Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

bht u r right ....................ukifanya kwa uwezo wako raha kweli kweli, lakini wabongo tunapenda faghari na tunapenda cha bure

mimi hii system iliyopo sasa siielewi hata kidogo
 
sasa sharti la kuwa toa 50000 ndio nikupe kadi si ni sawa na kiingilio tu!

mtu na afanye harusi kwa mujibu wa kipato chake .............kulazimisha wenziwe kumchangia ni tabia za ajabu tu. Hapo unamlazimisha na mtu kuvaa wenyewe wanaita theme color!

akanunue nguo ya rangi hiyo unayotaka na vikorombweza vyake na kisha alipe na kiingilio! .......mimi harusi za sare kwanza huwa siendi pia.....nimemaliza primary zamani, uniform basi kwa kwel
i

haki ya nani G leo umeamua kunimaliza...lol...nilikuwa moshi wkend hii mdogo wake na ma frnd alikuwa anaolewa, nilishaambiwa nipo kwenye kamati(japo ckuweza kuhudhuria kikao hata ki1 coz nipo mbali kidogo lakini hela ya kamati ni tofauti na wasio wanakamati)..nikaambiwa theme colour ni njano, kiatu cheupe au cheuc, na kamati tunashona mshono huu, nikatumiwa mail ya maelezo kibao ili niendelee kujiandaa nikiwa huku, nimeingia gharama ya nguo na vikorombezo kibao, bado mwanakamati ni lazima utoe laki 2, nimeweka chini kama laki 4 hivi ukiunga na wese la ku drive mpaka moshi....uwiii narudi njoro hivi hivi nikijiona....
 
Nyamayao dearest ukiendekeza hii mambo wala sitashangaa ukirudi Njoro ukakate baridi huko.

Lakini jamani kwa nini haya yote??
kama una uwezo wa kufanya such a wedding reception well and good
mi sitaki kusumbua mtu na vivyo hivyo sitapenda kusumbua mtu kwa shughuli yangu
 
hahaaa G unanichekesha sana aisee lol!!

suala la kufanya harusi kulingana na kipato watu naona halijawaingia akilini bado. tena mi naona hii inakufanya uwe 'stress free' kabisa. Plan it they way you can afford it, usiwe mzigo kwako mwenyewe na kwa wengine pia!!!

yaani kweli inaumiza sana,kweli mpaka mchango wa ubatizo? nilimuuliza huyo ndugu yangu mchango wa nini kwenye ubatizo akaniambia anafanyia kwenye hall sasa tusaidiane..i was lyke jamani kuna ulazima wa kufanya mambo makubwa na kusumbua watu....wa kwangu mie niltoka kanisani kubatiza narudi home kula ugali na matembele.....
 
una uwezo fanya hata sie waalikwa wote utupe zawadi za dhahabu from tiffany za kuondoka nazo...........huna usituongeze gharama maisha magumu.

ubatizo ukafanye kwenye hall kwa kutumia pesa ya mwenzio.................na mara nyingi wenye kufanya vitendo hivi ni mama wa nyumbani, wenye kwenda kazini kidogo wana afadhali
 
ni mama mwenye vibiznec vyake, pesa ipo ya kubadili mboga tu lakini nashangaa kwenye hili mambo ni mengine...
 
ungemwambia kwa kweli mimi pesa ya ubatizo kwenye holi sina ya kukupa .....................mfanyie nyumbani na usialike watu zaidi ya watu waliomzunguka mtoto

ukimpa black and white huwa anajifunza ati mara moja moja
 
thanks for whoever started this topic since it has been pissing me off! mimi nikiletewa kadi (hasa ambzo zimepitia mikono mingi) I just dump them in the garbage can labda kama ni mtu wa karibu sana. to hell, nikiwa na sherehe ya mwanangu hata kama ina watu kumi its ok! what matters ni kufanikiwa kupata kilichotakiwa. tena nawatonya wale wanaochangia mapesa mengi kwenye shughuli kwamba pesa unazochangia hazifiki zote kule zinakotakiwa kwenda. zinachotwa nyingi na kiasi kidogo kinapelekwa maana hatuna utaratibu wa kumwandikia mchangiaji kumshukuru kwa kutaja kiwango alichochangia. kwenye matatizo k.v msiba nitachangia. no objection kwa hili.
 
what about this......Shemeji naomba mchango wako yule mwanangu anagraduate chekechea,tarehe....

