Kesi dhidi ya katiba mpya mahakama kuu

Unajua kikatiba, serikali ni ya muungano i.e URT

Kuupinga muungano ni sawa na ku- redefine territorial borders, almost an act of war.
Vyama vya siasa ni lazima viwepo bara na visiwani, just to verify their allegiance. Na ukiwa mwanachama maana yake umekubali muungano. Ndiyo maana KAMAHURU ilitakiwa iwe na wanachama bara ie CUF.

Sasa, mgombea binafsi atakuwa kiyume na matakwa ya katiba kuhusu vyama vya siasa, kuwa ni lazima viwe vya muungano.Na mtu mmoja hawezi kutambuliwa rasmi utiifu wake kwenye muungano eg. Mtikila.

Hii ground ni ngeni kwangu..na nimepata shida kidogo kuielewa kwa jinsi ulivoiandika...ngoja niisome judgement ile tena afu nirudi kuizungumzia ground yako..
 
Rais wa Tanganyika Law Society tunampa go ahead, uwezekano wa kunullfied hiyo sheria ya kuunda Katiba mpya upo.
Kushirikiana ndio muhimu sana, ikiwa Mahakama Kuu watachakachua, Muelekeo utakuwa sehemu husika ya kimataifa.
Ni "Internationa Court of Justice"
Peace Palace
Carnegienplein 2
25117 KJ
The Hague
Holland
Kwa maswali yanayohusika andika Email: information@icj.org Web site: w w w icj-icj. org
Haya watanzania wote tupiganie haki yetu. Hiyo web site nimeiandika kiaina kwa sababu kila nikiposti hii thread nakuta wamechakachua.
Katika kuandika utaziunganisha hizo w pamoja na kuweka dot, na hiyo org utaiweka kama kawaida baada ya dot.
 
... mahakama inaweza kudeclare hicho kipengele void tothe extent of inconcistence na katiba na sheria yenyewe kama yenyewe ikaendelea

... ikibainika na mahakama kweli procedure zilikiukwa basi sheria nzima inaweza kubatilishwa yani kuwa nullified na hivyo tukaanza mwanzo..which is what i pray for.
Ni lini sheria ya Tanzania iliwahi kubatilishwa na kufutwa na mahakama?
 
Ni lini sheria ya Tanzania iliwahi kubatilishwa na kufutwa na mahakama?

Kuna section katika the Government proceedings Act ilikuwa declared void(tafuta kesi ya Kukutia ole pumbun V.AG)
Hiyo section ilikuwa inataka ukitaka kuisue serikali lazima uombe consent kutoka kwa serikali yenyewe..which meant the government was a judge in her own cases contrary to Natural justice na pia ilikuwa inawanyima watu access to justice etc so katika hiyo kesi hicho kipengele kikawa declared void..
Matokeo ya kubatilishwa huko marekebisho yakafanyika sasa hivi huhitaji ruhusa(consent) kuishtaki serikali kama awali bali unachopaswa kufanya ni kuinotify tu...notice to sue ambayo kama sikosei ni siku tisini..

Pia nimesite hapo juu kesi ya takrima...
 
Hii ground ni ngeni kwangu..na nimepata shida kidogo kuielewa kwa jinsi ulivoiandika...ngoja niisome judgement ile tena afu nirudi kuizungumzia ground yako..
For a political party to be registered, one of the requirements is to have members in both sides of the union.

The president is one part of the Parliament representing the people of URT.
If he is against the union, he wouldn't be doing one side of our union justice in the Parliament.
Mwaimu used representation as a point of argument and was connected with the 1962,65,77 and 85 constitution to his failure mainly because he hesitated to include the union in his arguments.
That was the main reason for ammendments.
 
Huku kote ni kutaka kuchelewesha upatikanaji wa Katiba mpya na ni vyema suala hili lisiachwe hivi hivi, tunahitaji kusonga mbele na hatua zinazofuata tusikubali kurudi nyuma na wanaojiita wanasheria.

bora tuchelewe lakini tupate kitu kilicho bora. Mimi nawapongeza wanasheria kwa sababu mambo ya kupelekana kama mbuzi kwenye gunia yamepitwa na wakati. Mia
 
ni sawa sawa kufungua kesi hiyo kwani nac wanyonge tutapata walau haki yetu ya msingi ya kutoa maoni na kukosoa makosa
 
Hiyo ground ya kwanza mahakama inaweza kudeclare hicho kipengele void tothe extent of inconcistence na katiba na sheria yenyewe kama yenyewe ikaendelea.

Lakini hiyo ground ya pili ikibainika na mahakama kweli procedure zilikiukwa basi sheria nzima inaweza kubatilishwa yani kuwa nullified na hivyo tukaanza mwanzo..which is what i pray for.

Mamlaka ya raisi kuteua tume na mabunge mawili kushiriki katka kuinyambulisha katiba iliyopo ni vyema nayo yakahojiwa.....kwa sababu kwenye katiba iliyopo mamlaka hayo lazima yatafutwe kwa ridhaa ya wananchi kwanza hakuna suala la uwakilishi hadi ridhaa hiyo ipatikane kwanza soma hukumu ya mahakama kuu ya Kenya kwenye suala la kupinga mkutano wa Boma......
 
Ndugu ICC zinakwenda kesi za jinai za makosa ya uhalifu wa kimataifa yani international crimes..
So kisheria tunasema ICC haina jurisdiction (mamlaka/uwezo kisheria) kupokea kesi kama hii..

