Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

katika kumbukumbu zangu mimi Harusi mtu ulikuwa unafanya kwa uwezo wako... unaita marafiki zako na ndugu mnasherekea hicho kilichopo.

Sasa mtu anakuletea Kadi tena ina kiwango.... na Watu hawakuchangii sababu wanakupenda ni kama wanakukopesha kwamba na wao siku yao ikifika na wewe utachanga...

Michango Inafika mpaka mamilioni ya pesa.... watu wanakuja wanakunywa na kula.. wewe na mwenza wako mnaenda kuanza maisha (wengine hata nyumba hamna) na deni la watu kama mia moja waliokuchangia ambao na wewe inabidi uwachangie....

HIVI NI MIMI TU NINAYEONA KUWA HUU NI UPUUZI NA UJINGA... AU KUNA YEYOTE ANAYENIUNGA MKONO.....

Naunga mkono hoja 100%. Wengi ukiwauliza watakwambia hawapendi hako ka-utamaduni lakini hawana uwezo wa ku-resist kwakuwa jamii ndipo ilipofikia. Kama unavyosema, mtu unajikuta una madeni yasiyo rasmi lukuki, njia nzuri ya kuyakwepa hayo "madeni" ya kuchangia harusi inabidi na wewe ujiepusha kwa namna yoyote kuchangisha watu. Mie nina mpango nikifunga ndoa nitatenga kana mil. 2 hivi, na sitachangisha mtu, watakunywa chai na snacks na sherehe itaishia hapo.
 
bora sie wazaramo........bibi flani flani umekubali kuolewa na bwana flani flani kwa mahari ya shilingi elfu mbili imetangulizwa mia saba
deni elfu mia tatu? ndio nimekubali!....watu wanapiga vigelegele wanakunywa chai harusi imeisha!
 
Tatizo letu sisi Waafrika ni kuacha tamaduni zetu na kuiga. Kwa kawaida harusi ilikuwa ni jambo la familia na uwezo,nakumbuka vijijini utamkuta kijana akihangaika na ukimuuliza atakuambia tunatafuta pesa kaka anaoa. Siku ya siku watu watakaribishwa na kile kilichopo kitatumika, mtu ataozwa na ngoma zitachezwa baada ya hapo maisha mbele.

Kwa kuiga kutoka ugenini watu wakaanza kuchangishana, na sasa kila mwisho wa mwezi lazima kuna kadi tatu mezani, tena zina kiwango cha chini. Hivi kuna shida gani mtu akienda kwa askofu au sheikh na kuhalalishiwa ndoa yao kisha kuendelea na maisha.

Kukaja utamaduni wa kuchukua video wakati wa mazishi, ninauliza hivi ipo siku mtu ataweka mkanda wa video kuangalia mazishi ya ndugu yake yallivyokuwa? Labda tupo tofauti lakini mazishi au msiba si jambo la kukumbuka, cha kukumbuka ni maisha ya mpendwa aliyetutoka.

Sasa kumezuka utamaduni mwingine, sare za msiba, sijui hii inamaanisha nini, kwamba bila sare watu hawatawatambua wafiwa!

Kumekuja na utamaduni wa Birth day kuwa kama harusi, haa hili ni suala la kifamilia tu, sasa limekuzwa na kuwa kama harusi, tunaweza kupongezana bila kuchangishana au basi birth day iwe kwa kufanya mambo mazuri. Msaidie mwenye shida siku yako ya kuzaliwa kama shukurani, si kukodi kumbi na MC.

Ukiangalia mambo yote haya hayamsaidii mtu bali ni ufujaji wa fedha usio wa lazima. Kwanini watu wasipitishe kadi za kumsaidia mtoto wa mzee siboko au zomboko aliyeshindwa kulipa ada za shule!

Ni kwa kuiga utamaduni tunaona malumbano ya dini yanapamba moto, huko dini zilipoanzia wapo kimya. Kwanini tusilumbane kuhusu umasikini wa raia wetu wanaoishi chini ya dola moja kwa siku.

