Wabogojo
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 354
- 87
Wanajamvi, kesho ni siku ya maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na ninadhani maadhimisho yaha yatafanyika hapa hapa BANDARI SALAMA na Mkuu wetu wa nchi kama ilivyo ada anatazamiwa kuwa ndiye atakaye kuwa MGENI RASMI. Ninatabiri kuwa hapo kesho Mkulu wetu atatoka na kile ambacho watz hatutaamini na kuachwa vinywa wazi huku wengi wakifurahi na baadhi kusononeka.
Je wewe unategemea ataongea nini katika sherehe hizi wakati wananchi tumeachwa solemba kwenye ombwe la ufisadi uliokithiri wa vilanja wetu, CCM ikilegalega wakati CDM ikipaa kwa kasi ya Chopa, wengine wakiupinga Muungano huu kwa nguvu zao zote na lingine kubwa zaidi ni hili la mchakato wa kupata KATIBA MPYA ya JMT huku BABA akikataza watoto wake kuujadili muungano kwenye huo mchakato.
Nawasilisha ................