Kesho vipi ni maulidi au

Taarifa rasmi iliyotolewa na BAKWATA ni kuwa siku kuu ya maulid iliswaliwa Jumatano tarehe 16/02/11 mgeni rasmi ni mzee wetu rais mstaafu A.H.MWINYI.
 
tar 15 au 16? mimi nakula good time sasa hivi, kwa hiyo naongezea na kesho?
 
Maulid ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mtume mtukufu Muhammad s.a.w. Dunia nzima waislamu huiadhimisha siku hii ndio maana na hapa nchini hakutokuwa na kazi KESHO.
 



Maulidi ni nini?
Mawlid ni neno la kiarabu lilitokana na kitendo cha kuzawa kwa kidhungu (to give birth).
Bila shaka ulitaka kukusudia kutaja MAWLIDUN NABAWIY.
KUZAWA KWA MTUME MUHAMMAD S.A.W(PEACE BE UPON HIM).
PIA NI VIZURI NKAWAELEZEA WANAJAMVI JAPO KWA UCHACHE.
MAANA KUNA IKHTILAFU JUU YA SHEREHE HIZI NAMNA YA USHEREHEKEWAJI WAKE.
PIA KWANINI TUNA MKUMBUKA MTUME WETU STANDARD OF LEADING MUHAMMAD S.A.W.
 
Kabla ya kuzawa mtume Muhammad S.A.W babu yake mzaa baba yake alieitwa Abdul-mutwalib ..huyu mzee aliweka nadhiri kua iwapo atapojaaliwa kuwapata watoto wa kiume kumi atamchinja mtoto mmoja.
 
Kabla ya kuzawa mtume Muhammad S.A.W babu yake mzaa baba yake alieitwa Abdul-mutwalib ..huyu mzee aliweka nadhiri kua iwapo atapojaaliwa kuwapata watoto wa kiume kumi atamchinja mtoto mmoja.

IS it true? MMweye data zaidi atujuze jama?
 
Alipozaliwa watoto kumi ikabidi ipigwe kur'a yupi achinjwe?
Ikaangukia kwa Abdullah ambae ndie baba wa Mtume Muhammad s.a.w mzee akasita kutekeleza ahadi ikabidi irudiwe tena. Kwa kawaida zao ilikua inaporudiwa lazima utoe fidau/fidia ngamia kumi. Hivyo ilirudiwa ikamwangukia tena baba wa mtume s.a.w ....marq kumi ikawa zimetolewa ngamia mia moja. Na hapo ikawa mwisho wa utekelezwaji wa ahadi.
Kipi kilicho kua kina msitisha kutekeleza ahadi yake?
Ni uweza wake Allah s.w kwa kua mgongoni mwa baba wa mtume kuna kizazi kitukufu.
 
Mtume maisha yake ni mafunzo tosha katika muongozo wa
uadilifu kwenye maisha ya dunia.
-Jina lake ni Muhammad.
-Baba yake ni Abdullah.
-Mama yake ni Aamina.
-Aliemnyonyesha ni Halima.
-Mlezi wake(yaya) ni Barka(ummu ayman).
-Aliempokea wakt anazaliwa ni Shufa'a.
-Thuwayba alikua mjakazi wa baba'ke mdogo wa mtume (Abuu-lahab) siku aliyozawa mtume s.a.w alipopokea taarifa za uzawa wa mtoto wa ndugu yake hapo hapo alimwachia huru. Na ndie aliekwenda kunyonyesha tone la maziwa la kwanza kuingia kwa mtume.
Haya ni machache lakini yana hikma zaidi.
 
Mawlid is not permitted in the Koran. There is no any ayat that Allah is saying/commanding/authorizing people "muham-madans" to celebrate the birthday of Marehemu Muham-mad.

The Prophet said, "He who innovates something in this matter of ours that is not of it will have it rejected." He also said, "Beware of innovations, for every innovation (kul bida`) is misguidance."


The word every (kul) is a term of generalization, including all types of innovations, with no exception, and that therefore, celebrating Mawlid is misguidance.
 
Back
Top Bottom