Kwa ufupi utamaduni wowote wa kijinga ni rahisi kuigwa Afrika kuliko utamaduni mzuri. Ni kwasababu ya elimu na umasikini wa kufikiri.

Tumeshindwa kuiga utamaduni wa kupanda dala dala kwa foleni tunaiga michango ya harusi. Tumeshindwa kuiga utamaduni wa kuweka uchafu ndani ya mapipa tunaiga sare za mazishi.

Tumeacha tamaduni zetu nzuri na kuiga sasa tunaiga hata visivyoigika.
 
@Nguruvi3
Kweli kabisa kaka hata mimi mwanzo nilidhani kwamba hii tumeiga toka nje lakini si kweli kabisa nje hawafanyi huu upuuzi..... nilikuwa UK rafiki yangu akanialika kwenye wedding yake ambayo alifanyia kwenye ukumbi wenye bar.... yeye alichofanya ni kwamba aliprovide some bites na drink chache... pale bar ilikuwa imefunguliwa ukitaka drinks zaidi na za bei mbaya ulikuwa unakwenda kununua mwenyewe.... sisemi na sisi tuanze kufanya hivyo, lakini utamaduni wetu ulikuwa mzuri tu unapika pilau pale nyumbani na kila mwenye miguu anakuja hata haya mambo ya kadi yalikuwa hayapo..... sasa harusi zimekuwa na viingilio..... hivi mtu umefiwa muda wa kushona sare na kuchapisha tshirt unatoka wapi????
 
nguruvi

Tunaiga kwa nani? Umesikia ulaya au hata uhindini wakichangishana kuhusu harusi? Ni sisi na tabia yetu ya kupenda umaarufu na sifa bila kuzifanyia kazi. Video, sare, limozin n.k. ni katika kuonyesha jamii kuwa wewe ni mtu kwa siku moja badala ya kuhenyea kwa muda mrefu mpaka hapo jamaa itakapokutambua.

Mtazamo kama huu ndiyo unaoutufanya tuchangamkie madigirii feki badala ya kuhangaikia. Hao unaosema tunawaiga wanatushangaa jinsi tunavyotapanya mafweza kwenye harusi.

Kwao ukialikwa pati, unategemewa ubebe kilevi chako na kama utakikuta utaambiwa ulipie! Hakuna biashara ya kata mti panda mti.

Amandla....
 
Last edited by a moderator:
katika kumbukumbu zangu mimi Harusi mtu ulikuwa unafanya kwa uwezo wako... unaita marafiki zako na ndugu mnasherekea hicho kilichopo.

Sasa mtu anakuletea Kadi tena ina kiwango.... na Watu hawakuchangii sababu wanakupenda ni kama wanakukopesha kwamba na wao siku yao ikifika na wewe utachanga...

Michango Inafika mpaka mamilioni ya pesa.... watu wanakuja wanakunywa na kula.. wewe na mwenza wako mnaenda kuanza maisha (wengine hata nyumba hamna) na deni la watu kama mia moja waliokuchangia ambao na wewe inabidi uwachangie....

HIVI NI MIMI TU NINAYEONA KUWA HUU NI UPUUZI NA UJINGA... AU KUNA YEYOTE ANAYENIUNGA MKONO.....

wengi hata nyumba hamna ni sahihi zaidi
 
Tunaiga kwa nani? Umesikia ulaya au hata uhindini wakichangishana kuhusu harusi? Ni sisi na tabia yetu ya kupenda umaarufu na sifa bila kuzifanyia kazi. Video, sare, limozin n.k. ni katika kuonyesha jamii kuwa wewe ni mtu kwa siku moja badala ya kuhenyea kwa muda mrefu mpaka hapo jamaa itakapokutambua. Mtazamo kama huu ndiyo unaoutufanya tuchangamkie madigirii feki badala ya kuhangaikia. Hao unaosema tunawaiga wanatushangaa jinsi tunavyotapanya mafweza kwenye harusi. Kwao ukialikwa pati, unategemewa ubebe kilevi chako na kama utakikuta utaambiwa ulipie! Hakuna biashara ya kata mti panda mti.