Kwa mujibu wa ibara ya 30(3) ya katiba na kwa mujibu wa basic rights and duties enforcement Act, mahakama kuu ndio sehemu muafaka ya kuanzia.
Mnh!
Nakumbuka akina Palamagamba walivyoichakachua haki ya mgombea binafsi. Tusubiri na hii sijui watawaita tena hawa marafiki zao wa mahakama.
 
Mnh!
Nakumbuka akina Palamagamba walivyoichakachua haki ya mgombea binafsi. Tusubiri na hii sijui watawaita tena hawa marafiki zao wa mahakama.

Yah hao amicus curiae waliochaguliwa kipindi kile mi nlikua namkubali zaidi Jwani..
Palamagamba siku zote nimekuwa simwelewi ni mtu wa aina gani,hayuko consistent na mara kadhaa ametokea kulamba miguu serikali..
Sijui safari hii itakuwaje na nani wataitwa km friends of the court-that is,kama wataitwa.
 
Mamlaka ya raisi kuteua tume na mabunge mawili kushiriki katka kuinyambulisha katiba iliyopo ni vyema nayo yakahojiwa.....kwa sababu kwenye katiba iliyopo mamlaka hayo lazima yatafutwe kwa ridhaa ya wananchi kwanza hakuna suala la uwakilishi hadi ridhaa hiyo ipatikane kwanza soma hukumu ya mahakama kuu ya Kenya kwenye suala la kupinga mkutano wa Boma......

Nashkuru for information ngoja niitafute hiyo judgement nisome reasoning yao..
Although nafahamu unatambua hukumu ya mahakama kenya sio binding kwetu na wala haiform precedent kwa mujibu wa kanuni za precedent katika common law countries...ila it may be persuasive..
 
Mwanzo mzuri bt naingiwa na hofu kidogo kuhusu hiyo kesi, iv haki itapatikana kweli kwenye hizi mahakama zetu? labda ipelekwe ICC. Manake hiyo sheria inakiuka haki za binadamu.

unakumbuka pia matokeo ya kesi ya mgombea binafsi? Hii mihimili mitatu ya Tanzania bana... We acha tu!
 
Mbona ule muswada wa katiba uko poa tu?! Hao TLS wana lao jambo! Au kwa vile Pengo na maaskofi wamelalamika? Au wanataka kuwapa shavu la kuandamana magwanda? Haya sie yetu macho.
 
Juzi nilipendekeza hapa kuwa sheria ya mchakato wa uundwaji wa katiba mpya inaweza kuwa challenged mahakama kuu kwa kukinzana na katiba.

Leo mwananchi limeripoti na kumnukuu rais wa Tanganyika Law Society ndugu Stolla kuwa maandalizi yamekamilika kufungua kesi hiyo mahakama kuu.

Sheria hiyo inakinzana na ibara ya 18 ya uhuru wa maoni kwa kucriminalize shughuli yoyote ya kuelimisha kuhusu katiba nje ya sheria hiyo.

Sababu nyingine ni procedural irregularity kwa sababu kama mnavokumbuka ni kwamba muswada wa sheria hiyo ulikuwa withdrawn na ulivorudishwa ukapitishwa kana kwamba umesomwa mara ya tatu.
Tusubiri lakini binafsi naona dalili ni njema ingawaje ground ya pili ndio ina nguvu kwa sasa nadhani kwa sababu zifuatazo.

Hiyo ground ya kwanza mahakama inaweza kudeclare hicho kipengele void tothe extent of inconcistence na katiba na sheria yenyewe kama yenyewe ikaendelea.

Lakini hiyo ground ya pili ikibainika na mahakama kweli procedure zilikiukwa basi sheria nzima inaweza kubatilishwa yani kuwa nullified na hivyo tukaanza mwanzo..which is what i pray for.

Yaani hapo kwenye red kunachanganya! Hii katiba si tunasema ni MBOVU ndio maana tuanataka mpya? naomba nifahamishwe ni wakati gani ni mbovu na ni wakati gani ni nzuri! halafu

kwa mwenendo wa kesi zetu hadi hukumu inatoka ni 2014 na nususu so you can kiss goodbye the new katiba before 2015 elections! au katumwa huyu jamaa! in life there were three unpredictable creatures , now they are four thanks to bongolanders!
  1. a crab - you can never the direction it will go ukii kurupusha
  2. a diplomat - she/he never says no!
  3. a woman - she says no when she means yes and vice versa
  4. mbongo (this is a new one!) - he never knows what he/she wants and when!
 
Unapaswa kutambua ibara ya 18 imecodify tu uhuru wa mawazo..hiyo ni haki ya binadamu na ni inviolable regardless katiba ni nzuri ama mbaya..
Kumbuka human rights are not gifts from the state bali ni entitlement yetu by virtue of our being humans!
Katiba ya sasa ina mazuri na mapungufu yake..hata iyo ibara ya 18 kwa mujibu wa katiba yetu uhuru huo sio absolute unaweza kunyang‘anywa kwa maslahi ya umma(public interest) etc;hizi tunaita clawback clauses ndani ya katiba. Cha ajabu bado ni serikali ndo ina discretion ya kuamua maslahi ya umma ni yapi...

Kwa lugha nyingine ndani ya katiba yetu unapewa haki upande mmoja lakn unaweza kunyang‘anywa kwa upande mwingine,tena arbitrarily. So huwezi kuitetea katiba yetu.

Tunachofanya ni kutumia loopholes zilizopo sasa in our favour ili katiba mpya tunayoidai isiwe mbaya(na mapungufu) kama ya sasa au zaidi.
 
Back
Top Bottom