KESI hizi zimeishia wapi???

dguyana

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
423
110
Wanabod Waaasalamu aleikum & Bwana asifiwe,

Kuna yeyote mwenye update za kesi zifuatazo atujuze??

1. Karamagi na mwenzie kesi ya ubadhilifu.
2. Mwakalebela na Mrs Sitta - Kesi ya rushwa.
3. Mtoto wa liyumba - Madawa ya kulevya
4. Mtoto wa mengi - Madawa ya kulevya
5. Askofu na wenzie arumeru - Rushwa.
6. ....... Weka kama unayo...

Maana tunaona kesi zinazopewa coverage ni za uchaguzi tu hasa za chadema kunani hizi????
 
Kesi ya ndugu yake Rostam aliyekamatwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya mabillioni ya shilingi!

Kesi za Epa zinazomhusu Jeetu Patel?
 
Uchunguzi juu ya Hosea wa TAKUKURU
Uchunguzi wa polisi waliohusika na kumbambikia mtoto wa Mengi madawa
......................................

Kupitia thread hii naomba mods watuwekee thread moja ya kuendelea(ndiyo sticky?) kufuatilia kesi hizi na tume zinazoundwa kila kukicha kwani wanfanya hivyo kutupumbaza kuwa jambo linashughulikiwa.
 
Kesi hizi zilipitia tundu lilelile walipopitia waliouziana nyumba za serikali,kiwira,upakiaji na upakuaji makontena bandarini,lupembe chai,kapunga,richmond,meremeta,buzwagi nk.

Msijali kwa wanaojua historia ya madhalimu atajua ni nini kinafuata na lini.
Ila kwa wakwapuaji wanajificha kwa kufumba macho tunawapa pole.
 
Back
Top Bottom