Amandla....

Ambacho huwa kinanichekesha ni pale unakuta mtu anapokuomba huo mchango huwa inafika mahali inakuwa kama lazima, kana kwamba ni deni!
 
Hilo ni moja ya mambo ambayo yanadhihirisha kuwa jamii yetu vipaumbele vyake viko juu-chini.
 
Vyote hivi vimeanzia kwetu huku uchagani,ukijidai una fedha zako ukagoma kuwachangisha basi unasusiwa harusi.
Inashangaza mzaramo alipokuwa anatepembea kwa mdundiko alionekana mshamba wakati leo hii kuna matarumbeta yanayopiga style ile ile.
Mimi huwa sichangi na kwenye harusi yangu sitachangisha.
Naunga mkono hoja.
 
Sidhani kamani upuuzi . Kiasi fulani upuuzi unaweza kuwa kuweka viwango fulani vya michango. Lakini michango ya harusi in general sio Upuuzi


  • waafrika utamaduni wetu ni wa ki "society" zaidi. kuliko tamaduni nyingine. Ni utaduni huo ndio maana tuna extended family, tunashirikiana kwenye misiba/harusi. kule bukoba nasikia hata mtoto akishida darasa la saba kijiji kinachanga karo kama mzazi hana uwezo
Mambo hya ya michango yamechangiwa zaidi Uchumi. Uchumi wa sasa hauruhusu mtu binafsiuwez kuhimili gharama za harusi/msiba . wakati huchumi hauruhusu utamaduni unatutaka tuwashiri kishe ndugu jamana marafiki . Ndio maana kuna michango.
 
Tunaiga kwa nani? Umesikia ulaya au hata uhindini wakichangishana kuhusu harusi? Ni sisi na tabia yetu ya kupenda umaarufu na sifa bila kuzifanyia kazi. Video, sare, limozin n.k. ni katika kuonyesha jamii kuwa wewe ni mtu kwa siku moja badala ya kuhenyea kwa muda mrefu mpaka hapo jamaa itakapokutambua. Mtazamo kama huu ndiyo unaoutufanya tuchangamkie madigirii feki badala ya kuhangaikia. Hao unaosema tunawaiga wanatushangaa jinsi tunavyotapanya mafweza kwenye harusi. Kwao ukialikwa pati, unategemewa ubebe kilevi chako na kama utakikuta utaambiwa ulipie! Hakuna biashara ya kata mti panda mti.

Amandla....

Fundi, kama ulifuatilia kwa makini mambo haya yalikuwepo ulaya miaka mingi iliyopita na baada ya kuona hayana tija wakaachana nayo na kuja na staili ya kuja au kununua vinywaji. Nina uhakika na hili.
Nakumbuka kule kwetu zama hizo mzazi akijifungua basi wenzake huja na zawadi kama ndizi, mharage, mahindi n.k. Utamaduni huu umekufa sasa wanaleta kikaratasi kinaitwa Card. Yaani utamaduni wa kumsaidia mzazi umeonekana ni hafifu kuliko kadi.
Hili la sare za mazishi nalo tumeiga, wenzetu wakialikwa kwenye misiba na mazishi huvaa suti nyeusi kama ishara ya msiba, kwa bahati mbaya Waafrika tumeona kama wanavaa sare, sasa siku hizi mtu hazikwi hadi watu wawe na Sare!! Tumeiga bila kujua tunaiga nini.
Kuhusu wahindi, ah hawa wanachangishana sana huko majamatini lakini kama ujuavyo mambo yao ni siri.

