VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Ile kesi ya wanafunzi 172 na wengine inayohusu wanafunzi hao kukataa vyeti vya Chuo Kikuu cha Ardhi na kutaka vya UDSM imechukua sura mpya.Kesi hii iliyoanza mwaka 2007 ipo mbele ya Jaji Dr.Feuz Twaib wa Mahakama Kuu ya Tanzania,Kanda ya Dar es Salaam.
Ilivyokuwa: Wanafunzi walipata udahili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya UCLAS(sasa Ardhi University).Wakati wameshasajiliwa na kuanza masomo,UCLAS ikawa chuo kamili:Ardhi University.Walipomaliza masomo yao,Ardhi wakataka kuwatunuku vyeti wanafunzi hao.Wanafunzi wakagoma.Wakafungua kesi.Wakaiomba Mahakama Kuu itoe amri kukishinikiza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kiwape vyeti vyao.Jaji Twaib akawapa amri waliyoiomba.Utekelezaji ukaanza.Katikati pakatokeo jambo.UDSM na Ardhi wakataka kugawana wanafunzi wa kuwapa cheti huku na kule.
Wanafunzi wakagomea hilo tena.Wakamrudishia Jaji Dr.Feuz Twaib hukumu yake aitafsiri kwa njia ya maombi maalumu kisheria.Jana ilikuwa siku ya hukumu.Kesi imeahiriswa hadi tarehe 19 mwezi huu.
Kimsingi,wanafunzi hawa hadi sasa hawana vyeti.Hawaajiriki.Wataishije? Nani alaumiwe hapa?
Kesi yajulikana kama:Lelo Didas and 171 Others versus 1.ARDHI UNIVERSITY 2.UDSM 3.ATTORNEY GENERAL