KERO za Nyumba za Kupanga, Mali za Mpangaji Zatupwa Nje na Nyumba Kugeuzwa Kanisa

Babuji

Senior Member
Nov 27, 2008
197
3
Kero na karaha za nyumba za kupanga zimejidhirisha huko maeneo ya Mikocheni B baada ya mama mwenye nyumba kuvitoa vitu vyote vya mpangaji wake ambaye alikuwa safarini na kisha kuigeuza nyumba aliyokuwa amempangisha kuwa kanisa.

642.jpg


Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Rose ambaye alikuwa amepanga katika nyumba namba 104 iliyopo katika mtaa wa Nyumbu Mikocheni B, amejikuta katika wakati mgumu baada ya mwenye nyumba wake kumtolea vitu vyake vya thamani nje huku yeye akiwa safarini hajui sakata hilo.

651.jpg


Rose alimuanga mama mwenye nyumba yake aliyefahamika kwa jina la Joyce Mbunga kuwa anakwenda Mbeya kwa ajili ya matibabu ya mwanae anayesoma mkoani Mbeya ambaye alikuwa ni mgonjwa.

Wakati mama huyo akiwa bado safarini mama mwenye nyumba alivitoa vitu vyote vya mpangaji wake na kuviweka nje na kisha kuipangisha nyumba yake kwa watu walioigeuza kuwa kanisa ambao inasemekana si raia wa Tanzania.

Nyumba hiyo iligeuzwa kanisa linaloitwa KANISA LA KIMATAIFA LA LIGHT HOUSE CHAPEL likiwa na ujumbe unaosema THE MEGA CHURCH ( KANISA KUBWA).

646.jpg


Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Rose ambaye alikuwa amepanga katika nyumba namba 104 iliyopo katika mtaa wa Nyumbu Mikocheni B, amejikuta katika wakati mgumu baada ya mwenye nyumba wake kumtolea vitu vyake vya thamani nje huku yeye akiwa safarini hajui sakata hilo.

650.jpg


647.jpg


645.jpg


Rose baada ya kurudi na kukuta vitu vyake vyote vikiwa nje huku vingine wezi wakiwa wameishajichukulia na nyumba hiyo imeishageuzwa kuwa kanisa alisikitika sana na kutoa taarifa kwa mjumbe wa nyumba 10 ambaye alikiri kitendo cha mama mwenye nyumba si cha kiungwana.

Kesi hiyo ilifika kituo cha polisi Oysterbay na mama mwenye nyumba hivi sasa ameswekwa ndani.

Habari kamili na picha zaidi http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2520862&&Cat=1
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom