Kibanda
Member
- Aug 27, 2009
- 87
- 45
Makala hii ilichapwa katika Tanzania Daima Jumatano wiki hii.
Kikaango cha JK kitampiku Mkapa (1)
Na Absalom Kibanda
WIKI iliyopita nilihitimisha mjadala uliokuwa ukidurusu historia ya ushabiki wa kisiasa katika nchi hii ambao kwa mtazamo wangu nilieleza kwamba ndiyo uliolifikisha taifa katika ukomo wa kushindwa kufikiri na kuchukua maamuzi yanayofaa.
Mwisho wa mjadala huo nilieleza namna hulka za kishabiki katika taifa hili zilivyotufikisha Watanzania katika hatua ambayo sote tulijikuta hatimaye tukimfikisha Ikulu, mwanasiasa ambaye aghalab sifa na uwezo alionao kama kiongozi mkuu wa nchi vinaendelea kuibua maswali mengi kuliko majibu.
Aidha, katika mjadala huo ambao ulinichukua kuukamilisha kwa muhtasari tu katika kipindi cha wiki mbili, niliweza kuyaeleza pia matokeo ya ushabiki huo ambao kwa bahati mbaya ulifikia hatua hata ya kumtisha na kumyumbisha rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa ambaye ndiye aliyekuwa na turufu ya mwisho kabla ya kuwaaachia wananchi waamue nini cha kufanya.
Ninapogeuka nyuma leo hii na kuangalia mtitiriko wa matukio ya kihistoria ambayo hatimaye yalimfikisha Rais Jakaya Kikwete Ikulu, mwaka 2005, nabaini jambo moja kwamba, taifa lilikuwa likihitaji kuwa na kiongozi mwenye mamlaka ya ushawishi kama aliyokuwa nayo Baba wa Taifa mwaka 1995 ili kuzuia yale yaliyotokea wakati huo yasitokee.
Katika kusema hili simaanishi jambo jingine lolote, zaidi ya kueleza tu kwamba kama ilivyotokea mwaka 1995 wakati Mwalimu Julius Nyerere alivyofanikiwa kumzuia Augustine Mrema kuingia Ikulu ndivyo alivyopaswa kufanya Mkapa, miaka 10 baadaye.
Kwa maneno rahisi kabisa, alichopaswa kufanya Mkapa kilikuwa ni kuthubutu kuchukua maamuzi magumu ambayo hatimaye yangekiwezesha CCM kudhibiti kishindo cha Kikwete na jeshi lake la mtandao kuingia Ikulu kwa njia ya mlango wa nyuma.
Miaka mitano tangu Mkapa afanye kosa hilo, wadadisi wa mambo wameendelea kukuna vichwa vyao wakijiuliza ni kitu gani hasa kilimfika kiongozi huyo ambaye wengi walikuwa wakimuona kuwa mtu madhubuti hata afikie hatua ya kuyumba na kuongoza vikao katika mwelekeo ambao ulionyesha bayana kumbeba Kikwete na kuwaumiza wengine.
Pamoja na kukosekana kwa jibu halisi katika swali hilo hasa kutokana na ukweli kwamba, Mkapa mwenyewe hajapata kueleza kwa undani juu ya kile kilichomsibu hata akajikuta akiyumba na kupoteza mwelekeo, ni ukweli kwamba matokeo ya kosa hili ndiyo ambayo leo hii mbali ya kulitafuna taifa yanamtafuna hata yeye mwenyewe.
Ninayo imani ya dhati kwamba, katika hali ya uwazi na ukweli, iwapo Mkapa atapata fursa ya kusema kile kilicho moyoni mwake leo, si ajabu (nasisitiza si ajabu) kiongozi huyo mstaafu anaweza akaeleza majuto dhidi ya maamuzi aliyosimamia ambayo mbali ya kumgharimu yeye binafsi sasa yanaligharimu taifa.
Ni dhahiri kwamba, leo hii Mkapa huwa anaugulia maumivu makali kila anapogeuka nyuma na kuangalia namna Watanzania kwa makumi na mamia wanavyomsimanga, wakimhusisha na tuhuma za ufisadi, zake binafsi au zile zinazowagusa mawaziri na watendaji wakuu wa zama zake.
Hata hivyo, anachopaswa kutambua Mkapa ni kwamba, kuugulia maumivu kwake chinichini hakupaswi kuishia hapo, bali kama tulivyopata kuwaasa wengine kabla yake, anawajibika kujipanga kwa ajili ya kuomba toba ya wazi kwa wananchi kwa namna alivyoliingiza taifa matatizo.
