Kesho ni mapumziko!!?

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,466
9,028
wanajamvi salaam sana.

Nipo najiuliza hapa kuwa na kesho ni siku ya mapumziko kwa nchi hii iliyo ya pili kutoka mwisho kwa umasikini (Sijui ni mapumziku ya nini lakini).
Ukiangalia hali ya kipesa kwa wengi wetu ni mbaya sana, hii sio kwa sababu ya sikukuu zilizoisha bali ni hali ya uchumi kwa ujumla wake.

Hivi wanajamvi, ni siku ngapi za mwaka ambazo binadamu inapasa afanye kazi ili aendelee?

Naleta swali hili maana sasa tunakuwa ni watu wa kupumzika tu hata zile siku ambazo ingetupasa kufanya kazi kwa muda wa ziada kwa kuwaenzi watu tunaowatukuza badala ya kupumzika, maana wenyewe wakati wa uhai wao walipenda kazi na kuwajibika!

Sijui mapumziko yatakuwaje na hii mifuko mitupu!!!!

Nawasilisha
 
Mtu aliyechangia hii nchi kurudi nyuma kimaendeleo ni mzee Ali Hassan Mwinyi katika utawala wake, ilikua kama sikukuu inaangukia jumamosi basi Watanzania tutapunzika mpaka jumanne! Ndio maana hata alizabwa vibao.
 
kwa hakika hii nchi yetu vipaumbele vyake ndio kama vilivyo, mambo ya ufisadi, kutowajibika, uzembe nk nio vinakuwa na umuhimu maana nasikia nchi za wenzetu wanajitahidi sana kufanya kazi kwa siku nyingi iwezekanavyo kwa mwaka.
Nasikia eti kwa Japan mpaka serikali inaiingilia kati kuwapa watu likizo.
Ila sisi huku kwetu kesho tunafanya tu kazi hivyo vya sikukuu hauvijui
 
Mtu aliyechangia hii nchi kurudi nyuma kimaendeleo ni mzee Ali Hassan Mwinyi katika utawala wake, ilikua kama sikukuu inaangukia jumamosi basi Watanzania tutapunzika mpaka jumanne! Ndio maana hata alizabwa vibao.

Inategemea Mwinyi kipindi chake aliweka sikukuu nyingi ili kuinua vipato vya sekta ya starehe na kuongeza kodi zitokanazo na sekta hiyo.Uliza kipindi cha Mwinyi mabaa yalivyokuwa yakifurika watu siku hizo,madreva taxi walivyokuwa wakikodiwa hakuna dereva taxi atakuambia kipindi kile sikukuu zile alikuwa akivuna pesa hadi basi nenda kaulize wenye mahoteli hali ilikuwaje katika siku zile enzi za mwinyi kwenye hizo sikukuu walifanya biashara hasa.

Serikali kipindi kile sehemu kubwa ya kodi ilitokana na pombe sasa kama asingewapa muda wa kulewa wa kutosha kodi angetoa wapi.Njia ya kuwachomoa pesa zao ilikuwa ni kutoa siku nyingi za mapumziko wakatumie sana pesa zao sekta ya starehe.Na wengi waliokuwa sekta walifaidi hasa.Ukiacha watu washinde ofisini au kiwandani wazalishe masaa 24 bila kupumzika mwaka mzima kuna sekta utaziua kabisa ambazo ni mlango mkubwa wa kuingizia mapato serikali.Kupumzika si kupumzika tu ni kuendelea kuiingizia serikali mapato lakini ukiona watu wakipumzika hakuna badiliko la maana katika ongezeko la mapato ya serikali hata siku kuu unazifuta watu heri tu wabaki kazini kama ilivyo kwa Japan.Japan ni wabahili mno kama watani wangu wapare hata ukiwapa siku ya mapumziko hawatumii sana sekta ya starehe serikali ya japan ikaona ujinga dawa ni kufuta mapumziko mengi acha tu wafanye kazi wajaze mapesa yao kwenye savings na sasa limezuka tatizo la stress kwa wajapan wengi ndio serikali inahaha kuhamasisha watu waende likizo na kuajiri wataalamu wa saikolojia kuwasaidia wajapan wapende mapumziko.

Mwinyi alijua anachofanya tusimlaumu tu bure.Kutopumzika haina maana you are better.Unaweza kuwa hovyo kabisa na hoi kiuchumi na kiafya.

kingadvisor@yahoo.com
 
Acha mapumziko yaje kwa kweli wiki hii karibu yote nimepiga kazi overtime !
Nasubiri mapumziko kwa hamu kubwa ili nkusanye nguvu upya.
Nawaakia watanzania wote mapumziko mema hiyo kesho.
 
mimi sisherehekei si kwa sbb sina kitu ila kwa kuwa mimi ni Mtanganyika keshokutwa tutasherehekea siku ya uhuru wa uganda halafu kenya nk huu upuzi huu kwanza kesho naenda shamba hata kama mvua hamna
 
Mapumziko kwa wafanyakazi wa serikali sisi wafanyabiashara kazi kama kawa..
 
kama ni kweli hapokwenye red basi ilikuwa strategy nzuri lakini mkuu king, inasemekana wakati wa Mwinyi kodi haikukusanywa na watu walikuwa wanajipangia wenyewe ni kiasi gani walipe au wasilipe! Ndivyo inavyosemekana hivyo au unayo mawazo tofauti?
Inategemea Mwinyi kipindi chake aliweka sikukuu nyingi ili kuinua vipato vya sekta ya starehe na kuongeza kodi zitokanazo na sekta hiyo.Uliza kipindi cha Mwinyi mabaa yalivyokuwa yakifurika watu siku hizo,madreva taxi walivyokuwa wakikodiwa hakuna dereva taxi atakuambia kipindi kile sikukuu zile alikuwa akivuna pesa hadi basi nenda kaulize wenye mahoteli hali ilikuwaje katika siku zile enzi za mwinyi kwenye hizo sikukuu walifanya biashara hasa.
......
.....
Mwinyi alijua anachofanya tusimlaumu tu bure.Kutopumzika haina maana you are better.Unaweza kuwa hovyo kabisa na hoi kiuchumi na kiafya.

kingadvisor@yahoo.com
 
Back
Top Bottom