yani natamani ingekua twafanya harambee kama kule kenya za kuwapeleka watoto shule na sio kuombana viingilio vya party(kama alivosema mdau 1 hapa)
 
kunawengine huwa hawana haya wanaomba michango ya ubatizo, arobain iwe ya kuzaliwa kwa mtoto ama kumaliza msiba, kuna nyingine kali zaidi kuna jamaa flaniflani waliomba michango ya kutimiza mwaka tangu wafiwe na mamayao nilijiuliza hivi kweli mtu unakaa chini unafikiria akili inafika mwisho unataka kuachangiwa eti mama kafikisha mwaka tangu afariki kweli!! :mad2:
 
Kama ujajenga, tafuta kiwanja anza mara moja ujenzi ... usisubiri ifike milioni anza na hio laki nne !!!
Ukifikiria nyumba inahitaji mfuko wa saruji na at the same time kuna kadi ya ubatizo inahitaji 50,000 eti salio la chini !!!

Mimi kuna viself 2 nimeanza kujenga makusudi kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka ili kukabiliana na
hizi card za viingilio maana kwa sasa ninazo kama sita for the next month, nazipiga kumbo zote kwenye nyumba...
 
cjui kama nimkupata kaka, ssa kujenga kunahusianaje na kutoa mchango? au uantaka kusema kila atakaekuambia mambo ya mchango utamwambia unajenga, utatangazia wangapi?
 
i remember to do a simple function only with my family and few friends BILA kuchangisha coz sikutaka stress za kuchangisha watu...kilichofuatia ni lawama from "not invited" tena na kuambiwa naringa coz nilichagua watu wa kuwaalika,wengine wakadai wangenichangia na wasingekuja.Huwezi kuwaridhisha watu wote thats why i always do things the way i want,Tanzania bado tunathamini vitu visivyo na maana,wengine wanafunga Harusi kuubwa baadae wanabaki na madeni au hata cash ya kuanzia maisha after harusi hawana,why that?:doh:
 
hilo nalo ni tatizo pia, kwani kuna ulazima wa mtu kuhudhuria functions zote?
 
cjui kama nimkupata kaka, ssa kujenga kunahusianaje na kutoa mchango? au uantaka kusema kila atakaekuambia mambo ya mchango utamwambia unajenga, utatangazia wangapi?

Sio Kwamba utatangaza kwa nanayekupa kadi ya mchango kuwa wewe unajenga, hapana.

Maana yangu ni kwa wale ambao wanaoshindwa kuzikabili hizi kadi na kufanya hata 70% ya mshahara kuishia kwenye sherehe kadha wa kadha ! Unajua atleast ukiwa na shughuli ya maendeleo endelevu unaweza kufikiri mara mbili zaidi juu ya hio michango, either usimamishe kujenga ( mfano ) kwa mwezi or miezi na hata mwaka then mambo ni yale yale hata na mwakani !!! au uendelee na ujenzi ( muhimu ). Kuna watu wanadiriki hata kukopa kwa njia yeyote ile apate kuchangia sherehe husika, by the end of the day unalala njaaa !! Khaaa.. Ten hii ya kusema kiwango cha chini laki moja or elfu hamsini ndio balaa !! kama unacard sita hivi , then mshahara wote unaishia kwenye michango na madeni juu !!
 
thanks for whoever started this topic since it has been pissing me off! mimi nikiletewa kadi (hasa ambzo zimepitia mikono mingi) I just dump them in the garbage can labda kama ni mtu wa karibu sana. to hell, nikiwa na sherehe ya mwanangu hata kama ina watu kumi its ok! what matters ni kufanikiwa kupata kilichotakiwa. tena nawatonya wale wanaochangia mapesa mengi kwenye shughuli kwamba pesa unazochangia hazifiki zote kule zinakotakiwa kwenda. zinachotwa nyingi na kiasi kidogo kinapelekwa maana hatuna utaratibu wa kumwandikia mchangiaji kumshukuru kwa kutaja kiwango alichochangia. kwenye matatizo k.v msiba nitachangia. no objection kwa hili.