Hivi kwamfano ukifanya harusi yako na kualika nduguzo na marafiki wachache kwa uwezo wako kunaharibika nini. Mimi nimeona wenzetu wakioana wengine wanakuwa na watu kumi, cha muhimu ni wao kuwa na kumbu kumbu zao kama maharusi. Ina maana gani kuandaa sherehe na baada ya siku saba bwana na bibi harusi wanadiwa madeni ya waliogida kupita kiasi. Hivi ina maana gani kuwa na sare za mazishi na kuacha watoto au familia ya marehemu ikifukuzwa ndani ya nyumba.
Kwanini watu wasiige mfano wa Pope Joh Paul aliyezikwa simple tu hata kama uwezo wa kuwa na jeneza la dhahabu ulikwepo.
 
Mimi kwa ufahamu wangu mtu akitaka kuoa, he works hard and put saving for it and its not that you're expecting other people to pay for your expenses. If you can not meet the basic needs for the wedding, then you're not ready for it. Achane kuiga mambo msiyoyaweza au msiyokuwa na uwezo nao. Back in old days, harusi it remains the cost of the bride and groom and relative will help with whatever they can afford na si kuwa mtu anakuwekea kiwango. Na mambo yalikuwa safi tu, the most important is the blessing of the marriage from God but not bless ya kuwalisha watu 100 au 200 ambao hata siwajui, its totally insane.
 
Sidhani kamani upuuzi . Kiasi fulani upuuzi unaweza kuwa kuweka viwango fulani vya michango. Lakini michango ya harusi in general sio Upuuzi


  • waafrika utamaduni wetu ni wa ki "society" zaidi. kuliko tamaduni nyingine. Ni utaduni huo ndio maana tuna extended family, tunashirikiana kwenye misiba/harusi. kule bukoba nasikia hata mtoto akishida darasa la saba kijiji kinachanga karo kama mzazi hana uwezo
Mambo hya ya michango yamechangiwa zaidi Uchumi. Uchumi wa sasa hauruhusu mtu binafsiuwez kuhimili gharama za harusi/msiba . wakati huchumi hauruhusu utamaduni unatutaka tuwashiri kishe ndugu jamana marafiki . Ndio maana kuna michango.

Kaka mambo ya misiba ni shida na mtu lazima mnawajibika kwa hali na mali kusaidia hapa sijaongelea kwamba michango haifai (mtu yeyote aje saa yoyote kuchangisha elimu, nitampa bila shida..... Msiba tena bila mchango kupita mimi mwenyewe nina wajibu wa kuchanga) sasa basi kwenye msiba tunachanga ili kumzika mwenzetu na pesa zibaki kuwasaidia wafiwa (mambo ya sare na tshirt ni ya nini)?

Kuhusu harusi huwezi hukajustify michango.... hivi umeshaona cost ya harusi?, hivi bila kujifanya tajiri ukafanya harusi kubwa huyo mke humpati?, kuna faida gani ya kufuja mali kwa siku moja? extended family hazijaanza leo, mbona zamani watu walikuwa wanafanya harusi bila michango???? Sasa unakuta A anaoa, B yupo kwenye kamati ya michango, na anampa C kadi za michango asambaze, ambazo anakupa wewe uchange ambaye hata huyo A humjui ni nani.... matokeo yake D ambaye ni rafiki wa karibu wa A ila hana pesa za kuchanga anashindwa kuhudhuria kama huu si ulimbukeni ni nini???? Sasa hadi Anayeoa anapewa baadhi ya kadi za ndugu lets say 20, kwahiyo hadi mtu unapangiwa ndugu wa kuja kusherekea.
 
Nimekuwa nafuatilia jinsi desturi ya kuchangia na kufanya sherehe kubwa inavyozidi kushika kasi, ikipelekea ule wigo wa kuomba michango kupanuka kiasi kwamba sasa hata mtu ambaye jina lako halijui vizuri anaweza kukuomba mchango.