Ili kufanikisha hili, Mkapa anapaswa kufanya kile kilichopaswa kufranywa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere wakati alipokuwa amestaafu ambaye mara kadhaa alipata kuitisha mikutano na waandishi wa habari na kukiri kufanya makosa mbalimbali wakati akiwa madarakani.
Naamini Mkapa ambaye umakini wake si wa kutiliwa shaka katika masuala ya habari, anakumbuka namna Mwalimu alivyopata kueleza kusikitishwa na tabia ya Watanzania kuyaangalia mabaya tu yaliyopata kufanywa na serikali yake na kuyaacha mazuri mengi.
Katika kauli zake za namna hiyo, mara kadhaa, Mwalimu alipata kunukuliwa akiomba radhi, akifanya hivyo hadharani na wakati mwingine kwa kutoa machozi kabisa kama alivyofanywa wakati alipomuomba radhi Mzee Rashidi Kawawa kwa kubeba lawama nyingi kwa makosa ambayo wakati mwingine aliyafanya yeye.
Si Mwalimu tu, Mkapa anapaswa kujifunza kutoka kwa Papa Benedict na mtangulizi wake ambao wamepata kuomba radhi hadharani kwa makosa ambayo ama yalifanywa na kanisa au makasisi wake katika maeneo mbalimbali duniani.
Katika hili, Mkapa anapaswa kukiri hadharani kwa njia ya kuzungumza na wanahabari kama alivyokuwa akifanya Mwalimu na kueleza namna alivyoteleza katika kuvisimamia vyema vikao vya uteuzi ndani ya CCM ambavyo hatimaye chini ya uenyekiti wake, vilimpa fursa Kikwete kuteuliwa mwaka 2005.
Katika kuomba radhi kwa kosa hilo, Mkapa anapaswa kuwaeleza wananchi hadharani, kwamba kosa lake hilo ambalo alililifanya kwa kujua au kutokujua akiamini lingemsaidia kujihami akiwa mstaafu, leo hii linamgharimu kwa kiwango ambacho taswira yake katika jamii imechafuka.
Pamoja na kukiri kosa hilo, Mkapa ambaye kimsingi anapaswa kufanya hivyo kabla ya kuanza kwa kazi ya uteuzi ndani ya CCM, atatakiwa kueleza na kuyakiri hadharani baadhi ya makosa ya kimaamuzi na yale ya kimaadili ambayo aliyafanya yeye binafsi, mawaziri wake au serikali aliyokuwa akiiongoza kwa namna ile ile alivyopata kufanya Mwalimu Nyerere miaka ya mwanzo ya 1990.
Baada ya kuomba radhi kwa makosa hayo, Mkapa atapaswa kuweka sawasawa rekodi yake kwa kueleza namna jina lake linavyotajwa na kuhusishwa kwa makosa na umiliki wa mgodi wa makaa ya mawe Kiwira na namna ambavyo hakupata kuyatumia madaraka yake kufanya biashara au kujihusisha na rushwa au matendo ya ufisadi kwa namna yoyote ile katika kipindi chote cha miaka 10 cha utawala wake.
Ninao uhakika kwamba, iwapo Mkapa atauzingatia ushauri huu, kwanza atakuwa ametoa mchango muhimu kabisa wa tiba ya bongo za Watanzania ambao tumelishwa ujinga na uzushi mwingi kuhusu kiongozi huyo na serikali yake hata katika mambo ambayo wakati mwingine lawama zinapaswa kwenda kwingine na si kwake.
Lakini pia kwa kufanya hivyo, Mkapa atawapa fursa wana CCM wenzake na Watanzania kwa ujumla kupata fursa ya kutulia na kupima sawasawa mwenendo wa kikazi na kimaadili wa serikali ya Kikwete ambayo naamini, nyuma ya pazia imebeba uchafu mwingi ambao Watanzania wengi hatuujui.
Mwisho kwa kufanya hivyo, Mkapa atakuwa ameanza kujenga msingi imara kwa wananchi walio wengi katika kuwajua viongozi wao na hivyo kuwapa fursa ya kushiriki ipasavyo katika uteuzi na hatimaye uchaguzi wa viongozi wakati wa uchaguzi mkuu ujao.
Lakini kubwa katika yote ni kwamba, baada ya kufanya hivyo, kama ilivyo kuwa kwa Mwalimu Nyerere, basi na Mkapa naye ataweza kuanza upya kuwaeleza wananchi kwa kufanya ulinganifu na sasa, namna serikali yake ya awamu ya tatu ilivyofanya kazi kubwa katika kuwajengea wananchi wake misingi imara ya maendeleo kiuchumi na kijamii.