hii imenigusa sana nakumbuka niliwekwa muweka hazina wa shughulu moja ya rafiki yangu wa kartibu mno. Jamaa wakapendekeza mpishi sahani moja 6000 na kunatakiwa sahani 200 katika kufutialia na kwakuwa mpishi nilikuwa ninafahamiana naye akaniambia mwenyekiti kamuambia alipwe sahani 150 halafu ataongeza sahani 10 kama zawadi wakati wa kugawa chakula afanye manjonjo zitoshe mtu wa keki naye dilli kwa mwenyekiti na katibu na mc naye dili yaani kwa ujumla kuna kama Tshs 500000/= zilikuwa zipotee baada ya kukusanya michango nikawazunguka mwenyekiti nikawalipa wahusika mwenyewe, baada ya kulipa na michango iliyokusanywa zikabaki kama 1.4m wakati tulipokuwa kwenye sherehe katibu na mwenyekiti walikuwa wamenuna na wakawa wamenilazimisha eti baada ya sherehe hela yote 1.4m tuitumie kuvunja kamati nikawaambia hilo haliwezekani jamaa hawajaongea tena na mimi lakini shukrani tutaka maliza ile sherehe na alipoitwa mwenyekiti kutoa shukrani jamaa hakutaka kuongea akasingizia anaumwa na ninaweza kuongea kwaniaba yake wakati nilipoonge mwashoni baada ya kutoa zawadi ya kamati tukamkabidhi bibi na bwana harusi hela zilizobaki kama za kuanzia maisha hivyo tuweni makini haina haja ya kuwa na mambo makubwa wakati hatuna uwezo na wengine wapo kwa ajili ya kuiba kwenye hizo harusi na nafikiri ni kweli kabisa michango haifiki kama mtakavyotoa kwa hiyo haina haja ya kuchangia

Kwanini tusichangie kunua madawati kwenye shule zetu au madawa kwenye zahanati zetu, kwanini tusichangie kujenga nyumba za walimu? kwanini tusichangie kama rafiki yetu kashindwa kumlipia mwanaye ada shuleni au chuo kikuu? Kwanini tusichangie matibabu ya ndugu zetu wagonjwa kama tiba inahitaji gharama kubwa?

Kwanini tusichangie kuweka kifusi au kokoto sehemu korofi ya bara bara zinazoingia mitaani kwetu? kwanini mitaani kwetu tusichangie kuchimba kisima na kujenga tanki kwa ajili ya kupata maji safi?

Kwanini tuchangie hizi harusi ambazo baada ya siku tatu tu watu wameachana kwanini usioe kwa uwezo wako?

huo ni mtazamo wangu kutokana na hiyo harusi ambayo nilikuwa mwekahazina kama mnachangia hizo hela mumuachie bwana/bibi harusi kwajili ya kuanzia maisha hapo sawa kumbuka ndoa nyingi zisizona mbwembwe hudumu sana na hazina matatatizo sana kutokana na nilivyoona usiniulize kwanini?

na ndio maana kwa sasa wanaume wengi wakifikiria kuoa huwa wanafikiria gharama kubwa siku ya kufunga ndoa na ndio maana wengi wetu hatutaki kuoa
 
haha wazo zurii sana kwani baada ya miezi kadhaa hutakuwa mtumwa wa mwenye nyumba hongera.laki tatu ni nyingi sana kwa ujenzi
 
Hii safi sana kumbuka lawama ni sehemu ya maisha na si wote watakaokusema vizuri just MYOB
 
Duh Kasimba we kiboko nadhani huyo Mwenyekiti na Katibu hawatakusahau milele......ila ni fundisho kubwa,harusi nyingi hwa zinaenda mrama kwa ajili ya wanakamati waroho kama hao uliowataja...!:nod:
 
Duh Kasimba we kiboko nadhani huyo Mwenyekiti na Katibu hawatakusahau milele......ila ni fundisho kubwa,harusi nyingi hwa zinaenda mrama kwa ajili ya wanakamati waroho kama hao uliowataja...!:nod:

Ndugu we acha tu maana ile hela iliyobaki kwa kweli nadhani ilimsaidia bwana harusi kwani baada ya honey alikuja kunishukuru mno na kusema kuwa angalau ile hela italipia madeni na itakayobaki itamsaidia. Harusi hizi huwa zinawaachia maharusi mifuko mitupu na ndio maana mwanzoni nikasema basi kama ikibidi michango twaweza wapa hao maharusi kuanzia maisha.

Yule mwenyekiti na katibu wake mpaka leo hatuongei lakini sijali sana kwani nilizuia kaufisadi fulani. Kwa wale wanaoooa na kuolewa mlione hili ukiona mwenyekiti au katibu au mjumbe kashikia bango kuhusu MC,matarumbeta,chakula mapambo na keki tuwe makini huenda kuna kitu kipo nyuma ya pazia kwani kwa kawaida huwa inakuwa vizuri wajumbe wa pendekeze theni muwapigie kura tena baada ya kuwaita na kujieleza kwenye kikao otherwise wizi mtupu.
 
Back
Top Bottom