kesho asubuhi vijana wanajipanga kutekeleza agizo la mhe magofuli(kupiga mbizi)

kimboka one

JF-Expert Member
Jan 23, 2010
734
85
nipo maeneo ya ferry kigamboni maarufu kwa bi tulule opposite na kwa watoto yatima.vijana wameniita kutaka ushauri wa kisheria.wamepanga kesho wavuka kwa mbizi kwa pamoja kunusuru 200 zako.kimsingi nimewaeleza ni kosa lakini wamekomaa watatekeleza azimio lao kesho kwani wakifungwa ni sehemu ya kupata mahitaji yao bure wakiwa mahabusu
 
wanadhani wanamkomoa nani? naona wana-test sumu kwa kuilamba
 
Mungu akulaani kama Balaamu alivyosema, mimi na familia yangu tunakulani kwa uhovyo wako, hata mie kesho ntafika magogoni saa kumi na mbili asubuhi kuwaunga mkono wapiganaji wetu. Mungu yupo na atatulinda na mabaya yote.
wanadhani wanamkomoa nani? naona wana-test sumu kwa kuilamba
 
wacha wapige mbizi wanaelezea hisia zao sasa kama hawana hiyo 200 wafanye nini
 
nipo maeneo ya ferry kigamboni maarufu kwa bi tulule opposite na kwa watoto yatima.vijana wameniita kutaka ushauri wa kisheria.wamepanga kesho wavuka kwa mbizi kwa pamoja kunusuru 200 zako.kimsingi nimewaeleza ni kosa lakini wamekomaa watatekeleza azimio lao kesho kwani wakifungwa ni sehemu ya kupata mahitaji yao bure wakiwa mahabusu
......ni vizuri kama walimwelewa mh. Pombe, waachane na wabunge wao wa vijiweni wanaotafuta cheap popularity kupitia Magufuli ili wachaguliwe tena, hivi hii nchi tutachagua wabunge wanaojua kusoma na kuandika bila kufikiri hadi lini???????
 
Pengine wanafanya mazoezi maana kesho ni siku ya mapumziko.
 
wacha wapige mbizi wanaelezea hisia zao sasa kama hawana hiyo 200 wafanye nini

Unafiki mtupu, ina maana hiyo sh100 ndo inawafanya wapige mbizi? Hawa watu hawapandi daladala? Hawanywi hata maji? Hawanunui kondom? Pumbavu sana, halafu kwani eneo hilo la kivukoni hakuna papa wanisaidie kuwafundisha adabu hawa wanafiki?.
 
Mkuu wameambiwa kama hawana 200 wapige mbizi sasa wafanyeje
 
Swali la msingi la kujiuza ni "je kweli hawa watu watapiga mbizi kwa sababu hawana 200 au ndo unafiki na uzandiki?
 
Mungu akulaani kama Balaamu alivyosema, mimi na familia yangu tunakulani kwa uhovyo wako, hata mie kesho ntafika magogoni saa kumi na mbili asubuhi kuwaunga mkono wapiganaji wetu. Mungu yupo na atatulinda na mabaya yote.

maskini mnatabu sana
 
Atkaye zidiwa na maji asiombe msaada ruksa kufa. Wamechagua unafiki wacha waendelee nao. Kumbuka survival is for the fittest huna 200/ piga mbizi or else hamia kijijini.
 
YOU ARE A GREAT THINKER.Na hili ndio tatizo letu la msingi,hatuna viongozi wenye nia ya kweli ya kutupeleka NCHI YA AHADI.kweli a serious mp anaweza kupoteza muda wake kutetea ujinga wa aina hii kweli?they should think twice.
 
hawataki kulipa 200, kwani wakishuka kutoka kwenye kivuko kuna usafiri wanaolipa kwa nauli ya mia? au wanamwonea magufuli tu? kama vp kura zao hatuzitaki 2015, wafanyakazi walileta mashauzi hivyo hivyo 2010 lkn tukashinda.
 
Inaonyesha jinsi ulivyo kilaza,private sectors are profit motivated,kwa hiyo usilinganishe hela ya kulipa daladala na kupanda kivuko ambacho kinaendeshwa na serikal chin ya wizara ya maguful,hiyo ni service oriented,sh 100 ilikuwa inatosha kwa ajil ya kukiendesha hicho kivuko,tena report ambayo imechakachuliwa inadai kuwa kwa siku takriban milion tisa zlikuwa znakusanywa,mi nahc wana ajenda nyngne ikiwa ni makusanyo hata ya kulipa maden ya wafanyakaz
 
mkuu waandalie media tuone watu wakionyesha hisia zao.lazima baadhi ya watu wajitoe muhanga kwa manufaa ya wengi!
 
tatizo letu vijana siku hizi tumekuwa affected na mob psychology. Wanalo fanya halina maana mbona wanashindwa kupigania vitu vya msingi vinavyo wafanya wao wakose hiyo 200.
Mbona wameshindwa kuchukua hatua dhidi ya mfumuko wa bei za vyakula ambayo effect yake ni zaidi ya hiyo mia, mafta na kila kitu.
Hili jambo liko kisiasa zaidi ndiyo siasa ya tanzania ambayo kila mtu can do anything to earn piblic popularity am sure wanatumiwa bila kujua kama wanatumiwa.
 
hawataki kulipa 200, kwani wakishuka kutoka kwenye kivuko kuna usafiri wanaolipa kwa nauli ya mia? au wanamwonea magufuli tu? kama vp kura zao hatuzitaki 2015, wafanyakazi walileta mashauzi hivyo hivyo 2010 lkn tukashinda.

enyi wajinga! Mpaka lini mtapenda kuwa wajinga?
 
Acheni watu wapige mbizi kuonyesha hisia zao kupinga kitu wasichokubaliana nacho. Ni sawa tu na mantiki ya maandamano ya amani ambayo sasa tumeyazoea. Mbona kuna mahali tumesikia watu wamewahi kuandamana wakiwa uchi wa mnyama? Na wao je tutawaitaje? Wajinga?
 
Back
Top Bottom