polisi jamii.ili wawe wanapewa vipande vyao na wajue jamii kwa sasa inataka nini.sheri hayajui bali yape kukamata watu kwa nguvu
 
Penye mafanikio hapakosi challenge kama hizi Mungu yupo atawatetea kwani hamtupi mja wake
 
Ni kuwapa mambo mengi ili washindwe kuibana serikali kama leo hii si mmeona Dr. hakuwapo ikulu ni kwa sbb yupo arusha kwa ajili ya kesi
 
Nanyaro Ephata! Samahani sana kwani mambo yaliingiliana tunaomba utupe UPDATES,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,!!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom