Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

heeeeeeeee, yani hapo mkuu umelenga!.
ebwana kuna kikao kimoja nilihudhuria, mshkaji alikunywa bia 4, kumbe watu wanamuangalia tu spidi yake, kufika kwenye uchakavu si akatoa 1000/=, acha akunjwe shati alipie,. hakuna usawa mie ninywe maji ya 300 mwingine anywe bia 5 halafu tutoe sawa uchakavu, Lol.

Inawezekana watu design hii wakawa wengi sana, wanawahi kwenye vikao wanapiga beer zao taratibu wanajua atakuja MJ na George_Porjie kulipia bill....noma aisee..
 
nikifika kwenye kikao huwa naagiza kinywaji changu tena kwa sauti "MHUDUMU NILETEE KESTO BARIDIII, USISAHAU KUNIRUDISHIA NA CHENJI YANGU", baada ya hapo ujumbe unakua umefika na sihusiki na uchakavu baada ya hapo.
 
Mitanzania bana, yaani hata mambo yaliyoko nje ya katiba yanatuumiza kichwa. Hivi kuna mtu timamu bado anatoa michango ya harusi? Ili iweje? Kama ni kwa ajili ya kupata manufaa baadae, sawa. Ila mimi sitoi mchango wa harusi kama sijui nitafaidika au nilifaidika nini na ninayemchangia. Mke/mume wako yananihusu nini mimi? aaaaggggggggggggggggghhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Wantazania na Waganda bado mna hela za kuchezea! muda ukifika tutarekebisha wenyewe. Kila mtu ataandaa sherrhe kadri ya uwezo wake kama ni lazima. Kwa sasa tuendelee tu kutumika.
 
Hulka ya kusema "hapana" Tanzania haipo. With time, people will learn!
 
Hulka ya kusema "hapana" Tanzania haipo. With time, people will learn!

Kama hujaenda kwenye kikao cha harusi jamaa anakupigia simu anaweka kwenye speaker-phone anakuuliza unaahidi kiasi gani ili kila mtu asikie ukisema 50, watu kwenye background oooooohhh haiwezekani kima cha chini kilo....bongo bana..
 
Halafu mbaya ni pale unapodaiwa kuwa mwanakamati halafu kule kwenye kikao cha kamati unaambia kuahidi ni kuanzia laki moja kwa wanakamati. Kuwa mwanakamati kwenye unalazimishwa tu, halafu na pesa kutoa unalazimishwa. Ukisema sina pesa jamii inakutenga. Huu ni ujinga tu.
Hapo hujaingiza gharama za dawadi, usafiri wa kurudi usiku siku ya harusi, nk.
wizi mtupu!!!
 
sio siri hizi harusi za kuteketeza mamilioni ya pesa kwa masaa,najiuliza sipati jibu ila ndo hivyo mambo ya vipaumbele
 
halafu baada ya mwezi mmoja ndoa kwishney!, chali miguu juu
 
Mwezi huu unaokuja ni balaa tupu yaani harusi na send off zimefukuzana kila wiki na wanahitaji michango ya nguvu kweli, ukipata kijimshahara chako mwezi huu usipokuwa makini unaharibu kwako, shughuli hizi zimezidi kuliko hata shughuli zile za msingi na wabongo wanapenda sana kwa sababu ya ulevi na starehe nyingine na wanafanya ni sehemu ya mitoko, hata birth day, kipaimara na ubatizo siku hizi ni mchango tu kwa kwenda mbele.VITA NI VITA!!!
 
halafu ndoa zenyewe hazidumu, watu wanafikiri mapenzi ya ushikaji (uboy na ugirl friend) ni sawa na kwenye ndoa, kumbe SIYO!!!
 
Nitaingia kwenye ujasiriamali rasmi muda si mrefu. Nitakwenda kuvuna hizo pesa mnazochangishana. (Kwa kutoa jasho, of course!) Je, wewe umekaa upande gani wa TV - anayetizama au anayetizamwa?
 
Nitaingia kwenye ujasiriamali rasmi muda si mrefu. Nitakwenda kuvuna hizo pesa mnazochangishana. (Kwa kutoa jasho, of course!) Je, wewe umekaa upande gani wa TV - anayetizama au anayetizamwa?

Kuna jamaa mmoja Dar anahusika na biashara za kufunga mizingi na rims kwenye magari, huju jamaa alifanya kitu SAFI SANA alikusanya michango kama 30mil baada ya hapo akasambaza kadi za harusi, siku moja kabda ya harusi akatuma taarifa kuwa harusi inafungwa kama kawaida lakini sherehe ya harusi imesimamishwa ghafla kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake na kuwa angewajulisha ni lini sherehe itafanyika....huu ni mwaka nne kinywa hakuna sherehe na 30mil kamalizia nyumba yake mbezi.....hii safi sana...wabongo mkome kutoa michango
 
Athari za ujamaa ni nyingi jamani

kama ujamaa ni ukimwi basi michango hii ni moja ya dalili tu

The nation is sick
 
I think is about time now watanzania tuamke,
Why is it tunaweza kuchangia harusi lakini hatuwezi kuchangia fee watoto wetu wanapotaka kusoma? leo hii ukisema unaitata family and friends kichangia univesity fee ya mtoto wako, watakupeleka milembe! lakini ukuwaita kwa ajli ya kukaa vikao vya harusi, ooooo my God umewapa kazi, Katibu, mwenyekiti ect,

Lets start vikao kwa ajili ya Higher Education!

Tanzania yetu
 
Kuna jamaa mmoja Dar anahusika na biashara za kufunga mizingi na rims kwenye magari, huju jamaa alifanya kitu SAFI SANA alikusanya michango kama 30mil baada ya hapo akasambaza kadi za harusi, siku moja kabda ya harusi akatuma taarifa kuwa harusi inafungwa kama kawaida lakini sherehe ya harusi imesimamishwa ghafla kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake na kuwa angewajulisha ni lini sherehe itafanyika....huu ni mwaka nne kinywa hakuna sherehe na 30mil kamalizia nyumba yake mbezi.....hii safi sana...wabongo mkome kutoa michango

Yaani ukusanye 30M wewe pekee yako na kuziweka kibindoni bila kamati yako kukupa kibano?
 
hii mentality ya michango ya harusi ishatuingia watanzania kiasi cha kuwa ukifanya harui yako bla ya kuchangisha utasikia unaambiwa "anataka kutuonyeha kama yeye ana pesa "
 
Back
Top Bottom