Aidha michango na sherehe hizi zimekuwa mzigo mkubwa sana kwa baadhi ya watu, ikiwa ni pamoja na wale wenye kipato kidogo wanaochangiwa na kulazimika kulipa michango hiyo kwa miaka mingi. Je, wajua kuwa kuna familia ambazo zimefikia kulazimisha ndugu wauze mashamba au mifugo mtaji ili kupata fedha za kuchangia sherehe?. Je, wajua kuwa kuna watu ambao zaidi ya nusu ya kipato chao wanatumia kuchangia sherehe na huku wakishindwa kulipia huduma muhimu kama shule, matibabu, lishe, nk. Na kuwa wakati mwingine wewe au mimi (au wengine kama mimi na wewe) ndio wenyeviti na makatibu wa sherehe hiyo?.

Na ni sisi tunaoona fahari ya kutumia milioni 30 au zaidi kwenye sherehe usiku mmoja?
Kuna kijana mmoja jamaa yetu juzi juzi alipata shule Australia akawa anatafuta mchango wa dola 5,000 aende. Alipata 2,000 na amwekwama kwenda.

Mwaka kesho akisema anaoa tutamchangia milioni 15-20!!!. Hii si hadithi, ni ukweli, na ni kielelezo cha ulimbukeni tuliofikia.

Siku za karibuni nimetambua kuwa kuna kundi kubwa tu linasikitishwa na huu mwenendo, na hata kutambua kuwa tunaweza kuwa tunaandikiwa dhambi kubwa (na hukumu yatusubiri) kwa jinsi wengi wetu tunashindwa kusaidia mambo ya msingi lakini tunakuwa wepesi kutoa kwenye sherehe. Wengi wanaamini kuwa tumeshatumbukia kwenye lindi la mazoea ambapo hatuwezi kujitoa mpaka upepo uje ubadilike wenyewe!.
Mimi nafikiri wasomi tuna jukumu muhimu la kuwa chachu ya mabadiliko pale ambapo mazoea yenye madhara yanavuka mipaka na kuweza hata kuwa chanzo cha ufukara na kuviza maendeleo.

Ili kubadilisha hili jambo, lazima tuanzie mahali. Mimi napendeleza na kuanza kutekeleza. Kuanzia Januari 2011, nitapunguza michango ninayotoa.

Nitatoa tu kwa mtu wa karibu sana, na nitachanga kidogo. Usishangae nikakuchangia 20,000/= kama ulitegemea 50,000/= kwa mfano. Kuanzia July 2011, nitaacha kabisa kuchangia sherehe. Badala yake nitakuwa nachangia elimu pale ambapo mzazi hayupo au mhusika kweli hana uwezo na pia nitachangia miradi mingine ya jamii na maendeleo.

Je waniunga mkono? Kama ndiyo sambaza huu ujumbe kwa mtandao wako.

Dr. D.R.Olomi
Box 35036
Dar es Salaam, Tanzania
 
Nimeshangaa juzi nimetumiwa minutes za kikao cha harusi yenye bajeti ya Mil 21 huko Dar, eti nichangie...Kwa hili nitaonekana mbaya, hawapati mia yangu!
 
Kuchangia harusi ni gharama kubwa sana.
Unatoa pesa ya mchango, unanunu zawadi ya maharusi na inabidi uweke mafuta mengi kwenye gari ili kuweza kushiriki kwenye harusi.
Mi sioni haja ya watu kuchangiwa.
Mmependana, nendeni kanisani rudini nyumbani yatosha
 
Ni ulimbukeni na hauna tija milion 20 mnaichoma siku moja.

Baada ya harusi wachangiaji na maharusi ni majuto kwenda mbele.

Kuna watu wamechangiwa mapesa tele wakanunuliwa na mazawadi tele na mzazi wa mwanamke. Mume hata nyumba yakuweka hizo zawadi hana kapanga chumba na sebule.


Sherehe ikawa kabambe ya mamilioni,
bora wangempa bwana harusi hata 5 m akakate kakiwanja pugu.

Hii tabia ni butu kabisa haina maendeleo.
 
Back
Top Bottom