Ni wazi kwamba, leo hii kabla ya toba hiyo, Mkapa anapata wakati mgumu kuitetea rekodi ya kipekee iliyosheheni nidhamu ya hali ya juu ya utendaji katika serikali yake ambayo ilikuwa na matokeo mema kiuchumi.
Leo hii kabla hajafanya toba hiyo, ni wazi kwamba, Mkapa anapata shida hata kutetea rekodi yake kipekee ya miaka 10 ya kujenga upya uchumi ulioparanganyika kwa kuudhibiti mfumuko wa bei kutoka kiwango cha asilimia 27.1 mwaka 1995 hadi asilimia 4.2 mwaka 2004.
Ni katika misingi hiyo hiyo ya kuandamwa na kivuli cha dhambi ya maamuzi ya hovyo ndicho kinachomfanya Mkapa leo hii akwame kujivunia kupandisha pato la taifa imeongezeka kutoka asilimia 3.6 mwaka 1995 hadi 6.7 mwaka 2004.
Kama hiyo haitoshi, jeuri ya Mkapa kukataa kujiona mnyonge kwa kutuomba radhi inamnyima fursa pia ya kutembea kifua mbele kwamba, zama zake aliweza kuongeza pato la serikali kutoka wastani wa sh.37.4 bilioni kwa mwezi katika mwaka wa fedha wa 1995/96 hadi kufikia wastani wa zaidi ya sh.140 bilioni kwa mwezi katika mwaka wa fedha wa 2004/05.
Matokeo ya jeuri hii ya Mkapa kudharau vyombo vya habari na kukataa kuomba radhi ndiyo ambayo inamfanya Mkapa kujitokeza hadharani na kutetea sera na sheria ya madini ambayo pamoja na mapungufu yake ilichangia ukuaji wa rekodi kiuchumi.
Ni wazi kwamba kiburi hiki cha Mkapa cha kutotaka kuonekana mnyonge, au mtu mwenye makosa ndicho ambacho kinasababisha ashindwe hata kujitokeza na kutamba kwamba katika kipindi cha miaka 10 cha utawala wake, zaidi ya dola za Marekani 1.4 bilioni kiliwekezwa katika sekta ya madini na kubabisha migodi mikubwa sita ya dhahabu kuanzishwa.
Angeachana na jeuri yake hii ya kibabe, Mkapa angeweza leo kuitisha mkutano wa waandishi wa habari na akamjibu kwa kishindo Waziri wa Kilimo na Chakula Stephen Wasira ambaye majuzi aliweza kusimama kwa mbwembwe na kuinyoshea kidole serikali kuhusu sekta ya madini.
Katika hili Mkapa angeweza kumkumbusha kirahisi Wasira na wanasiasa wengine kwamba pamoja na kuinyoshea serikali kidole kwa kuruhusu madini yaibwe na wawekezaji wa nje, sera zake ziliiwezesha Tanzania kuwa ni nchi ya tatu barani Afrika kwa wingi wa dhahabu inayozalishwa, baada ya Afrika Kusini na Ghana.
Katika hili, Mkapa angeweza kumkumbusha Wasira kwamba kabla ya kuruhusu uchimbaji mkubwa, mwaka 1995 Tanzania ilizalisha tani tatu tu za dhahabu na miaka 10 baadaye wakati akiondoka madarakani kiwango rasmi kilipanda hadi kufikia tani 50, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya mara 16.
Kwa hakika katika hilo, majibu hayo ya Mkapa kwa Wasira ambaye hakuna shaka kwamba mawazo aliyonayo ndiyo pia anayo Kikwete (rejea sera ya uwajibikaji wa pamoja serikalini) yasingeishia hapo bali yangekwenda mbele zaidi kwa kueleza kuwa mauzo ya dhahabu nje ya nchi katika kipindi cha kati ya mwaka 1997 na 2004 yaliongezeka kutoka dola za Marekani milioni 2 hadi kufikia dola 593.2 milioni kiwango ambacho ni ongezeko la karibu mara 300.
Ni wazi kwamba majibu hayo ya Mkapa kwa mara ya kwanza yangekuwa turufu ya kwanza ya kupima utendaji wa zama ya serikali yake dhidi ya huu wa serikali ya Kikwete uliojaa blah blah, majungu, fitina, uzushi, ushabiki, visasi na mambo yanayofanana na hayo. Tutaendelea na mada hii wiki ijayo.